MAKAZI YA GAVANA WA BENKI KUU

TAARIFA KUHUSU UJENZI WA MAKAZI YA VIONGOZI WAKUU WA BENKI KUU YA TANZANIA

GAVANA WA Benki Kuu na manaibu wake kwa mujibu wa mikataba ya kazi zao, wanastahili kupewa nyumba ya kuishi kila mmoja. Hapo awali Gavana alikuwa anaishi Barabara ya Mahando kiwanja namba 387Masaki na Naibu Gavana Barabara ya Msese kiwanja Namba 43.

Awali Benki Kuu ilikuwa na viongozi wakuu wawili, Gavana na Naibu wake mmoja. Baada ya mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2006, Benki Kuu ina viongozi wakuu wanne; Gavana na Manaibu wake watatu. Kila mmoja wao, kwa mikataba iliyowekwa anastahili kupata nyumba ya kuishi.

Mwaka 2006, kabla ya uteuzi wa viongozi wa sasa wa juu, Benki Kuu ilifanya uamuzi wa kujenga nyumba mbili zaidi kwa makazi ya viongozi walioongezeka. Iliamuliwa nyumba hizi zijengwe kiwanja namba 57 Barabara ya Mtwara Crescent na kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe maeneo ya Oysterbay.Viwanja vyote viwili vilikuwa ni mali ya Benki Kuu vilivyokuwa na magofu yaliyopigwa marufuku kuishi wanadamu (condemned).

Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizi ni pamoja na mashine ya umeme (generator), mashine ya kupoza hewa na matenki ya kuhifadhi maji. Wakati huohuo, shughuli zingine zilizofanyika ilikuwa ni kutengeneza mahali pa kuegesha magari pamoja na bustani.

Wataalamu hawa baada ya uchoraji huu walifanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na maelekezo kwa wazabuni ili itumike kualika zabuni. Taratibu zote za manunuzi zilifuata sheria ya manunuzi katika kuwaalika wazabuni na kuteua wakandarasi. Kila nyumba ilikuwa ni mradi unaojitegemea na kila moja ilifanyiwa zabuni peke yake.

Izingatiwe kuwa ujenzi wa nyumba hizi ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Profesa Benno Ndulu kujiunga na Benki Kuu Septemba 2007.

Tangazo la kuwaalika wazabuni kwenye kiwanja namba 12 Barabara ya Tumbawe lilichaapishwa katika gazeti la Daily News la Februari 26,2008.Wakandarasi wote wa daraja la pili au la juu zaidi walialikwa kuwasilisha zabuni na walitakiwa kulipa ada ya shilingi 50,000. Wakandarasi 12 walituma maombi na kuchukua hati za zabuni.Lakini kati ya hao 10, waliwasilisha maombi yao kabla ya kufikia tamati ya kupokelewa maombi hayo Machi 25,2008.

Zabuni hizi zilifunguliwa na Bodi ya Zabuni ya Benki Kuu na kufanyiwa tathimini ikishirikisha mtaalamu mwelekezi wa mradi huo na Idara ya Miliki ya Benki Kuu. Mapendekezo kutoka kwa wakandarasi yalikuwa na viwango vya gharama kuanzia Shilingi 1,399,184,549.00 hadi shilingi 1,847,763,537.00 kwa kiwango cha juu. Baada ya tathmini ya zabuni hizo na kufanya masahihisho ya tarakimu zilizowasilishwa, mzabuni aliyeshinda kwa kuwa na gharama ya chini kuliko wote alikuwa ni M/S Eletrics International Co. Limited. Gharama yake baada ya masahihisho ilikuwa ni Shilingi 1,274,295,025.26.

Taarifa ya tathimini hiyo ilipitia tena kwenye Bodi ya Wazabuni na ndipo ilipofikia uamuzi wa kumteua M/S Eletrics International Co. Limited kwa bei ambayo haitabadilika (fixed price) ya Shilingi 1,274,295,025.26 ya kukamilisha ujenzi huu katika wiki 32.Mkataba wa ujenzi na mkandarasi huyo ulitiwa sahihi Juni 03,2008 na kazi ya ujenzi ikaanza mara moja. Mkandarasi huyu aliteuliwa na Bodi Zabuni (DSM) ya Benki Kuu ikaridhia kuwa M/S Remco (International) Limited ishughulikie maswala aya vipoza hewa; M/s Ginde EAP Services Ltd ishughulikie maswala ya maji safi, mabomba na maji taka na M/s Pomy Engineering Co.Ltd ishughulikie maswala ya umeme. Makampuni yote hayo yamesajiliwa Tanzania.

Wazabuni wa nyumba Namba 57 Mtwara Crescent nao pia walialikwa kwa mfumo huohuo wa ushindani wakianza na wakandarasi watano (5) ambao waliwasilisha maombi yao na kuishia na uteuzi wa M/s Holtan Builders Ltd ambayo gharama yake ya Shilingi 1,272,348,512.00 (fixed price) ilikuwa ni ya chini kuwashinda wengine na makubaliano ya kukamilisha ujenzi katika muda wa wiki 24. Mkandarasi huyo alitumia kampuni zifuatazo kwa shughuli zingine: M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd kwa shughuli za mabomba, maji safi, na maji taka, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd kwa maswala ya umeme na M/s Remco (International) Ltd kwa shughuli za vipoza hewa. Mkandarasi ndiye mlipaji wa gharama za shughuli hizi zote zinalipiwa kutokana na gharama ileile iliyokubalika kwa mkandarasi mkuu.

Watendaji wote wa miradi hii wanaonyeshwa kwenye mabango ambayo bado yapo kwenye viwanja hivyo. Uteuzi wa Gavana Ndulu, Manaibu Gavana, Dkt. Enos Bukuku na Bw.Lila Mkila ulifanyika wakati mipango ya awali ya kujenga nyumba hizi

ilikuwa imeshaanza. Benki Kuu ilikodisha nyumba mbili, mojakiwanja namba 480 Barabara ya Bray, Masaki na nyingine kiwanja namba 591,Msasani Peninsular kwa matumizi ya viongozi hao wawili ambao walikuwa bado wanaishi kwenye nyumba zao mbali na ofisi.

Kati ya Oktoba 2007 aliporipoti kazini kama Naibu Gavana hadi Aprili 2008, Profesa Ndulu aliishi kwenye nyumba yake iliyoko Mbezi Beach, na Naibu Gavana Mkila naye pia aliishi nyumbani kwake kabla ya kuhamia kwenye nyumba hizi zilizokodishwa.

Benki Kuu iliamua kumhamisha Naibu Gavana Juma Reli kwenda Barabara ya Mahando Masaki ili kuruhusu matengenezo ya nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni Barabara ya Msese. Naibu Gavana Dkt.Bukuku anaishi kwenye nyumba yake na Benki Kuu inatoa posho ya nyumba kulingana na mkataba.

Nyumba hizo mbili zilizojengwa chini ya miradi iliyotajwa, sasa hivi zimekamilika.Gavana wa Benki Kuu, Profesa Ndulu alihamia nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe Desemba 17,2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba namba 57 Mtwara Crescent Desemba 4,2009

Kama ilivyo kiutaratibu, ukaguzi wa mahesabu yanayohusu miradi hiyo utafanyika kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006, Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ndiye mkaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu; ambaye ameanza kufanya kazi hii tangu mwaka 2007. Yeye ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hili.

IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA UMMA NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
SEPTEMBA 30, 2009
BOT GOVERNOR'S OFFICIAL RESIDENCE

CONSTRUCTION OF THE BANK OF TANZANIA EXECUTIVE RESIDENCES

Bank of Tanzania Executive officers are entitled to official residence provided by the Bank. Initially the Bank used to have only two executive officers, the Governor and one Deputy Governor. The Governor was living at BOT house No. 387 Mahando Street and Deputy Governor at BOT house No. 43 Msese Road. As a result of the changes made in section 8 of the Bank of Tanzania Act, 2006, the Bank has now four Executives, the Governor and three Deputy Governors, for whom it is obliged to provide official accommodation.

In 2006, in advance of the presidential appointment of the current office bearers, the Bank decided to construct two additional executive accommodations, one on plot No. 12 Tumbawe Road and another on plot No. 57 Mtwara Crescent at Oysterbay, Dar es Salaam. A team of consultants led by M/S SKY Architects Consultants was engaged to provide schematic drawings that were reviewed by the Bank and two of these, one for each plot, were selected for detailed design stage.


Each residence was designed to be a one storey building with five bedrooms, visitors lounge, family lounge, dining area and associated service rooms. The outbuildings include servant’s quarter, car ports, swimming pool, boundary wall, security systems and guard house. Services include power generator, central cooling system and water storage facilities while external works include landscaping and paved car park.

The consultants then prepared bills of quantities and technical specification that were compiled to form tender documents ready for tender process. All procedures in line with procurement laws and regulation were adhered to, when determining the cost of each of the residences as well as in selecting contractors and sub contractors. Each residence was considered as an independent project and a separate tender process was carried out for each one.

It is important for the public to know that, the planning and decision to have these houses constructed was done before Prof Benno Ndulu was appointed at the Bank of Tanzania.

Tenderers for works at plot No. 12 Tumbawe Street were invited using competitive open tender advertised on the Daily News of 26th February 2008. Interested contractors of class II and above were invited to apply for tender document and were instructed to pay non-refundable tender fee of Tshs 50,000/=.

A total of 12 contractors applied and collected the tender documents, but only 10 submitted their bids before deadline, 25th March 2008. The received tenders were opened by BOT Tender Board and forwarded to Project Consultant via the Bank of Tanzania Estate Management Department for evaluation. Tender results read during tender opening ranged from the lowest tender price of Tshs 1,399,184,549.00 to the highest price of Tshs 1,847,763,537.00.

After tender evaluation, which involved preliminary examination of tender, arithmetic correction and detailed analysis, the lowest evaluated bidder was determined to be M/s Electrics International Co. Limited at a corrected tender price of Tshs 1,274,295,025.26. Evaluation report was deliberated by BOT Tender Board and it was approved to award construction works to M/s Electrics International Co. Limited at a fixed contract price of Tshs 1,274,295,025.26 and 32 weeks completion period.

Contract agreement between the Bank and the contractor was signed on 3rd June 2008 and construction works started immediately thereafter. Subcontractors for specialized works were nominated and approved by the BOT Tender Board. These included M/s Remco (International) Ltd for Air Conditioning installation, M/s Ginde EAP Services Ltd for plumbing and drainage systems and M/s Pomy Engineering Co. Ltd for Electrical installations. All these companies are registered in Tanzania.

Tenderers for house no. 57 Mtwara Crescent were invited through a competitive tender method where 5 short-listed contractors were invited to collect tender documents and bid for work. Submitted tenders went through the same tender process detailed above that resulted into M/s Holtan Builders Ltd being determined the lowest evaluated bidder at Tshs 1,272,348,512.00 and 24 weeks completion period.

Subcontractor nominated and approved in this case were M/s Jandu Construction & Plumbers Ltd for plumbing and drainage systems, M/s Barkley Electrical Contractors Ltd for electrical installation and M/s Remco (International) Ltd for Air Conditioning installation. The cost for specialized works undertaken by subcontractors for each site is included on the fixed contract prices for respective main contractor. Likewise, lists of project parties for both works are displayed on the sign boards that are still erected at the front side of respective plots.

While the two projects were still on preliminarily stages, appointment of the three new executive officers to Bank of Tanzania was completed. The Bank was thus compelled to rent two residential houses one on plot No. 480 Bray Road Masaki and another on plot No. 591 at Msasani Peninsular.

One house was allocated to Professor Benno Ndulu, by then the first Deputy Governor, and another to Deputy Governor Lila Mkila. Prior to moving to this rented house; between October 2007 and April 2008, Prof Ndulu lived in his own house in Mbezi Beach. Likewise Deputy Governor Mkila stayed in his own house before moving to the rented premise.

These movements were to facilitate easy access to the office in light of traffic congestion in the city. It was decided to relocate Deputy Governor Juma Reli to house No. 387 Mahando Street to give way for planned refurbishment required at house No. 43 Msese road. Deputy Governor Enos Bukuku is residing in his own private house, and is paid housing allowance in lieu of occupying official residence as entitled – pending the planned refurbishment of Plot No. 43 Msese road residence.

The construction of the two executive residences has now been completed. Both Governor Ndulu and Deputy Governor Mkila, who were residing in rented houses have relocated to the new Bank of Tanzania official residences. The Governor has relocated to house No. 12 Tumbawe Road since 17th December 2009 and Deputy Governor Mkila to house No. 57 Mtwara Crescent since 4th December 2009.

As it is with all other Bank of Tanzania projects, these too will be subject to the usual audit process. It might be important for the public to know that, as stipulated in the Bank of Tanzania Act 2006 the Controller and Auditor General (CAG) is the external auditor for the Bank. The CAG has retained the services of the Ernst and Young, an international audit firm to support the external audit work of the Bank.

Issued by Public Relations & Protocol Department
BANK OF TANZANIA
30TH DECEMBER 2009

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 49 mpaka sasa

  1. IT DOESN'T RING THE BELL STILL, I AM AFRAID!!

    ReplyDelete
  2. Kinachopigiwa kelele kwenye huo ujenzi ni kwamba hizo hela zilizotumika kwenye huo ujenzi ni nyingi mno kulingana na jengo lenyewe. Na hapo changa la macho limeanzia kwenye hiyo M/S SKY Architects Consultants na hizo estimates zao.

    Binafsi siamini kwamba kati ya zabuni zote zilizoletwa hakukuwa na ya chini kuliko hiyo ya M/S Eletrics International Co. Limited, ila nadhani kulifanyika usanii wa kukataa hizo zabuni za chini sana kwa kisingizio kwamba hizo kampuni husika hazina uwezo au uzoefu wa kutosha, kwa vile tayari mlikuwa mislead na hao Sky Architects au kwa makusudi.

    Hapo hata akiitwa mkaguzi wa mahesabu kutoka mbinguni hawezi kuona kasoro yeyote kwa vile hata kama kuna ufisadi umefanyika basi itaonekana kwamba funds zote zilipelekwa huko Electrics International, ila ukweli utabaki pale pale kwamba gharama halisi za huo ujenzi haifiki hiyo bilioni, sasa either BOT imelanguliwa bila kujua au mbaya zaidi kuna watu wamekula sahani moja na hao walanguzi period.

    Mimi nina uzoefu wa kusimamia majengo, nimesimamia jengo letu na gharama hazikukaribia hata nusu ya hiyo bilioni na siwezi hata kuwaza mara mbili ku trade hiyo nyumba ya gavana kwa nyumba yetu. Hapo ni hiyo street tu ndo ya maana ila hilo jengo halina hata curb appeal.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  3. Sasa naona tutakuwa tumeelewa tatizo/ukweli uko wapi.Hapa kwa ujumla gavana kama gavana hausiki.Mchakato uko wazi na gharama inaonekana inalingana na quality ya nyumba.Hapa nataka kuamini kuwa lile ni "Zengwe" kwa gavana. Upotoshwaji wa mambo bongo unazidi na unakatisha tamaa kwa watu wenye nia nzuri na taifa lao. Naomba kuwakilisha!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza, U still afraiding!? May U better expose Ur doubt! Kwa mtazamo wangu naona kutokana na vitu vilivyokuwa listed hapo ni sawa, ignore inflated prices ya kibongo bongo!

    ReplyDelete
  5. JOHN MASHAKA
    DR. HILDREBRAND SHAYO
    JANUARY MAKAMBA
    MDAU JOHN(uk)

    HILI TAIFA NI LENU, TUNAWAOMBA MUUNGANE ILI MLIOKOE TAIFA LETU. MWAKA 2015 SIYO MBALI HATUTAKI MAFISADI TENA. TUNATAKA TAIFA LETU LA VIJANA WETU. NJOONI MSIOGOPE NI SISI WAPIGA KURA NA WANCHI NDIO WALINZI WENU NA MKUU NI MUNGU. NYIE NI WACHUMI, WASOMI WALIOBOBEA AMBAO HATA SASA HIVI WANAOGOPWA HAPA NCHINI, MKIKOOA KILA MTU ANASHTUKA. DAKITARI SHAYO ANAHESHIMIKA SANA, JANUARY NAY NDO USIOMBE. MASHAKA NDIYE KIBOKO YA MAFISADI, NJOONI, TUNAWAAMINIA, UBUNGE ISIWE WAZO TU, MTAPATA KURA %100

    ReplyDelete
  6. ndugu zangu watz,hii nyumba kulingana na vitu vilivyomo inaweza kugharimu hio hela,tunachoweza kujadili ni kwamba HAYO MATUMIZI YA TSHS 1.4BILLION ya mlipa kodi yanaingia akilini???unaweza kujenga hata nyumba ya $50million tanzania,ila swali la msingi ni sahihi kutumia kodi ya watu ambao wanataabika na shida ya maji kwa jinsi hii??

    ReplyDelete
  7. Wivu mtamu yeye wala hausiki na kupasisha tenda

    ReplyDelete
  8. Mhh! sioni hata nyumba yenye thamani ya hizo milioni elfu moja, huo ni wizi mtupu.sana sana ukinambia imetumia milioni mia tatu kidogo nitaelewa, vinginevyo ni yaleyale tuu, Wandugu tuwe na uchungu na watanzania wenzetu wanateseka, hivi wakisikia kwamba gavana anaishi kwenye nyumba ya thamani ya milioni elfu moja wakati yeye hata hiyo laki moja kwake anasikia kwenye bomba kweli patakalika?

    ReplyDelete
  9. Wewe Ahmad changa la macho lipi? Hivi nyie mnaelewa maana ya professionalism kwenye masuala haya? Au mnakurupuka tu na kuleta ushabiki? Unaambiwa mpaka wakaguzi waliobobea wamekagua hakuna shida. Mlitaka nyumba ya gavana yenye vikolombwezo vyote hivyo iwe na bei sawa na vibanfa vyenu mnavyojenga huko mbezi au huko kibamba? Vipi nyie. Hebu mwacheni Gavana Ndulu afanye kazi. Beno endelea na kazi nzuri unaoifanya Sir. The matter should now be put to rest.

    ReplyDelete
  10. Gavana hahusiki na maamuzi ya kujenga nyumba hizo, kwani yalifanyika kabla hajajiunga na benki kuu.
    Jamani mwacheni profesa wa watu, anafanya kazi nzuri ya kujenga uchumi na kuondoa ufisadi pale benki kuu. Haya yote ya EPA, etc. yamegundulika baada ya yeye kuondoa usiri uliokuwa umejaa pale benki.

    ReplyDelete
  11. okay sasa nimeelewa kwamba gavana hausiki.tatizo langu ni kwambaaaa hiyo pesa ni nyingi saaanah,hayo maelezo marefu kama msafara wa siafu hayajapunguza uchungu moyoni mwangu,kwa nini hao BOT wasingeweka budget ndogo ya kukubalika waseme "eeh bwana eeh sisi fungu letu ni hili piga ua isijengwe nyumba ya kuzidi gharama hizi".nchi yetu ni masikini viongozi wetu kichwani kumejaa urojo moyoni wamegubikwa na uroho na ujanjaujanja.hii ni sawa na baba wa familia maskini mwenye nyumba yake yenye kuhitaji marekebisho karibu kila mahali lkn pesa zinapopatikana anatumia karibu zote kuboresha masterbedroom wkt vyumba vya watoto vinavuja paani na havina hata madirisha ya uhakika ilihali masterbedroom lake utadhani yuko ulaya lkn vyumba vya watoto ni kama jalala lisilofaa kuishi binadamu.this is still shit for me hakuna maelezo yatakayoturn it into kitumbua wadau,hee!nchi yetu masikini inatakiwa pesa zitumike kiubahilibahili ili kila mtu anufaike sio kina gavana waishi peponi sie kina karubandika tuishi kuzimu lkn ni ktk same nchi.kwani ingejenwa nyumba ya kawaida tu nzuri yenye hadhi gavana angekufa akiishi hapo?urojo urojo urojo and more urojoz.
    bibi nyau.

    ReplyDelete
  12. Bado ni ngumu kutushawishi kwa maelezo yaliyotolewa na Bank kuu, gharama bado ni juu sana kwa ujenzi wa nyumba hizo kwani zinaonekana ni za kawaida muundo wake ni wa kawaida sema kinachovutia ni hiyo rangi lakini materials na labor kwa kiwango cha wiki hizo 32 hazilingani na aina ya nyumba hiyo. Kwa jinsi mahesabu yalivyorekebishwa hata akienda huyo mkaguzi mkuu atakuta mahesabu yameenda sawa lakini ila inaonekana hapo kuna percentage nyingi zimetembea kwa waliotoa hizo tenda tunawajua watanzania hakuna mtu atatoa tenda bure lazima ale percent fulani hapo! Viwanja vilikuwepo tayari vinamilikiwa na bank kuu hakuna ununuzi wa viwanja hapo, kwa uzoefu wa material ya bongo hapo ni chenga ya macho.
    Hiyo nyumba hata kwa market value haifikii hiyo bei iliyotajwa! Nikupe mfano kwa hii nyumba iliyopo Marekani market value yake ni $850000 laki saba na nusu itakuwa imejengwa kwa gharama za kama $350000 hiyo ni materials na labor.
    Ninaambatanisha kwenye email
    Hizi nyumba zote zipo kwenye same neighborhood nchini marekani. Nyumba hizi zinatofautiana kwa market value from cities to cities lakini thamani ya ujenzi ni zile zile.
    Kwahiyo inaonyesha gharama za nyumba hizo za gavana na hao maofisa wengine zimejenga nyumba zingine kwa waliotoa zabuni hizo.
    Hizi ni zama za ukweli na uwazi watanzania sasa hivi wengi tumeelimika japo bado ni wanyonge.

    ReplyDelete
  13. construction always is costly. our stake is still small but what we demand is higher compared to what we have. what went wrong was the requirement of the needs of the house. let us not just discuss the outlook of the house but we need to go deep and see what it contains. further more if the estimates were advertised in the gazette then it is time for us to be good readers that we can speak before things happens. being advertised in the gazette implies other authorities also were aware of what is planned to happen then why now the minister should say it is too much?????????

    ReplyDelete
  14. hapa hakuna kitu tanzania tumezoea kutengeneza hesabu za uongo hapa utaona mahesabu yamekwenda sawa kabisa hila mi najua mi mwenyewe nimewai kufanya kazi niliacha kwavile wengi wa wafanyakazi ni wezi maana utaona mtu amekuambia kuwa jana kulikua na mvua nikarudi nyumbani kwa tax kutoka posta mpaka mikocheni ni 50,000/= na risiti kaweka mpaka unashangaa alipita nyia ya wapi?
    kuhusu gavana yeye ndio bosi wa benki na amesomea mambo ya pesa nyumba gani bongo itajengwa kwa kiasi cha 1 bilioni alafu ni gorofa moja?jamani mi naomba watanzani tukipata madaraka tuwe na uchungu kidogo na nchi yetu sio kila kitu bora liende nchi hii tutafika kweli?

    ReplyDelete
  15. TATIZO NI PESA SIO MAELEZO JAMAA WATANZANIA TUKO WAPI?WATOTO BADO WANAKAA CHINI MASHULENI RAISI UNAFANYA NINI JAMAA KWANI HUONI VIJIJINI TANZANIA SIO DAR TU TUANGALIE HATA NNJE YA DAR...TUMECHOKA...

    ReplyDelete
  16. Kwa mahesabu na masheria mtatushinda. Lakini waalimu na wauguzi kule mikindani au namanyere fungu lao ni lipi kutoka kwenye fedha hiyo ya walipa kodi? CIG atakagua nini huko ikiwa waalimu wanabadilisha vyumba vya madarasa kuwa nyumba zao za kulala? CIG atakagua mahesabu gani kwa watoto yatima wanaoshindia maharage na chai chukuchuku ya wahisani? Hivi serikali iliuza nyumba zake kwa bei gani kule masaki na Oysterbay? sio chini ya Tsh 70mil?

    ReplyDelete
  17. Basi baada ya maelezo mazuri ya utawala wa bot, tunaomba kuhakikishiwa kuwa hatimaye wakazi wa sasa wa nyumba hizo hawatauziwa kwa Tsh milioni 60!!! huo ndio ufisadi mpya uliobuniwa katika mfumo wa zama hizi maarufu kleptocracy (mfumo wa ufisadi). wabongo tu wepesi wa kusahau - baada ya miaka mitano tutakuwa tumesahau tuliyohadithiwa!!!mimi taarifa hii nitaitunza.

    ReplyDelete
  18. serikali kwa vile inasema haina hela na bado nchi yetu ni maskini and tunategemea donors kuna benefits nyingine wanazopewa viongozi inabidi zikatwe mfano nyumba wanaweza wakaishi kwenye nyumba zao, hizo hela zikatukika kwenye mambo mengine,thats all i think wananchi ndo wanakipigia makelele

    ReplyDelete
  19. napata shida kuelewa ni vipi viongozi wetu wanaweza kulala usiku..kipato cha mtanzania wa kawaida (per capital income-2008) ni dola 2 kwa siku (Sh.2500), hospitali hazina dawa..mashule yanakosa madawati, wanafunzi hawana vitabu, vijiji havina mabomba ya maji kila kukicha mama zetu wanapoteza maisha kwa uzazi kwa sababu ya kukosa huduma bora, watoto wanakufa kwa kukosa dawa za kutibu malaria..tena hizo dawa hazifiki hata dola 1...hii list inaweza kuendelea nayo mpaka kesho....lakini juu ya yote hayo wanadhubutu kutupa maelezo ya namna viongozozi wa benki kuu wanavyoishi kwenye majumba ya sh. bilioni moja na..($970,000), kwa mahesabu rahisi, gavana agejengewa nyumba ya s. milioni 300, hiyo chenji ambayo ingebaki ingeweza kununua dozi 45000, za malaria kila moja kwa sh.20,000, yaani labda hizo pesa zingeokoa maisha ya watoto elfu arobaini na tano, au ingenunua madawati 9000, kwa kila dawati kugarimu Sh.100,000..naamini kwa gavana wa nchi masikini kama tanzania kuishi kwenye nyumba ya bei chee kama sh. milioni 300 bado angeishi kwa raha tu..tena sana...viongozi wa tanzania mna tia aibu..yaani mnahuzunisha..hiyo taarifa ya huo ujenzi nikiisoma nabaki kujiuliza ..hivi mliandika isomwe na watanzania wenzenu au isomwe na wamarekani..maana sijui kipi ni bora zaidi..wamarekani watawacheka kwa ulimbukeni..na watanzania tutasononeka kwa kutonesha madonda ya umasikini wetu..nawatakia ujenzi mwema wa taifa letu!!

    ReplyDelete
  20. fixed price.!!! naelewa sana hizo tenda za serikali zinavyokwenda

    ReplyDelete
  21. Perfect explainations..inaonekana public relation Department wanajua kazi yao..sasa hapo tunarudi kwenye uhalali wa kuwa na nyumba ya bei ghali namna hiyo..anyway nawaachia wabeba box kwa maoni zaidi najua mida hii wamepinda migongo..wakirudi na stress za maisha ugaibuni watakuja na comment zao ingawa nyingine za chuki zaidi na chache za manufaa

    ReplyDelete
  22. mhhh!!! sijui, ngoja waosha vinywa waamke tusikie...

    ReplyDelete
  23. crap crap crap....blah bla bla
    kiini macho
    endeleeni kuuiba mpaka mchoke

    ReplyDelete
  24. Serikali ilikuwa nyumba zake nyingi tuu Oysterbay ikaamua kuziuza kwa bei che sasa mnaamua kujenga mpya!

    ReplyDelete
  25. sasa mnataka gavana akakae manzese akabwe na vibaka?

    ReplyDelete
  26. tatizo gharama zetu zinaendana na umaskini wetu kama kweli nchi yetu maskini? manake hizi gharama kubwa kila siku zikitajwa serikali inasema kwamba spika anastahili kukaa kwenye nyumba hii au hile.je kama gavana anaona nyumba haina hadhi yake kwanini asitafute kazi kwingine akapata nyumba yenye hadhi yake na serikali yetu ikajenga nyumba za viongozi kwa uwezo wa nchi yetu au kwanini viongozi wasikae kwenye nyumba zao si wanalipwa mishahara? kama mtu hataki kazi wapewe wengine.


    na je serikali inavyosema viongozi kama wakina spika na gavana wana stahili nyumba zenye hadhi ya uspika je mama zetu hawastahili hospitali zenye hadhi kujifungulia watoto? au hadhi za mama zetu ni kuzaa kwenye sakfu hospitalini au kulala chini baada kujifungua pamoja na wagonjwa wengine.


    ianamana serikali yetu haina akili timamu kujua kwamba kuna kosa kama hospitali zenu zinakosa madawa,vitanda na huku bilioni inaenda kutumiaka kujenga nyumba ya kiongozi?


    ninacho washauri serikali waanze kufanya mambo kwa kutumia akili na malengo sio kukurupuka tu.serikali isio kuwa na malengo haitopiga hatua hata siku moja ni kama binadamu hasiyekuwa na malengo kwenye maisha yake.
    mdau mzawa.

    ReplyDelete
  27. Naomba kutoa Utabiri wa mwaka, Kuna mtu mmoja maarufu sana atakufa mwaka huu, Issa Michuzi atapanda cheo, Nyota inasema atakuwa Billionea na kujimilikia Jumba kama la Bwana Gavana , na wananchi itabidi wajisajiri kwenye globu yake na itakuwa ya kulipia.
    Pia naona manyunyu ya Uchaguzi , rabsha za hapa na pale, mapambano yataongozwa na Upinzani ila ushindi wa kishindo uko ndani ya waiba kura(siwataji jina)!
    Huko Zanzibar hali ya umeme na ukosefu wa maji bado vitaendelea kuwepo mpaka pale watakapoamua kuchoka na hali hiyo(hawajaamua kuchoka na Uongozi)!
    Mchungaji mmoja atakufa ghafla, na Kiongozi mmoja wa dini ya Kiisilamu atapoteza maisha.Ni mwaka uliojaa simanzi tele kwa wananchi.....
    Kuna kiongozi hupenda kuvaa miwani ya macho atapewa tuzo ya Udaktari(Doctor of Letters) ifikapo mwishoni mwa mwaka 2010
    Na kuna haja ya Issa Michuzi kupewa Hiyo Tuzo ya Dr of letters kwa kazi yake nzuri na kutumia Elimu yake kwa kuwaunganisha Wadau Ulimwengu mzima!Au Mnasemaje??
    Mdau
    Chuo cha Uganga
    Ugiriki ya kati

    ReplyDelete
  28. wadau, ninapendekeza mtembelee blogu/globu ya JIACHIE mkaone picha iliyotundikwa leo (12-30-09) ikionyesha darasa la shule ya msingi katika wilaya ya kigoma vijijini nchini Tanzania ndipo mnaweza kuelewa hoja za baadhi ya wadau wanaolaani ufisadi huu!! Au ankal unaweza kututundukia hapa tukaijadili. inatisha, inasikitisha, inakasirisha, ina..

    ReplyDelete
  29. Wapi Mashaka na swali lake la kizushi sasa. Eti huyo ndiye mtarajiwa sijui wa nini, labda apewe uwenyekiti wa kamati ya misiba huko Rorya hasa kuwa kiranja wakati wa kupitisha ngómbe kwenye makabuli kwa mbio za mita mia.


    Jamani ujenzi wa nyumba kwa taratibu za serikali ni tofauti na za binafsi ambapo katika kazi za binafsi hata wewe mwenyewe mara unaweza kuamua kufyatua matofali mara ukaamua kupaka rangi mwenyewe mara ukabadili madirisha kutoka katika mpango wa awali na mara ukapunguza milango na mara ukiona unazidiwa n.k.

    Gharama za ujenzi wa binafsi ni chini hata ya robo ya gharama za utaratibu wa tenda. Kama unabisha basi tafiti uone!

    ReplyDelete
  30. sasa wewe anonymous Wed Dec 30, 06:20:00 PM,unachotetea nini hapa upumbavu mtupu unataka kuniambia hakuweza kukaa kwenye nyumba ya kawaida mpaka iwe ya gharama kubwa hivyo sehemu muhimu kama shule hakuna kitu utaambiwa hawana pesa gavana kukaa kwenye nyumba ya bilioni moja pesa za walipa kodi inamsaidia nini mtanzania? serikali inatumia vibaya pesa za walipa kodi fullstop hakuna mambo ya kutetea ujinga hapa.

    ReplyDelete
  31. Bwana Gavana hii kitu sijanunua,hata mtoe taarifa kwa lugha zoote mnazozijua haiingii akilini. Kawauzieni wengine.

    ReplyDelete
  32. kwa mimi ninavyoelewa bilioni moja inaweza kujenga shule ya ghorofa hata tatu sio nyumba ya ghorofa moja... hapa kazi ipo

    ReplyDelete
  33. Watanzania wenzangu tusiwe na tabia ya kuropoka tu bila kujua hali halisi ya sekta ya ujenzi. Kwa bahati nzuri mimi ni mtaalamu wa ujenzi na nimefanya kazi katika sekta hii kwa miaka kadhaa hapa nchini na nchi za nje. Hio bei ni ya kawaida sana sana ukichukulia kwamba hio contract imegawanyika mara tatu, manake kuna sub contractors wa umeme, air conditioning na mambo ya maji. Kila contractor anakua na bei yake, ndio maana bei hii imekua juu. Ninafahamu kwamba Watanzania mambo ya ufisadi BOT bado hayajashughulikiwa na ndio maana watu bado wana uchungu. Kwa hio kitu chohote kikitokea benki kuu inakua ishu!

    ReplyDelete
  34. We anonymous wa Wed Dec 30, 06:20:00 PM professionalism gani hiyo unayoiona katika hilo jengo hadi ukadharau nyumba za huko mbezi? Hiyo nyumba kwa standards za Tanzania ya leo ni nyumba ya kawaida tu, naweza kusema yawezekana hata huyo gavana nyumba yake binafsi inavutia zaidi ya hiyo mara mbili.

    Hilo si jengo la maajabu, ni kwa vile majority Tanzania ni maskini tu watu sasa msiotembea mtaona ni mansion. Hizo kampuni zina professionalism gani wakati sote tunaelewa huo ujenzi hufanywa na mafundi wetu wale wale wa mtaani na hata huwa hawawalipi vizuri.

    Kwa vile estimates ziliandaliwa na hao wanaoitwa wataalam waliobobewa kwa hiyo lazima ziwe ndio gharama halisi? Kama wamebobea kucook numbers je? Mimi sina hakika kwamba kumefanyika ufisadi ila ninachoweza kusema, huo ujenzi uliofanyika hapo haufikii hiyo hela iliotajwa, inawezekana pengine BOT imeonewa na hiyo kampuni ya Electrics International.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  35. HUO NI WIZI WA KIINI MACHO TU HAKUKUWA NA HAJA YA KUJENGA NYUMBA HIZO ANGEWEZA KUKAA KWAKE MBEZI BEACH, MBONA MAGAVA WA NCHI KUBWA DUNIANI WANAKAA MAKWAO, AMERIKA OBAMA TU NDO ANAKAA NYUMBA YA SERIKALI, UK BROWN NA WAZIRI WA PESA TU NDO WANAKA NYUMBA ZA SERIKALI, WENGINE WOTE WANAKAA KWENYE NYUMBA ZAO. TANZANIA NCHI MASIKINI EVEN PESA YA KUJITOWA TOKA KWENYE RECESSION TUMEPEWA NA WAKUBWA NA BADO TUNAJENGA NYUMBA ZA SERIKALI NA ZA ZAMANI TUMEUZIANA SHILINI MBILI MBILI KAMA NJUGU HATA HAINGII AKILINI, KUNA KASORO NA TUNATAKA MAJIBU YA KUTOSHA SI HIYO BARUA NDEFU YA NINI HATUNA MUDA WA KUSOMA SWALA NI PESA NI NYINGI SANA KWA JENGI HILO.

    ReplyDelete
  36. Baada ya kuisoma hii ripoti nimepata fundisho moja. Kama watu wazima wenye akili zao timamu walikaa chini na kuamua kujenga "quality" house kwa gavana.. je inakuaje watu wabovu wakawa wanakaa chini na kufanya maamuzi ya kujenga hospitali mbovu zisizokuwa na viwango? ama mashule-mabanda yasiyowekewa madirisha? ama barabara uchwara zisizo na mifereji ya kuzuia maji yasiharibu barabara. Mbona tunafanya mambo ki double-standard jamani?

    Tunashindwaje kufanya "quality decisions" kuwaondolea watanzania umaskini uliotukuka kama at the same time twaweza tayarisha quality report kutetea quality house ya gavana? Mi naona kama tunalambishana michanga tu hapa. Hakuna lolote la maana.

    Samahani kaka Michuzi, ila inaboa sana kuona mambo yanaendeshwa kienyeji kwenye Tanzania yetu. Kwa jinsi mambo yanavyofanywa na waliokalia "utamu" utafikiri wanafikiria watu wote hatuna akili timamu.

    ReplyDelete
  37. Mr. Relation Manager, BOT.
    Mnacho jaribu kufanya kwenye taarifa yenu ni kuhalalisha ufujaji wa pesa za walipa kodi kwa kuzungumzia mchakato wa tenda ya ujenzi wa nyumba hizo, kwamba ulikiuwa halali. Labda ni kweli ulipitia taratibu zote husika, pamoja na hizo well-crafted bill of quantities at a tune of $1m/- in cost. That is "ONE MILLION USD". Lakini, usitwambie kwamba hizo gharama zimetoka hewani tu, kana kwamba wazabuni(contractors) husika ndiyo wa kulaumiwa kutoa makasio yao ya ujenzi. Kila mtu mwenye akili anajua kwamba kila mradi una makisio (estimates) ya awali kabla hata hajatafuta mjenzi. Ni wazi kwamba BOT ilikuwa na ilijua ni nini wanatarajia kutoka kwa wazabuni kulingana na details zenu kwenye BOQ, na kwa maana hiyo kutenga fungu pesa kwa ajili ya mradi huo. Well, masikitiko ya watanzania yanalenga kujua ni upi kikomo cha ufujaji za pesa za walipa kodi!! Taarifa yenu kwenye blog hii inaonyesha kana kwamba ni sawa tu hata kama nyumba zingetumia $5m/- each so long as zimepitia mchakato halali wa uzabuni!! That is insane. Ebu fikiria baadhi ya picha za shule kadhaa za msingi zenye nyasi na kuta za tope zilizowahi kutolewa kwenye blog hii; au hodi ya wazazi muhimbili ambayo ilimtoa machozi Naomi Campbell; n.k. I guarantee you, Governor wa US Fedral Bank hana nyumba ya $1M/- inayogharamiwa na walipa kodi wa nchi hiyo; the richest and most powerful country in the world. Sembuse Bongo ?? Hii kweli inahitaji an Harvard University graduate kuhoji Why? Iweje taasisi muhimu nchini kama BOT iwe kwenye matukio ya aina hii all the time? Au ndo yale yale aliyosema Mwl. Nyerere kwamba "ukisha kula nyama ya mtu utaendelea kuila tu". Juzi juzi TANESCO wameondoka na TZs 16B/- (tax free) kwa ajili ya magari ya maboss, at a price of TZs 1.6B/-a piece (Approx. $123,000/- each). Labda huu ni uzalendo mpya wa kuimaliza nchi. Vingenevyo, hakuna mwendawazimu anayeweza ku-justfy matumizi ya aina hii. NI AIBU TUPU.

    ReplyDelete
  38. Bro Mithupu hebu tutafutie gharama za nyumba zinazouzwa kwenye web site ya www.my-beach.com kwani hapo kuna nyumba nzuri na zinaonekana bomba zaidi na ramani nzuri kuliko hiyo ya Gavana. Sisi hatuna ugomvi na Gavana wetu wala manaibu gavana ugomvi wetu mkubwa ni jinsi gani pesa za walipa kodi zinavyotumika kwa kuwanufaisha watu wachache. Na ugomvi wetu mkubwa ni hao walioidhinisha hizo hela kutoka na kukarabati nyumba ya kawaida kwa gharama kubwa namna hiyo. Hebu wadau tufanye comparison ya bei ya baadhi ya nyumba kwenye hiyo website ya www.my-beach.com kisha tuone gharama zake na bei zake zitakuwa katika market value sio construction value. Brotha Mathupu tunakupa kazi hiyo kisha tutumie picha ya baadhi ya nyumba na gharama zake.
    Asante sana.

    ReplyDelete
  39. Wewe mdudu hulali hivi unapatawapi muda wa kusoma comments zote hizi na kusipost hewani, hapo si utakuwa unampunja mama Mithupu muda wake wa quality time! kwani muda mwingi nipo kwenyewe matumizi ya computer kila nikifungua blogu yetu ninakuta comments mpya!!!!!! kweli wewe ni mwana blogu wa damu! Mimi ninaifungua blogu hii labda mara 20 to 30 kwa siku ndo maana nikituma comments usipozipost ninakasirika sana kwani ninatumia muda mwingi sana kusoma comments za watu kama wewe unavyotumia muda mwingi kusoma na kupost. Kazi nzuri braza yangu.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  40. BOT MSIWAFANYE WATANZANIA WAJINGA BWANA. ISSUE HAPA SI TENDA HALALI BALI GHARAMA ZA HUO UJENZI.

    MSILETE MAMBO YA ZAMANI YA KUTUMIA RISITI KUTETEA BEI.

    KWA MFANO HUWEZI KUKODI TAXI KUTOKA BOT KWENDA AIRPORT HALAFU UKALETA RISITI YA TAXI YA LAKI MOJA.

    HIVI NI VITU RAHISI KABISA VYA KUANGALIA KATIKA MATUMIZI YA HELA.

    PIGA UA HAPO KUNA CHA JUU.

    ReplyDelete
  41. Mkae nyie mnaosupport huo ujenzi ni hivi nyumba ya Gavana wa nchi yenye uchumi mkubwa duniani inacost $549,000, Gavana wa nchi yenye sarafu stong duniani inacost £420,000 haya Gavana wa Tanzania moja kati ya nchi 10 duniani za mwisho kwa umaskini inacost $1.2 Million na naibu wake pia $1.2 Million sasa mtatuambia mkija na hoja zenu za tufunge mikanda kisa nchi maskini hela za kujenga hizi nyumba mmezitoa wapi????

    Jamani tuwe na huruma na imani nina hakika hiyo nyumba Ndullu atakaa kwa wasiwasi kwasababu kila atakapopita watu watamchukia kama sio kuanza kumrushia mawe. Ni bora kama anataka A million dollar house angelijenga nyumba Malibu wanakokaa matajiri wenzie akaishi kwa amani but Dar sidhani sijui labda watanzania watamsamehe

    ReplyDelete
  42. Anon 30th December, 07:38 a.m, siyo CIG, ni CAG yaani Controller and Auditor General.

    ReplyDelete
  43. sijaelewa hiyo kamati ya BOT inachotakatukikubali nini hasa?kama hasara mmeshatutia,kesho mtatuambia mshahara wa Gavana ni mil50 kwamwezi,namtatulazimisha tukubali kwakuwaulishapangwa kabla hajaingia madarakani,Mbagala watu wamebomokewa nyumba zao/nawengine kupoteza maisha kwauzembe wa serikali lakini hakuna hatammoja aliyejengewa nyumba au kupewa posho yaaina yoyote ile.Pesa zetu zirudishwe kwenye A/C tafadhali kunamambo mengi muhimu yakufanya na Gavana arudi kwenye nyumba yake yazamani aliyokuwa akiishi,Pia tunahitajikujua majina yawajumbe wahiyo bodi ambao waliipitisha hii bajeti.kama Tanzania ninchi yakidemokrasia natumai mtayafanyia kazi malalamiko yetu.

    ReplyDelete
  44. Michuzi jamani, nilimfagilia Ahmed waa waa kwa comments zake zote mbili, mbona umebana? New Year yote hii! Mara moja moja uwe unaachia.

    ReplyDelete
  45. Michuzi, kama unaweza fikisha ujumbe huu kwa Mr. Gavana, ni hivi: yeye mwenyewe personally anaamini hizi ni valid cost for za ujenzi? Kama sivyo; alichukua atua gani on his power to question this issue, and were was it stuck - this will at least isolate himself and his activities from Mafisadi; otherwise, it is very hard to convince anybody that he is working in good faith. Remember, if you look like a duck,walk like a duck, squack like a duck - for sure, you just another duck!

    ReplyDelete
  46. JAMANI MIMI SINA USEMI TIZAMENI NYUMBA ZA ULAYA ZENNYE THAMANI YA HIYO NYUMBA YA GAVANA HALAFU AMUA MWENYEWE. HIYO NYUMBA YA GAVANA INAONEKANA KAMA NYUMBA YA WAFANYA KAZI (SERVANTS QUATERS). KWELI TANZANIA TUNIBIWA KIMACHO MACHO. TANZANIA TUNASEMA TUKO UHURU. LAKINI NDANI YA MIOYO YA WATU BADO NI WATUMWA. NA HUWO UHURU NI WA MATAJIRI TUU. JAMANI ROHO INAUMA. VIONGOZI KUWENI IMANI. ASANTENI.

    ReplyDelete
  47. Hakika Bro. Mathupu blog hii ni kioo cha jamii na inavyanya kazi ipasavyo kwani nimeona reactions tayari nilikuwa ninasoma habari hii kwenye ippmedia leo tushirikiane wote wadau kusoma habari hiyo kuhusu uchunguzi wa ujenzi wa hizo nyumba na ukweli utabainika sasa! I love democracy viongozi wajue watanzania sasa hivi tupo macho hatuwezi kudanganywa kwa lolote kwani tumeenda shule sasa hivi.

    Nyumba za vigogo BoT zaanza
    kukaguliwa
    Na Mwandishi wetu
    1st January 2010B-pepeChapaMaoni
    Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu
    Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema imeanza kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba mbili za viongozi wa benki hiyo, zinazodaiwa kujengwa kwa gharama kubwa.

    Taarifa ya BoT iliyotolewa na Idara ya Uhusiano ya Umma na Itifaki kwa vyombo vya habari Dar es Salaam juzi jioni ilieleza kuwa zoezi la ukaguzi wa hesabu za BoT limeanza tangu mwaka 2007.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sheria ya BoT ya mwaka 2006 inampa mamlaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kukagua hesabu ya Benki Kuu ambaye hata hivyo ameiteua kampuni ya Ernst & Young kama wakaguzi wa kumsaidia kutekeleza jukumu hilo.

    Taarifa hiyo ilieleza kuwa ujenzi wa nyumba za viongozi hao ulizingatia sheria na kanuni za manunuzi ya umma kama ilivyopaswa.

    Taarifa hiyo ilieleza pia kuwa nyumba zote mbili za viongozi hao ni za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba.

    Nyumba hizo pia zina majengo ya nje ambayo ni nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

    Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya BoT, huduma zilizogharimiwa katika ujenzi wa nyumba hizo ni jenereta, mashine ya kupoza hewa, matenki ya kuhifadhi maji mahali pa kuegesha magari na bustani.

    BoT katika taarifa yake hiyo, imeeleza kuwa ujenzi wa nyumba hizo ulipangwa na kuamuliwa kabla ya uteuzi wa Gavana wa sasa wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, ambaye aliteuliwa Septemba 2007.

    Taarifa hiyo inafafanua gharama za ujenzi wa nyumba namba 12 Barabara ya Tumbawe ambayo ni ya Gavana Ndulu kuwa ni Sh. 1,274,295,025.26 wakati gharama za ujenzi wa nyumba namba 57 Mtwara Crescent ambayo ni ya Naibu Gavana Lila Mkila kuwa ni Sh. 1,272,348,512.

    Tayari Profesa Ndulu amehamia katika makazi yake mapya Desemba 17, 2009 na Naibu Gavana Mkila alihamia nyumba yake hiyo Desemba 4, mwaka huu.


    CHANZO: NIPASHE

    ReplyDelete
  48. 1.tatizo kwa Watanzania ni kuwa hatujui gharama halisi za ujenzi wa nyumba hata za kawaida tunazoishi.Utakuta mtu anajenga kwa sababu ya hela zetu hizi za kudunduliza tunakuwa, mwishoni hatujui tumetumia gharama shilingi ngapi. Ukweli kwa Gharama za jengo kama hilo na kama vigezo vimezingatiwa na pia kama hatukuwekewa vifaa vya CHINa kwa utaalamu halisi hilo jengo litakuwa limejengwa kwa gharama iliyotajwa.
    2.Sisi watanzania tumekuwa tunajenga nyumba zetu hatutumii wakandarasi kwani gharama zao ni kubwa kwani wao wanatoa huduma kibiashara zaidi, sasa kama hilo jengo amepewa mkandarasi, je yeye atoe sadaka asipate faida? sisi tunafanya hesabu kuwa mfuko mmoja wa cement uswahilini ni sh 12,000, lakini tunasahau huyu mkandarasi anafanya biashara. Hebu fikiria cocacola mmoja uswazi ni shilingi 500/= lakini ukienda yale maeneo ambayo hata kwa karibu tunaogopa kuyaangalia, hata pale tu mlimani city unauziwa si chini ya shilingi 1000/=. Hii inatokana na eneo la biashara na ubora wa eneo. Hivyo hivyo na ujenzi, kulingana na ubora unaotakiwa ni lazima atafutwe mkandarasi bora na anayeweza kukidhidhi yale mahitaji. Hapo ndipo unapokuta itabidi tuchague mkandarasi wa daraja la kwanza au la pili, ambaye hata TRA inamwangalia kwa jicho lingine katika kodi ukilinganisha na yule wa daraja la 7 au 6 au 5. wakandarasi wengine ukiwapa hela wanakwenda kutatua matatizo yao kifamilia.
    Nafikiri tunahitaji zaidi kuangalia haya mambo kitaalamu zaidi kuliko kulalamika.
    La msingi hapa tujiulize ni kwa kiasi gani tulikuwa na huitaji wa hizo nyumba kwa wakati huu? Je hatukwa na mbadala?

    ReplyDelete
  49. sasa jamani mbona ni kama hamjui taratibu za serikali yetu inavyofanya kazi!!!????
    hata wizarani pesa inayotolewa kwenda kuendesha shughuli za kila siku za taasisi za serikali zilizo chini ya wizara husika huwa inabidi libaki fungu maalumu kwa ajili ya wakubwa wa wizara kuanzia huko unakochukua hizo cheque hadi kwa makatibu mbali na kuwa hiyo pesa ilishapangiwa bajeti ambayo wewe kama mkuu wa taasisi lazima uoneshe ni namna gani ilitumika bila kuamsha hisia za ufujaji(yani mahesabu ya-balance)
    Sasa kama utaratibu huo ndo ulotumika hapo ni wazi kuwa hata hao walochukua tenda waliambiwa warudishe hata 400M ili wapate zabuni nao wakarekebisha masuala mengine ya kwenye makaratasi bila shida.
    Na haya mambo hutokea hivyo hapa kwetu(tz).
    Haya yote yatafikia kikomo iwapo wananchi watatumia vema haki yao ya kupiga kura kuweka viongozi wasio MAJUHA uwasioweza hata kusimamia matumizi ya kodi za wananchi wake.
    Ni nchi ngapi zenye sehemu tu ya resource tulizonazo ila ziko mbali sana,ila sisi tuna ardhi ya kutosha,madini,vivutio vya utalii,nguvu kazi ya kutosha,vyanzo vya maji na vingnevyo vingi ila hakuna mabadiliko miongo hadi miongo.
    Hata tungeamua tu kuimarisha suala zima la utalii au kilimo tu kwa kuwekeza katika kuboresha miundombinu kazi katika viwango vya juu matunda yangeonekana just within five to ten years lakini tumekuwa ni kama vipofu tusiojua tunaenda wapi na tunatoka wapi na tumebakia kuburuzwa na washenzi wachache ambao wanasimamia maslahi binafsi.
    Inauma sana.Napenda kuwasilisha hoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...