February 2009
mashabiki wa taifa stars wakiwa wamenywea baada ya zambia kusawzisha bao dakika ya 93 katia ya tano za ziada zilizoongezwa wakati Taifa Stars ikiwa inaongoza kwa bao la dakika 88 la tutazzz.
baada ya ivory coast kutoka suluhu ya 0-0 na senegal ndiyo kusema taifa stars wanapanda ndege ya kwanza kurejea bongo baada ya kukosa kuingia nusu fainali kiduuuchu.
nawashangaa wadau wengine wanaoniuliza matokeo ya ligi kuu ukerewe wakata mie macho na masikio vyote vilikuwa ivory coast. isitoshe niko kwenye mnuso wa harusi na blackberry yangu betri imeisha na hii ni post ya mwisho kwa sasa hadi baaaadayeeeeeeeeeeeeeeeeee.
uwanja wa bouke ambapo taifa stars watacheza na zambia takriba dakika 25 zijazo. cheki linki ya
jisajili mapema, kisha angalia ndiga laivu. usijesema hukuambiwa. mie leo naenda kwenye mnuso wa olive na epifania hapo chini. naomba ofu wadau
maharusi wakitoka kanisani jioni hii kuelekea photo point kula snepu kisha diamond jubilee
oliver kubaga na mai waifu wake epifania wakimeremeta
maharusi na wazazi wao. pili shoto ni mama bi harusi wakati winga ya shoto ni mzee raphael kubaga na winga ya kulia anapiga mama kubaga pamba kali sannaaaaaa oliver kubaga na mai waifu wake mara tu baada ya kumeremeta

fujo za bwana harusi unaweza kuzipata
http://www.ratiomediaproductions.com/
maofisa wa kamisheni ya ushindani wa haki (fair competition commission) wakis=choma moto bidhaa feki zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwenye dampo la pugu kinyamwezi nje ya jiji la dar. msemaji wa kamisheni hiyo amesema bidhaa hizo zilizoteketezwa zinafanya hesabu ya bidjhaa feki zilizochomwa moto kati ya mei 2007 na sasa kufikia thamani ya shilingi 1.625 bilioni. amesema karibu bidhaa zote, ikiwa ni pamoja na balbu, spe za magazi, vifaa vya umeme, feni, waya na kadhalika, zinatoka china

Mdau!
Hapa ndio hoteli
tulipo fikia na taifa stars hapa yamasoukro. Ni mwendo wa saa 1 mpaka Bouake. Mechi ya taifa stars na zambia lweo inachezwa kuanzia saa kumi za huku ivory coast ambazo ni saa moja kamili jioni huko bongo. vijana wako katika hali nzuri na ari kubwa na hakuna zengwe lolote kambini. wazambia wameshaanza kujinyea
unaweza kudekshia gemu hilo kupitia
ila inabidi ujiandikishe kwanza

Ndugu zangu,
Baadhi yenu mtakuwa nimekutaarifuni kuhusu kitabu hiki kipya. Nasikitika kukuelezeni kuwa kitabu kimeanza kupigwa vita ya chinichini.

Kwa wale ambao watakuwa hawajakisoma hawatapata tabu kujua sababu. University Bookshop na Dar es Salaam Bookshop wamepokea kitabu lakini sasa inaingia juma la pili hawataki kukiweka 'on dispaly' wala kukiuza.

Watu wakienda kukiuliza wanawaambia hawana taarifa ya kitabu hicho.Nakuombeni ndugu zangu hebu nanyi fikeni katika maduka hayo mpate uhakika wa haya nisemayo Hata hivyo kitabu kinapatikana:


Slip Way

Sea Cliff

Ibn Hazim Mkabala wa Msikiti wa Manyema

Khartan Bookshop Narung'ombe na Swahili karibu na Kariakoo Bureau du Change

Furaha Bookshop Msimbazi na Uhuru

Amnet Bookshop Msimbazi

na Livingstone Bookshop Mkabala na Msikiti wa Kipata


Mjini Tanga Duka la Maalim Masud Br. 18 kwa Pangani Road

Cathedral Bookshop wao wamekirudisha kwa Publisher.


Nini kinawatisha?

Nini kinakera katika kitabu?
Hiki ni kitabu kipya kinachoelezea mchango wa wazalendo waliopigania uhuru.
Kitabu kinaeleza yale yaliyotendeka mwaka 1958 wakati TANU ilipoingia katika uchaguzi wake wa kwanza uliojulikana kama Uchaguzi wa Kura Tatu.
Waingereza waliweka masharti ya kibaguzi yaliyopelekea TANU itishie kususa kuingia katika uchaguzi.

Matokeo yake TANU ilikuwa karibu ijigawe katika mapande mawili hasimu - ya wale wanaounga mkono kushiriki uchaguzi wakiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere Rais wa TANU na wale wanaopinga wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Kitabu kimewafufua wazalendo wengi ambao leo wamesahaulika.

Mohamed Said
Mtunzi
no image
kama ulidhania mahakama ya mbuzi ni jina la uzushi fikiria tena !! hili ni jina la kijiji huko wales LLANFAIRPWLLGWYNGYLLGOGERYCHWYRNDROBWLLLLANTYSILIOGOGOGOCH, halafu kuna kituo cha gari moshi.
mdau Gas
kaka Michuzi,
Hivi karibuni nilikuwa mjini Antwerp, nikakutana na vijana wa kitanzania waliokuwa wakiwania kupata nondoz za pili huko Ubeligiji, nikawauliza kama kuna wabongo wengi kule, wakaniambia wapo na wakamtaja Manara, nikagundua hawakuwa wanafahamu wasifu wake kamili.

nikawafahamisha mimi nilikuwa mshabiki wake mkubwa wakati anacheza soka bongo i.e. Pan African SC. Wakafanya mawasiliano tukaenda kumtembelea nyumbani kwake.

Tulikuta ''hapatoshi'' wabongo warundi wakenya wakiwa wanapiga stori.

Jamaa yuko fiti kama unavyomuona kushoto (mie nipo shoto kwake), na anafanya kazi kama kawaida ila wengi hawajui kwamba huko bongo ni bonge la staa wa enzi hizo.

Nimeona nikutumie hii picha ili wadau wamwone mtu wao, ameishi ubeligiji zaidi ya miaka 25, na alikuwa hajawahi kufika Bongo mpaka mwaka jana kwa miaka zaidi ya miaka 23
Mdau Geoff

KILA LA HERI TAIFA STARS LEO DHIDI YA ZAMBIA HUKO IVORY COAST

MAMBO YAKIENDA SAWA UNAWEZA KULIONA GEMU HILI KUPITIA
http://www.tvchannelsfree.com/watch/6241/RTS1-senegal.html
kwa maelezo zaidi ya michuano hii
no image

Dates: May 21-24, 2009. [Memorial week-end]
Place: Howard Johnson Hotel, Birmingham, Alabama.
275 OXMOOR ROAD, BRIMINGHAM, AL 35209.

SPEAKERS: Christopher
& Diana Mwakasege
-Tanzania.

Will provide free accommodations in the Howard Johnson hotel for the people who are coming out of Alabama. You need to register as soon as possible since we have very few rooms left.

There will be special session for the prayer for the needy and sick people.

Let’s come together to receiving the prophetic message for the Season!

It is the life changing Conference and your life will never be the same again.

Bring your family, friends and neighbors..!!

Register at :kula.mana@yahoo.com

For more details about ministers you can visit:
www.mwakasege.org

Pole na mihangaiko ya kila siku ya kutu Update!
Natumaini u mzima kabisa!Mimi ni mdau mkubwa sana wa Blog yako kutoka A-taun!Nimependa kuwapa hii na nyie wa mijini mjionee wenyewe!Kwa Picha kidogo najitahidi! Bongo tuko juu!
Mdau Noel Otaro



A-taun
no image
Dear all,
We invite you to participate in the tenth anniversary of Karibu Travel and Tourism Fair to be held in Arusha - Tanzania from 5th to 7th JUNE, 2009 at the Magereza Grounds next to Arusha Airport.
Book and pay early for your booth as best locations are offered on a "first come, first served" basis.
BOOKING
Bookings are now open, Prices are reasonable, we have stands from $270 and upwards.
Booking is made easy. You can book a stand online by clicking http://www.karibufair.com/flash/bkstand.swf.
Simple instructions will guide you through the booking procedure.
You can register yourself as a Delegate (International Visitor) on http://www.karibufair.com/visit/deleg.php
so as to enjoy special services at the fair.
For further information please visit our website
Looking forward to seeing you in Arusha in JUNE.
Thanks and Best Regards,
Bonny
MGENI RASMI DK. MWINYIHAJI MAKAME MWADINI AAKISALIMIANA NA WACHEZAJI WA TIMU YA MUNDU WAKATI WA UFUNGUZI WA LIGI KUU YA ZANZIBAR KABLA YA KUPAMBANA NA MIEMBENI KATIKA UWANJA WA MAO TSE TUNG JANA AMBAPO MIEMBENI WALISHINDA 2-1. PICHA ZOTE NA MDAU MARTIN KABEMBA
MSHAMBULIAJI WA MIEMBENI YUSUF KUNASA KULIA AKICHUANA NA TAN ALEX WA MUNDU, LIGI KUU YA ZANZIBAR KWENYE UWANJA WA MAO TSE TUNG JANA
KIKOSI CHA MABINGWA WATETEZI LIGI YA ZANZIBAR MIEMBENI
KIKOSI CHA TIMU YA MUNDU




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Rais wa Ireland, Mary McAleese kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Dublin kabla ya mazungumzo yao
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe, Tunu (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pmoja na baadhi ya watanzania wanaoishi nchini Ireland katika hafla aliyoandaliwa Waziri Mkuu, Na Waziri wa Nchi wa Ireland, Peter Power, jijini Dublin
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati) na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani (kushoto) wkaiwa na baadhi ya watanzania wanaoishi nchini Ireland katika hafla aliyoandaliwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi wa Ireland, Peter Power jijini Dublin. Picha na mdau Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri mkuu



no image
Shkamoo kaka Michuzi na wanablogu wako kutoka pande zote za dunia.
Mi hua nimezoe kupita 2 kwa mbali ila leo nimeamua kugonga hodi na natumaini ntakaribishwa. Wabongo wana tabia yakuitana wakabila mtu anapojivunia anapotokea...mi sioni kama ni sawa that's why nikaamua kuandika kuhusu hiii mada!

Usiporinga utaishia KURINGIWA!
Siku zote mtu akisifia asili yake haswa kabila sometimes anaitwa MKABILA au MBINAFSI.Jiulize kama mtu hajaupathamani ukabila wake na kujivunia atafikia wapi kujivunia utaifa wake??Kama we huwezi kusema mimi ni MMASSAI,MJALUO au hata MMAKONDE kwa majivuno utafika sehemuuseme wewe ni MTANZANIA kwa majivuno???
Nikiwa bongomtu akiniuliza ''we mtu wa wapi?'' ntamjibu ''uchaggani'' bilakujali sifa mbaya tunazobambikiwa wachagga kwasababu napenda asili yangu.Nikiwa nje ya nchi ntajitambulisha kamaMtanzania even though tunaweza kujulikana kwa sifa ambazosio nzuri sana.Ukikaa na kufikiria sana tena kwa makini utagundua kwamba kila kitu kina faults,ziwe za kweli au la,watu wanazitilia maanani.
Utasikia....WAZUNGU ni wabaya(roho),wachoyo,wabinafsi...WAAFRIKA au watu weusi ni wezi,wakorofi,wajinga n.k.Sasa wewe utakataa sio mwafrikka kwasababu wanaitwa wezi???Labda unaweza ila hutakiwi kufanya hivyo,unatakiwa ujivune na una nafasi yakuonyesha kwamba wasemavyo SIVYO.
Mtanzania akiwa nje anajiskia raha sana kuongelea anapotokea(asili yake)...Tanzania this..Tanzania that!!Unaowaelezea wanakuita mtaifa au mbinafsi???I don't think so!Actually watakuona kama mzalendo anaependa, anaejali na kujivunia asili yake.Mtu wa maana ni yule anaeitambua thamani yake,anapotokea na kile alichonacho.
So the next time someone is proud of being from a certain tribe and ain't afraid of saying so,don't go around hating nakumwita mkabila.Kwanza kama hamjui,the fact kwamba Tanzania ina makabila mengi yenye mila na desturi ,lugha na sifa tofauti inafanya nchi yetu iwe na mvuto zaidi.Kama wote tungekua WAMASSAI nani angemu-admire mwenzake?.Nani angemtania mwenzake??Think about it.
Mimi ni MCHAGGA and I'm more than proud. Hata mkisema wachagga wezi na wanawake wanaua waume zao I don't care. I'm CHAGGA for life.
''YOU CAN ONLY ACHIEVE WHAT YOU GIVE YOURSELF CREDIT FOR''
Mwisho wa yote nakushukuru kaka Michuzi kwakupost mada yangu na wote walitumia muda wao wa thamani kusoma nilichokiandika.Kama kuna nilimuudha kwa namna yoyote ile, iwe kwakuchanganya lugha au kutetea ukabila naomba anisamehe sana.
By Lillian
maandalizi ya kili marathon 2009 ambapo wakimbiaji 4,000 toka kila pembe ya dunia wapo

Mashindano ya kimataifa ya marathoni yajulikanayo kama ‘Kilimanjaro International Marathon’ yanatarajiwa kufanyika Jumapili hii tarehe Mosi Machi 2009 mjini Moshi, na kwa mwaka wa pili mfululizo mtandao unaoongoza nchini Tanzania – Vodacom inadhamini mashindano yajulikanayo kama ‘Vodacom 5KM Fun Run’.


Kulingana na matayarisho yaliyokwisha andaliwa, Vodacom Tanzania inaamini kuwa mahudhurio ya mwaka huu yatakuwa makubwa zaidi ya mwaka jana na kufanya mashindano hayo kuendelea kuwa na hadhi bora zaidi ya kimataifa, na inawahakikishia wakimbiaji wote kuwa watafurahia zaidi mashindano ya mwaka huu.
Njia mpya ya Vodacom 5KM Fun Run:
Tofauti na mwaka jana, mwaka huu mashindano ya Vodacom 5KM Fun Run yataanzia Moshi Golf Club na kumalizia MUCCOBS.
Mashindano yatapita barabara ya Sekou Toure, kupitia Arusha roundabout, na kisha itapita barabara ya Boma mpaka Clock Tower Vodashop, na wakati wa kurudi itapita barabara ya

Uru (Keys Hotel) mpaka MUCCOBS.


Ratiba:

Kuanza: Corporate relay Saa 1:15 asubuhi

Kuanza: Vodacom 5KM Fun Run Saa 1:30 asubuhi


JK akimpongeza Mzee Kawawa baada ya kuzindua kitabu chake Ikulu leo. Kitabu hicho, kinachoelezea maisha ya Mzee huyu ambaye wengi wanamwita Simba wa Vita, kimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Profesa John Magoti, Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere cha Kivukoni. Sherehe za usinduzi wa kitabu hicho unaendelea nyumbani kwa Mzee Kawawa huko Madale jioni hii
JK na rais mstaafu Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mzee Kawawa


Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh. Pius Msekwa kwenye uzinduzi huo
Mama Maria Nyerere akiongea na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho leo Ikulu






Ratiba ya LAdy JD na Machozi band ni kama ifuatavyo
Leo Ijumaa: atakuwa Bull Dogs, Masaki.
Kesho Jumamosi: Atakuwa SweetEAsy kama kawa
Jumapili: Thai Village, barabara ya Chole road, Masaki
o
MBUNIFU wa mavazi wa muda mrefu Fatma Amour (pichani) anatarajia kufanya onyesho la mavazi litakalojulikana kwa jina la Kakakuona 2009. Onyesho hilo linakuja mahsusi katika kusherehekea siku kuu ya Wanawake duniani.

Onyesho hilo limepangwa kufanyika tarehe 7 Machi, 2009 katika ukumbi wa Dar alive zamani Malaika karibu na Cine club jijini Dar es salaam.. Onyesho litakalofanyika by the sea side na lina kuja na ujumbe “Unavyovaa ndivyo ulivyo”

Balozi wa Redds 2007 Victoria Martin, Miss Tanania 2008 Nasreen Karim, na Jamila Nyangasa Miss Internaional 2008, ni miongoni mwa wanamitindo watakaopita jukwani pamoja na wanamitindo wengine mahiri kutoka kampuni ya Dollywood Tz.
Kusindikiza shoo atakuwepo mwanamuziki anayekuja juu kwa sasa Angeris, pamoja na Ngoma za asili pia zitakuwepo kutoka kwa kundi maarufu la Simba Arts. Tiketi za onyesho zipo taryari mtaa kwa shilingi 20000/- tu (Piga namba 07137363610 ama 0713 689689 utaletewa ulipo).


Usiku huo wa aina yake utaweka kumbukumbu ya aina yake katika medani ya mitindo nchini kwa kuwa mavazi yatakayoonyeshwa ni yale ya kiasili, yaliyonakshiwa kwa vito vya kiafrika yanayojali rangi za kitaifa na muonekanao wa kupendeza.

Onyesho hilo linakuja juu ya udhamini makini wa Jarida la Exel, Dollywood Tanzania Ltd, DTP, Vayle Spring, British Council, JD Entertainment, Aqua Drill, Easy Finance, Sofia Productions, CxC Tours na Raque.com.
Fatma Amour ni mmoja wa wabunifu waliobobea nchini. Ni mbunifu wa mataji ya Redds Ambassador na mshindi wa shindano la ubunifu wa mavazi la Rafda kwa miaka miwili mfululizo.
Kwa wapenzi wa mitindo hii si ya kukosa.
Kwa mawasiliano Zaidi Simu
hizi hapa:
0784 700866
/ 0713 689 689
no image
Baada ya waalimu kucharazwa bakora, sasa ratiba ni kama ifuatavyo:

March---------------------Madaktari
April---------------------Wahandisi
May-----------------------Wachumi
June----------------------Wanasheria
July----------------------Wahasibu
August----------Wanafunzi vyuo vikuu
September-----------------Masekretari
October-------------------IT/paparazzi
November------------------Wainjilisti
December----Maaskofu/Wachungaji/Paroko/Mashehe


Wanafunzi nje ya nchi wasiliana na balozi nchi unayosoma.

Mwendo ndio huo mpaka heshima irudi. Mnali karejeshwa wizarani kuratibu utaratibu huu.

N.B: Usipoona kundi lako wasiliana haraka na DC aliye karibu na kituo chako cha kazi!
no image
Bw. Michuzi,
tunashukuru sana kwa blogi yako inatupa faida zaidi kuliko hata magaezi ya ipp,swali langu ni hili kwa nini mtu anapotoa hewa chafu(kujamba) baadhi ya watu hufanya kama wanakohowa au kubanja na wengine kwa nini wanakua wanafanya kama kuvuta pumzi kwa nguvu?
Ahsante
JK amemteua Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Albert Samatta (pichani) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuanzia tarehe 13 Mwezi wa Kwanza 2009.

Kwa mujibu wa taarifa ilyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Hamis Dihenga imesema Uteuzi huo wa Jaji Mstaafu Samatta umekuja baada ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Balozi Dokta Ibrahim Kaduma kumaliza kipindi chake cha uongozi.

Wakati huo huo Rais Kikwete amemteua Balozi Nicholas Alfred Kuhanga kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kipindi kingine cha miaka minne kuanzia tarehe 1 mwezi wa 11 mwaka 2008.

Aidha Profesa Idris Kikula ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia tarehe 29 mwezi wa kwanza mwaka huu kufuatia Profesa Issa Omari kumaliza kipindi chake cha Uongozi
no image
APPLICATIONS INVITED FOR UNITED NATIONS JOURNALISM FELLOWSHIPS
The Dag Hammarskjöld Scholarship Fund for Journalists is now accepting applications from professional journalists from developing countries for its 2009 Fellowship Program.
The application deadline is Friday, March 20, 2009.
The Fellowships are available to radio, television, print and web journalists, age 25 to 35, from developing countries who are interested in coming to New York to report on international affairs during the 64th session of the United Nations General Assembly.
The Fellowships will begin in mid-September and extend to late November and will include the cost of travel and accommodations in New York, as well as a per diem allowance.
The Fellowship Program is open to journalists who are native to one of the developing countries in Africa, Asia, South America and the Caribbean, and are currently working full-time for a bona fide media organization in a developing nation.
Applicants must demonstrate an interest in and commitment to international affairs and to conveying a better understanding of the United Nations to their readers and audiences. They must also have approval from their media organizations to spend up to two months in New York to report from the United Nations.
The journalists who are awarded Fellowships are given the incomparable opportunity to observe international diplomatic deliberations at the United Nations, to make professional contacts that will serve them for many years to come, to interact with seasoned journalists from around the world, and to gain a broader perspective and understanding of matters of global concern.
Many past Fellows have risen to prominence in their professional and countries.
This is the 48th year the Dag Hammarskjöld Scholarship Fund has sponsored the Fellowship Program for Journalists. The program is administered on a volunteer basis by journalists at the United Nations, who raise money from foundations, corporations and diplomatic missions.
Questions about the program, eligibility and application process can be directed to
SOURCE
FOR MORE SCHOLARSHIPS,
VISIT
MAKULILO Jr,
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (muungano) Mohamed seif Khatib (pili shoto juu, na tatu shoto chini) mbali ya kuongoza msafara wa Taifa Stars huko Abidjan pia anafanya ziara nyingine kadhaa za kuangalia miradi ya maendeleo kama hapa akionyeshwa jinsi ya upandaji wa migomba katika ziara yake leo hii



Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Peter Correia(katikati) akimkabidhi Mganga mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Suleiman Mutani (kulia) moja ya vitanda vilivyotolewa na Vodacom Foundation vyenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kusherehekea siku yao,(kushoto)Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba.
Mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom Peter Correia akimkabidhi Bi Mariam Hamidu aliyelazwa katika hospitali ya Mwananyamala moja ya zawadi zilizotolewa kwa wagonjwa wakati wa kusherehekea siku ya vodacom foundation Day ambapo walikabidhi msada wa Vitanda kwa Hospitali za mkoa wa Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40.
Mfanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom akiwa amembeba mtoto mchanga katika hospitali ya Temeke mara baada ya kutoa msaada wa vitanda na mashuka yaliyotolewa na Vodacom foundation yenye thamani ya shilingi milioni 40.


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania jana imesherehekea siku maalumu ya mfuko huo wa kusaidia jamii ( Vodacom Foundation) katika kusherehekea siku hiyo, Mfuko huo wa Vodacom umezikabidhi hospitali za wilaya za mkoa wa Dar es Salaam msaada wa vitanda maalum kwa akina mama wajawazito vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40.

Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Dietof Mare kwa Waganga Wakuu wa hospitali hizo.

Baadhi wa waganga hao waliipongeza Vodacom kwa msaada huo kwani utasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika hospitali zao.

Hospitali zilizofaidika kwa msaada huo ni Amana (Ilala) ,Temeke na Mwananyamala (Kinondoni) .

Sanjari na utoaji wa msaada huo kwa mkoa wa Dar es Salaam, Vodacom ilitoa misaada ya aina hiyo katika hospitali za serikali katika mikoa ya Kigoma,Iringa,Kagera na Tanga kupitia kwa wawakilishi wake waliko mikoani.

Waganga hao walisema msaada huo ni uthibitisho wa ushirikiano imara baina ya Vodacom na sekta ya afya hapa nchini na kwamba ushirikiano huo umekuwa ukiimarika kadri muda unavyokwenda.

Walisema serikali mara nyingi imekuwa ikiiomba sekta binafsi kushiriki katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma bora za afya hapa nchini, hivyo basi ushiriki wa Vodacom ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi kwa maendeleo ya jamii.

"Tumefarijika sana kuwaona Vodacom wanashirikiana katika sekta hii muhimu ya maendeleo ya jamii," walisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietof Mare, alisema Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake itaendelea kuiunga mkono serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

waziri mkuu mh. mizengo pinda akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika chuo kikuu cha University College Dublin huko ireland ambako yuko ziarani
baadhi ya wadau wanaokula nondozzz za PhD katika chuo hicho wakimsikiliza waziri mkuu
wadau wanaokula nondozzz chuoni hapo wakipozi na mh. waziri mkuu


baadhi ya wadau wanaopiga nondozz za PhD chuo kikuu cha University College Dublin (UCD)

katibu mkuu wa umoja wa mataifa ki-moon ban akitoa lekcha jioni hii katika hoteli ya movenpick
sehemu wa wadau waliohudhuria lekcha hiyo
JK akiwa na mgeni wake kwa mazungumzo Ikulu

umati mkubwa ulijitokeza kumpokea katibu mkuu wa umoja wa mataifa dar mgeni akisalimiana na baadhi ya viongozi waliojitokeza uwanja wa ndege wa julius nyerere kumpokea
JK na mam Salma Kikwete wakiwapokea katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ki-moon Ban na mai waifu wake Ban Soon-taek Ikulu jioni hii mara baada ya kiongozi huyo wa umoja wa mataifa kutua dar kwa ziara rasmi ya siku mbili. Jioni hii yupo hoteli ya movenpick akimwaga lekcha ya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mazingira na uchumi wa dunia

Wadau msiwe na mashaka na kujiuliza wapi wapo INAFRIKA BAND?
Inafrika wametua ulaya kwa kishindo na kuanza kutingisha na kukamua vibaya vibaya!bendi hiyo ya mziki wa dansi inafanya tour ya ulaya kwa udhamini wa "Mama Afrika"bendi hiyo maarufu kutoka jijini Dar, imeshafanikiwa kutingisha katika majukwaa makubwa mbali mbali nchini Ujerumani,Uswiss,Austria na inaendelea kupeperusha bendera ya bongo kwa mlingoti wa mziki.
Inafrika band pia inawajulisha washabiki na wadau wote wa nyumbani Tanzania wasiwe na wasi wasi mara watakapo rudi bongo wanakuja na ALBUM MPYA ambayo ina mziki moto moto.
Inafrika jana walikuwa mjini Oldenburg,Ujerumani na walilakiwa na kiongozi wa bendi ya "The ngoma Africa" mwanamziki mashuhuri Ras Makunja aka bwana kichwa ngumu.