Sunday, May 31, 2009
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 7






wananchi wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali kuunga juhuhudi za kupiga vita matumizi ya tumbaku duniani katika sherehe zilizofanyika jana kitaifa eneo la Horiri – Rombo mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Kenya na Tanzania.
wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali kuunga juhuhudi za kupiga vita matumizi ya tumbaku duniani katika sherehe zilizofanyika jana kitaifa eneo la Horiri – Rombo mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Gunule ambayo iko Horiri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro Twaha Bakari akiwa amebeba bango lenye ujumbe wa kupiga vita matumizi ya tumbaku katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kuttotumia tumbaku duniani
Meli ya MV Fatih ikiwa imezama katika eneo la Bandari ya Malindi ndani yake ikiwa na abiria wanaokisiwa kuwa zaidi ya 100. Abiria 27 walikuwa wameokolewa na maiti watatu tu ndio waliopatikana. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam ilikuwa imebeba abiria pamoja na shehena ya mizigo mbalimbali. Picha na mdau Mwajuma Juma - Zanzibar.
ukumbi mpya a mlimani city conference center kwa nje. hapa ndipo miss universe tz 2009 imefanyikia
iluminata james miss universe tz 2009
tano bora
iluminata james akiwa na majaji baada ya mchuano. toka shoto ni rosie motene mtangazaji wa tv ya channel 53 ya sauzi, masudi kipanya na mbunge wa viti maalumu mh. al sharyamaa kwegyabir.
wadau wa kenya airways na mrembo iluminata
meza ya mabosi wa sumsung tanzania, wafadhili wakuu wa miss universe tz
gwaride la warembo
kumi bora
mwandaaji maria sarungi-tsehai akielekeza jambo kwa majaji
maria akieleza jambo majaji. kulia ni mzee mzima john kitime ambaye naye alikuwa jaji. cheki alivyotoka pina!
msanii wahuu toka kenya akitumbuiza
ambwene yesaya a.k.a ay alikuwepo kuwapa watu raha
kikundi cha ngoma cha albino kilitia fora katika shoo hiyo
sindimba toka mang'aka lilimwaga na wasanii albino
sebene lilimwagwa na diamon musica
Mnenguaji wa FM Academia Queen Suzy ambaye kwa sasa yuko Malaysia ziarani na Bendi ya The Kilimanjaro Connections amepata mchumba ambaye anatarajia kufunga naye ndoa baadaye mwaka huu.
mgeni rasmi mkurugenzi mkuu wa kenya breweries ltd Baker Magunda akitoa darasa wakati wa sherehe ya usiku wa masoko kwa wana afrika mashariki uliofanyika hoteli ya kempinski kilimanjaro jijini dar usiku wa kuamkia leo ambapo wafanyakazi katika vitengo vya masoko toka makampuni mbalimbali walikusanyika pamoja katika mnuso huo uliodhaminiwa na vodacom, tbl na mwananchi
bosi wa masoko wa vodacom ephraim mafuru akiongea wakati wa mnuso huo
meneja wa kilaji cha ndovu wa tbl george kavishe akimwaga sera
mashindano yaliyoshirikisha wadau mbalimbali yalikuwepo. hapo ni kabla ya kuanza kwa shindano la kusakata rhumba
bosi wa masoko wa vodacom tanzania ephraim mafuru akishuhudia mai waifu wake akikata keki aliyomwandalia ikiwa ni sapraizi kwani siku hii iliangukia siku ya mnuso wa wana masoko
wasanii wakali wa afrika mashariki kwa sasa amani toka kenya (shoto) akila pozi na marlaw kabla hawajatumbuiza
amani akitumbuiza
bebe cool toka uganda alikuwepo kutia radha mnuso huu

