In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for November 2009

profesa mwandosya atembelea MORUWASA

Waziri wa Maji na umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya ( kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mkemia wa Mabara ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya Manispaa ya Morogoro ( MORUWASA) Lide Mwakalukwa ( kulia) katika kituo cha maabara ya kuweka dawa kwenye mfumo wa maji kutoka Bwawa la Mindu linalohudumia zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa Manispaa hiyo wakati alipotembelea wikiendi ilopita.

Waziri wa Maji na umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya ( mwenye miwani ) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya Manispaa ya Morogoro ( MORUWASA) , John Mtaita ( wapili kutoka kushoto) jinsi kituo cha maabara cha Mamlaka hiyo kinavyofanya kazi kwenye mfumo wa maji kutoka Bwawa la Mindu linalihudumia zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa Manispaa hiyo wakati alipotembelea. Picha na John Nditi.



DK. KARUME AFUNGUA TAWI JIPYA LA NMB ZENJ

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. AMANI ABEID KARUME AKIONDOA KIPAZIA KUASHIRIA KUFUNGUWA TAWI LA BANKI YA NMB ZANZIBAR MTAA WA DARAJANI, KUSHOTO MTENDAJI MKUU WA NMB BENN CHRISTIAANSE.
RAIS WA ZANZIBAR DK. AMANI ABNEID KARUME AKIKATA UTEPE KUFUNGUWA RASMINI TAWI LA BANKI YA NMB ZANZIBAR

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. AMANI ABEID KARUME AKIMKABIDHI MPIRA MWANAFUNZI WA SKULI YA KAJIFICHENI YUNUS RAMADHANI KWA NIABA YA WANAFUNZI WA MKOA WA MJINI. KATIKA SHEREHE ZA KUZINDUWA TAWI LA BANKI YA NMB.


MTENDAJI MKUU WA NMB BEN CHRISTIAANSE AKITOWA HUTUBA KATIKA UZINDUZI WA BANKI YA NMB TAWI LA ZANZIBAR DARAJANI.




RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. AMANI ABEID KARUME AKIPOKEA HUNDI YA 12M/- KAMA MSAADA KWA JAMII YA ZANZIBAR TOKA BENKI YA NMB
SEHEMU YA UMATI ULIOHUDHURIA SHEREHE HIZO
WANANCHI WAKIFUNGUA AKAUNTI KWENYE TAWI JIPYA LA BENKI YA NMB ZENJI LEO
WANAFUNZI WA SKULI MBALIMBALI WAKIWA NA ZAWADI ZA MIPIRA ZILIZOTOLEWA NA BENKI YA NMB WAKATI WA UZINDUZI WA TAWI LAKE ZENJI









Mh. spika katika tamasha la nyimbo za injili mwanza

Mbunge wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni akinadi saa yenye picha ya Spika katika tamasha la injili na Kusaidia walemavu jana katika uwanja wa CCM Kirumba. ambapo Jumla ya Tsh 49, 9850 zilipatikana baada ya wananchi kujichangisha kwa lengo la kumnunulia Spika Saa hiyo na fedha kutumika kusaidia walemavu mkoani Mwanza. Spika alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha hilo.

Mhe. Chegeni akikusanya michango kwa ajili ya kununulia saa yenye picha ya Spika. Chini waimbaji wa injili wakimkabidhi Mh. Spika saa hiyo

Rose Mhando na kundi lake wakitumbuiza kwenye tamasha hilo
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akipokea tuzo kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania ikiwa ni kutambua mchango wa Spika katika kuliongoza Bunge la Tanzania kwa ujasiri mkubwa haki na uadilifu chini ya kauli mbiu “kasi na viwango”. Spika alipewa tuzo hiyo jana mjini mwanza mara baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la injili na kusaidia walemavu katika uwanja wa CCM kirumba – Mwanza. Toka kushoto ni John Shabani, afisa habari wa Christian Promoters ambaye ndio wadhamini wa tamasha hilo na Bi Stella Joel, Mwimbaji wa nyimbo za Injili.

Spika Akifurahia tuzo yake

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akikabidhi Fulana, kofia na mafuta maalumu kwa ajili ya walemavu wa Ngozi, Miamvuli, na vyakula katika hafla iliyofanyika wakati tamasha la injili na kusaidia walemavu katika uwanja wa CCM kirumba – Mwanza. Spika alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge








mskimamo wa Barrick Goldkuhusu Muswada nambari C-300


Barrick Gold Yatoa Msimamo kuhusu Muswada nambari C-
300 na Kueleza Ukweli


Shirika la Dhahabu la Barrick (NYSE:ABX) (TSX:ABX) leo limeelezea msimamo
wake kuhusu muswada wa wanachama binafsi (C-300) ambao kwa sasa uko mbele ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nchi za Nje na Maendeleo ya Kimataifa ya Kanada, kwa kusisitiza kwamba, Muswada hauna umuhimu na kwamba huleta athari mbaya kwa biashara za Kanada. Vile vile Barrick imeeleza ukweli kuhusu madai yasiyothibitishwa ambayo yamekuwa yakitolewa na watu kwenye Kamati hiyo.

Katika taarifa yao ya pamoja na Kampuni ya Goldcorp Inc. na Shirika la Kinross Gold, makampuni hayo yamedokeza kwamba Muswada nambari C-300 utaathiri vibaya sana sekta ya uchimbaji madini ya Kanada kwa vipengele vikuu vitano:


1. Kuihatarisha nafasi ya ushindani ya makampuni ya Kikanada;
2. Kusababisha kushuka kwa heshima ya makampuni ya Kikanada;
3. Kudhoofisha ushirikiano na ubia katika Wajibu wa Mashirika kwa Jamii (CSR);
4. Kuchagiza makampuni kuhamia sehemu nyingine; na
5. Kudharau taratibu za sasa za kisheria za Wajibu wa Mashirika kwa Jamii.
(ili kupata nakala ya mawasilisho, tafadhali ingia kwenye tovuti hii:
www.barrick.com


“Leo hii tunawapa wanakamati maelezo ya kina, ukweli na uhakika ili kujibu
shutuma mbalimbali kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi. Masuala ya uchunguzi makini na hata ukosoaji ni sehemu ya ufanyaji biashara, lakini yanapaswa kuwa ya haki na ukweli,” alisema Bwana Vincent Borg, Makamu Mtendaji wa Rais, Mawasiliano Ngazi ya Shirika.


“Kitu kimoja kimeonekana dhahiri wakati vikao vya mashauriano vikiendelea: baadhi ya watu hawakuletwa hata kuthibitisha shutuma zao kali juu ya sekta ya uchimbaji madini ya Kanada pamoja na Barrick Gold - leo hii nyingi kati ya hizo zimebainika bayana kuwa ni za uwongo. Hawakuipatia Kamati hii
taarifa za ukweli na uhakika wala ushahidi kwa ajili ya kusimamia madai yao wakati wakitoa chokochoko za hapa na pale za kupaka matope kampuni.”

“ Vikao vya kusikiliza kesi hiyo vimetoa nafasi kubwa ya kudhihirisha ni
namna gani Muswada nambari C-300 ulivyogeuka kuwa sumaku ya kuvutia madai ya uwongo na yasiyothibitishwa yatokayo kwa watu mbalimbali kutoka sehemu yoyote ile duniani na hakuna kinachofanyika zaidi ya kuiathiri sekta ya uchimbaji madini ya Kanada,” aliongeza Bw. Borg.

Katika kila nchi huru ambamo Barrick huendesha shughuli zake, kuna taasisi
za serikali, mifumo ya sheria, mamlaka zinazohusika na sera, taratibu za kisheria pamoja na mahakama. Barrick inaamini kwamba katika nchi hizi shutuma za namna hiyo hutolewa inavyostahiki zikiambatana na maelezo yote ya ukweli na yanayohusiana na madai hayo na si kamati ya bunge ya Kanada ambayo haikutoa uhakiki wala maelezo. Zaidi ya mataifa hayo huru, makampuni huwa yanawajibika katika ngazi ya kimataifa na kwa kufuata miongozo inayohusu uwajibikaji.


“Chombo husika kwa ajili ya urekebishi na utatuzi ni mahakama au mamlaka
huria zinazohusika ambapo masuala yanaweza kuchunguzwa ipasavyo kwa wakati muafaka - na si majukwaa ya kisiasa,” aliongeza Bw. Borg.
Dhamira ya Shirika la Dhahabu la Barrick ni kuwa kampuni bora zaidi ya
dhahabu ulimwenguni kwa kutafuta, kutwaa, kuendeleza na kuzalisha rizavu zenye kiwango bora kwa usalama, kwa faida na kwa kuwajibika kwa jamii.

MAWASILIANO NA WAWEKEZAJI:
Deni Nicoski
Makamu wa Rais,
Mahusiano na Wawekezaji
Simu: (416) 307-7410
Barua-pepe: dnicoski@barrick.com

MAWASILIANO NA VYOMBO VYA HABARI:
Vincent Borg
Makamu Mtendaji wa Rais,
Mawasiliano Ngazi ya Shirika
Simu: (416) 307-7477
Barua-pepe: vborg@barrick.com




miradi ya makaa ya mawe na chuma ngaka na liganga

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Chrisant Mzindakaya akianglia moja ya malighafi ya kuzalisha chuma katika Eneo la Liganga mkoani Iringa.. Kulia ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanziba ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo Dk Gharib Bilal na katikati ni Katibu Tarafa wa Ludewa.Bodi hiyo ilitembelea miradi mbalimbali ya Makaa ya mawe na Uzalishaji chuma.
Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Masoko Joyce Mapunjo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Gideon Nasari (wapili kushoto) na mjumbe wa Bodio ya NDD Prof. Idris Kikula (wapili kushoto) wakiangalia moja ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika macho ya Ngaka Wilayani Mbinga unaofanywa nakampuni ya Tancoal Enegy. Wajumbe wa Bodi ya NDC walitembelea mradi huo na ule wa kuchimba chuma Liganga mkoani Iringa.



kiplefti mjini sumbawanga


MKAAZI wa mjini Sumbawanga , mkoani Rukwa akiwaonyesha watoto wake kwa mshangao mkubwa , shimo kubwa kando ya barabara ya Kiwelu ni mojawapo ya barabara zilizofanyiwa ukarabati mkubwa na kuwekewa lami hivi karibuni , pamoja na kwamba shimo hilo ni uharibifu ulosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbali mbali mkoani hapa , lakini bado wakaazi wengi wa mjini i hapa wanadai barabara hizo zote zenye zaidi ya urefu wa kilomita zimejengwa chini sana ya kiwango. Picha na mdau Peti Siyame.


*Calling All Entrepreneurs*

There is no formula or method for entrepreneurship. At least that is what I know. All you need is to be at the right place and the right time, to realize that an opportunity is presenting itself to you.

Entrepreneurship knows no boundaries; it sets no limits for the size and/or nature of a venture. All you need is your self-confidence and the courage to say: This is not difficult, I can do it.

If you believe you have what it takes to be an entrepreneur, email me your CV (which is not really you qualification) so that we may start discussing your immediate future.

I am leaving Dar es Salaam, moving to Arusha. I have a business that I need to hand over – in 30 days – to someone who will qualify for it.

I can teach you the basics of the business – Hint: Think COMMUNICATIONS! – but the rest will be your own effort, drive and initiative.
Are you ready, to conquer the world?
If you are… drop me a line.

Who you are:
* Male or female
* Between 18 and 30 years of age
* Tanzanian citizen

Your qualifications:

* Academic: Form VI leaver (minimum)
* Fluency in Kiswahili and English languages
* Computer Skills
* Communication Skills (Can you write with fluency and no
grammatical errors? Can you speak in public, or to a small group
of people? Can you make a PowerPoint Presentation, from scratch?)


If you have the above qualifications, STOP WASTING TIME and get in touch with me, at
ASAP!
Remember, this is NOT a job application…
this is YOUR LIFE!


KUMBUKUMBU


THE LATE MERCY PATIENCE KAZI MAGANGA

DIED 03 DECEMBER 1996

Dear Mum, It’s been 13 years already and yet it feels like yesterday when you spilled into that eternal sleep. Things are not the same anymore…..It’s not easy to keep going. A lot has happened & changed…..Sister Nelly has become our mother a sister and a close friend at the same time.. your daughter Susan can’t stop wishing you were here to see her Awarded Bachelor Degree of Science in Technical Management (Magna Cum Laude) this December, you have 4 grandchildren who will just grow to hear about grandma… your wish for us to become stronger person has come to pass… you must be the proudest Mum !

We are trying so hard to be strong enough to carry on as you would expect us to. You have made Sister Nelly the strongest pillar ever…she carries your torch for us.

God looked around His garden on that fateful day, and He saw an empty place. He then looked down upon the earth and saw your peaceful sleep. He put his arms around you and He lifted you to rest. God’s garden must be beautiful, He always takes the best. He knew that you were having heart attack and wanted you to die peaceful on your sleep without going through any pain. He knew that you would never see the morning again. He saw the road was getting rough; the hills were hard to climb. So he closed your weary eyes and whispered, “Peace Be Thine”.

It broke our hearts to loose both parents, but you did not go alone, for part of us went with you the day God called you home.

Mum to the world you were just one; to us you were our world. We are at peace knowing that you are watching over us. May your soul remain blessed… we will always celebrate your life. We love you so much Mama.

Fondly remembered by your loving children Nelly, Gerald, Louisa, Alice, Susan and Andrew, son in-laws Pascal, Rikard & Peter, grand children Jadden, Nelly Jr, Andrew Jr, Simon, and friends.

Rest in Peace Mama.




dk. buriani azindua programu ya kukabiliana na tabianchi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Batilda Burian akizindua Program ya Miaka Mitano ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi inayoratibiwa na Vyuo vikuu vya Sokoine, Dar es Salaam na Ardhi kwa kushirikiana na Chuo cha Life Sciences cha Norway.kulia Prof Idris Mshoro, Prof Y Mgaya, Prof Geraid Monella na Balozi wa Royal Norwegian Bw Jon Lomoy Leo Huko Ubungo Plaza jijini Dar leo. Picha na Ali Meja


rufaa ya babu seya yaahirishwa hadi desemba 3, 2009

Babu Seya (mwenye bazee kulia) akiwa na wanawe kizimbani leo Mahakama ya Rufaa jijini Dar
Askari magereza akiwatia pingu Babu Seya na mwanae Papii Kocha Mtoto wa Mfalme tayari kurudishwa gerezani leo baada ya rufani yao kuahirishwa

Rufaa ya mwanamuziki maarufu, Nguza Viking (pichani kulia) maarufu kwa jina la Babu Seya na wanawe watatu, imehairishwa hadi Desemba 3 mwaka huu, ili upande wa Jamhuri uweze kupitia nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi.
Katika rufani hiyo pia wamo watoto wake ambao ni Papii Nguza, Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanapinga hukumu waliyohukumiwa kutumikia jela maisha iliyotolewa mwaka 2004 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Rufani hiyo iliahirishwa jana mbele ya jopo la majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Nathalia Kimaro pamoja na wenzake ambao ni jaji Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati.

Awali upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili wa kujitegemea Mabere Malando aliiomba Mahakama hiyo ya Rufaa kupokea maombi yake yakurekebisha maombi ya rufani iliyowasilishwa Mahakamani hapo na iweze kusomeka kesi namba 56/2005 ya makosa ya jinai badala ya kesi namba 56/2009.

Mbali na ombi hilo pia aliiomba Mahakama kuongeza sababu nne za kufungua rufani hiyo na hivyo kuwa na sababu 19, alidai kuwa ameamua kuongeza sababu hizo kutokana na kuona baadhi ya vitu vilisahaurika katika rufaa iliyowasilishwa awali na wakili Nyange.

“Licha ya kuongeza hizi nne baadhi ya sababu nitaziacha wakati tukiendelea kusikiliza rufaa hii,” alidai Marando.

Upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi, ulikubaliana na maombi hayo na kudai kuwa maombi hayo waliyapokea wiki iliyopita.

Mlokozi alidai kuwa baadhi ya vielelezo vya ushahidi vilichelewesha kufikishwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) ambapo alidai nyaraka hizo alizipata Novemba 27 wakati muda wa kazi ukiwa umeisha.
Alidai kuw akutokana na hali hiyo hajaweza kuzipitia kwa haraka kutokana na kuwa nyingi ambapo alidai kuwa nyaraka hizo ni zaidi ya 20 ambako alidai kuwa atakuwa akisoma taratibu.

Pia alidai kuwa kabla ya kesi hiyo kuanza jana Mahakamani hapo Malando alimpatia nyaraka nyingine ambazo bado hajajua zinasema nini ambapo alidai kuwa kutokana na uwingi huo aliiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo ili kuweza kupata muda wa kusoma.

Mbali na hayo Mlokozi alidai kutoelewa sababu ya 14 na 15 ambapo alidai kuwa sababu ya 14 inashambulia Mahakama ya Mkoa kwakutoweka kumbukumbu vizuri wakati sababu namba 15 nayo pia inashambulia Mahakama Kuu kwa kutokuweza kumbukumbu vizuri.

Wakili huyo wa Jamuhuri alidai kuwa kutokana na sababu hizo aliutaka upande wa utetezi kuelezea kwa kina sababu hizo kutokana na kutokuwa wazi na pia aliiomba Mahakama kuruhusu upande wa utetezi kuleta mashahidi ambao wataweza kuthibitisha madai yao yaliyotolewa katika sababu ya 14 na 15.

Kwa upande wake Marando aliiomba Mahakama kuongeza muda ili kuweza kupata muda wa kuweza kusoma nyaraka hizo ambapo alipoulizwa na Jaji Mbarouk kama kunamawakili waliojitoa katika kesi hiyo alidai kuwa hakuna aliyejitoa zaidi ya idadi ya mawakili kuongezeka.

Akitoa amri ya Mahakama kwa niaaba ya Majaji wenzake, Mbarouk alisema kuwa Mahakama imekubaliana na maombi ya upande wa utetezi ikiwa ni pamoja na kuongeza sababu nne katika rufaa hiyo.

Pia alisema kuhusu maombi ya Jamuhuri ya kutaka kuongezewa muda ili kuweza kupitia nyaraka zilizotolewa na upande wa utetezi alisema Mahakama imekubaliana na ombi hilo kwakuwa ni haki yake ili rufaa hiyo iweze kuendeshwa kwa haki.

Mbarouk alihairisha rufaa hiyo hadi Disemba 3 mwaka huu ili pande hizo mbili ziweze kupitia nyaraka za rufaa hiyo.

Babu seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamuhuri dhidi ya kesi ya kudhalilisha kijinsia watoto wa kike.

Kesi hiyo iliyovuma kwa wakati huo ambayo ilikuwa ikisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Mkazi Addy Lyamuya ambaye amestaafu hivi karibuni.


Wateja wa Vodafone M-PESA kujishindia mamilioni

Meneja matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania , Rukia Mtingwa, akisisitiza jambo wakati wa uzindua wa promosheni ya Vodafone M- PESA ,kushoto ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya,kulia ni Afisa huduma na bidhaa Elihuruma Ngowi.
Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania , Rukia Mtingwa, akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kushiriki promosheni mpya ya Vodafone M-Pesa mbele ya Waandishi wa Habari. kushoto ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya,kulia ni Afisa huduma na bidhaa Elihuruma Ngowi.

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Vodafone M-Pesa(katikati) Meneja matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania , Rukia Mtingwa, kulia ni Afisa huduma na bidhaa Elihuruma Ngowi.

Vodacom Tanzania imetangaza kuanzishwa kwa promosheni ya TUZO M-PESA ambapo itatoa zawadi ya mamilioni ya shilingi kwa wateja wake waliojisajili na huduma yake ya Vodafone M-Pesa zitatolewa.


Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa aliwaambia Waandishi wa Habari Jijini kuwa promosheni hiyo ya “Tumia huduma za M-PESA na Ushinde” inaanza kesho tarehe mosi na kumalizika tarehe 31 Desemba mwaka huu.


“Kupitia promosheni hiyo, wateja wetu wataweza kujishindia shilingi milioni arobaini kwa mwezi huu wa Desemba,” amesema.


Alisema wateja 20 wa Vodafone M-PESA watajishindia kila wiki shilingi 500,000/- na hivyo kufanya jumla ya zawadi za fedha taslim kwa wiki kuwa shilingi milioni 10.

Alisema kushiriki ni rahisi kwani kila wakati mteja atakapotumia huduma mojawapo ya Vodafone M-PESA atakuwa ameweza kuingia kwenye droo hiyo na kupata nafasi ya kujishindia Zawadi.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni pomoja na kutuma pesa, kununua muda wa maongezi pamoja na kulipia ankara za huduma mbalimbali.

Alibainisha kuwa hivi sasa kupitia Vodafone M-PESA Vodacom Tanzania inawawezesha Watanzania kutuma pesa kwa ndugu na jamaa zao wa karibu pamoja kuhifadhi amana zao.

“Kwa maana nyingine huduma hii inawaingiza Watanzania wengi waliokuwa wako mbali na mfumo rasmi wa kifedha,” Alifafanua

Alibainisha kwamba hivi sasa kupitia Vodafone M-PESA wateja wa Vodacom Tanzania pia wanaweza kulipia Ankara mbalimbali za huduma muhimu za kila siku kama vile maji, nishati ya umeme na huduma nyingine nyingi.

Aliwaomba wateja wa Vodacom kuitumia huduma hii ya Vodafone M-PESA katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu kwa kutuma pesa kwa ndugu na jamaa pamoja na kuitumia kupata huduma mbalimbali katika msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya




kumbukumbu



Mama EMILY TIKU GELLEGE.
( 24 /05/ 1948---29 /11/ 1996 )

Jana mama tarehe 29 /11/ 2009 Umetimiza miaka 13 tangu ulipoaitwa na Bwana tarehe 29 /11/ 1996 saa 2 asubuhi.
Mama tunakukumbuka sana Upendo wako,Hekima zako,busara zako na ulikuwa mshauri mzuri sana katika familia.Unakumbukwa sana na mwanao mpendwa na wa pekee Ruth,mkweo Eugene na wajukuu zako Emily na Ervin.
Pia unakumbukwa sana na Dada zako,Kaka zako,wadogo zako,wifi zako,wajukuu zako,shemeji zako,ndugu,jamaa na marafiki.Tulikupenda sana mama MUNGU alikupenda zaidi.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Lihimidiwe. Amen!!!.


majembe yakabidhiwa rungu kusimamia huduma za safari


Mkuu wa Usalama barabarani James Kombe (pichani) akizungumza leo jijini Dar kuhusu utoaji huduma ya usafiri kupitia kampuni ya Majembe Auction Mart.

SUMATRA imeanzisha utaratibu mpya wa kuleta maboresho katika usafiri wa umma na kuondoa kero kwa wakazi wa jiji wa Dar.
Yaania Kuanzia Desemba 1, 2009 Kampuni ya MAJEMBE AUCTION MART imekasimiwa kazi ya kusimamia, kufuatilia na kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa masharti ya leseni ya kusafirisha abiria katika jiji la Dar na kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo.

Mbli na kufanya kazi kwa karibu na Trafiki ambao ndio wanawajibu wa kusimamia sheria zote za nchi, Mamlaka itakuwa na utaratibu wake wa kufuatilia utendaji wao.

Wenye vyombo vya Usafiri, wafanyakazi wao, abiria na wananchi kwa ujumla wanaombwa kutoa ushirikianao wa hali ya juu ili kuleta maboresho yenye manufaa kwa umma.


seminar on Pan-Africanism coming thursday at UDSM

Dear all
MWALIMU NYERERE CHAIR-UDSM AND CODESRIA
WELCOME YOU TO A SEMINAR ON:
PAN-AFRICANISM IN THE ERA OF GLOBALISATION
VENUE: COUNCIL CHAMBER, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
DATE: 3RD DECEMBER 2009 (THURSDAY)
TIME: 4.00 – 6.00 PM (1600 – 1800 HRS)
PRESENTERS:
MEMBERS OF THE EXECUTIVE COMMITTEE OF CODESRIA INCLUDING:
Prof. SAM MOYO (PRESIDENT - Zimbabwe)
Prof: FATIMA HARRAK (VICE-PRESIDENT – Morocco))
Prof. KOFI ANYIDOHO (Kwame Nkrumah Chair – University of Ghana)
Dr. GODWIN MURUNGA (Lecturer, Kenyatta University, Kenya)
Dr. SHAHIDA EL BAZ (Life-long activist – Egypt)
Prof. ONALENNA SELOLAWAN (University of Botswana – Botswana)
Dr. NOEL OBOTELA RASHIDI (University of Kinshasha, DRC)
Prof. FEMK SENKORO (University of Dar es Salaam)
Moderator: Prof. Issa Shivji


rufaa ya babu seya na wanawe yaanza kusikilizwa leo

Nguza Viking na wanawe watatu wakiwa kizimbani Januari 27, 2005 kusikiliza uamuzi wa Rufaa yao dhidi ya hukumu ya kifungo cha maisha waliyokata kutokana na kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wa shule, lakini Jaji Thomas Mihayo aliyekuwa anaisikiliza aliitupilia mbali.

Leo jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania (Wah. Natalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salim Massati) linakaa kusikiliza rufani ingine ambayo Babu Seya na wanawe wamekata wakiwa wanawakilishwa na Wakili Mabere Marando.

Wasanii hao walituhumiwa kutenda makosa kumi ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo.

Washitakiwa kwa pamoja walidaiwa kutenda makosa yao kati ya Aprili na Oktoba 2003 maeneo ya Sinza kwa Remmy jijini Dar.


kiapo cha utii JKT enzi za mwalimu

viongozi mbalimbali wakila kiapo cha utii wakati walipkuwa JKT enzi za mwalimu ambapo jeshi la kujenga taifa ilikuwa ni wajibu wa kila mtu jambo ambalo linasemekana lilisaidia mno kujenga nidhamu, umoja na uzalendo na kutoendekeza matabaka ya aina yoyote ile


uhuru day in helsinki



dully sykes aongea



SWALI: Je unadhani elimu ina nafasi yoyote katika soko la muziki?


DULLY: Ndiyo ni kweli elimu ina nafasi kubwa sana kwenye soko,sio letu tu bali na kimataifa pia,na ndio sababu tunaanza kusema tunaibiwa na hatufiki mbali sababu vilevile hatuna japo upeo wa elimu ya masoko ambayo ni muhimu kiliko elimu yoyote hasa kwa sisi wanamuziki,pia wakati mwingine tunajaribu kufanya mawasiliano na wasanii wenzetu wa nje,ila ukijaribu hata kuomba kufanya nyimbo ya pamoja au kushirikishwa unakuta mnapishana maneno kutokana na wewe kutoitambua lugha husika ya unayetaka kufanya naye kazi,mfano yeye anazungumza kiingereza nawewe hukifahamu.


SWALI: Kama msanii wa bongo flava,unadhani kutoa Album na kutoa single kipi kinalipa zaidi?


DULLY: Kutoa single inalipa zaidi,kushinda Album

SWALI: Kwa nini?

DULLY: Sababu wasanii wamekuwa wengi sana na ndio maana msamabazaji anashindwa kukidhi mahitaji ya kila mmoja, ina muwiya vigumu kuchagua Album ipi ni bora zaidi ya zingine lakini ukitoa single nzuri itakulipa zaidi kupitia show za hapa na pale.
Kupata intavyuu yote


Baby Powder Shuts down Houston!!

The second movie premiere of Baby Powder in Houston, Texas was again very successful. People who attended this premiere were very happy to be a part of this historical turn up. The red carpet was unbeleavable!!(see the pictures).
People from Boston, NYC, NJC, Philly, DC, MD, Alabama, ATL, Minnesota were among hundreds who attended. "We had to have another session here in Houston because the first day seemed not enough to satisfy the fans, they requested us to show the movie once more and we accepeted their requests.
This was because on the first day of the premiere many people were spending time with their families for the thanksgiving day and not to forget those who were on the journey to Houston especially for this event. So we decided to grant their requests" ..The diector L. Karabani said.

Next weekend (5th of December) the Baby Powder "Red Carpet" will move to Washington DC for another premiere. All People, Friends and Wadau from Washington and the area are welcome to be part of this historical event. Please dress to impress because this is the night to shine! "Vunja Kabati" to reach for that last necely dress!!

After Dc the premiere will move to the next cities according to the schedule. Please follow the website for more informations. We thank everybody who joined us and for those who couldn't make it. "Thank You So Much" www.babypowderthemovie.com



















Globu ya Jamii Ipo Juuuuuuu, kwa mjibu wa Google!

I was perusing through Google Insights for search and I decided to run a simple search about Tanzania Web Search Interest from 2009. It showed some interesting results I would like to share.
(Based on 29/11/2009 query result)

TOP TEN:
1. Tanzania
This is the most searched keyword from compound keywords (Bank Of Tanzania, Open University Tanzania, Tanzania news, Tanzania government, Tanzania online, Tanzania daima, Vodacom tanzania and Air tanzania)

2. Yahoo
The second most searched keyword from compound keywords (mail yahoo, yahoo messenger, yahoo sign in, yahoo.com mail, yahoo.com)

3. Michuzi
From compound keywords (michuzi blog, michuzi issa, michuzi tanzania, michuzi blogspot, michuzi blog tanzania, issa michuzi blog,michuzi news)

4. Mail
From compound keywords (yahoo mail, yahoo.com mail, www.yahoo.com mail, the mail, google mail)

5.Yahoo.com
From compound keywords (yahoo.com mail, yahoo, yahoo mail, www.yahoo.com)

6. Yahoo mail
From compound keywords (yahoo sign in,yahoo.com mail, yahoo.com)

7. Yahoo.com
From compound keywords (www.yahoo.com mail, yahoo, yahoo.com, www.yahoomail. com)

8.Lyrics
From compound keywords (song lyrics, music lyrics, beyonce lyrics, lil wayne lyrics, akon lyrics, michael jackson lyrics, michael jackson)

9.Google
From compound keywords (google earth, google tanzania, google maps, google map, google chrome, google mail, search google, scholar google, google talk, google earth download)

10. Facebook
From compound keywords (login facebook, facebook Tanzania)

Based on the above data; My views
1. We don't know the URLs of our important websites (Bank Of Tanzania, Open University Tanzania, Tanzania news, Tanzania government, Tanzania online, Tanzania daima, Vodacom tanzania and Air tanzania) thats why we use an american based website (google) to help us get to our websites.

2.Yahoo appeared on no.2, 4, 5, 6 & 7. This shows most of Tanzanians we use yahoo mail and we don't type the yahoo address in address bar (why? - may be we don't know the address / we don't know how to use address bar/ It is easy by using Google/ we don't bother to know as long as Google is there / That is how we are used to do it ).

3. There is no doubt that Michuzi blog is among the famous blogs in Tanzania. For the keyword "michuzi " to appear on the most searched keyword, this means either its URL " http://www.issamichuzi.blogspot. com" is complicated/ not known for most of its users /known but users are lazy to type it in the address bar /users don't know how to use the address bar/ user have fear of misspelling the URL

4. keyword lyrics and facebook shows that we like to know about the lyrics of the songs (from America), and also we are social networking. Its good to see most of the Google search engine users know/want to know about other Google services like Google scholar, Google maps, Google earth and Google talk.
Mdau RahaLeo


wake wa wakuu wa jumuiya ya madola walipokutana

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi yaWanawake na Maendeleo WAMA Mama Salma
Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wake wa wakuu wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Madola kwenye kituo cha kidiplomasia mjini Port of Spain Trinidad
Tobago


nondozzz chuo kikuu arusha university

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Arusha, Askofu Joshua Kajula akiwatunuku shahada wahitimu katika mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo wilayani Arumeru wikiendi hii
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Arusha, Askofu Joshua Kajula akiwatunuku shahada wahitimu katika mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo wilayani Arumeru

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiteta na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Arusha, Askofu Joshua Kajula katika mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo, wilayani Arumeru




moshi by night

DJ akifanya vitu vyake Pub Alberto, moja ya viota vya maraha mjini moshi mjini usiku wa kuamkia leo.
wadau wakijimwayamwaya kwenye kiota cha maraha cha Pub Alberto moshi mjini


Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker