Salam Mheshmiwa.

Naandika hii kutoa taarifa kwa wadau wale ambao wangependa kuja kusoma Finland. Shule ni bure yaani hakuna school fees ila unachotakiwa ni kujilipia malazi na chakula. Kwa wale wenzangu na mimi ambao wanandoto za kusoma nje kwa ajili ya masters au hata PDH mfumo ni ule ule, no school fees bali unajilipia accommodation tu. Admission zinaendelea kwa iyo wenye nia wanaweza kutembelea hii link www.admissions.fi

Elimu yao inathamani na inatambulika duniani hasa kwa masomo ya technology. Nafikiri siku moja itapendeza tukiwa na Watanzania wengi wasomi na wenye exposure kwani ndio mwanzo wa mabadiliko na changamoto nyingi kwa jamii yetu.

Ni hayo tu

Pamoja
Mdau Finland
Web: www.milimanitours.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Asante kwa taarifa, ila tafadhali rekebisha, inaitwa PhD
    sio PDH... lol

    ReplyDelete
  2. Mdau,
    Truly, education is of zero costs. Agree.My concern is about the expensive and how to manage the life while you are studying. Can one study and work simultaneously? In case its affirmative reply ,I'd love to get more about job availability within the country especial to foreign students who their mouth cannot even open and say one finish word. Better you share experience you have for us to follow. We love coming to Finiland, but we scare the living cost and job opportunity to keep us there.Sory for my low standard "ung'eng'e",I am writing while I am in Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Ubarikiwe mdau kwa kutoa tangazo kama hili ili watuwafaidike na masomo.

    ReplyDelete
  4. tunashukuru sana kwa msada wako, ila mimi naomba unipe information kuhusu Master. nataka apply. nisaidie kwa hilo.

    ReplyDelete
  5. annon wa #2 toka juu

    hahahahhaaaa tumekusamehe sana tu

    ReplyDelete
  6. Tunashukuru for such a good information and be blessed naungana na Mdau hapo juu more Info on Masters as wadau wengi TZ degree mkononi masters kimbembe.

    ReplyDelete
  7. Kwa mdau wa pili: kusema kweli shule na kazi inawezekana ila kazi zenyewe ndio hizo za mabox lakini nia na kikubwa kilichokuleta kinapatikana mwisho wa siku. Sisemi ni rahisi ila opportunities zipo. Kwa wenye bahati ya kuishi miji mikubwa yenye foreigners wengi inakua even better. Nakubali kuwa it is still not easy but many have gone through it na wamemaliza shule. Ukilinganisha na wenzetu walio UK au USA ambao wanajilipia ada na kila kitu, naamini ni ngumu kuliko huku.

    Kwa mdau anaetafuta masters, cheki hii link
    http://www.studyinfinland.fi/contact_us.html
    au click Studying then click International Study Programmes

    ReplyDelete
  8. Aksante sana, tuwekee information za Masters plse

    ReplyDelete
  9. aisee asante sana kwa taarifa, ila naomba unipe tu rough idea unadhani room inaweza kukost how much per month? na kwa mahesabu ya haraka hakara unadhani kama dola ngapi hivi au shilingi ngapi kwa mwezi mtu anaweza kujibana angalau aweze kutimiza hizo goals? nina mdogo wangu nataka nimpeleke ila kama tution ni bure nadhani malazi na chakula naweza kujibana nimsaidie. shukrani mtoa habari!

    ReplyDelete
  10. hebu kuweni wastaarabu,wwewe unayewsema unataka kusoma masters unataka usaidiwe nini sasa?? ushaambiwa fee ni bure, then what? wewe umepewa website halafu unataka usaidiwe nini sasa, unataka apply onyour behalf or vipi?? wacha ujinga ingia kwenye hiyo website uliyopewa then apply ebo!!! kila kitu kimejieleza vizuri sana kuanzia aliyetoa habari na mpaka kwenye hiyo web everything is clear, what is wrong with you?????

    ReplyDelete
  11. A non-EU student must prove that he/she is able to support his or her living in Finland during the studies. The required sum of money is 500 euros per month or 6000 euros per year. See also Visa and residence permit.

    ReplyDelete
  12. ahsante sana. ila ingelikuwa vizuri kama ungelitupa mwanga kidogo juu ya average ya rent pamoja na bei ya nguo na vyakula kwani hivo ndio muhimu. ni lazima tuangalie bajeti zetu kama tunaweza au la.

    ReplyDelete
  13. MH jamani ni kweli kusoma ni Bure huko SUOMI "FINLAND" Lakini kwa yule anayetegemea asome kwa kufanya kazi, ningekushauri ufute wazo hilo ndugu yangu. Finland ya zamani kuanzia miaka ya 2000 kurudi nyuma, ndio ilikuwa na hivyo vibarua, japo vya kufagia vyoo lakini vilikuwa vinapatikana. Siku hizi ndugu yangu ni kasheshe. Warusi, Waestonia, Waalbania, Waitaliano, na wafini wenyewe wasoenda shule wanazitafuta kazi hizohizo!!! You can imagine how tough it is. Kwa sie tulosoma enzi hizo zilikuwa zinapatikana lakini sio siku hizi.Kifupi tu nisingemshauri mtu kufanya patapotea kama hiyo. Utaishia KUJILIPUA kama wengi walivyofanya kutokana na ugumu wa maisha!!!

    ReplyDelete
  14. vipi hata kwa bacholor? vile vile tueleze hali ya maisha ya huko.

    ReplyDelete
  15. Mdau sasa kama elimu ni bure huko, ina maana mtu yeyeto anaweza kuja na kusoma huko? Hakuna vipingamizi? Ina maana watu wa mataifa ya nje ya hapo wanapata nafasi kwa wingi sana ya kuja kusoma hapo?

    Kama ni bure basi wabongo wachukue mabegi waende kupanda ndege tu kirahisi?

    Tupe details za kutosha, maana sijakuelewa hiyo elimu ya bure nitaipata vipi mimi mtoto wa mkulima hapa Kilosa Morogoro.

    ReplyDelete
  16. Mi nilishatembelea finland kwa miezi miwili.

    Yaani kila mtu anakazi kwa hiyo kupata kazi ni rahisi sana.Watanzania wote wanafanya kazi na maisha sio magumu.

    Vyakula bei poa nafikiri hata kupata nyumba ni rahisi kwasababu hakuna rushwa.

    wasalimie wadau wote finland.

    mdau UK

    ReplyDelete
  17. mie naomba unielekeze jinsi gani ya kuomba PDH asante lol

    ReplyDelete
  18. tungepata mtu kama wewe siku nyingi taifa lingejengeka, kuna mijitu naijua imekaa hapo ufini na inajua kuhusu hio issue na kusema imeshindwa na kusoma haisomi, bora wewe utamhamasisha mtu asomee daktari arudi kuja kututibu kapa namanyele sumbawanga,una akili nyingi sana

    ReplyDelete
  19. Wadau hapo juu maswali kibaooo kwa nini lakini au 'mu-wavivu wa kufikiria' yaani ooh maisha expensive? nitaishije? nipe habari zaidi!

    Mna -'bore' kwa nini msiende ktk linki ya webusaiti, au websaiti ya Ufini n.k n.k mpate habari kibao, hii sio 'admission site ya wanafunzi'

    Umeweza kusoma hili tangazo, kwa nini usifanye research ktk intaneti au ulikuwa unatumia muda wako ki-duchu kusoma magazeti ya udaku ktk intaneti.

    Next taimu wadau wawekeeni post fupi na kuwaelekeza wafuate link kwa maelezo au maswali zaidi.

    Wenzenu kina Nkrumah walipanda meli ya mizigo na mifugo kwenda soma USA hata Dkt Kaborou pia alichachalika baada tu ya kupata 'hints', nyie wakati scholarship ipo mezani(ktk blogu), mnataka mtafuniwe halafu mlishwe kwa kijiko!

    Mdau
    Graduate2009.

    ReplyDelete
  20. mweee kweli kwa wenzetu kuzuri yaani karo za sare za shule bureee

    ReplyDelete
  21. MUNGU KAMPS KILA MTU BURE MAJIZI NA MAJAMBAZI YANATAKA MAPESA KIBAO SHUKURANI KWA HIZI NYAKATI WATU WETU WATASOMA BURE. SHULE SIO MAJENGO NI VITABU. VITABU HAVIDAI POSHO

    ReplyDelete
  22. Anon#2 juu,
    Jaribu kuwa mungwana na kubadilisha tabia,yaani uwe na matazamo mzuri,maana ya jamii mtandaoni ni kupashana habari ambazo zitaleta maana kamili ya maisha,mojawapo ni habari alizoleta mdau kuwa kuna nafasi za masomo UFINI,na kaonyesha njia au dira ya mwelekeo.sasa sio kama una haja ya kuleta nuksani ktk heri?

    ReplyDelete
  23. kwakweli mimi nina miaka kama mitatu hapa ufini.maisha si rahisi kama unavyo fikiria ni expensive sana.kuhusu kodi ya chumba kwa mwezi ni euro,500mpaka 700 inategemea na ukubwa wa chumba na chakula kipo lakini sio bei kubwa sana na kuna vyakula pia vya nyumbanikwenye maduka yawahindi utapatasio maduka ya wafini.na huku kupata kazi ni conetion yako uliyo nayo na si rahisi mpaka ujue lugha yao hata kama wewe una vyeti vya elim zote lugha yao kwanza.kwa ujumla maisha kwa finland ni magumu ukilinganisha na sweeden sweeden ni kama bongo kazi kibao na kuna waafrika kibao hawana ubaguzi kama hawa wafini na wanachangamka sana na waafrica kuongea nao kujoin kwenye mambo mbali mbali yanayo husu kazi na furaha zote kwakweli sweeden kuzuri zaidi.kwahiyo ni wewe tu kuchagua wapi pa kwenda kati ya finland au sweeden japo baadhi ya vitu vina fanana.

    ReplyDelete
  24. mtu atataka hadi afanyiwe application. Kama hauna nia ya kujishughulisha mwenyewe nadhani hata hiyo shule itakushinda. Website mmepewa, tatizo nini?

    ReplyDelete
  25. Link hii hapa inadetails zote kuhusu shule
    https://www.cimo.fi:443/Resource.phx/cimo/lehdpalv.htx

    Pia tazameni hii link ya pili
    http://www.minedu.fi/OPM/Koulutus/?lang=en

    Lastly mnaweza kupata more details kwenye embassy au kuwasiliana na shule ambayo inatoa kozi unayotaka kusomea.

    Maisha ni magumu, rent kwa wanafunzi zinaanzia 250€ in average. Sio wote waliokuja walikua na uwezo lakini ni vizuri ukijiandaa kifedha kwani things are constantly changing.

    Pamoja

    ReplyDelete
  26. Nimeishi Finland mwaka wa 13 sasa, nimesoma, nafanya kazi japo sio level ya juu sana, ila inatosha na SIONDOKI NG'OO.
    Mdau unayewaambia watu nyumba ni euro 500 hemu acha kuwatisha, 500 kama ni mtu unayetaka kuishi peke yako, maisha ya hali ya juu hayo.Chumba cha mwanafunzi kwa mwezi ni euro 180-200.Hizo euro 6000 unatakiwa tu kuonyesha kwenye statement yako mwanzoni ili uweze kupewa permit ya mwaka ukae hapa, ukishakuwa mwenyeji na marafiki kila mwaka watu wanachangishana hizo ili kuweza kuextend visa na ukishamaliza kutoa statement unarudisha pesa za watu, uaminifu tu, enzi zetu sisi tulifanya sana ila sikuhizi kidogo uaminifu umepungua.Vibarua kwa sasa sio siri ngumu kupata lakini bado ukichakarika na ukawa na network nzuri na wabongo au wawest eventually utapata tu,ila muhimu ujitahidi pia kumumunya hapo maneno kadhaa ya lugha yao itakusaidia sana mbeleni.Mimi nilishamaliza kusoma miaka kama 5 iliyopita,ila najua mana wadogo zangu wanasoma kwa sasa.
    Chekini pia www.universityadmissions.fi
    chakula bei sio mbaya sana ila kama unataka kula nyama ng'ombe kila siku basi hapo utaishiwa...ila hali ya hewa siwafichi winters are too damn cold, but ofcourse kuna makoti so ni kuvumilia na kujua nini unachotaka.
    Upatikanaji wa decent jobs bado ni mgumu,so may be mtu usome then usipopata cha maana uanze mbele.Then kuhusu nguo ni bei sana, nguo za quality i mean, bora mtu ununue mijeans yako bongo, huku gharama sana, ila kama unataka tu nguo za kawaida sio za majina, ziko kibao, bei sio ya kutisha.Ila nashauri kama mtu unataka bana matumizi, njoo na nguo zako mwanzoni, utanza kununua nuo baadae ukija kupata kakibarua.
    NAWASHAURI OMBENI SHULE ILA TU KAMA MTU UNAWEZA UNAPOKUJA UJE NA VIPESA VYA KUKUSUKUMA JAPO KWA MIEZI 6 INACASE USIPOPATA KAZI MAPEMA, AU UWE NA MTU HOME WA KUWEZA KUKUSUPPORT KAMA UNAKWAMA ANAKUTUMIA VISENTI, UTASURVIVE TU,CHA MUHIMU UNASOMA,au vipi?
    KARIBUNI SANA HILI BEACH BADO NYANYA KABISAAAA NA FOR YOUR INFO WAFINI WANATUPENDELEA SANA WATANZANIA KUANZIA KWENYE KUTUPA VISA NA MENGINE MENGI TU UKILINGANISHA NA NCHI ZINGINE, NI SABABU FINLAND NA BONGO TUNA URAFIKI WA MUDA MREFU SANA.

    ReplyDelete
  27. Jamani mimi ni mtanzania nasoma huku kusema UKWELI huyo mdau aliyesema kazi zinapatikana kiurahisi SIYO KWELI KABISA!!! kazi ni za kufagia na kwamba siyo rahisi kupata ilikuwa hivyo zamani na siyo sasa plz!! kwa wanaotaka kuja wanahitaji kuelezwa hali halisi wewe mpita njia huujui ukweli. Elimu ni bure gharama za maisha zipo juu sana.

    ReplyDelete
  28. Mdau jan 29 09:59, Alwuwatan ameongea ukweli, ametoa hali halisi kwa mtu yeyote mwenye mawazo ya kusoma Ufini basi fuata ushauri wa huyu jamaa, nipo Scandinavia na naweza kusema kuwa shule sio bure bali inagharamia na serikali kwa wanafunzi wote kutoka nje ya ufini na wafini wenyewe isipokuwa gharama za maisha itabidi ujitegemee.

    ReplyDelete
  29. shule zipo za bure lakini cha moto utakiona.kuna watu walikuja wa kakibia nahea ya watu euro 6000 kwa ajili ya viza. na kama upotayari kusoma na kuhamka saa 8 kwenda kugawa magazeti na kifagio karibu lakini game is not easy. hata wanao sema chakula bei poa sio kihivyo. kwa elimu na unga mkono ni bure na mnakalibishw. terve tuloa suome. ja täytty puhuu suomi kieli jos sinä haluat asua tällä. saada työ ei helpo.

    ReplyDelete
  30. Bro michu,mimi ningependa kueleza ukweli jamani msije mkaruka mkojo na kukanyaga choo!!!kwni jinsi ambavyo maisha ni magumu sana hapa Finland si rahisi heti 6000euro ndio master unayo!!!!or phd!!!kwani kama wewe si mtoto wa meni au kikwete ningekushauri wazalendo muangalie sana kwanirent ni kuanzia 450 mpaka 820 euro kwa mwezi halafu kwa sasa kazi hakuna,wale wenye ndugu zao hapa ndio wanasaidiana lakini ukiwa kama mimi basi waweza jikuta wabeba maboksi ambayo hakuna kwa sasa kwani kwanza they look for european kama romania,russa estonian,waturuki mwisho ni sisi blacks,ningeshauri muangalie vizuri kwani wabongo wa hapa Finland ni wanafiki hawapendi kusaidia wako tayari kusaidia mpopo au mkenya but sio mtanzania,ukiendewa vibaya na mambo wanakucheka na kukuweka midomoni mpak utoke kwenye hili janga basi au uwekwe kinyumba au uolewe na msenge.so please guys angalieni kabla hujauza mali zako na kujikuta uko beach!!!!unashangaa ferry au uokote makopo upate senti mili za kununua mkate.yako mengi ya kusema but hakuna huo muda wa kueleza yote,hivyo jitayarishe utakapo kuja hapa you need at least 20,000eur a year na sio 6000. By Mlalahoi,Helsinki,Finland

    ReplyDelete
  31. wewe aluatan umekuja hapa finland ulisota na sasa una mama la kifini tingatinga mbona huwaelezi ukweli???waeleze waelewe.na kama sio huyo mfini ndugu zako wasingekuwa hapa bwanaa aah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...