Kiongozi wa Libya Kanali Muamar Gadaffi

Kuwajengea Nyumba 200 Nyumba Waathirika
Na Jovina Bujulu, Maelezo.
Jamhuri ya watu wa Libya imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko ya Kilosa mkoani Morogoro. ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba 200 zenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.

Akiongea na wanahabari katika uwanja wa ndege Dar es Salaam Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Mheshimiwa Philip Marmo alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani hali ya wahanga hao si ya kuridhisha

Aidha Waziri Marmo alizitaka nchi rafiki,Jumuiya za Kimataifa pamoja na Watanzania kwa ujumla kutoa misaada kwa hiari yao kwa kadri wanavyoguswa kwa wahanga wa mafuriko ya Kilosa.

“Uwezo wa Serikali ni mdogo na hauwezi kutosheleza kila kitu hivyo tunaomba Jumuiya mabalimbali za Kimataifa na Watanzania Kushirikiana katika kutoa misaada”.Alisema.

Pia alizitaka Kamati za maafa husika kutekeleza wajibu wao kwa kufikisha misaada hiyo kwa wahusika na alimhakikishia balozi wa Libya nchini Ahmed Abdusalaam Al Ashaab ambaye alikabidhi msaada huo kwa niaba ya nchi yake kuwa itawafikia walengwa na magari yataanza kupeleka misaada hiyo kesho.

Akikabidhi msaada huo balozi wa Libya nchini bwana Ahmed Abdulsalaam Al Ashaab alisema msaada huo umetolewa na jumuiya mbalimbali nchini humo kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Libya.

Vifaa vilivyotolewa ni magaro 1100, Blanketi 400, Mahema 1300, Mito 1200, Maboksi 500 ya madawa ikiwa ni pamoja na vifaa vya huduma ya kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. nyumba 200, thamani yake ni sawa na nyumba 1 tuu ya gavana wa BOT.

    Afrika afrika afrika.

    ReplyDelete
  2. kama ndio hivyoo bas mzee wa vjisenti akibanwa vizuri atajenga nyumba 800

    ReplyDelete
  3. Anon wa kwanza umesema ukweli kabisa, serekali inasema haina uwezo inapata wapi almost the same amount of money kujenga nyumba moja ya Gavana lakini wananchi wake wanapata mafuriko na wengine wanakufa serekali hiyo hiyo haijali na kuomba watu wengine wasaidie, kama Mungu yupo hawa viongozi lazima watatakiwa kujibu kwa Mungu jinsi wanavyoendesha nchi maana hii sio haki kabisa.

    ReplyDelete
  4. kunafaida gani ya kuwa na uongozi wa kidemokrasia na udikteta ktk uchumi? miaka 10 ijayo tutaendaa kuwaomba rwanda,kenya watujengee barabara
    sijui ni lini na sisis tuakuja kutoa msaada wa mali na fedha kwa nchi nyingine zaidi ya msaada wa nguvu

    ReplyDelete
  5. Haya yule Mdau anayemsema Gadafi yuko wapi?????? Gadafi anawasaidia wa Africa wenzake si Nchi zile za nje Welldone Gadafi. Nchi ya Mali iliulizwa na Gadafi mnataka msaada gani wakasema wao hawataki nyumba wala umeme wao wanataka maji jamaa alichimba kutoka kwake kupeleka maji Mali. Gadafi safi sana lazima uigwe na wafrica. KImaro,Moshi.

    ReplyDelete
  6. si huwa hamumpendi kwa sababu alimsaidia nduli, kataeni basi mchango huo.

    msisahau ugaidi pia ni sababu.

    ReplyDelete
  7. Shameful na ni hatari mno, tutakua makini 2010ingawa uchaguzi hua na yake ila ni aibu kubwa nyumba moja ya gavana tutajenga nyumba 200 kwa waathirika. Viongozi liangalieni hili.

    HYD.

    ReplyDelete
  8. yaani hawa viongozi wetu Mungu atawahuliza kwanini mlikuwa viongozi na ali yakuwa hamkutimiza wajibu wenu katika jamii, mtu mwenye akili ya utu uzima hata mtoto Nyumba mmoja ya BOT ya bwana Ndulu bilion 1.3 lakini serikali kutoa hata milioni 200 kuwafariji wale watu hakuna, mpaka watu binfsi wenye upendo na imani ndo wanasaidia sio wa nje wa hapa ndani nyinyi hamna kitu ya kweli haya, basi serikali haina ela hata CCM tawala ruzuku kwa mwezi milion 500 toa hata 100 msaidie ili mpigie kampeni 2010 nchi hii wote ni sio waadilifu kazi kutukana wanapoambiwa ukweli kama Ngeleja alivyofanya shame on them kuna leo na kesho kaburini.

    ReplyDelete
  9. unajua watabiri wa hali ya hewa walituambia kuwa kutakuwa na mvua za elinino tulichukua taadhari gani kujikinga na mafuriko??? kama Anon wa hapo juu alivosema kuna watu wanavijisenti vya kujenga nyumba 800 lakini tunapata misaada toka nje sasa na hiyo misaada kuwafikia walengwa itakuwa kazi nyingine tena. mizigo ipo airport kupeleka kilosa itahiji usafiri, hapo sasa.
    unajua sisi waafrika sijue tukoje, nipo nyumbani naagalia news ya ITV mheshimiwa waziri mkuu and mzee makufuli wameenda kuangalia samaki waliokamatwa na sasa wanapewa watu bureeeee na wale jamaa wapo jela sijui wanasubiri nini.... ningekuwa ni mimi nigewakamata hao wachina na meli yao halafu nawaambia twende tukawauze hao samaki halafu nigepata hizo milion dollars, narudi kuwashitaki kwa kuwabiga faini au nawachia kwa kuwa kujua soko lipo wapi. but now samaki hawaedi na walipohifadhiwa mwenyewe anataka pesa yake kwa hiyo serikali itamlipa na yale madola yamepotea. na hao wachina sijui hatima yao itakuwaje.. hiyo dio tanzania
    yetu. inauma sana mjomba.

    ReplyDelete
  10. HIvi kila siku twaomba misaada nchi nyingine TZ sisi wenyewe tunajisaidiaje na haya,weye watu wanatoa kodi haya hizo pesa zao zaenda wapi?na kila siku wanadai serikali haina pesa kama ni hivyo hizo za kujenga nyumba ya gavana zimetoka wapi huoni hii inakuwa inawaondoa ata imani watu wenye mioyo yao kutoa jamani serikali yetu ni vipi?kwa kweli hii inasikitisha sana..

    ReplyDelete
  11. Swali kwa Mh Marmo, tulioko znz sio sehemu ya msaada wa serikali ya muunguno?? ni jitihada gani selikari ya muungano imefanya kutuondelea dhiki ya umeme? longolongo nyiiiiingi ya malidhiano baina ya Karume n Seif kama c CCM na CUF.....Balozi Mithupu, kweli hii HAKI sawa kama wasemavyo wana CUF, au ndo kuthibitish kwamba znz c nchiiiiiiiii???

    ReplyDelete
  12. Hii ni aibu sasa, hivi kweli MH rais anasoma hizi blogs?

    ReplyDelete
  13. Gavana analipwa vizuri akajenge hukonyumba iuziwe balozi za nje pesa ikasaidie wahanga!
    Mawaziri wote/wabunge wajitolee mishahara na marupurupu yao ya januari pesa itatosha kabisa kumaliza shida za wahanga!
    Wabongo muache kujirusha angalau kwa mwezi mmoja[kitchen party,harusi za mamilioni n.k na upupu mwingine]pesa ipo tu ya kutosha tena hapo darisalama tuu ya kusaidia hili tatizo hakuna kabisa sababu ya kila kitu kukinga mkono na kuwa ombaomba ila basi tu sie bongo ni bongo kweli yaani tambarare we acha tuu.Sijui siku tukikumbwa na kama haya ya Haiti[Mungu epushilia mbali] itakuwaje?Wenye vijisenti watalala mbele na kuwaacha walala hoi wanasuguana!

    ReplyDelete
  14. Bora Gadafi anajua umuhimu wa kuwa na resources na kuzitumia kwa manufaa ya wasio nacho japo mtoto wake alichemsha baada ya kuchangia £20 million kwa London School of Economics ili awekwe kwenye group la watu muhimu na chuo

    ReplyDelete
  15. Hii ni aibu kwa taifa ukizingatia Gavana wa Bank kuu ya tanzania anaishikatika nyumba moja inayo gharimu zaidi ya nyumba 200 za watanzania wakawaida na bado serikali wanaomba msaada kutoka kwa wananchi eti serikali haina pesa za kutosha!

    ReplyDelete
  16. Wakati inapitishwa tenda yakujenga nyumba ya Gavana iliyogharimu zaidi ya Bill 4 zakitanzania,serikali ilikuwa na pesa yakutosha lakini tukija katika suala lakuwasaidia wananchi serikali haina Pesa!!??..sisi tunamuachia Mungu yeye ndio Hakimu wa Haki na yeye ndiye mwenye nguvu zaidi.

    ReplyDelete
  17. HIVI WATO 200 WAWEZA KUPATA HIFADHI SAWASAWA NA KIBOSILE MMOJA?TUNAWASHUKURU ILA TU MSAADA UWAFIKIE WALENGWA.MAKE HAPO WATU MATE YAMESHAANZA KUWATOKA

    ReplyDelete
  18. hongera libya kwa kuonesha ukomavu wa kujijua,nyinyi ni waafrica maana mko bara la africa.hapo ndo ninapomkubali gadafi,your the man,huwatupi waafrica wenmzako,ni tofauti na viongozi wengine wa nchi za kiarabu za africa.hatumjui hata rais la tunisia au moroco.

    ReplyDelete
  19. eeeeh bwana kumbe kuna mafuriko bongo? sasa watanzania wanajidai na comments zao facebook eti wana toa rambi rambi haiti.mbona hamsemi chochote kuhusu kilosa malimbukeni bwana,eti my prayers go with haiti pple.how abt with kilosa pple?
    sikatalii haiti kweli wanasikisha sema wabongo wamezidi.

    ReplyDelete
  20. hawa viongozi ni wazushi 2 mi sidhani kabisaa kama kweli uwezo hakuna wa kusaidia ila ni ulafi wa badhi ya viongozi ambao wanadhani madaraka ni shamba la pesa kazi yao kuvuna 2

    ReplyDelete
  21. Crazy Tanzania yaani bwana Beno Ndulu analala katika nyumba ambayo wanaweza kuishi waTZ zaidi ya 200. heeeh. Bwana Gadaffi angejua anaowasaidia wana hulka gani, anyway return yake ni kubwa sana asingetoa msaadahuu hivihivi tuu

    ReplyDelete
  22. Gaddafi's son Saif Al Islam Al Gaddafi alichangia £1.5M to LSE, please naomba nirekebishe hapo juu kuwa si £20M maana magazeti ya bongo yatoa habari humuhumu kwenye globu ya jamii.

    ReplyDelete
  23. NIMESOMA MAONI YENU WADAU NUSU NIPASUE SCREEN ILI NIINGIE HUMU NDANI NIJE NIZABE VIBAO WATU!! ETII ...HAYA BWANA VIONGOZI WETU SISI TUNAMWACHIA MUNGU!...UNAMWACHIA MUNGU ILI AFANYEJE? WAKATI MUNGU KASEMA BISHA ODI NAWE UTAFUNGULIA, SHUGHULIKA NAWE UTAPATA!! SASA UNADHANI KUNA KIONGOZI ATAKUONEA HURUMA HAPO KWA KUSEMA HIVYO! WATANZANIA ACHENI U......!! HAMKENI MPIGANIE CHENU MTAKAA HIVYO HIVYO TU MUNGUUU MUNGU!! UMWINYI TU UMEWAJAA HATA KUTETEA KILICHO CHENU MNAONA UVIVU! NCHI NDOGO KAMA RWANDA NA BURUNDI ZINAWASHINDA WALISIMAMA KIDETE WAKADAI KILICHO CHAO SASA KIONGOZI AKIWEKWA KULE ANATIA AKILI NA HAKUNA MZAHA NA NCHI SI HIZO MNAZIONA ZINAKUJA! NYIE MTAKAA NA YAKHEEE HAY BWANAAA...MPAKA MUOTE VIBIONGO NA WENZENU WANAPETA!! NA SASA WAMESHAJILIMBIKIZIA HAOOOO WANAHAMIA KIGAMBONI NA WATAJIJENGEA DARAJA NA KUWEKA GETI TUONE KAMA MTAWAONA!! MMMMH MNADHANI WANAWAFUKUZA ILI IWE NINI....AAAAH HAMJUI EEENH?? SASA MTAJUA SASA!! TATIZO LA TANZANIA KILA MTU ANJIFANYA NDUGU.....MH. KITASA KAMUOA DADA WA MAMA YAKE MJOMBA MKUBWA WA KILOKA KARIBU NA YULE MUUZA MKAA WA NYUMBA YA PILI.....ETI NDUGU!! NDUGU YAKO NI KAKA, DADA, BABA, MAMA, MJOMBA, SHANGAZI, BINAMU TU WENGINE SIJUI KAMUOA NANI NI BAKORA TU!! MBONA KAMA NDUGU YAKO AKIJENGA HEKARU HATA KWAKE KWENDA HUENDI!! ETI TUNATOKA KIJIJI KIMOJA BWANA! UPUMBAVU HUO ..MTAKAA HIVYO HIVYO NA KIJIJI KIMOJA WENZZENU WANAPETA!! HII NI AIBU KUBWA KWA NCHI YETU KUPATA MISAADA KUTOKA KWA NCHI NYINGINE YA KIAFRIKA MABAYO TUMEPATA UHURU MUDA SAWA! WAKATI WENZENU WANATAFUTA MAENDELEO NYIE SI MLIKUWA MNAGAWA ETI UKOMBOZI WA AFRIKA ....AFRIKA MY .....!!WATU WAMEIBA MABILIONI HAPO BENKI KUU HATA KUWAKAMATA MKASHINDWA ETI ...UNAJUA ITAATARISHA USALAMA WA NCHI!! YANI WEWE WAZIRI NA AKILI YAKO UNASIMAMA NA KUWAAMBIA WANANCHI HIVYO!! HIZO FEDHA SI MNGEWAJENGEA WANANCHI BARABARA AU NYUMBA?? WANANCHI WANAJENGA MABONDENI ILI WAWE KARIBU NA MAHITAJI YAO MUHIMU. JENGA BARABARA MILIMANI KAMA UTASIKIA IKO SIKU KUNA MAFURIKO!! AAAAAAH MIMI HAWA VIONGOZI SIJUI HUYU NYERERE ALIWATOA WAPI!!

    ReplyDelete
  24. Mafisadi wasije wakawazunguka tu, hawana utu hawa jamaa.lol

    ReplyDelete
  25. Kumbe nyumba moja wa mtu mfanyakazi mmoja wa BoT Tanzania ni sawa na nyumba 200???? Kweli Bongo ilishauzwa.......halafu viongozi wanaliona sawa tu la gavana kuwa na nyumba hiyo, ahaaaaaaaa jamani jamani.

    ReplyDelete
  26. I SECOND U @Sun Jan 17, 04:14:00 AM...UMESEMA YOTE HATA SIJUI NI ADD NINI. INAKATISHA TAMAA NA NI AIBU HATA MWEZI HAUJAPITA KWELI TUNAAMBIWA MSAADA WA HELA HIZO UNAWEZAJENGA NYUMBA 200!!!!!!!!!!AGHRRRRRRRR

    WATU WENGI WAKUCHAPA VIBOKO HAPO TU... LAKINI WATU KILA SIKU HAYA BWANA.....BONGO YETU SIKU HIZI TAMBARARE.....TAMBARARE KWA MAFISADI TU...........NDIO NYIE MNAKULA UGALI KWA SAMAKI WA HARUFU ZA JIRANI...MAGARI MAZURI MNAYATAZAMA TU WALA HAMYAJUI NDANI YAKOJE, MAHOTEL MAZURI WALA HAMYAJUII NDANI YAKOJE NA YAPO HAPO HAPO TANZANIA...NYUMBA NZURI KILA SIKU MWATAZAMA NJE YA MAGAIT TU...KILA UKIPITA NIKUSIKIA HIYO NYUMBA YA FULANI ...NA ILE NI NYUMBA YA MTOTO WAKE ...HIYO NYUMBA MTOTO WAKE AMEJENGA AKIWA ANASOMA NA AMEMTUMIA BABA YAKE GARI TENA JUZI JUZI.....UKIULIZA HUYO MTOTO KAENDA LINI KUSOMA UNAAMBIWA HATA MIAKA MIWILI HANA HUKO MAREKANI.....SWAIN....MWAKA MAREKANI UWEZE KUJENGA NYUMBA NA KUTUMA GARI TANZANIA???? WADANGANYE HAO HAO WAJINGA (MONEY LAUNDERING) WABONGO VIPOFU TU.....ATI MWASEMA BONGO SIKU HIZI KAMA MAREKANI ...JE HIVYO VITU MWAFAIDI AU MWAVITAZAMA TU WAKATI MAFISADI WANAVIENJOY......


    HALAFU MAFISADI SIKU HIZI WAMEANZISHA KAMCHEZO KAO HAKA KA KUPELEKA WAKE ZAO KUJIFUNGUA WATOTO HOSPITALI ZA MAREKANI ILI WATOTO HAO WAPATE URAIA WA HUKO.....MJUE HAPO WATU WAMESHAPIGA MAHESABU WAMEHAMISHA NA MAHELA YAO YOTE ....WANASUBIRI TU SIKU WAKISHAKAMUA KILA KONA WAACHIE BONGO YENU NA VUMBI...MAFISADI MGUU MMOJA UPO NJE MWINGINE UPO NDANI....AMKENI......BONGO YETU INA AMANI ...BONGO YETU INA AMANI KILA SIKU WAKATI MNALALA NA NJAA...I HATE THAT SAYING.

    ReplyDelete
  27. Halafu profesa "mbele" anatuambia lahisi kikwete ndiye anayetufaa.

    Na msomi mwengine "profesa Beno Ndulu" haoni kama ni kosa la jinai kwa yeye kuishi katika nyumba ya shiling billioni 1.4 katika nchi ambayo "per capita income" ni chini ya shiling 500,000.

    Alisema "hii nyumba siyo kwamba imekarabatiwa, bali imejengwa from the ground". To this profesa, that is enough justification to spend all that money in that way.

    I would rather have profesa Vulata than this profesa Ndulu, as at least Vulata would have some moral compass.

    Kama hawa ndiyo wasomi wetu, inabidi tuanze kujiuliza kama ni kweli kuna faida yoyote ya serikali yetu kuwekeza katika sekta ya elimu.

    ReplyDelete
  28. ka nimeshaanza kuogopa hivi kwani bongo hatuna mfuko wa dharura yaani tumezoea kuomba tu hata kujihami na majanga hatuwezi japo tulionywa kuwa kuna elnino inakuja yaani aibu mpaka libya itupe vihela mwe,je tukipatwa na majanga kama ya tsunani au earth quick.

    ReplyDelete
  29. JAMANI WATANZANIA TUUNGANE TUNALIWA NA VIONGOZI MAKANJANJA.PIGANENI.INATIA MACHUNGU KUSEMA SERIKALI HAINA UWEZO.MAFISADI WANAIPELEKA PABAYA NCHI YETU.HIVI HUKO SHULE ZINAZOWAANDAA WATZ ZINAPHD ZA UFISADI?MIMI NAAMINI MSOMI ANAPIGANA KUWEKA RECORD YA USOMI WAKE.ZAMANI HATA VIONGOZI WALIKUWA NA MOYO WA KUSHARPEN PROFFESSIONS ZAO WALIANDIKA HATA VITABU.LEO HII TZ PROFFESSIONA NI UFISADI,UFISADI,UFISADI.MSOMI ATAKUWAJE KIOO NDANI YA JAMII KWA KUWA MFANO WA UFISADI?KUNA GAP KUBWA SANA KATI YA MASKINI WA TZ NA MAFISADI WETU WA NCHI.UKITATHMINI BILLION 1.4 INAYOTUMIWA KUKALIWA NA NYANGUMI MMOJA TU UKALINGANISHA INGEZALISHA NAFASI NGAPI ZA KAZI ZA WATANZANIA UNAWEZA UKASHIKWA KICHAA.NCHI YETU INA MATATIZO YA KUSHINDWA KUCHAGUA.KILA MIPANGO IKIJA KILA MMOJA ANAANGALIA ATABENEFIT VIPI.NDUGU ZANGU TZ HAMUIJUI UFISADI UMETAWALA.NENDA MAWILANI MUONE JINSI WAKURUGENZI WANAVYOJIMEGEA NA WAHASIBU.NI VERY NORMAL KUWA MHASIBU LAZIMA AWE NA VIJIGARI NDO ATAJENGA NYUMBA NZURI HARAFU NDO ATAKUWA NA SAUTI NA HESHIMA.WHY NOT AFISA MAENDELEO YA JAMII.PESA ZA KODI ZETU NI ECONOMIC STIMULUS TOSHA KABISA TZ KU TAKE OFF ILA MIPANGO MIBOVU.USIMAMIZI FEKI,SHERIA HAZIFANYI KAZI,BASI UKANJANJA KILA KONA.HIYO NCHI NI BABU KUBWA IKIPATA WATU SMART.SASA HIVI WAZUNGU WANASEMA KABISA VI NCHI VYAO VIMEJAA WANAONA NEEMA ILIKO ILA SISI HATUIONI TUNAICHEZEA.ITS CRAZE,HIVYO VI NCHI VYETU VINA NEEMA YA HALI YA JUU.HIZI NCHI ZA WENZETU UKITEMBEA HATA JIWE HULIONI.HIVI MWAFRIKA ALILAANIWA KUTOKUWA MAKINI KWELI????.NI WAKATI MUAFAKA WA KUWA TUNAANGALIA BACKGROUND ZA HAWA VIONGOZI KABLA HATUJAWAKABIDHI NAFASI.UNAJUA MTOTO AKIFUNGIWA TANGU UTOTONI ASIJICHANGANYE AKIPATA NAFASI ANAKUWA DANGEROUS NDO HAO MAFISADI WENGI WANATOKA HUKO WALIKO SIJUI WAPI AKIPEWA RUNGU NDO ANASAHAU ALIKOTOKA.MIAKA NENDA MIAKA RUDI BADO TUNATAKA KUTAWALIWA TU.SHAME ON US.TUNAWATAKA MAFISADI WA RADA,LAZIMA WATUONYESHE MAFISADI WA BOT WAMEPEWA FUNDISHO GANI,LAZIMA NYUMBA WALIZOJIGAWIA ZIRUDI.NA UFISADI KEDEKEDE OTHERWISE TUTAWASHA MOTO TU.TUHAKIKISHE MATUMIZI YASIYOKUWA FAIR YAREKEBISHWE HAYO MASHANGINGI YAINGIZWE YAUZWE.JIANDAENI DAWA IKO JIKONI.

    ReplyDelete
  30. WAJE WAJENGE WENYEWE WASIIACHIE SERIKALI WATAZILA BADALA YA KUWAJENGEA NYUMBA BORA WATAJENGA ZA MABUA NA PESA KUJENGA ZA KWAO MBEZI BEACH. IT IS NOT A JOKE WAJE WASIMAMIE WENYEWE HIZO PESA WASIACHE ZIENDE BANKI KUU WAKAJIJENGEE NYUMBA OYSTER BAY ZA BILIONI MBILI JINSI WANAVYOJIPENDA! I HATE THAT HABIT OF SELFISHNESS, SHAME ON YOU SO CALLED ELITE.

    ReplyDelete
  31. Hahahhaa

    Hizi hela zinapitia serikalini...hizo nyumba hazitajengwa Kilosa ngooo...nyie hamuijui Serikali ya Tanzania.

    ReplyDelete
  32. Tanzania inahitaji Viongozi washupavu. Lakini hao hawana haki TZ. Yetu ni mambo ya unafiki tu yanendelezwa na nchi inaaibishwa na nchi ndogondogo kimaendeleo wakati rasilimali zetu zinajulikana duniani. Eti tunashabikia propaganda ya magazeti, na timu za nje.
    Walianza Masultani, kisha wakoloni, na sasa ni wkimbizi nchini kwao. Halafu tunaruhusu shetani atugawe kwa misingi ya udini, uchumi na ukabila. Tutaponaje? Wanaoteseka ni wanyonge, wanokaa ghorofani hawajui hilo mpaka yawatoke puani.

    Wananchi tokea zamani, tulinyonywa na kukuzaburi oya, tulijengee Taifa letu...

    ReplyDelete
  33. Wadau eeeeeeeeeeeeeeeeeehh! wakati umefika hawa wababaishaji tuwapige chini!! Viongozi wetu wengi wananunua kura ili wafanye ufisadi inakera sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!! Na ukiona sheria zipo wanaofanya makosa hawachukuliwi hatua hawa jamaa wanatufanya sisi ni watoto na wanadhani nchi hii ni yao wanasahau kwamba ni yetu, tuendelee kuwakosoa nasi tukipata nafasi tuwe mifano ya kuigwa!!! Tatizo la Kilosa ni kwamba hakuna viongozi ambao wana dhamila ya dhati kabisa ya maendeleo ya wananchi, kwasababu tatizo la mafuliko ya kilosa lilikuwa ni muendelezo wa mafuliko ya miaka ya nyuma ambayo yalivunja daraja la waenda kwa miguu na magari, likabaki daraja moja tuu la traini ambalo likawa linatumika na wote, mto ulibadili muelekeo na kingo vilivunjika na pia kina cha maji kikapungua kutokana na kuongezeka kwa mchanga, sasa nashindwa kuwaelewa hawa jamaa zetu wanaoitwa viongozi hawakujua kuwa mafuriko yatakuja??? kwao halikuwa jambo la umuhimu maana linawaathiri walalahoi tuu, Hoja yangu hapa ni kwamba mafuliko ya kilosa yangeweza kuzuiliwa kama uongozi ungeweka kipaumbele maana ni tatizo lililo anza tangu miaka ya nyuma, sasa hata daraja la reli limevinjika hakuna connectivity. Inakera sanaaaaaa, watu wanachekacheka tuuu, na kuvaa mabuti na kupiga kerere za misaada na kujidai wameguswa sana!! shame on them!! Nashindwa elewa kwanini tusiweke sheria kuwa kiongozi akishindwa kutimiza malengo flani aende jela then tutapata viongozi wa kweli na sio wababahishaji. Shwala la facebook ndio watanzania wengi walivyo wanahisi ni umaarufu kuabudu nchi nyingine (hawa ni wale ambao hawajui nini kuwa mtanzania- shame on them).
    Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  34. GADAFI wewe ndio BABA wa AFRICA ndio alama ya AFRICA ndio WIMBO wa AFRICA na ndio AFRICA sio Gaidi kama wengine wanavyodai,Hongera sana kwakuonyesha uzalendo,kip it up.sisi tunakukubali wewe mwanamapinduzi,mnaonaje wadau tufanye maandamano mpaka ubalozi wa libya Nchini kuonyesha shukurani zetu kwamsaada tuliopewa tusiishie tu kutoa maoni kwenye mtandao,Ankal fanyamambo tukatoe shukurani zetu,ikishindikana maandamano basi hata wawakilishi kutoka kwawananchi tuwachague waende,kazi hiyo tunakukabidhi wewe Ankal.

    ReplyDelete
  35. Mnaoandika kwa herufi kubwa mnaboa; ni sawa na kutupigia kelele!

    ReplyDelete
  36. Hakuna kitu kibaya kama wananchi kukosa imani na serikali yao. Maoni yote yanaonesha jinsi gani wananchi wasivyoiamini hata serikali yao. Something must be done Tanzania kwa kweli. Huko tuendako pabaya, Viongozi wetu wanatuangangusha wanakuwa watawala zaidi ya uongozi na ujanjaujanja mwingiiii. Mtu akifulia ndiyo anajidai mkereketwa wa chama ili apate Ubunge au uwaziri aweke mambo yake safi Inaumaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  37. tungempelekea Gadafi ujumbe kwamba tulikuwa nayo hiyo hela, ila ilibidi tumjengee nyumba Gavana wetu, kwa sababu hawezi kukaa kwenye nyumba ya bei ndogo, ni mtu muhimu sana!
    na mdau unaetusema sie wa nje tunasikitika kuhusu Haiti, kwa taarifa yako mimi nimetoa mchango kwa Wycleaf na wiki ijayo ntatoa kwa Red cross, na sitoi kwa kilosa ng'o, hela si serikali yenu inazo za kumjengea gavana? nitoe mchango wakati wabunge wananunuliwa maprada kila mwaka, miradi hewa imejaa na hela ya serikali inaliwa na mafisadi mchana mchana na mnaona na hamna cha kufanya. sahau mchango wangu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...