Mshindi wa jumla kwa masomo yote nchini na kuwa mshindi wa kwanza pia katika masomo ya sayansi kwa kupata "A" katika masomo yote ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2009 Imaculate Mosha, akipokea zawadi yake ya Kompyuta aliyopewa na Chuo cha Clever Tourisim & Hotel Management Hotel kutoka kwa Afisa Elimu Mkuu Wizara ya Elimu Bi. Doroth Mwaluko katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo , Imaculata pia alikabidhiwa shiligi 100.000 kutoka kwa chuo hicho.

Immaculata Mosha akiangalia zawadi yake
Juhudi, ufundishaji mzuri wa walimu, na malezi bora ya wazazi ndiyo siri kubwa ya mafanikio ya mwanafunzi bora wa kidato cha nne kwa mwaka 2009 nchini Tanzania, Imaculate Mosha.

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limemtangaza, Imaculate Mosha(16) kuwa ni kinara wa matokeo hayo, amewabwaga watahiniwa wenzake 315,151 waliofanya mtihani huo. Msichana huyo amesema, hakuna kitu cha ziada kilichompa matokeo hayo zaidi ya hivyo.

“Ni furaha kubwa sana kwangu, namshukuru Mungu, wazazi na walimu kwa hili kwani bila wao na jitihada zangu binafsi hakika nisingefikia hapa nilipofikia,” alisema Mosha mjini Bagamoyo muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo hayo.

Mosha alipokea matokeo hayo muda mfupi baada ya kutoka katika chumba cha mtihani katika Shule ya Sekondari St. Marian iliyopo Bagamoyo alipokuwa akifanya usaili pamoja na wanafunzi wengine wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu.

Mosha ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa Resto Mosha wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro na mama Agatha Mosha Mhasibu wa NSSF mkoni humo.

Mwanafunzi huyo kinara kutoka shule ya sekondari St Marian alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi 84 waliofanya mtihani huo mwaka 2009 shuleni hapo.

Akielezea historia yake ya mwenendo wa masomo yake darasani Mosha, alisema, nyota yake kishule ilinaza kung’ara tangu akiwa kidato cha kwanza shuleni hapo muhula wa pili aliposhika nafasi ya kwanza darasani.

“Nilianza kidato cha kwanza na katika mitihani ya muhula wa kwanza nilikuwa mtu wa nne darasani, niliongeza bidii na mwisho wa mwaka nilikuwa wa kwanza hadi namaliza kidato cha nne darasani sikuwahi kuachia hiyo namba,” alisema Mosha.

Amesema, katika mitihani ya mchujo wa kidato cha pili yeye alishika nafasi ya 7 Kanda ya Mashariki jambo ambalo pia lilimsukuma kufanya vizuri zaidi.

Mosha aliyezaliwa katika Hospitali ya taifa Muhumbili, Mei 6 mwaka 1993 alianza elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Ann mjini Morogoro na baadae kuanzia hapo darasa la kwanza hadi la tatu alipohama.

Darasa la nne alihamia katika shule ya Msingi Mukidoma iliyopo mkoani Arusha alipo malizia darasa la 7 mwaka 2005 na baadaye kalijiunga na sekondari ya St. Marian mjini Bagamoyo.

Mosha anasema, anamuombva Mungu amsaidie katika masomo yake ili ndoto yake ya kuwa mhandisi wa mitambo(Mechanics Engineer) itimie.

“Napenda sana hapo baadae niwe Injinia, hivyo nitaongeza bidii na kumuomba Mungu sana anitimizie hiyo ndoto yangu,” alisema Mosha.

Akizungumzia maisha binafsi anasema miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni vile ambavyo watu wanaweza kumhukumu mtu kutokana na mwonekano wake wa nje.

“Sipendi sana watu ambao wana 'judge the book by its cover' bila ya kujua undani halisi wa mtu mwenye kama anaendana kweli na muonekano huo.

Akiwa ni msichana mwenye kupenda sana kula wali nyama kuliko vyakula vyoyote, pia hupendelea kuvaa suruali na ndiyo vazi ambalo hulipenda na kinywaji chake kikubwa ni soda iitwayo Fanta.

Pia anapenda kuwausia wanafunzi wenzake hasa wasichana kutojihusiha na vitendo visivyo faa katika kipindi cha shule kwani anaamini kuwa ndiyo msingi mbaya wa maendeleo yao shuleni.

“Mimi naamini kila kitu kina wakati wake, ukifika nitafanya hivyo ila kwa sasa sijawahi kujiingiza katika vitendo vya anasa na nawahusia wanafunzi wenzangu kuwa waachane na vitendo hivyo,” aliongeza Mosha.
--------------------------
Kwa niaba ya wadau wote, Globu ya Jamii inampongeza Imaculate kwa fanaka hiyo katika masomo na kumtaka alenge alipofikia baba yake. Pia inawaasa vijana wengine walio mashuleni waige mfano huu
-Michuzi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Mie nimetokea wa 315,151 Watu weweeeeeeeeeeeee mie ndio wa mwisho. Kimaro.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana sana mdogo wangu Emmaculate. Unefanya wonders ila tu nakushauri sana kuwa usijisahau hata kidogo maana, unaanza ukurasa mpya kabisa wa academics na baada ya hapo tena utaingia ukurasa mwingne wa Unversity level. Kaza mwendo na wala usije kata tamaa. Utaona tofauti kubwa sana ila usikate tamaa. Utafikia tu ndoto zako na iwapo Munbgu atapenda kuzibadili kiasi basi usimbishie, fuata mwelekeo wake maana yeye anakujua tangu ulipozaliwa, Kikubwa kuliko yote ni SHIKILIA IMANI YAKO NA MTEGEMEE MUNGU SANA". Ibilisi ana nguvu pia ila ukiwa unamtegemea Mungu yeye hana nguvu juu yako. Epuka kula na kufuata mtu yoyote usiemjua vema maana si wengi wapendao maendeleo yako na ya wazazi na ndugu zako. Kaza Mwendo na kila la kheri.

    ReplyDelete
  3. Ankal, habari za shughuli.
    Vipi huyu mshindi mbona wanampatia zawadi ya kizamaani sana? Siku hizi computer ni flat sreen and slim...huu mchogo ataubebaje hata kwenye bweni hana pa kuweka...waache kujifanya wametowa zawadi kama hiyo kwa mtu ambaye amefanya vizuri kwenye masomo yake...zawadi kama hii ya kizamani haina motisha kwa vijana wengine...wadau mnasemaje?
    Mdau wa kudumu,

    ReplyDelete
  4. Halafu Miduvi mingine inathubutu kusema Wachagga wamependelewa. Tufanyeni kazi jamani na kupeleka watoto shule si kuzubaa, waChagga wanachakarika halafu tunabaki kushangaa!

    Hongera sana binti. Na M'Mungu akujaalie upate hiyo kozi ya Engineering unayotaka!!

    ReplyDelete
  5. mmh kakaa kisomisomi.

    ReplyDelete
  6. Here is the simple theory I came up with: Professor + Accountant= Genius

    Good Job Emaculata!!!

    ReplyDelete
  7. Go Ima go. I can see you out there among the great scientists of our country in a few years to come. Congrats...

    ReplyDelete
  8. Imaculata mwanangu, HONGERA SAAAANA. mimi nimefurahi sana kwa ushindi wako, hiyo ndio dalili inayoonyesha kuwa wanawake tukipewa nafasi tunaweza. wanaumeee kuna ubishi tena?jibu ni hakuna. nimefurahi sana kwa sababu ile dhana ya kuona wanawake kuwa sisi ni watu wa kuishia tu form 4 na kupata kazi za ualimu, ukarani, sijui receptionist, HAKUNA, SASA MWENDO NI KUSAKA UINJINIA KWA KWENDA MBELEEE. WANAWAKE JUU? WANAWAKE NA ELIMU TUSONGE MBELE TUSIRUDI NYUMA EEEE.

    ReplyDelete
  9. By looking at the shape of her head you can tell Manka is smart.
    Congaratulations, keep it up, and keep on dreaming big.

    ReplyDelete
  10. Ni kweli usije ukajisahau halafu ukaacha kusoma kwa bidii bado unasafari ndefu,nakumbuka enzi zetu kuna jamaa mmoja alitoka form 4 na one point seven akasifiwa sana na idara zote akaendo ilboro form 5 and 6 akatoka na zero,hakuamin na watu hawakuamin pia wakamshauri arudie mtihani kama private candidate akatoka na zero tena.teh teh.

    ReplyDelete
  11. Hongera sana, ila anaonekana kama mkubwa vilee? Yaani haonekani kama ni 16 yrs. Mimi nidhani yupo 24.

    ReplyDelete
  12. Ningependa na mimi nimtumie zawadi. Je Michuzi tutume katika account gani#. Ninataka kutuma kama "Anonymous person". Ningeshukuru kama tungeweka account maalum kwa vijana kama hawa! Mungu akubariki Imaculata na akuepushe na vishawishi vya aina yoyote ile.

    ReplyDelete
  13. Hongera Sana Binti...ongeza bidii maana huko A-Level moto wake sio mdogo.

    Zawadi ni zawadi wajameni acheni kunyanyapaa..lol

    ReplyDelete
  14. Hi Michuzi,
    Mimi pia nataka nimzawadie..naweza kupata contact yake?

    ReplyDelete
  15. Hivi mnajua bei ya mtungi ni ELFU AROBAIBI TSHS 40,000. Zawadi yake Wizara ilibidi imlipie ada ya miaka miwili ili aongeze bidii zaidi kwenye masomo. Huu mtungi utamsumbua wakati akifunga shule. Flat ni rahisi sana.

    Mdau wa mabox USA

    ReplyDelete
  16. hongera binti kwa kujitahidi,lakini ukumbuke hiyo ilikuwa ni jezi tofauti na uwanja tofauti kama ulivyosema mwenyewe ulikuwa wa 7 kikanda na sasa ni wa 1 kitaifa. sasa ujue huko A-level mambo yanaweza kugeuka kama hutakaza kamba. ila kuhusu ndoto za kuwa muhandisi wa mitambo angalia sana,ndoto zingine zinaweza kufanya ujute baadaye. go for it if that is what you realy want!lakini kama ni kwasababu umepata div 1,7pts basi ujuwe maisha ni tofauti kabisa unapokuwa una ya kabili alone tofauti na unapokuwa katika kundi likikushangilia kuwa hongeraa hongeraa. natumaini when te time comes you will make an informed decision and choice.
    iwish you good luck.
    mdau

    ReplyDelete
  17. Hongera mdogo wangu, mafanikio mema mbeleni. Ila I am just wondering what happened to Mr President na wizara yake because this was not it four years ago. What's happening? St Francis nao sijui ndo vipi.. and I would suggest you consider IST..just food for thought!

    ReplyDelete
  18. I am dissapointed na hiyo zawadi. Zawadi ni zawadi but kwa msichana kama huyo kapiga bao nchi nzima halafu anazawadiwa kompyta ya kizamani hivyo? Wabongo wanapenda sana kutumia migongo ya watu wengine ili nao waonekane wa maana. If they were serious wangemzawadia hata latest laptop ambayo at least ni mobile kulinganisha na huo mdesktop wa kizamani.

    ReplyDelete
  19. zawadi ni zawadi ila hii mhhh!mbona ni zile za kizamani, Hata chibiriti alishabadilisha yake na anaenda na wakati...........!

    ReplyDelete
  20. hongera binti... ila kaka michuzi, hiyo zawadi duu, wangewapatia kina mama wanaofanya biashara ndogo ndogo nyumbani kwa sababu haina haja ya kubeba. sasa binti akifunga shule hapo shughuli. lol.

    ReplyDelete
  21. haaaaaa i can just see it baada ya father bayo na matusi yake akili lazima iingie kichwani unataka one tena bora urudi huko huko wish u lucky binti ex marian waanzilishi

    ReplyDelete
  22. SAFARI NI NDEFU VISHAWISHI NA VIKWAZO NI VINGI, KUSOMA VIZURI NA KUFAULU VIZURI SI AKILI TU INAHITAJI MAMBO MENGI YAKAE SAWA, MIMI NILISOMA NA JAMAA MMOJA MZUMBE SECONDARY SCHOOL MIAKA HIYO YA 47 ALIKUWA KICHWA KWELI, SIKUMBUKI HATA SI MTIHANI, TEST, QUIZ AMBAYO HAJAWAHI KUWA WA KWANZA TOKA FORM ONE HADI FOUR FOUR, UKIMUULIZA SWALA AKUELEWESHE UTASEMA KWA NINI HAKUWA MWALIMU WETU, FORM FOUR ALIKUNG'UTA "A" ZOTE MASOMO YOTE, AKAENDA PCM AKAKUNG'TA "A" ZOTE HUYU BWAA WALA AKWENDA KOKOTE ALIKWENDA CANADA KUSOMEA UANDISI WA MAJENGO TENA HAPO BAADA YA KUKATAA YEYE MWENYEWE UDSM NA INDIA AKISEMA HAWEZI KUSOMA HAPA WALA INDIA ATASOMA WEST. HAKUMALIZA ALIKULA DISCO NA MPAKA LEO HII NI MTU WA MITAANI HAPO KARIAKOO NA SISI AKINA KAJAMBA NANI TULIKUWA TUNASHIKA NAFASI ZA 20 KWA KWENDA MBELE TUNA PhD SASA TENA ZA HUKO HUKO WEST.

    SO DADA YANGU KUWA MAKINI SANA SI NA MASOMO TU NA MASWALA MENGINE AMBAYO YANACHANGIA KUFANYA VIZURI KIMASOMO, HUITAJI AKILI TU KUFANYA VIZURI UNAHITAJI MAMBO MENGI YAKAE SAWA ILI UFANYE VIZURI. SO BE BROAD MINDED ON ALL CONTIBUTORS FOR GOOD CLASS PERFORMANCE

    ReplyDelete
  23. Hongera dada, ila nadhani hiyo zawadi wangekupa kimya kimya maana duh, mtungi bwana!. mabweni yenyewe si unajua yalivyo? Ushauri wangu ungeiacha tu chumbani na huko bwenini uingie na Beckhouse 1&2,Tranter,kina Rogers Muncaster,Nelkon& Parker,kina Tom Duncan n.k. Labda wangekupa LCD monitor sio Cathode Ray Tube tena sio flat screen. Siku hizi unjinyoosha tu na Liquid Crystal display ambayo kwa dada inamlinda macho yasiharibike

    ReplyDelete
  24. Unajua waTZ tunachekesha. Huyu binti wasifikiri hana akili. Mpaka anakuwa namabari wani si mchezo. Sasa hiyo kompyuta jamani.!!! naye anaiona ,lakini kwa kuwa ni binti mwenye hekima ameonyesha kuifurahia ili asiwavunje moyo muendelee na ujanja wenu. Wamechukua ile mbovu amabayo hawaihitaji eti wanampa zawadi.Waende University Computing Centre wapate ushauri kuhusu kompyuta bora ya kumpa mtu zawadi. Sio huyo yenye kichogo.

    ReplyDelete
  25. Jamani tuseme ukweli: wachagga na wahaya kwa elimu wanajitahidi. Pamoja na kuwa Nyerere aliwanyima uongozi ni sawat tu. Maana ukimpa mahaya urais wahaya wote watahamia ikulu, na nchi italazimiswa kubadiri makabila yote wawe wahaya. Ukimpa mchagga hapo ndio kabisaaaa. Hela zooooote bank kuu zitaondoka. Sasa immculate kazana uwe injinia hakuna cheo kingine mwanagu kwa mchagga katika nchi hii. labda uwe rafiki wa rais atakayekuwa madarakani ndio utapata cheo zaid ya uinjinia

    ReplyDelete
  26. Hongera sana na usijisahau kabisa. Mdogo wangu alifanya vizuri sana form four, form six akafeli vibaya sana.

    jingine shule zifundishe lishe bora wali wa nyama na fanta achana navyo. Bp na kisukari vitakukimbili soon wee bado mdogo...Child obesity sio nzuri

    ReplyDelete
  27. Hongera.
    Ila Mechanics sijui Mechanical Engineering unayotaka naomba naomba na kukusihi ufikiri mara ya pili!

    ReplyDelete
  28. Ukweli this is a old computer, a genius like her does not diserve it. Find her a modern one

    ReplyDelete
  29. congrats my dear,

    Mwenyezi Mungu akubariki na uzidi kumuomba yeye ktk mipango yako yote. Usikate tamaa ya wewe kuwa mechanics engeneer,kwani unaweza. fuata nyayo za kaka yako Domi ambaye naye ni engeneer.

    All the Best.

    ReplyDelete
  30. Hongera sana mangi mwenzangu...
    Kusema kweli zawadi ni zawadi, ila hapa wamekuonea na wamedharau maana ya zawadi ni nini.
    Zawadi kwa kitu ni kitu mabacho hakijatumika wala kufunguliwa, bora basi hata wangekupatia fedha kiasi kadhaa, lakini hii ni mbaya sana nduguzangu.

    hao watu nao wamekosa akili, na wanataka tu kupata jina kwa dizaini isiyofurahisha, na hakika wenyewe itafika point kukumbuka na itawauma sana hao watoaji zawadi hiyo.

    Mangi usijali, unajua tena utakuwa na uwezo wa kununua yako hapo baadae na ukawapatia hao waliokupatia zawadi toto mpya kabisa kwa kuashukuru kwa zawadi yao.

    Ukihitaji laptop, wewe niko razi kukutumia laptop kwaajili ya masomo yako, ni kiasi cha kuandika msaada katika tuta tu na michuzi tunamuamini saanaa, hivyo tunauhakika mzigo utafika pila shaka.

    ReplyDelete
  31. safi sana sana,,,binti buluza wavulana wooote bongo adi waingie akili.nipedna sana mabinti kama nyie msiotaka michezo tumia muda wako shuleni vizuri sana na Mungu usimsahau

    kuna wale mabinti wa Tambaza kule nao wanatesa vibaya-vibaya safi sana,jamani somesheni kwa bidii na muwaendeleza sana watoto wa kike km uyu ni faida sana kwa wazazi na taifa

    watoto wa kike oyeeeeeeeee!!

    ReplyDelete
  32. hongere miss wachagga ndo wenyewe
    hata mwalimu nyerere alitoa hiyo.
    madau ujerumani.

    ReplyDelete
  33. Hiyo zawadi imepitia (mchakato) process zote za ununuzi wa umma (PPRA) kwa hiyo I can tell you siyo Tsh 40,000/= kama mdau mmoja alivyosema hapo juu ila zaidi ya 2.0m. Kama unabisha kaulizie wizara ya elimu kwenye risiti zao utaona mwenyewe amount. Mgeni njoo mwenyeji apone

    Pia hapo naona wazazi ni muunganiko wa "vichwa" vilivyotulia lazima lazima offspring nayo itulie upstair. Kama unabisha hebu muoane watu ambao hamjaenda shule uone kama utatoa zao la aina gani. kiazi

    ReplyDelete
  34. Hawa watakuwa walipewa hela ya kununulia zawadi wakaila wakaishia kununua hicho kimeo hapo. Kha!!!!! Inamaana halishindwa kumtafutia hata laptop ya bei rahisi? Watu wengine bwana.........

    ReplyDelete
  35. Mechanics/Mechanical engineering!! Nakuomba dada yangu, jaribu kufikiria electrical, telecomunication, au computer engineering.etc Mechanics dada yangu kimeo kwa sasa.........

    ReplyDelete
  36. watanzania tunapenda kuosha vinywa bila kutumia akili. hao waliotoa zawadi, wao hiyo kompyuta mnaiita mtungi ni maili kubwa, maana wao wamejinyima hata kuanzisha chuo hicho. Zawaidi sio lazima kuwa mpya, binafsi niliwahi kuata zawaidi toka wak dada ambayo alikuwa anaitumia...binafis nilitafsiri kuwa huu ni upenmdo mkubwa kwani amejinyima. Kwa hiyo Hongera sana Clever Tours & Hotel Mgt. Kutamba kwa upiga box na pesa ipo kibao, wenzako hapa Bongo, pesa inakuja kwa taabu, kama sio mwanachama wa EPA.
    acheni unafiki.

    ReplyDelete
  37. MIMI NIMEKUWA NA BOY FRIENDS TANGU NIKIWA FORM ONE, LAKINI FORM FOUR NIMEPIGA ONE POINT 11. HAKUNA FORMULA YA MAISHA. KWANZA NIKIWA HIVYO NAONA SHULE NDIYO INAPANDA ZAIDI KWA UPANDE WANGU. MUDA WA SHULE NI SHULE, MUDA WA MAMBO MENGINE NI WA MAMBO MENGINE.

    TUTAKUTANA FORM FIVE.

    MIMI NATAKA KUWA LAWYER.

    ReplyDelete
  38. sasa hilo kabati hata atakapoenda shule atalibeba? yani mmeshindwa kufikiria kumpa laptop? nyie mmemtumia huyo mtoto kujipigia debe muonekane wa maana kumbe zero, its dissapointing kwa sababu huyo binti anastahili zawadi lakini siyo hilo kabati, muone haya mnunulieni laptop mpya! shame on u tourism shule uchwara.

    ReplyDelete
  39. 16yrs?! duuuuuuuuh

    ReplyDelete
  40. Kufaulu umefaulu..lakini je serikali inafahamu uwepo wako hapo baadae?mimi mwenyewe nilikuwa mkali sana.lakini cha ajabu wale mambumbu ndoo wanapeta Tanzania.shida ikitokea baada ya tusolve wenyewe ..tunaenda kuombaomba

    ReplyDelete
  41. kuna mdau kanichekesha sana hapo 16 yrs duuu.ni kweli wenzetu wanasomea ukubwani......halafu kremu sanaaaaa....hongera

    ReplyDelete
  42. Hii zawadi imetolewa na hicho chuo cha mama anayetoa zawadi na sio wizara ya elimu kama wadau walivyo hoji hapo juu.
    Hongera sana mdogo wangu. Safari bado ni ndefu kaza mwendo na mungu atakusaidia.
    Siku hizi top student haendi United World college tena? Enzi sio 47 kulikuwa na hizo nafasi.
    Aim high and spare no pains to reach the standards.

    ReplyDelete
  43. Huyu Imma nimeona jina lake anarudi tena Marian. Hata mimi namshauri arudi tena kule kule, maana ile shule balaa>Ila kwa hiyo fani unayotaka kwenda kusomea ni jambo zuri sana maana mafundi mchundo hatuna wa kutosha Tanzania. Ila nina uhakika hayo ni mawazo ya utoto ukishapata vyeti vyako si ajabu kusikia umekua mkuu wa wilaya,au mbunge wa jimbo fulani. Mfano si unaona vichwa kama waheshimiwa kina Kapuya, Sarungi, Mwinyi,Lipumba, Mwandosya, nk wote wamekimbilia siasa na kutupa vyeti vyao kabatini.

    ReplyDelete
  44. Congrats Imma.your hard work paid girl!n congrats to Marian (by the way Ankal, ts Marian and not St.Marian), for wndrful results.God bless the school and the founder Fr. Valentine Bayo.

    ReplyDelete
  45. Sasa si angalau apewe new laptop, anapewa computer ya kizamani...halafu pirika tena hadi waandishi akikabidhiwa computer iliyopitwa na muda :D

    Give her something usefull, a nice brand laptop prefferably IBM or so with dual core processors.

    Anyways, congrats girl you did well.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...