WANAHABARI TUMEPATA PIGO KUBWA MNO KWA KUONDOKEWA NA MKONGWE WA HABARI NCHINI MZEE REGINALD MHANGO ALIYETUTOKA JANA MAJIRA YA SAA TISA ALASIRI KATIKA HOSPITALI YA HINDU MANDAL JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA TOKA JUZI JUMATANO KWA KIHARUSI (STROKE) ALICHOKUWA AKISUMBULIWA NACHO KWA MUDA MREFU.
MACHOZI YANANIDONDOKA NINAPOANDIKA HABARI HII KWANI REGGIE, KAMA TULIVYOKUWA TUNAMWITA WATU WOTE, AMETUFUNDISHA KAZI NA KUTULEA WADAU WENGI WA FANI HII KWA KIPINDI CHOTE CHA MAISHA YAKE. HE MENTOR AND WAS A FATHER FIGURE TO SO MANY OF US...
REGGIE AMEFANYA KAZI TANZANIA, ZIMBABWE NA MALAWI KATIKA NYAKATI TOFAUTI, LAKINI ALIKAA KWA MUDA MREFU DAILY NEWS KABLA YA KUHAMIA GUARDIAN AMBAPO ALISTAAFU NA KUBAKI NYUMBANI KWAKE MAGOMENI MTAA WA MIKUMI AMBAKO NDIKO MSIBA ULIPO.
MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.
HABARI ZAIDI ZITAFUATA BAADAE

NIKIWA NA REGGIE NYUMBANKI KWAKE SIKU FILAMU YA BONGOLAND II ILIPOKUWA INASHUTIWA AMBAPO KUNA KIPANDE KILICHEZEWA HAPO KWA REGGIE AMBAYE ALIPOOMBWA NA MWANDAJI BW. JOSHUA KIBIRA HAKUSITA KUKUBALI

DA'CHEMI CHEMPONDA ALIYESHIRIKI KATIKA BONGOLAND II AKIWA NA REGGIE WAKATI WA KUSHUTI FILAMU HIYO
REGGIE AKIPEANA MIKONO NA KAIMU MHARIRI MTENDAJI WA DAILY NEWS NA HABARI LEO MKUMBWA ALI HUKU BOSI WA ZAMANI WA GAZETI HILO MZEE ULI MWAMBULUKUTU AKIWA KATI YAO, WAKATI WA MAZISHI YA MKONGWE MWINGINE WA HABARI, MAREHEMU HAMIDU BISANGA KWENYE MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR MWAKA JANA. ILIKUWA NADRA SANA KUMUONA MAREHEMU REGGIE AMENUNA NA WOTE TULIMPENDA ILA MOLA KAMPENDA ZAIDI
REGGIE AKIWA NA ALIYEWAHI KUWA MPIGA PICHA MKUU WA DAILY NEWS ADARSH NAYAR (SHOTO) MZEE MWAMBULUKUTU NA MCHORAJI WA KATUNI ZA KALIKENYE DAVID KYUNGU KATIKA MAZISHI YA HAMIDU BISANGA.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa, pole sana, may Love of God and His wisdom guide you through this hard time. I went to school with Milka,pale Mzizima secondary school

    ReplyDelete
  2. Bosi wangu mpendwa Reggie jamani! Nalia. Namshukuru Mungu kuwa niliweza kumwona 2006/2007 na 2009 nilipokuwa Tanzania. Reggie alikuwa na utu roho ya upendo hakuna mfano.

    REST IN ETERNAL PEACE REGGIE. WE WILL MISS YOU DEARLY BUT YOU IMPARTED GREAT KNOWLEDGE AND WISDOM IN US AND WE WILL PASS IT ON!

    ReplyDelete
  3. buriani mzee wetu,ama kwa hakika ulimwengu wa habari utakukosa daima kwa ushauri madhubuti.
    poleni wafiwa na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akawepeni subira ktk kipindi hiki kigumu.
    BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

    ReplyDelete
  4. Poleni kwa msiba wanahabari. Pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa.
    Apumzike pema Reggie.
    Amin.

    ReplyDelete
  5. mungu amlaze mahala pema peponi alikuwa mtu mwema sana nasema hivi sio sababu amefariki nasema hivi kwa moyo mmoja kwa jinsi nilivyomfahamu poleni sana James,aika na Reggiejr

    ReplyDelete
  6. Dah poleni sana familia ya Mhango mungu ailaze mahali pema peponi roho ya baba yenu ,,Pole Jems pole Reggie na Aika
    ...Chulu frm The Netherland

    ReplyDelete
  7. RIP MZEE REGGIE WE PROMISE WE WILL FOLLOW YOUR STEPS

    ReplyDelete
  8. May God rest mzee's soul in peace. The late Reggie Mhando taught me alot of things during his tenure as managing editor of The Daily Mail.

    ReplyDelete
  9. RIP Mzee Mhango, nimekuwa mwanafunzi wako pale Guardian na ulinielekeza kazi kama mtoto wako tofauti na wahariri wengine wewe ni baba, poleni familia na wanahabari wenzangu wote. RIP

    ReplyDelete
  10. Jamani michuzi badilisha hiyo t shirt yako, jamani kila siku ni hiyo hiyo tu, pole najua utakwazika ila ukweli ndio huo.

    ReplyDelete
  11. Jamani michuzi badilisha hiyo t shirt yako, jamani kila siku ni hiyo hiyo tu, pole najua utakwazika ila ukweli ndio huo.

    ReplyDelete
  12. pole sana James(A GUY CALLED LONDON) pole sana Regi Jr, poleni sana vijana wote wa Mikumi, enzi izo BIG APPLE na AFTER 7, CHULU wa Holland mbona AIKA MHANGO ameshafariki kitambo

    ReplyDelete
  13. Mungu amlaze pema peponi...alikuwa ni mwalim mzuri kwa wanahabari nilipokuwa THE GUARDIAN! Poleni wafiwa..yote ni kazi ya Mungu.

    ReplyDelete
  14. YES WE LOVED HIM BUT GOD LOVES HIM MUCH AND WE"LL ALWAYS TREASURE HIS WISDOM....Infact i wanna say Thanks to every one who participated on one way or another to make sure that MR.REGGIE goes in peace especially through prayers and condolences..MAY GOD BLESS YOU ALL......And in the case of AIKA MHANGO's death i can say it's a rumor because she is alive and she works at IMMIGRATION TANGA.....@Says James Mhango's Daughter,AIKA MHANGO's Niece,REGGIE MHANGO's First Grand Daught.er

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...