Kaka mithupu pole kwa libeneke.

Mie ni mdau wa blog ya jamii. Napenda kuishirikisha jamii na kuisisitiza iwe makini wanapokuja sokoni hapa Mlimani City jijini Dar. Tayari mwanajamii mmoja akiwa anapata huduma gari yake iliibwa katika parking za hapa Mlimani City. Wakati anatoka ndiyo anaona gari inakata kona kuelekea Sam Nujoma Road na haikuwa rahisi kuiserve.

Nimejiuliza jamani hivi VIJIKADI tunavyopewa tunapoingia humu sokoni kumbe havina msaada hata kidogo. Basi ni vyema uongozi wa humu uweke vibao vya 'PARKING AT YOUR OWN RISK' ili kieleweke maana hata hawa askari wao naona hawasaidii kitu. Wametanda kila mahali kazi yao nini basi?

Imeniuma sana na sidhani kama hii kampuni ya ulinzi hapa inamsaada wowote kwa hili. Wawekee wadau kaka ili kuwapa angalisho.

Ni mimi Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Pole sana mdau inasikitisha...kile kikadi alikiacha kwenye gari au kashuka nacho?? maana wengi hupenda kuacha kwenye gari.Hata hivyo security za pale ni mbovu mimi mwenyewe nimeshaibiwa side mirror pale kwenye parking na hata hicho kikadi sidhani kama kinasaidia.

    ReplyDelete
  2. Vikadi havisaidii kitu. Mwizi anaweza kutengeneza vya kwake, kwa size ile ile na kuvichakaza kidogo ikibidi, akavitumia vizuri tu. Mtu anapotoka mlinzi hupokea kadi wakati mwingine gari likiwa kwenye mwendo mdogo na hakuna anayeisoma kujiridhisha kuwa ni yenyewe. Na hasa kama kuna msururu wa magari itakuwa ni kupokea haraka na kujiandaa kupokea nyingine bila hata ya kuitupia jicho. Something must be done now!

    ReplyDelete
  3. hapo mlimani city watu washalalamika sana,wizi umezidi na kuna walinzi sijui wanafanya nini? inasikitisha sana kuona sehemu kama hiyo inavibaka na mijambazi ya magari,uongozi wa mlimani city hawajali coz hawaathiriki na huo wizi maanake wateja hawapungui, NAWASHAURI WATEJA MGOME KWENDA HAPO MUONE KAMA HAWATASHUGHULIKIA HIO ISSUE YA SECURITY....WATANZANIA TUSIWE KAMA KONDOO TUNABURUZWA TUSIMAMIE HAKI ZETU....tukigoma wiki tu bila kwenda hapo mlimani city watachukua hatua.

    ReplyDelete
  4. Hatari kweli wakati mwingine ukitaka kuingia unaambia kadi zimekwisha hivyo unaruhusiwa kuingia bila kadi. Sawa wakati wa kutoka hata kama ni mwizi hawawezi kukugundua. Ila msipende kuacha kadi kwenye gari ondokeni nazo ingawa pia haisaidii ila mlangoni anaweza kuzuiwa kwa maswali.

    ReplyDelete
  5. Kwa macho yangu nilishuhudia gari inatoka bila kukabidhi kikadi, jamaa baada ya kufika mbele kidogo akajishtukia akaamua kuirudisha kwa kupiga reverse, hiyo ni moja. Siku zingine tunaingia pale bila kadi nadhani wadau mmeshajionea hilo. Tatu, geti zote ziko wazi muda wote hivyo hakuna strong access control pale labda kama itatokea liibiwe gari la mmoja wa wawamiliki wa eneo hilo naamini security itaboreshwa kuliko ilivyo sasa ya vijana wetu yaani security guards kushinda juani wakigawa na kupokea vikadi huku mageti yakiwa wazi tena yamefungwa na kamba kabisa! Kuanzia sasa mimi nitaanza kwenda na Bajaj japo hawaziruhusu ziingie ndani itapaki nje na gari langu litakuwa salama car wash linapatiwa usafi

    ReplyDelete
  6. Ankal,tuletee taswira za ile gari iliyopaa ikatua juu ya mti pale Mbezi darajani,maana kila mtu anaizungumzia.

    ReplyDelete
  7. Kikadi Hakisaidii... lazima watafute security measure ya aina nyingine. The same applies to all the hotels and parking lots in the country. Nina suggest CCTV cameras, lakini hata hivyo bado cjui kama hao maaskari wataweza kuzitumia kuIdentify the owner of the car.

    Naomba wadau waje na mbinu zingine.

    ReplyDelete
  8. Da ile parking ya pale kawe darajani ingefaa sana pale mlimani city, nadhani magari yasingeibwa pale.

    ReplyDelete
  9. Mdau unaetaka picha ya gari iliyopaa nenda kwenye ippmedia gazeti la Nipashe ipo picha.

    Wahi mapemba kabla hawajaiondoa

    ReplyDelete
  10. KAMA UNAINGIA KWA KUPEWA KADI NA KUNA ULINZI THEN THE MLIMANI CITY HAVE LEGAL RESPONSIBILTY TO MAKE SURE THAT YOUR CAR IS SAFE, AND AFTER ALL IT IS THEIR PARKING GARI IKIIBIWA WANA KESI YA KUJIBU, NA KAMA UNAAMBIWA INGIA TU KADI ZIMEKWISHA WEWE GEUZA GARI YAKO NA UONDOKE WANATAKA KUKWEPA LEGAL RESPONSIBILTY.

    ReplyDelete
  11. Pole sana mdau, aah! mimi nilishaamua niwe naenda pale kwa taxi. That place is terrible!!

    Waliniliza power windows nikapata shida sana kupata tena za aina ile. The next time nimekwenda pale nimemaliza mambo yangu narudi kwenye gari nilikuta watu wawili wakiitazama gari yangu kwa chini. Shocked!!

    ReplyDelete
  12. 1.Walinzi wenyewe mishahara yao midogo kulingana na hela mteja anayowalipa wenye kampuni za ulinzi, hivyo wao wanacheza dili na wezi wa magari.
    2.Kuna siku ukiingia unaambiwa kadi zimekwisha, Je kwa muda wamefanya kazi hapo hawajaweza kukadiria wingi wa magari kwa siku au ndio mipango yenyewe?.
    kwanza wale walinzi wanatuchelewesha, wangeondolewa ili kila mtu apaki kwa dhamana yake mwenyewe, nakuambia tukimkamata mwizi, tunanyonya petroli tuna mwasha. itakuwa fundisho.

    ReplyDelete
  13. wADAU MI NADHANI NI KUSHINIKIZA UONGOZI WA SERIKALI NA MLIMANI CITY KUWEKA CCTV MAENEO KAMA HAYA KWA AJILI YA ULINZI.. MAANA KUNA SIKU ATATOKEA KICHAA ATATEGA BOMU BILA WATU KUJUA.. HIVYO NI HAKI YA RAIA KULINDWA WAO NA MALI ZAO.. NI JUKUMU LA SERIKALI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...