Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya mabao yao 6 waliyowafunga Toto Africa ya Mwanza katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom uwanja wa Uhuru jijini Dar leo
Jerryson Tegete wa YAnga akijaribu kumuhadaaa Tete Kang'anga wa Toto Africa. Chini Shamte Ali akijaribu kumtoka beki wa Toto Africa Juma Abdul
Kipa wa Toto, Hussein Katandula akiwa chini huku ,sha,uliaji wa Yanga, Boniface Ambani akiwania mpira.
Mshambuliaji wa Yanga, Boniface Ambani (kulia) akichuana na mchezaji wa Toto Africa, Aboubakary Mnyambegu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Uhuru jijini Dar leo. Yanga imeshinda bao 6-0.
Jerryson Tegete akiifungia timu yake ya Yanga Tik-Tak
Fred Mbuna (kulia) akimtoka mchezaji wa Toto, Maulid Haniu
Mshambuliaji wa pembeni wa Yanga,Nurdin Bakar akimtoka beki wa Toto Africa, Wiliamu Busweru wakati wa mchezo wa Ligi ya Vodacom uliofanyika leo kwenye dimba la Uhuru. Yanga ilishinda 6-0. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ushindi Mzuri sana ila Jamani tulikuwa wapi raundi ya kwanza?ona sasa Simba washatuzidi na kuwafikia!! sijiu!!
    Mwana Yanga halisi India.

    ReplyDelete
  2. Watani zangu wa jadi mbona zikija mechi za kimataifa hamuyafanyi haya mauaji?

    ReplyDelete
  3. Pole sana Mwana Yanga halisi,ndio imeshakula kwako na Yanga yako.Ni kweli kama ulivyosema Yanga kuifikia Simba kwa mwaka huu ni ndoto,labda mwakani ila kwa mwaka huu sahau kabisa.Kumbuka kuwa mpaka sasa Lunyasi tunahitaji pointi sita tu kujitangazia ubingwa mapemaaaaa!!!,we baki tu uking'aaa macho.Kwaheriiii!!!.Mwana Simba halisi India.

    ReplyDelete
  4. ADILI NA NDUGUZEFebruary 23, 2010

    Hiyo ndiyo Dar Young Africans. Swaafi sana. Yanga Yanga Yanga!!!

    ReplyDelete
  5. duuu chama langu lazima livunje record ya walugaluga tutashinda mechi zote...

    ReplyDelete
  6. jamani mbona tuko nyuma sana , yanga hii mechi yangi inacheza hapo dar sija wahi kuona hii dunia kote bora turudi kukule vituo,na sita bora sikutane dar, TENGA UMEKUA KAMA HUKUCHEZA MPIRA PROGRAM YAKO MBOVU NA AMKA ULIPO LALA MPIRA NI SAYANSI SIO UMAARUFU

    ReplyDelete
  7. kuku wako mwenyewe unamshikia manati!!!!. Toto waliambiwa mapema kwamba undugu wake na yanga ndio utamteremsha daraja.

    ReplyDelete
  8. ,,,,ivi kwanini wanaume wanasuka mabutu kama haya(sorry nywele) sana siku izi???,,,
    wake zenu wanyoe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...