Waziri wa afya na ustawi wa jamii Profesa David Mwakyusa akipokea zawadi toka kwa gavana huyo Sun Liang wa Jimbo la Zhangdong ,Nchini ChinaGavana wa Jimbo la Zhangdong,nchini China bw.Sun Liang akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.Mgeni huyo pamoja na ujumbe wake walifika Wizarani hapo kwa mazungumzo mafupi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa juu ya mkakati wao wa kujitolea kujenga kituo cha kutibu magonjwa ya moyo na upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Gavana Sun Liang (kushoto) akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa mara baada ya mazungumzo mafupi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hivi hatuwezi hata na sisi kujinyanyua kila siku tuna pewa misaada tu kama omba omba!!

    ReplyDelete
  2. NDIO BASI TENA TANZANIA INANUNULIWA TARATIBU, COLONIZATION IS BACK!
    KILA MTANZANIA NAOMBA ASOME HIKI KITABU HAPA, "China Safari: On the Trail of Beijing's Expansion in Africa"
    Mdau Mkereketwa

    ReplyDelete
  3. Kwa nini wajenge kituo kipya? Why dont they expand the Tanzania Heart Institute? Hivi kweli ni sawa wakati THI wanashida hawakupewa support na sasa tunakubali kujengewa kituo kipya. What about madaktari? Je wapo kuwahudumia wagonjwa???? Bado natafakari maana mambo mengine siyaelewi nchi hii....

    ReplyDelete
  4. ha ha... Tumeisha!

    ReplyDelete
  5. wewe ujui hata marekani inakopa na inadaiwa pesa nyingi sana kuliko hata tz unajua china inaidai pesa kiasi gani marekani siri ya pesa usitumie pesa yako mfukoni wewe kopa watz wengi hilo hawiliju wahindi kule mjini wote wamekopa tena hapahapa tz wakuacha ww unaduwaa cha msingi jiwekee mazingira ya kukopesheka haya by lyimo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...