KIWANJA CHA HEKARI NNE (4) KILICHO MAENEO TAMBARARE KIGAMBONI MWASONGA KARIBU NA DAR ES SALAAM ZOO JIJINI DAR KINAUZWA. KIWANJA KINAFAA KWA UJENZI WA SHULE, HOSTELI AMA CHUO NA ENEO HALIPO KWENYE ULE MRADI WA NANIHII...
BEI NI MILIONI 20,
MAELEWANO YAPO ILA SIO SANA KIIIVYO
MAANA ENEO LIKO BOMBA SANA (PRIME AREA), BARABARANI KABISA, NA BEI NI YA DUKANI.
SABABU YA KUUZA: NAHAMA NCHI
MADALALI WAKAE MBALI, HAIWAHUSU
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA KWA NAMBA
+255 716 1717 37
ULIZA JOE
au
katikati ya kiwanja
upande huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Kama ni Chekeni-Mwasonga, sema unauza shamba ni si kiwanja.mdau

    ReplyDelete
  2. Jamaa anawahi kubeba Box Kazi ya Ufisadi ishamshinda. Jamani changamkieni hataki mafisadi(madalali) waingilie dili. Mdau wa Brazil.

    ReplyDelete
  3. Sio unauza kwa sababu MTU WA MWISHO KUKUPINGA KESHAKUFA?? i mean we ndo umebaki KIDUME na HUNA HELA...anyways, nice area..ila bei unaua...unaweza nifanyie breakdown kwa nini umekuja na hiyo DOLA Elfu 20???????????

    ReplyDelete
  4. Mimi huwa sielewi. Ardhi ni mali ya umma.
    Sasa millioni ishirini ni compensation ya nini hapo pasipo hata na structure wala miti au mazao ya kufika kiasi hicho?

    Eleza vizuri au kuna kumfidia mtu ambaye ana makazi hapo?

    Hivi kisheria hii inakubalika na utalipa kodi ya hilo pato au niaje?

    ReplyDelete
  5. Ahaaa ni saafi sana hapa kwa uwekezaji ni poa kabisa.
    Lakini ushame nchi kwako ni kwako tu japo hakuliwi.

    ReplyDelete
  6. Ok...mimi sina uhakika hiki ni kiwanja au pori maana siyo shamba...halina hata kitu kimoja cha kuonyesha kuwa ni shamba....Lazima uwaambie watu kuwa huduma muhimu ziko mbali kiasi gani, shule, maduka, hospitali, umeme n.k...

    ReplyDelete
  7. teheheheee,sipakuingia kichwa kichwa,mwenye kupapenda awe makini,aende kwanza ardhi yeye mwenyewe ajirizishe na huo mpango wa mji mpya,aone kama hilo eneo liko salama.Maana wabongo bwana kwa kulizana hawajambo.Kama hilo eneo lina hati ,basi ziendane na hati halisi iliyoko wizarani,M20 kutapeliwa waweza kuwa kichaa ukamkasirikia michuzi bure kwa kutuwekea hii,kumbe ulitakiwa kuwa makini mwenyewe.

    ReplyDelete
  8. tupe data za urefu na upana wa kiwanja.. itasaidia kuelewa hasa ukubwa wa hicho kiwanja..

    ReplyDelete
  9. Eti madalali tukae mbali, hivi wewe unataka sisi tukale wapi? hebu nikabidhi mi hilo shamba nitaliuza kwa mil 25 then nakupa mil 20 yako unayoitaka,na kila mteja ninayemleta kuliona ananilipa elfu 40 ya kuonea hiyo ni yangu na mke wangu we haikuhusu kaa mbali nayo.Na kwa taarifa yako nimeshaanza kuwataarifu wateja wangu kwamba kuna kiwanja ekari nne ninauza kigamboni na kuanzia kesho naanza kula hizo elfu 40 za kuonyeshea watu. by Dalali Mwanyika

    ReplyDelete
  10. I am confused. It all looks like a virgin piece of land purportedly belonging to mankind. Just what gives one a right to claim ownership over a piece of land as his/hers, sale it at a price s/he wants and pockets the money? Some go as far as fencing it off barring "tresspassers" from coming anywhere near it. Is it a historical blessing - that is, getting there first - as did the white settlers in the New Lands and elsewhere?

    ReplyDelete
  11. Mkisikia Tsunami, mnauza viwanja!! Huko sio mahali pa kuishi sasa hivi.

    Mjenzi wa hii dunia anarekebisha foundation uko chini ndo maana Tsunami na matetemeko yanaongezeka. It is time to run to/for the hills.

    Tusishindane na Asili (Nature). Labda kununua hiki kiwanja kwa ajili ya kuweka mahema ya kambi (picnic etc etc) na sio kuweka majengo ya kudumu!!

    Hivyo bei makubaliano kwa kwenda chini!!

    ReplyDelete
  12. Sababu ya kuuza nahama nchi? Sema sababu ya kuuza nahitaji hela kwa matumizi mengine ya msingi zaidi au vipi.

    ReplyDelete
  13. Kigamboni kumeshauzwa..kwani nani hajui...Bush alishanunua hilo eneo lote.Hilo jumba halimdondokei mtu ng'oooooo.

    ReplyDelete
  14. bei sio mbaya ni nzuri sana,lakin mimi hizo sababu za kukiuza hazijanirizisha.

    ReplyDelete
  15. Wewe unauza heka 4 kwa sh 20m mim nahitaji heka moja tu ya kujenge nyumba yangu ya kuishi nikupe 5m unasemaje?

    ReplyDelete
  16. HONGERA SANA KWA KUHAMA NCHI UTUACHIE HUU UOZO WETU SISI TUSIO NA KWA KWENDA, UMEFANYA LA MAANA SANA KUAMUA KUCHANJA MBUGA, MJOMBA NENDA MJOMBA USIANGALIE NYUMA MJOMBA UTAGEUKA GUZO LA CHUMVI MJOMBA, MVUA IKIJA UTAYEYUKA MJOMBA

    ReplyDelete
  17. 20.MILIONI KINGAMBONI NA HIYO PULUSHENI AU WANAUZIWA WASIOSIKILIZA WALA KUSOMA TAARIFA ZA HABARI?

    ReplyDelete
  18. dunia inamambo, kama unahama ndiyo uuze bora usingetoa sababu mimi nataka kupanga hicho kiwanja chako unasemaje? je unacho kibali cha kufungua shule au wamekunyima ndiyo maana unakiuza?

    ReplyDelete
  19. mimi nakihitaji hiki kiwanja yakhe

    ReplyDelete
  20. mafisadi wanakimbia nchi sasa

    ReplyDelete
  21. Hilo ni Shamba sio Kiwanja ebo!

    ReplyDelete
  22. Sasa mkuu kama unahama Nchi si ungewaachia ndugu zako ili waendeleze kwa kujenga shule au chuo au hospitali?? Huko unakokwenda hakuna kazi ya kubeba mabox? kwasababu Tsh. 20m unaweza ukaipata kwa Miezi sita tu ughaibuni kama ukigangamala na box...Nakushauri usiuze hilo shamba kwa hizo sababu ulizozitoa. Lakini inawezekana ulilinunua kwa Tsh. 500,000

    ReplyDelete
  23. Kigamboni kulishauzwa, Kauziwa Bushi, na alipokuja safari ile alileta Cheki na aliikabidhi siku ile pale ikulu hadi mvua ikanyesha!!! tunasubiri pamoja na mambo mengine madogo madogo cheki iive tugaiwe hiyo hela...sisi wakazi wa kigamboni tunatembea kitajiri sasa hivi, njoo feri utuone wakati tunapanda na kushuka kwenye feri!!!Sasa wewe unayeuza hiyo ardhi ya Bushi utatucheleweshea mgao wetu

    ReplyDelete
  24. Sema mshikaji anatafuta nauli ya kwenda nje kama angekua nayo na balance ya kumwezesha atleast kukaa huko wiki 3 ,asingeliuza,manake angetakiwa akameki kwa kubeba box huko ili ainvest huku vitega uchumi vya maana kwa sababu ana eneo lizuri sana.HIVYO AMEFULIA NDIO SABABU YA KUUZA.say JAS.

    ReplyDelete
  25. Mie kuna mambo mengi yananitia huzuni kubwa. Hawa jamaa wanaouza ardhi, jee wanajua kuwa ardhi hiyo ni yetu sote na ilikuwaje aweze kuiuza na kutia pesa mfukoni kwake. Mtu akiuza nyumba naelewa kwani auza matofali yake aliyotoka jasho kuyafyatua au akiuza shamba auza jasho alilotokewa kwa kuvuta jembe. Dont sell our land what will happen to our children, you cant sell a piece of Tanzania to a chinaman or kaburu.I was amazed when I was in Scotland someone advertised, he was selling a river!
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  26. jamani kiwanja kinauzwa. untaka nunua, hautaki basi. una hla nunua, huna basi. sheria imevunjwa, nenda polisi. mbona longolongo nyingi wakati mtu anauza chake? mara umefikiaje dola elfu 20, mara ardhi ni mali ya serikali na domo jingi.

    ReplyDelete
  27. Huyu aliyetangaza hapa mwenyewe dalali. Kwani dalali hawezi piga picha na kumtumia michuzi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...