Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Prof. Jumanne Maghembe katikati akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa kuingia kidato cha tano (5) na katika Vyuo vya Ufundi Mwaka 2010 kwa Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani. Kulia ni Mratibu Msaidizi wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) Bw. Alpius Machage na Shoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Sekondari Bw. Charles Philemon. Shughuli hii ilifanyika kwenye Ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. MBONA MATOKEO YENYEWE HAKUNA? KUNA MTU ANAEJUA NITAYASOMA WAPI? NAOMBENI MSAADA.

    ReplyDelete
  2. USIKIMBILIA KUTANGAZA MATOKEO KWANZA,WALA KUBADILISHA VITABU NA MITAALA BORESHA KIWANGO CHA ELIMU KWANZA.SHULE NYINGI KATIKA JIMBO LAKO HAZINA WAALIMU WALA VITABU.

    ReplyDelete
  3. Si unajua mambo ya kibongo bongo yapo slow mpaka mchana huu bado hawajayarusha, subiri labda jioni ya leo utayapata kwenye: www.necta.go.tz. Ila mpaka muda huu bado hayajarushwa.

    Mdau

    ReplyDelete
  4. hata mimi siyaoni nikiingia necta.go.tz napata hii msg "Warning: Visiting this site may harm your computer!
    The website at www.tanzania.go.tz contains elements from the site www.tanzania.go.tz, which appears to host malware - software that can hurt your computer or otherwise operate without your consent. Just visiting a site that contains malware can infect your computer."

    ReplyDelete
  5. watanzania tusipende kulaumu, wewe Anonymous wa 03;23;00, mbona matokeo yapo kwenye website ya wizara ya elimu.
    Kumbuka kuchagua ni wapi mwanafunzi aende sio kazi ya baraza la mitihani(NECTA) bali ni kazi ya wizara ya elimu moja kwa moja. NECTA kazi yake ni mitihani na matokeo yake.

    ReplyDelete
  6. www.moe.go.tz

    ReplyDelete
  7. matokeo yanapatikana website ya ministry of education
    http://www.moe.go.tz/

    mdau
    Chapaulaya-Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...