Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa akiwatoka mabeki wa timu ya Somalia, Mohamed Hassan Ali (kushoto) na Hussein Ali Robile wakati wa mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanocheza ligi za ndani (CHAN) uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Stars imeshinda 6-0.
Kipa wa Somalia, Kamal Ali Omer akiwa amekaa chini baada ya kufungwa goli la sita
Kipa wa Somalia, Kamal Ali Omer akiuangalia mpira uliopigwa na Uhuru Seleman ukiingia Wavuni wakati wa mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanocheza ligi za ndani (CHAN) uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Stars imeigaragaza Somalia kwa idadi ya mabao 6-0.
Kipa wa Somalia, Kamal Ali Omer akiwa amekaa chini baada ya kufungwa goli la sita.magoli hayo yamefungwa na mchezaji John Boko (dk. 17), Kigi Makasi dakika (dk.33),Mrisho Ngasa (dk 55), Erasto Nyoni (dk. 74), Muss Hassan Mgosi (dk. 83) Nadir Haroub "Canavaro" akimalizia kwa kufunga goli la sita dakika ya 87 na kufanya matokea yasomeke 6-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Somalia.
Picha na Francis Dande wa Blog Ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. du kweli vibonde

    ReplyDelete
  2. Hongereni stars, lakini msibweteke

    ReplyDelete
  3. Kwa jinsi nnavyoifahamu Bongo na Wabongo wenzangu, hapo tutapiga kelele na kuisifu Staaz na maksimo (likiwa moja ni Ksimo au Liksimo) kama vile tumeifunga Kameruni au Bolivia. Maksimo juu!!! ndiyooo, juu ... juuu, ... juuu zaidiii, ... kaziiii!!!

    Kwa timu kama hiyo, ilibidi Staaz wavunje rekodi ya mabao katika futiboli sio kuishia magoli sita tu. Wachezaji ambao wako kwenye ligi msimu mzima ni aibu kupata mabao sita tu dhidi ya timu ambayo nchi yao haina ligi, wanakusanyana vijana kutoka kambi ya wakimbizi na kufanya timu na kuiita ya taifa ambayo inawatunishia misuli Taifa Staazz! Aibu. Aibuuu, ... aibu kabisa!

    Hata Sifa Renjaaazz wanatakiwa kuwamiminia kapu la magoli wakicheza na timu kama ya Taifa ya Somalia. Eti mastaa wa timu za ligi za juu za Bongo wanafunga goli sita tu jamani? Liksimo inabidi lijiuzuru kabla ya mkataba wake kwisha, hata kama zimebakia siku nne tu kwa mkataba huo kukatika!

    Mkereketwa wa Nchi inayoteketea kila engo (afya, lishe, elimu,viwanda, uongozi bora, utamaduni, uchumi, maadili, miundombinu, na kila kitu)
    UGHAIBUNI
    DAYASPORA

    ReplyDelete
  4. SPMALIA HAKUNA NCHI WATU WAKO VITANI TOKA MIAKA 30 ILIYOPITA HATA MKIWAFUNGA MAGOLI 1,000,000 KWA ZERO NI SAWA TU

    ReplyDelete
  5. yaani mdau wa kisiju una majungu sanaaaaaaa!! wewe mwanga nini? manake hutaki kusifia kwenu kabisaaa?! but kumbuka dua la kuku alimpati maximo!!!! utashanga miujiza na huta kaaa ukaamini kwani imani yako ni ndogo yakuwaza majungu na fitna Ushindwe na ulegee!! mdau Dayaspora!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. aaah wapi mmepata mteremko kachezeni na cameron isipokuwa 4 oclock in the morning! hadi ze comedy waliirusha hii hawana lolote harembwi mtu kwa kombe lipi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...