Idara ya Huduma kwa Wateja ya kampuni ya
AGASTA ya Japan ikiwa bize kutoa huduma ya
kwa wateja kutoka sehemu mbalimbali duniani

Hapana shaka unaamini vitu viwili kuwa kweli wakati ukisaka kitu. Kila unapozidi kukisaka, ndipo fursa ya kukipata itapojitokeza. Kitu cha pili ni kwamba kila siku kuna kitu kipya. Kuna wakati hapo awali ilibidi uridhike tu na ukipatacho na kukikosa kilicho bora. Leo kuna fursa kibao za kuchagua. Mojawapo ni kuwa na fursa ya kuchagua magari ya bei poa yanayouzwa kupitia www.picknbuy24.com ambayo kila siku kuna mambo mapya. Hii inamaanisha kuwa ni tovuti linalokupa mambo mapya kila siku kuhusu magari ya bei poa.

Inafanyaje Kazi?
Kuna njia kadhaa ambayo unaweza kunufaika nazo. Mojawapo ya uhakika ni kwenda moja kwa moja www.picknbuy24.com. Ukifika hapo utakuta kuna njia rahisi ya kupata ukitakacho. Kama kuna aina ya gari inalitafuta wewe kazi yako ni kubofya katika sehemu ya aina (category) iliyo upande wa kushoto ya ukurasa mkuu. Mfano unataka Jeep. Basi we bofya tu juu yake Hapo unapata magari yote ya Jeep yaliyopo dukani. Ama kama hutaki kupekua aina mia za magari zilizopo, basi tumia njia mbadala iliyopo juu ya tovuti hiyo, na utapata ukitakacho

Njia ingine ya kutafuta gari ulitakalo ni kwa njia ya kubofya jina la aina ya gari ulitakalo. Ama unaweza kutafuta kwa kubofya mwaka, muundo ama hata jina la gari. Matokeo ni ya haraka na ya moja kwa moja hata kama huna ufahamu wa unachokitaka tokea mwanzo.

Kisichokuwepo leo hapa, huenda kikawepo kesho
Kanuni ya ununuzi ni kwamba vitu huwa vinahitajika sana ila huwa si vingi sokoni. Hivyo endapo utalikosa gari unalolitaka leo, haimaanishi kwamba gari hilo halitokuwepo kesho. Ndio kusema ukibofya sehemu ya magari ya leo (new arrivals) kuangalia kuna gari gani jipya sokoni

Cha Ziada
Kuna mengi ya ziada katika tovuti hiyo. Mbali na kuwekwa mambo mapya kila siku na njia zake rahisi za kusakia magari, utakuta hutuma kwa wateja safi kabisa. Unaweza kuwasiliana na wafanyakazi wa huduma kwa wateja yenye weledi ambao watakusaidia kupata gari ulitakalo. Hivyo basi, endapo huna muda wa kuhakiki kama gari ulitakalo lipo ama halipo katika tovuti, watoa huduma kwa wateja wapo tayari kukusaidia.

Tena basi unaweza kupata vipuli kadhaa vya gari unayonunua. Hii ikimaanisha unaweza kuongeza maagizo ya nini unataka zaidi kwa ajili ya gari ulitakalo. Ikutaka kipuli tofauti na gari ulilochagua ukiuliza unaweza kupatiwa pia, tokea aina ya DVD player hadi spea za magari yanayouzwa.

email: pboffer@picknbuy24.com
URL: http://www.picknbuy24.com
http://www.picknbuy24.com/sales2_tz.html?bnr_issa



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Biashara ni matangazo.. na Japan ndiyo jiko la Magari.

    Kuna wazalendo kadhaa ambao waniliwakuta wakijishughulisha na biashara ya magari pale Japan.. tukiweza kuwaunga mkono tutakuwa tumeisaidia Tanzania, kwani pesa hizo hizo ndizo zitarudi kwenya mabenki ya Tanzania na wananchi wengine watanufaika na mikopo.

    Ni kama jinsi wahindi na wachina walivyopata maendeleo kwa kasi kubwa kutokana na kusaidiana wao kwa wao kwa kununua bidhaa toka kwa wenzao.

    Hope Michuzi utaiona hiyo na kuiwekea post maalum ili tulijenge Taifa letu changa.

    ReplyDelete
  2. Sawa ankal kwa ujumbe huu.Tatizo kubwa ni hawa jamaa zetu wa TRA, wao hawajui kua magari huko yapo ya bei rahisi na watu wanashushana bei vizuri tu. Ukileta gari wanajua kila gari ni kuiuplift tu bei wao.Tuwaombe nao wawe wasome huu mtandao afu wajionee wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Michuzi huyo dada Violeth hapo juu kabisa ameongea maneno ya busara sana..
    Mimi naishi hapa Frankfurt Ujerumani na biashara yangu ni kuuza vinyago na vikorokro kutoka Africa-Tanzania..

    katika mtaa nifanyao shughuli zangu wapo wazungu pia ambao nao huuza bidhaa hizi hizi kama zangu, lakini utakuta wazungu wenzao hujaa kwenye mabanda yao na kwangu wanapita mmoja mmoja..

    Well, naelewa kuwa siyo kama ni Ubaguzi ila tu ni uzalendo wa kusaidiana wao kwa wao.. nashukuru sana Waafrica wenzangu huwaleta marafiki zao wazungu kuja kuniungisha... Ila naelewa ndo soko huria lilivyo.

    Nimeona hiyo kampuni uliyoitambulisha ni ya wajapan watupu, hivyo si vibaya kama tutawafahamu wenzetu waliopo huko Japan, ni vema tukawasiliana nao kwa hizo issue za magari,
    kwani kama alivyosema huyo dada hapo juu ni sawa kabisa, pesa hizo hizo zitarudi tu TZ na wengine watanufaika.

    Mungu tubariki pia sisi waafrika!!

    ReplyDelete
  4. Wee Anonym wa Tarehe Mon Apr 19, 10:01:00 AM,embu fungua macho na uzitoe zitongozitongo machoni kwako.

    Hao TRA wako katika biziness pia. Ni lazima watukwangue kiaina, na lengo lao kubwa ni kufanya waagizaji wa magari washindwe kuyakomboa halafu wanapigiana minada kwa dola 600 wao kwa wao kwa kila gari. Nani mjanja ndugu yangu?

    Uzalendo utachimbuliwa wapi katika nchi ya wajanja wachache hiyo? Ni bora kudayasporeka na viboxi na kisha kuidayaspora dayaspora yote uipatayo udayasporani!

    Dayasipora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...