Hi Ankal...Haapy Easter.
Naomba uniwekee hii kitu katika Blog Ya Jamii ili wadau wawenisaidia ushauri.
Ndugu zangu naombeni ushauri wenu wa kina, please be conviced that ushauri wenu ndiyo utaamua hili swali na si vinginevyo.Mimi ni kijana wa kike mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa nasoma chuo kimoja cha tiba hapa Tanzania.
Nina "boy friend" wangu ambaye ndiye mvulana wangu wa kwanza na wa pekee kuniingiza kwenye huu ulimwengu wa relationishp/love. Kwa sasa mtu huyo yuko masomoni huko Ughaibuni, akisoma masomo ya tiba pia moja ya majimbo maarufu nchini humo.
Boy friend wangu anafahamika hadi kwa wazazi wangu, ndugu zangu na jamaa na marafiki zangu wote, kwani alishatoa barua ya poza siku chache kabla hajaondoka nchini. Tatizo kubwa lililonifanya niwapigie magoti ni kwamba jamaa huyo hataki kutoa mahari kwa sasa, wazazi wanataka atoe mahari ili niwe na uhakika wa mume, ndoa na awezi kukabidhiwa "mzigo" rasmi.
Kila nikimwambia anadai ,elimu kwanza, ujenzi kwanza, maandalizi ya maisha kwanza. Ni kweli kuwa ananihudumia kwa kila kitu, anahudumia wazazi wangu, ndugu zangu kwa mambo mengi.
Hata account yake ya bank ya hapa nchini mimi ndiyo ninayoi-run,mashamba yake, ujenzi, wafanya wake, ndugu zake mimi ndiye ninaye wahudumia kwa yeye kunitumia dollars. Ananipa huduma kila mwezi, ananipigia simu asubuhi na jioni.
Hata chuo ninachosoma ni yeye mwenyewe alinitafutia na akanilipia hela na ananedelea kulipa akishilikiana na wazazi wangu. Anasema hatoi mahari kwa sasa maana ananitafutia shule nikasome huko nje, analipa school fees yake nyingi kwa sasa, anatumia hela nyingi sana kunishughulikia niweze kwenda huko nje kimasomo,anataka anituie hela nishughulikie passport ila me nastita, namzungusha ili kwanza atoe mahari .
Mimi binafsi nakubiliana nae, ila ni juzi tu wazazi wangu wamesema atoe mahari, kama hatohi hiyo mahari sasa hivi basi,huko nje nisende na nisitishe mahusiano nae na nitafute mwanaume mwingine.Nimempa hilo jibu akasema yeye hatobadilisha msimamo wake, anaweka elimu yetu ,ujenzi mbele zaidi kwa sasa na sio mahari.
Hela anayotuma kila mwezi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni zaidi ya mara tano ya mahari inayotakiwa, kitu kinanifanya niaamini kuwa uwezo wa kutoa mahari anao, ila ni uhamuzi tu. Ndugu zangu nipeni ushauri hapo, nimuache huyu mwanaume, nitafute mwanaume mwingine au nimfanyeje..???.
Thank you all for at least reading.
YOU HAVE A GREAT AND BLESSED EASTER WEEK END.
MDAU NJIA PANDA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 62 mpaka sasa

  1. hey mdada waeleze wazazi wako huwezi kumuacha huyu mtu wewe unafikiri utaweza kupata mtu mwenye roho nzuri kama ya huyu bwana jaribu kufuata anacho shauri inaelekea huyu jamaa mtu wa maendeleo sana ukipoteza bahati hii utaijutia ushauri wangu komaaa nae

    ReplyDelete
  2. sijawahi kuona mtu asie na akili kama wewe, yaani na akili zako unasema kabisa nimuache au la. muache uone joto ya jiwe utapata mtu atakutolea mahali lkn utajuta

    ReplyDelete
  3. Men always want to be in charge of their life! You have a bright future with him! Don’t push him!! Money is something else and commitment is something else! He doesn’t want to pay dowry because it doesn’t make any difference, besides, he is in Ughaibuini and you expect to be with him after schools if they think dowry will tie him to you that is a mistake, couples divorces even after many years of marriage!

    Let him take charge of your r/ship

    ReplyDelete
  4. Shosti mahari ya nini wakati keshakuoa! Kulingana na maelezo yako huna haja yakudai mahari maana umeshasema anawahudumia wazazi wako na ndugu zako isitoshe wewe ndio unacontrol kula kitu cha familia yake ikiwepo na account yake sasa tayari wewe ni mke, mnataka mahar ya nini! Wewe huna hata haja yakutafuta mwanaume huyo mbona mume tayari! Hao wazazi wako wafikirie mara mbili kitendo cha kudai mahari wanajitusi wenyewe kistarabu kama ni mimi ningewaeleza wakae kimya! Mtu anawahudumia mnadai mahari ya kazi gani? Kama rizki ipo ipo tu mamy! Ni hayo tu

    ReplyDelete
  5. dada naomba usinielewe vibaya ila naona wewe huna usomi wowote..... kwa maelezo yako nashangaaaa hiyo mahali inakusumbua nini wakati mtu yuko tayari kukuendeleza na bila shaka anakupenda....
    wangapi wanatafuta wapenzi wenye akili kama huyo mchumba wako???? mi nahisi wewe humstaili na uwaachie wenzako nafasi.
    Dunia ya sasa ni ya maendeleo sasa wewe umekalia mila za kijinga eti mahalii mahali kitu gani kwani akishaitoa una uhakika gani mtadumu ao ndio atakuoa maana anaweza akaitoa kukufurahisha...

    Embu acha ulimbukeni na tumia usomi wako...hakika ukimwacha huyo mtu hutoendelea na unaweza kupata shida maishani mwako...

    ReplyDelete
  6. we chakubimbi umbea huu ungeuleta kule u-turn ndo ungenoga kule mambo hadharani huku mzee wa libeneke atakuwa kipofu kusoma komenti za kusisimua huku si mahala pake si unajua tena komenti zikizidi kilo ankal anabana laivu we ilete u-turn utapata ushauri wa kina

    ReplyDelete
  7. Wewe utakuwa daktari wa hatari sana kwa wagonjwa wako (kama utamaliza medical school). Nina wasiwasi kuwa hutamaliza medical school. Nilipokuwa medical school niliambiwa kuingia medical school unahitaji IQ ya kuanzia 120. Sasa kama kweli una IQ angalau ya 120, huwezi kukosa jibu la suala lililo wazi kama hili. Wewe jaribu kumwacha uone. Fanya jaribio. Baada ya mwaka mmoja post hapa kwa Michuzi twambie nini kimekutokea.

    ReplyDelete
  8. JAMANI HAPA TATIZO SIO HUYO DADA, NI WAZAZI WAKE WENYE TAMAA!! AIBU SANA! YAANI TAMAA TUPU HAPO, WANAONA JAMAA YUKO NJE TUMLE, HAVITOSHI ANAVYO WAPA KILA MWEZI? BIBI UTAACHWA WEWE NA FAMILIA YAKO ISIYOKUWA NA UFAHAMU, HESHIMA KUBWA AMESHAONYESHA KUKUTOLEA POSA, HEE JAMANI! HELA HII! UMASIKINI TUU, WAZUNGU HAWANA MAHARI! NI LOVE TU, IKIISHA NDIO HIVYO TENA, LAKINI WAMATUMBWI MKE UNAENDA KULALAMIKA KWENU UNANYANYASIKA, WAZEE WANAWAZA MAHARI WALIOCHUKUA, WANABAKI KUKWAMBIA VUMILIA TUU!! EMBU AMKA DADA VUNJA HUO UJINGA,NA KUWENI NA JEURI YA HESHIMA, SIO KUJIAIBISHA HIVYO, JENGA MAISHA YENU, MSIKILIZE MCHUMBA HUYO UTAKAYE ZEEKA NAE, WAZEE WATAONDOKA WATAKUACHA WEWE NA DUNIA, ANGALIA SANA.

    ReplyDelete
  9. We mjinga usibabaike na mali na hiyo familia yako? Hawatosheki tu? Kuna mwanaume gani siku hizi anaehudumia familia ya mke au mchumba kihivyo?

    Sikiliza nafsi yako bwana acha ulofa hapa,nijuavyo mimi wasomi hawapaparikii ndoa tena hasa wewe wa 24. Maandalizi kwanza kama inawezekana, mwenzio amepiga mahesabu yakutosha ndo maana akatoa posa ambayo kimila nitosha kabisa.

    Wangapi wametolewa mali na wakaachwa? Acha ujinga weye!

    ReplyDelete
  10. Ndio muache mi nitatoa Mahali,wambie wazazi wako kabisa baada ya mahali kitachofuata ni watoto mfululizo na huduma nitakata, nyang´afu.

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli mawazo yake ni yeye na mungu anayajua yeye

    kingine ameshajisoma humu kwa hiyo
    mie nakupa hili

    anaweza kuwa anakutumia umsaidie kushughulikia shughuli zake as ni wewe tu anaamini hutolalamika au kumlia pesa. majina unaweka yake basi halafu siku moja anaweza hamua akuache as unamsaidia kwa sasa na anakuhitaji. silaumu wazazi wako wanaona mbali

    huyu kijana anaweza kuwa anakutumia yote itategemeana na majibu yake kwako roho yako isipoanimi maneno yake basi jua kuna jamboooooooooooooooooooo

    wanaume sio wakuchezea na mtu akiwa ulaya ni ngumu kupata mtu wa kumuamini kumsaidia mambo huko nyumbani bila kuwa na matatizo hivyo huyu anakutumia sababu anajua unampenda

    NAKUSHAURI ANDIKA MAKARATASI KATIKA MAJINA YENU WOTE 50:50 NDIO MWENDO

    ukilemaaa mwanamke mwingine labda anae huko atakuja enjoy jasho lako

    ndio anakusomesha anasaidia familia jua unalipa kwa kumsaidia...

    ReplyDelete
  12. wazazi wako wanataka mahari gani tena? shule anakulipia, matumizi ya kila mwezi anakupatia, anawasaidia wazazi wako na bado wanataka mahari? kwa nini wazazi wako wasikatae yeye kukutunza na kukulipia shule hadi pale akishakuoa? kwani hadi hilo kufanyika hayo ni majukumu ya wazazi wako. infact nadhani huyo jamaa adai rifandi yake kwa wazazi wako as soon as posible

    ReplyDelete
  13. We dada zero. Shukuru kwa ulicho nacho. Binafsi hata asipokuoa., hapo ulipo ushalamba bingo.
    Bwege

    ReplyDelete
  14. ObhwatasyoApril 04, 2010

    Asante kwa hii hekaya ya wewe mwenyewe kujilabel 'mzigo'.

    binafsi huwa sipendi kujipa 'mizigo' ya kufikirika!

    ReplyDelete
  15. We dada, waelimishe wazazi wako, na km hawaamini,then labda hao wazazi au ndugu wa kijana then wanaweza saidia kuhakikisha kuwa mwanao atakuoa,na wameridhia hilo.Mahari sio issue kabisa!!! We upate wapi mwananume akuamini na kukusaidia ww na wazazi wako na ndigu zako kihivyo and then bado hao wazazi wako wanashindwa kuona ukweli uko wapi!!!! mimi namuunga mkono huyo kijana kwa kuona mbele,elimu,ujenzi muhimu sana,Sasa km wawasikiliza wazazi wako, na hutaki kwenda mfuata aliko,then utaachwa na hapo ndo utajua thamani ya penzi.Wangapi bf zao wanaenda nje na uhusiano unakufa??? wewe anataka uende unasusua kisa mahari????????????? Tafadhali,think twice.

    ReplyDelete
  16. binti wazazi wapo sawa. hapo sio suala la ulafi wa mahari ila mila. huyo jamaa anawahudumia wazazi wako kama nani? kimila hatambuliki na wazazi wako wanaona aibu mbele ya wazee wenzao.

    kitu gani kinamsitisha jamaa kutoa mahali au kishika uchumba kama anaweza kutoa huduma zote unazotaja? naona huyo jamaa ana jeuri ya pesa na anaamini pesa yake inaweza wanunua wazazi wako wasifuate mila. aidha naona huyo jamaa anakutumia usimamie miradi yake kwa malipo mazuri wakati yeye hayupo nchini. pindi arudipo atakutosa huyo!

    nakushauri akili mukichwa, jitayarishe kwa lolote usije pata kichaa akijasema amebadili mawazo.

    ReplyDelete
  17. IF YOU AND YOUR PARENTS REALLY CARE ABOUT TRADITIONAL VALUES,STOP TAKING THAT GUY'S MONEY UNTILL HE PAYS DOWRY.OTHEWISE YOU NEED TO PAY ATTENTION IN CLASSES BECAUSE YOUR THINKING CAPACITY IS WAY TOO LOW AND YOUR REASONING ABILITY CANNOT EVEN COMPARE APLE TO APLE.GOOD LUCK.

    ReplyDelete
  18. HII NI STORY YA KUTUNGA, HAKUNA KITU KAMA HICHO DUNIA HII YA SASA.

    ReplyDelete
  19. WE DADA KISEBUSEBU KICHWANI HAZIMO. SASA UNAFIKIRI HUYO BWANA AKO HASOMI HII GLOBU?? HATA USHAURI SIKUPI. HIVI UNADHANI AKISOMA HII ATAJISIKIAJE? DUMB.

    ReplyDelete
  20. CUTIE upo sahihi kabisa , wee dada huyo mwanaume sio material, nina wasi wasi kuna kitu bado hana uhakika nacho kutoka kwako ndio maana anagoma kutoa mahali. Sasa mimi nakushauri yafuatayo, tafuta passport, waage wazazi au toroka mfuate huko ulaya, alafu ukaishi naye, ukiwa Ulaya naye mshawishi face 2 face atume mahali kwa ndugu zake ili wamtolee kwa wazazi wake maana unaishi naye tayari.

    Usipoangalia utamsaidia kwa kazi zake alafu uje utoswe, shauri zako haya kalagha baho, tumeshawatosa wengi sisi wa majuu

    ReplyDelete
  21. Ushauri wangu kata fungu katika hizo pesa za matumizi wape wazazi waambie mahari hii, uwazibe mdomo.

    Aaaala!

    ReplyDelete
  22. Ushauri wangu kata fungu katika hizo pesa za matumizi wape wazazi waambie mahari hii, uwazibe mdomo.

    Aaaala!

    ReplyDelete
  23. Huyu ni mmojawapo wa akina "SITAKI NATAKA"

    Ha ha haaaaa............

    ReplyDelete
  24. Dada yangu inabidi kuwa makini sana na huyu jamaa. Ndio anakusaidia na analipa shule na wewe ndio upo kidedea na ishu zake hapa nyumbani. Sasa kama mapene anayo mengi, na anakupenda sana, na anataka wote mfunge pingu za maisha, then Mahari sio ishu. Si atoe mahari halafu muendelee kuishi "happily ever after".

    Kitu kingine, kama yeye hataki kusikiliza washua wako kwenye ishu ndogo tu kama mahari, inaonekana ana madharau. Wazazi wetu bwana hata kama hawajasoma sana ila wana hekima na ni muhimu kufuata mila. Yeye anawatia aibu wazazi wako maana anakutumia kama kimada tu na wazazi wako wanapata fedheha mtaani.

    Mpe ultimatum, mwambie toa mahari kieleweke au unakula kona. Mwambie mahari is symbolism, it important for your parents and an assurance for you that he is gonna come back. Akileta ubishi mtose kama mwezi mmoja tu atie akili. Atakutafuta mwenyewe.

    ReplyDelete
  25. Wazee maoni yote ni mazuri ila anony 12:00pm,mimi naona amenena.Kutokana na mahelezo ya huyu binti tatizo kubwa ni wazazi wake wanaolazimisha mahari.Tatizo lake yeye mwenyewe ni udhaifu wa kushindwa kuwashawishi wazazi wake kuwa anampenda jamaa yake, anamuamnini na anakubariana na "life strategies" zake alizojiwekea yeye mwenyewe kwenye maisha yake an huyo mchumba wake. Dada, be stronger, do what you believe will be of helpful in your own life,convice your parents that this is the only man in this world you have and you will always have for the rest of your life.
    Good luck shost.

    ReplyDelete
  26. wewe mdada nina wasiwasi na elimu yako. hili swala wala halihitaji kumaliza kidato cha nne kulifikiria kwa makini. Siwalaumu wazazi kwa kudai mahari, wewe ndo unayetaka hiyo mahari. kama kuna mwingine umempata umwambie tu jamaa kuwa kuna mwingine, sio kuja kutudanganya sisi kuwa wazazi wanataka mahari.
    huyo kaka anakujali hivyo, unataka nini tena msichana? na kwanza wazazi wa siku hizi wakiona mabinti zao wana mtu anayemjali kama huyo wako huwa wanamshukuru Mungu. Unadhani huyo jamaa akitoa mahari ndo itamfunga kuwa nawe? tena ningekuwa wewe wala nisingehitaji kujifunga kwa mtu ambaye hayupo tayari kwa kifungo, ni hatari sana hasa kwako. wewe endelea kufanya yanayokupata kuyafanya na kusali ili (kama unampenda kweli) awe wako atakapokuwa tayari.
    Kumbuka dada ndoa sio kitu cha kulazimisha, mpe muda afikirie kwanza anachotaka kufanya then mtaoana. Kumbuka Mungu alipomuumba Adam alimpa kwanza kazi za kufanya (kuwapa majina wanyama wote), alipomaliza kazi zote then Mungu akamuumba Eve.
    Think for your future my dear, sio mahari.

    ReplyDelete
  27. Upewe nini tena. Watoto wa kiswahili mnawaza kuolewa tu.... sio vibaya. Jijenge kwanza, ndio uangalie mambo mengine. Kama vp mwache,ukutane na matapeli.... na wako wengi sana.

    ReplyDelete
  28. Wee binti unasoma ngumbaru au chuo cha tiba kweli?

    Mahari ya nini binti kama anahudumia na kulipa ada yako?tena wewe ni incharge wa shughuli zake zote pesa inapitia mikononi mwako wewe ndiye unawapa hata ndugu zake?

    Hao wazaqzi wako maskini sana nini?Vipi kama wewe umesoma kwa mnajiri wa maelezo yako huwezi kumwashauri wazazi wazingatie anachofanya huyo b/friend wako?au ndo mambo ya mila?

    Utamkose huyo bwana.Eti nimuache nitafute mwingine, unafikiri ni rahisi tu kutafuta mwanaume kama si kutombwa tu na kuachwa soremba.Au umeishapata mtu anakushaua ndo maana uko njia ya panda?
    Acha ujinga huo kama kweli unasoma level hiyo nisingetegemea uwe gizani kiasi hicho.

    ReplyDelete
  29. ..........."PAMBAFU SANA WEWE.."

    ReplyDelete
  30. Wewe dada wachana na huyu kijana mara moja, you are on the wrong lane.Tafuta mmatumbi mwezio huyu mzungu humuwezi kabisa.Mimi mwenzio ni mzngung,embe nipe contact zake fastafasta.Kwanza mimi passport tayari ninayo mkononi na sio ya kutafuta kama wewe.

    ReplyDelete
  31. dada mimi nakutahadharisha,tumeona wakina kaka wengi wanaokuja huku nje uvumulivu wao ni mdogo sana,wanakuwa na wachumba jina tu nyumbani wakifika huku wanabadilika wanasema fimbo ya mbali haiuwi nyoka,kama yuko serious kweli atoe mahali,maana kutoa mahali si kuoa siku hiyohiyo,mahali itawapa wazazi wako heshima.chao

    ReplyDelete
  32. Haya kweli ni ya kweli au umejitungia tu!! Dada kwanza kama kweli huo ni umri wako bado hujakomaa kuwa na mume, naona wewe kinachokusumbua ni materials yaliyopo sasa sio future yenu. Watu huangalaia future sio material yaliyopo sasa kwani yanaweza yakayeyuka. Huyo mchumba wako hii 100% right elimu kwanza na mnachotakiwa wote wawili ni kujenga misingi ya maisha. Inaelekea wazazi wako wanatamaa sana na materials ndo maana wanang'ang'ania atoe mahari sasa hivi kwa maana hiyo mpaka amalize masomo hiyo mahari itakuwa imeyeyuka na wakati wa kukaribia na harusi wazazi wako watadai mahari nyingine! Hebu achana na mambo ya mahari unachotakiwa sasa hivi na wewe ni kusoma na mjijenge kwani yote mnayoyafanya ni zaidi ya mahari kwani ni kwaajili ya future yenu. Acha ujinga na vipesa unavyovipokea wala visikusumbue ukifanya mchezo jamaa atatafuta mwingine na kukuacha wewe kwenye mataa.
    You need to grow up girl!

    ReplyDelete
  33. What is mahari seriously these days???????????tand I don't think it is that important. As long as you love and understand each other.Stand by your man.Mie naona dada umeshaanza anza kuwa na walakini na huyu jamaa yako ndo mana unaomba ushauri hapa.Ungekuwa unamuamini na kuthamini mchango huyo kaka anakupa katika maisha yako ungesimama na kuwaeleza wazazi wako kuwa wawape muda mjijenge kwanza.Usimwache mpenzi wako sababu ya shinikizo la wazazi wako, unless uwe na sababu zako mwenyewe.

    ReplyDelete
  34. PETER NALITOLELAApril 04, 2010

    DADA MI KWA MAHESABU YANGU YA CHAP CHAP. NAKUONA KAMA WWEWE MJINGA FULANI HIVI. UNANTIA KICHEFU CHEFU HATA KUSOMA KOMENTI YAKO. JARIBU KUMUACHA HUYO KAKA ULIONE JOTO LA JIWE. WATAMRUKIA MACHANGU KAMA VILE HAWANA AKILI. NA UKISHAMPOTEZA TENA HAUNA CHAKO, HUYO KAKA ATASAKWA HATA KWA DAWA YA RAMLI, WANAUME WA SHOKA KAMA MIMI WALIYOSOMA MUZUMBE NI ADIMU SANA. NADHANI WEWE HAUJASOMA KWENYE CHUO CHETU TUKUFU CHA MUZUMBE UNIVESITY YA CHUO KIKUU CHA KULE MOLOGOLO. WEWE NAONA UNARUKWA NA AKILI, NA KAMA NI RAFIKI ZAKO WENYE WIVU, INABIDI UJIPANGE NAO, KAMA KAWA MAJUTO NI NJUKUU, WEWE MSIKILIZE MAMA HETI UMUACHE HUYO KAKA UTALIONA JOTO LA JIWE... HAKI YA MAMA WATU WAJINGA. WEWE INABIDI UKAMTEMBELEE MWALIMU NDO UJUWE WEWE NI MJINGA

    ReplyDelete
  35. Dah Naona watu wengi humu wametoa Comments kwa kulingana na tamaa tu bila kuangalia uhalisia wa jambo lenyewe.Sidhan kama jamaa alilazimishwa kuhudumia wazazi na ndugu wa bint Yeye aliamua tu kulingana na sababu zake mwenyewe,so sidhan hilo linaweza kusababisha wazazi eti wasidai mahali.Na kama kweli huyo jamaa ana pesa kinachomshinda kutoa hizo pesa ni nini wakati anajua hiyo ni katika taratibu za ndoa?
    Kuwa makini Dada yangu na asikutishe mtu kuwa eti "MUACHE UONE",kwani ulipompata ulijua kuwa yuko hivyo?Qur'an inasema" Halita kupata Jambo,ila lile tu alilokupangia mwenyezi mungu......Surat TAWBA:51.So Kama uliweza kumpata huyo basi kuna uwezekano wa kumpata mwingine na si kwa uwezo wako ila kwa matakwa ya Mungu,usiweke tamaa mbele,kwa sbb inawezekana ni kweli kabisa kama walivyotangulia watu kusema kuwa anataka akutumie tu kumsaidia katika mambo yake lkn ili na wewe uridhike ni lazima akufanyie vitu fulani fulani na kwake si ngumu kwa sbb pesa anayo.Nakushauri usikubali kutoa mguu wako kwenda nje kabla hujaolewa.

    ReplyDelete
  36. Dada, nakusikitikia sana, na ungekuwa na akili timamu, yaani hili siyo swala la kuuliza, jibu unalijua mwenywe. mie naishi ughaibuni, wanaume kama hao ni vigumu sana kuwapata, ukimpata kama huyo shukuru mungu, lakini ukileta kujua, basi utajuta sana. wapo wasichana warembo sana hapa marekani, na hata nyumbani tanzania, na ili wale, hacha ya kwenda shule, ni lazima wauze uchi wao. wee bahati ikuijiye mara ngapi, ichezee basi uione ikikimbia tena kwenye macho yako.

    ReplyDelete
  37. Miss TZ 20XXXApril 04, 2010

    HUYU dada ana matatizo ya akili. Mimi ni miss TZ natamani tu Mungu anipe mtu kama huyo. Dada nakuomba tu namba ya huyo kaka siku mnaachana. Nyumbani kwetu hawataki cha mahari wala cha nini, kiasi tu cha kuonyesha ananipenda itawarishidha wazazi wangu

    ReplyDelete
  38. Michuzi, kuna wakati unatunga story kuchangamsha ukumbi, nini?

    1) Hakuna mwanaume anayeweza kufanya mambo yaliyoorodheshwa katika story yako.

    2) Huyu mwanaume kama yupo basi atakuwa anasoma medical school huku akibebea box lake Wall street. Vinginevyo hawezi kuwa na uwezo huo kifedha hata kama moyo wa kusaidia anao. Kuna vijana wengi tu wameshindwa kulipa karo zao wenyewe kwa kubeba box USA. Au kama wameweza ni kwa mbinde sana - wakati mwingine kwa kuahirisha masomo.

    3) Hakuna medical student mwenye akili tumamu ambaye ataomba aina hii ya ushauri.

    4) Hakuna mzazi yeyote mwenye akili timamu ataomba mahali kwa binti yake mdogo ambaye yuko medical school bado. Kama ni uhusiano unatakiwa uwe uchumba. Na ndoa itafuta baadae.

    5) Hakuna mzazi mwenye akili timamu atakayefanyiwa mambo makubwa hizi na mkwe mtarajiwa halafu akata kuvunja uhusiano wa aina hii.

    Nadhani Michuzi na wadau mmenipata. Ankal usinibanie comment tafadhali.

    ReplyDelete
  39. wee mdada ukianza kuwa kicheche na kiruka njia, shauri yako. mume wako tunamjua sana. nabii yohana johni mashaka ni jina kubwa ukiteleza tu, lazima ule tope. Unadhani wadada millioni ngapi wanatamani hizo western union kila mwezi? gari nzuri na nyumba masaki? wangapi wanatamani hadhi uliyonayo? nadhani kikubwa ni wewe kwenda kanisani kuomba na kujitizama upya. una matatizo fulani jaribu ukaombewe yaani heshima kwako imekwisha. wewe ni mpuuzi sana, heti ni muache? jaribu basi uone watakavyomng'anga'nia. unazania unamfanyia nabii favor, yeye ndo anayekufanyia feva kukupa maisha ambayo hauyawezi. mjinga ni mnjinga tu. dada wewe ni zaidi ya mjinga, wewe ni mpumbavu

    ReplyDelete
  40. US-BLOGGERApril 04, 2010

    US Blogger)

    Dada nadhani itakuwa vyema sana ukaenda kumuona Dr. Manyuki. Mimi nina hela sana lakini siwezi kumpa changudoa hela zangu bongo, hiyo sahamu

    mimi philosia yangu ni kwamba out of sight ni out of mind. Kama ni ndugu zako, basi waambie maamuzi ni yako wewe kwa hiyo wakwa wanakulazima basi wanakuharibia fucha yako

    Dr.US-Blogger
    Alumni Oxford University
    School of Economics

    ReplyDelete
  41. WEE DADA KICHWANI ZERO. NAOMBA TIGO YA HUYO MKAKA

    ReplyDelete
  42. dada jaribu kumuacha huyo kaka hata kwa mwezi uone.mim nitakuunganisha na kaka yangu ambaye yuko tayari kufanya harusi na kila kitu chini ya miezi miwili

    thubutu !!!!

    ReplyDelete
  43. dada wewe ni limbukeni. mimi ni mmoja wa wadada warembo hapa jijini. nafanya kazi tena nzuri tu kwa hadhi za kitanzania, lakini maisha kama hayo unayopewa na mchumba wako yapo zaidi ya uwezi wangu. ma boifrendi ninaowapata hapa mjini ambao ndio wanajiona wako juu, hawawezi kunisaidia hata kulipia hada ya shule. nakuhurumia sana sana unapokuwa na akili finyu kama hiyo huku unajidai umeenda shule. hawa siyo wazazi wako. wanaokudanganya ni ndugu zako wenye wivu kuona unaolea na dakitari. wanachotaka ni kwamba udidimie kwenye ufukara kam wa wazazi wako

    ReplyDelete
  44. Majuro mara nyingi ni mjukuu. Hata Kama mtagombana na mchumba wako, vumilia kwani mvumilivu hula mbivu. Nawatakia kila la kheri. Pia nampongeza nchumba wako kwa kuwa na msimamo imara. Kwa hiyo ndo uamue lakini usilfanyr maamuzi ya kijinga

    ReplyDelete
  45. May be hii scenario sio ya kweli, huyu dada ni wa kubuni tu. Mdada gani atajiuliza mara mbili mbili kwa jamaa kama huyu.Wabongo bwana mtu anakuudumia wewe na familia yako alafu ati unadai mahari kwa mabavu.

    ReplyDelete
  46. Hivi weye wajiona mzuri kuliko hao wazungu anaowalamba kila siku, hadi umdengulie mtoto wa mwanamke mwezio. Kalaga bao,ukijakustuka utakuta mume si wako tena. Teheee tehee tehee kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  47. binti, wanaokuponda ni wale wanaokuonea wivu kutokana na msimamo wa familia yako. watu maarfu na wenye majina kmakubwa kama joni mashaka siyo watu wa kuoa ni watu wa kutoka nao tu. kwa hiyo ningelikuwa ni mimi, huyo kaka ningeachana naye kabisa.kwa sababu hataki kukulipia mahari, ushauri wangu ni mzuri sana

    ReplyDelete
  48. katika kundi la watu wanaofaa kuitwa matahira, wewe humo.unajua ni wanawake wangapi wanatamani nafasi kama yako????
    Basi muache kaka wa watu aendelee na maisha yake tuone kama siku tatu haujakimbia kupiga magoti. nyie wanawake ni wajinga sana muda mwingine

    ReplyDelete
  49. muache nimchukue wewe ukamtafute mzungu. mijitu mingine bwana unafikiri wanaume wa aina hiyo kupata ni rahisi, pengine hadi uzeeni kwako hautopata kutia macho yako kwa mwingine kama huyo, mjinga
    najua utarudi kutuadisia paukwa pakawa....

    ReplyDelete
  50. Mimi sina cha kukushauri leo,kama ni ushauri umeishaupata, ila wa Alfonso huweka maanani, maana amesumarise maoni yoote ya glob juu ya ombi lako.Kama wewe ni muhumini wa dini ujumbe umeupata.

    Kwaheri.

    ReplyDelete
  51. Duh..Damn..Lol..Umm..!!! Kumbe humu kuna Miss Tz 20xxx..!!. Jamani wewe miss wachana na huyo dada kichaa, mimi niko ughaibuni, na ninaprovide kuliko hata huyo jamaa yake,please come to me babe.
    Wow..!!.

    ReplyDelete
  52. Wanaosema hii story sio ya kweli ni ya kufikirika,sio kweli, naamini ni ya kweli kwani hata mimi yaliwahi kunikuta kama haya haya ya mwenzetu.Kumbuka hakuna definition mahalumu ya neno "love",love is a too complicated stuff,with unlimited bounderies.Ila inasikitisha kuona mpaka karine hii bado kuna wazazi wana mind mahari kiasi hiki hata kufikia kusitisha mahusiano ya vijana wao.

    Mdau.
    USA.

    ReplyDelete
  53. USA Blogger you have missed the point.Kama umesoma vizuri mahelezo ya huyu dada amesema huyu jamaa ni boy friend wake, ameishaimtolea hata barua ya poza na si Changu Doa kama ulivyosema wewe.Hivyo wameisha vuka kwenye stage ya uchangu doa,they are processing the mariege protocol.So, ukimuhita huyu dada changu doa unakuwa umemkosea, ni mchumba wa mtu.(You have to apologise for this,otherwise you are convicted of assult).

    ReplyDelete
  54. PESA ANAYOKUTUMIA NI MARA TANO YA MAHALI INAYOTAKIWA? SASA KUNA UGUMU GANI HAPO? CHUKUWA HIYO PESA ANAYOKUTUMIA MTAFUTE JAMAA WA MCHUMBA WAKO MUELEZE STORY HII NA MPEHIYO PESA AKAWAPE WAZEE WAKO, KITU KINGINE KAMA HILO HAPO JUU HUWEZI KULIAFIKI BASI ACHANA NA WAZEE WAKO TAFUTA MAISHA YAKO YA BAADAYE, UTAMUACHA HUYO UTAPATA MTU MBAYA NA AKULETEE UKIMWI BURE, MIMI NA MAMA WATOTO WANGU TULIKAA MIAKA KUMI NDO NIKATOWA MAHALI NA WALA SIJATOWA ZOTE WALIZONITAJIA NA SASA TUNAMIAKA 24 PAMOJA TUKO ULAYA HUU MWAKA 15 NA TUMEPATA WATOTO WAWILI MMOJA AMEMALIZA UNIVERSITY NA MWINGINE ANAMALIZIA SECONDARY NA HALI YETU SI MBAYA SANA TUNGEWASIKILIZA TUNGEACHANA NA PENGINE KILA MMOJA WETU TUSINGEFIKA HAPA TULIPO, ACHANA NAO ANGALIA USAWA WA MAISHA YAKO YA MBELE, UTAKUJA KUWASAIDIA WENYEWE BAADAYE

    ReplyDelete
  55. ankal wee need conclusion katika mda hii. Kwani imepata wachangiaji wengi sana sasa tunachotaka ni wewe utoe tamati, kama umetunga story hii tafadhali tuambie you are the winner! Kama kweli huyo dada yupo asome maoni yote kisha ataoe mawazo yake ya mwisho tumsikilize anasemaje kama ushauri amepata wa kutosha. Binafsi ninawasiwasi na ukweli wa muuliza swali mimi nipo ughaibuni ninaona hali halisi ya uchumi unavyosumbua, kwa USA kuna watu zaidi ya milioni 15 hawana kazi wanategemea unemployment Europe nako wamepigika vibaya, watu wanaishi kwa maisha ya wasiwasi kwani unafanya kazi lakini ujui kesho utaambiwa nini kwani watu wengi wanazidi kupunguzwa kazi. Kwa huyo jamaa kutuma pesa ziende bongo sidhani kazi za ubebaji boxii zimepungua wanazichukua wazawa wenyewe, Na nature ya kusoma medical school zidhani hata atapata muda wa kubeba boxii kitabu ni kigumu na muda hakuna na sijui ni nani anamsponsor huyo jamaa kisu cha kulipia tuition ni kirefu kiasi kwamba sidhani hata kama mtu ataweza kutuma hizo pesa bongo. We have a doubtifull mind about this story!
    Mdau wa damu USA.

    ReplyDelete
  56. Mimi anaona kwamba ile kitu yote watu wanasema humu kwa ndani na hadisi mwenyewe fyote hio ni forojo tu.

    ReplyDelete
  57. Len Dancun usaApril 05, 2010

    Dadangu mimi nimmoja wa wale wanaoishi ng'ambo kama boyfriend wako,na nimemwacha mpenzi kwetu kenya na sijawahi kumtumia hata shillingi kumi za tanzania,simu nampigia mara moja kwa mwezi lakini wazazi wake wanipenda na huniombea mema.

    Mapenzi kati yako na boyfriend wako ni tofauti na ya wazazi,ukimpoteza utakuja kutoa ushuhuda kama wafanya dhambi kwa mungu hutoa hushuhuda.

    ReplyDelete
  58. Mimi ninahitimisha, huyu dada ana haki ya kuuliza swali, sisi wanaumme ni watu wa kugeuka mara moja, huduma siyo hoja, wazazi wako sahihi, it is a matter of principle, wanapata shida ya kusema kwa ndugu zao kuwa mkwe katoa matunzo, sisi waAfrica tuna Mahali ni vitu vidogo lakini vina maana kubwa sana wazazi wetu wanajua, vijana kama wakina DR. US blogger ambao African philosopher Fanon aliwaita Black skin, white marks, wanataka kuiga uzungu, mahali ni vitu kama Blacket ya shangazi, sufulia na mbuzi au ng'ombe vitu ambayo huyo jamaa anaweza kuvitimiza, ni sehemu ya African rituals, African traditions ndiyo maana wazazi wanajua zaidi umuhimu wake kuliko wachangiaji wengi ambao ni ignorant of the social anthropology of their people.

    Dada muombe mpenzi wako atoe mahali, na wewe kaka ukisoma maoni yangu nakuomba usimlaumu mpenzi wako, sisi WAAFRICA TUNA MILA ZETU ambazo ni muhimu kuziheshimu, Kwanza kitendo chamahali ni heshima kwa wazazi na kwako pia muohaji mbele ya jamii.

    Dada wewe unayo akili, maana forum kama global ya jamii unapata mawazo tofauti.

    ReplyDelete
  59. asante michuzi kwa mara ya kwanza umepost maoni yangu, mimi ndiye niliyetoa maoni number 60 ya hitimisho, lakini nimerudi tena, Dr US blogger lugha yako ni ya kipuuzi huwezi kuwaita dada zetu eti machangudoa wa bongo, malaya wa kizungu wapo wengi pia, hivyo wewe kuwa Alumin wa Oxford sio hoja wapo wengine wa Havad lakini kazi ni kuwatumikia wazungu tu, na kuajiliwa huko ulaya, nakushauri dada yangu maoni ya mtu kama Us Blogger yapuuze ni majivuno tu, halafu maoni ya wanawake wengine kwa assessment yangu ni wivu na desperation za kukosa wanaumme wa kuwaoa haziko rational,

    Jambo la msingi huyo kaka ni mfano wa kuigwa katika jamii na mtu anayekupenda sana dada, usikubali hakupotee, do anything in your power to marry him, he will be a good and responsible husband,

    Narudia, mahali ni kitu muhimu sana, it is part of our African cultural heritage and rituals, vijana hasa hasa wasomi wanataka kuiga uzungu mpaka hata wazungu wanawacheka, mimi nipo ughaibuni miaka mingi na nina PhD pia ingawa sio oxford kama US blogger.

    Kaka mpendwa najua na wewe tuko pamoja ughaibuni, umekula Ng'ombe mzima kwa nini ushindwe mkia, kama kweli huyo ni mtu mmemchagua, kwanza unaonyesha kumpenda, na kumuamini, tafadhali wewe tuma wazee wawili na ndugu zako wakuwakilishe utoe mahali ni ndogo sana, wala mahali huwa hailipwi yote, hata mpenzi wako atajisikia heshima mbele ya familia yake na jamii, pia hata wazazi wake utawapatia heshima ukizingatia siku hizi watoto wakike wengi wanakaa kwa wazazi mpaka wanazalia hapo, siku hizi wahoaji walio serious kama wewe ni wachache, nakuomba kaka mpe raha mpenzi wako, wape heshima wakwe zako, jipe heshima wewe mwenyewe, lipa mahali- mungu akubaliki, huyu dada ana-akili sana, maana ni afadhali kutafuta ushauri hapa kuliko rafiki au jirani, maana hao ndiyo maadui namba moja siku hizi

    ReplyDelete
  60. Wewe dada! yu cant be serious! yani at this era unazungumzia suala la kutaka kumuacha mwanaume kwa7bu ya mahari tena sio kwamba amekataa ni kwamba tu anasema mfanye mambo ya msingi kwanza, binafsi nimesikitika saaanaM KWAKWELI UNGEKUA KARIBU NINGEKUCHAPA MAKOFI...hao wazazi wako wana mambo ya kizamani sana jaribu kuwaelewesha usikubali wakuendeshe kwa jambo la kipuuzi kama hilo, uyo mwanaume wako ana akili sana ndo maana hataki kukuimbilia kulipa mahari kwaku iyo sio ishu, tena nijuavyo mimi mahari ni jambo la ,mwisho kbs na kama nilivyosema kwa nyakati hizi 2nazoishi umuhimu wake ni mdogo sana, kwa kifupi achana na mawazo ya kutaka kumuacha mchumba wako otherwise UTAJUUUTA!

    ReplyDelete
  61. if this story is true, then the man has contacted a strong LIMBWATA and he is not in his mind.

    ReplyDelete
  62. Huyo mwanaume lazima mgonjwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...