Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes , Thomas Ulimwengu (kulia) akimtoka beki wa timu ya vijana ya Malawi, Lucky Malata (5) katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes , Thomas Ulimwengu (kulia) akiwania mpira sambamba na beki wa timu ya vijana ya Malawi, Limbikani Mzava katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Golikipa wa timu ya taifa ya Malawi ya vijana chini ya miaka 20, Alex Makina akiuangalia mpira ukitinga wavuni na kuhesabu bao la pili kwa timu ya taifa ya Ngorongoro Heroes. kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Malawi akiwa ameeduwaa baada ya mchezo kumalizika
Kocha wa timu ya vijana chini ya 20, Rodrigo Stockler akimpongeza mfungaji wa bao la pili la timu hiyo, Omega Seme wakati mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Ngorongoro ilishinda 3-1. Kwa matokeo hayo timu ya ngorongoro itakutana na timu ya vijana ya Ivory Coast wiki ya tatu ya mwezi mei ambapo mchezo wa kwanza utafanyika katika nchini Ivory Coast na baada ya wiki mbili timu hizo zitarudiana katika dimba uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
wachezaji wa timu za Tanzania na Malawi wakiomba dua kwa pamoja mara baada ya mchezo kumalizika.
Mashabiki walioingia bure kuipa sapoti NgorongoroHeroes

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2010

    Is Ngorongoro Heroes any different from Serengeti Boys? Kindly Explain!

    It's a good thing that they did, beating Malawi that is. Facilitations!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2010

    Kama sijakosea Serengeti ni U-17 na Ngorongoro ni U-20.
    HEKO!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2010

    Ngorongoro Heroes is the Youth national team whose players are aging under-20
    WHILE
    the Serengeti Boys is the youth national team whose players are aging under-17.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2010

    NDUGU WAHUSIKA MIMI NAPENDA KUTOA ONYO KUHUSU UZIO (fence) HAPO JUU ZIMEKA KINOMA SANA.HII NI HATARI SANA IKITOKEA FUJO ISIJE IKATOKEA KAMA HILLSBOROGH soma hapa .

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2010

    Hongera vijana wetu, kazeni buti kwa safari bado ni ndefu sana.

    Ankal tunashukuru kwa hizi habari za picha ambazo kwa kawaida huleta kutoka katika viwanja vyetu. Ni more reliable kuliko kurasa na michezo za magazeti yetu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2010

    picha ya kwanza hilo bango la biashara or whatever lilitakiwa liwe nje ya uwanja. Wabongo akili zipo wapi?

    ReplyDelete
  7. mbona uwanjani mashabiki ni wachache?
    watanzania lazima tujifunze kusupport wachezaji. sioni haja ya watu kuingia bure uwanjani, kwa nini hata kama hamna pesa ya kutosha walipe kiasi fulani nafuu japo kuchangia gharama za kuutunza uwanja? hiyo tabia ya BURE...bure inanikela. pay something. and anything makes a difference. fikra za kutaka vya bure haziishii hapo kesho mkiwa viongozi mnaishia kuomba hata vitu ambavyo mnaweza kufanya wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...