Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza jana kwenye mkutano wa Uchumi Duniani unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Katika Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha Rose Migiro, kulia Rais wa Zambia Mhe. Ruphia Banda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Zambia Mhe. Ruphia Banda walipokutana jana katika mkutano wa Uchumi Duniani unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kushoto, akizungumza na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein kulia, Rais wa Zambia Mhe. Ruphia Banda na Waziri Mkuu wa Kenya Mhe. Raila Omolo Odinga, nje ya ukumbi wa mkutano wa Mlimani City Dar es salaam jana, baada ya kumalizika kwa mkutano uliozungumzia mambo ya kilimo Barani Afrika.
Rais wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katikati, Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Wazi Mkuu wa Kenya Mhe.RailaOdinga na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Dk. Salim Ahmed Salim, wakisakata Rumba katika Tafrija ya kukamilisha Mkutano wa Uchumi Duniani iliyofanyika jana katika Viwanja vya Ikulu Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akisakata Rumba na Elsia Kanza kwenye Tafrija ya kukamilisha mkutano wa Uchumi Duniani iliyofanyika jana Usiku katika Viwanja vya Ikulu Dar es salaam.
(picha na Amour Nassor VPO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2010

    You surely deserve this after tough deliberations on our economies! Rhumba Hoyeee! I did not know some people were this talented!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2010

    Raila anazuga live, anaombea mziki uishe

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2010

    Hii kusakata rumba safi sana. si aibu aibu tuuu...!! jackob zuma anajua hiyo...

    ReplyDelete
  4. Hapo nina hakika hakuna atakaemshinda Mwanangu mwenyewe Mzee Zuma kwa kusakata dansi hapo.
    Amini msiamini. Zuma namuaminia babake mwanangu mwenyewe!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2010

    Tumefunga mkutano vizuri ila kuna kauli moja nimeisikia hakika ilinisikitisha inasema hivi "we are producing what we can't spend, and we are spending on what we can't produce". Sikutarajia kama ingesemwa na yule aliyeisema kwenye jukwaa la kimataifa kama lile!. Hard to believe!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2010

    Tulikuwa tunasema Baada ya Kazi Kunywa CHIBUKU. Sasa baada ya kazi cheza ngoma!

    ReplyDelete
  7. mtzwadarMay 08, 2010

    Aise huyo mtoto Elsie Kanza bomba kweli, yuko natural kabisa, hana hata nywele za badia, ebu tazama mguu!

    Anyway they its a typical african affair, they are different, living in their own bubble, sie walalahoi will be picking up the expensive tab, and everything will be forgotten!

    Oye JK kwa kuonyesha ulivyo hodari kujali wananchi!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2010

    La salale!!!
    Mzee mwenzangu Mh. Dr Shein, kumbe yakhe wajua kuyarudi magoma vilivyo!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2010

    Mimi nafikiri huyo mshirirka alisema "we're producing what we cant spend and spend what we dont produce kaona mbali saana,kwani mara nyingi mikutano kama hii inaishia kwenye papers tu then in fews month time the organizers will be thinking of another venue some where else and the life goes on and on and on...

    ReplyDelete
  10. hapo wamekosea wangemuekea Mzee ZUMA kwaito au house ahahahaha wangezimika mzee anazirudi kama hana akili vile

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...