Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Mh. Pascal Mabiti akimpokngeza Fancy Nkuhi kwa kupata nafasi hiyo.
Fancy Nkuhi akiwa na mpinzani wake wa karibu Jamila Hasani mara baada ya matokeo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano huo mara baada ya uchaguzi kwisha.



Na Hillary Shoo,Singida.

KATIBU wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya (UNA) United Nation Asociation iliyopo kwenye jengo la umoja wa mataifa jijini Dare s salaam Fancy Nkuhi (25) amechaguliwa kuwa mmoja wa wagombe Ubunge kundi la vijana kutoka mkoani Singida.

Fancy aliibuka kidedea kwa kupata kura 16 kati ya kura 29 zilizopigwa jana na wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani hapa.

Katika uchaguzi huo mshindi alipata upinzani mkali kutoka kwa msindi wa pili Jamila Hasan aliyepata kura 10 huku Vailet Eliasi ambaye ni mfanyakazi wa ofisi ya UVCCM makao makuu akiambulia kura 3.

Mjasiriamali kutoka Kinondoni Mosi Ntandu aliambulia patupu baada ya kupata kura sifuri.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo Fancy mwenye shahada ya sheria kutoka chuo kikuu huria,alisema matarajio yake ni kuhakikisha fursa wanazopata vijana katika nyanja mbalimbali zinafanikiwa.

Alisema atahakikisha kuwa fursa hizo zinapata msimamizi mwenye uwezo wa kuzitetea katika bunge pindi atakapochaguliwa kushika nafasi hiyo.

Hata hivyo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Pascal Mabiti aliwataka vijana hao kuunganisha nguvu ya pamoja na kuvunja makundi ili kuhakikisha mwakilishi huyo kutoka mkoani hapa anaibuka mshindi katika awamu ya pili Mkoani dodoma Agosti 3 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2010

    is she Fancy or Zaitun of Mnazi Mmoja Dar?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2010

    Ankal naomba namba ya Nancy...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2010

    She is so Cute na pia anaelimu hao ndio watu wanaofaa kutuwakilisha Vijana wenzao,sio mnatuwekea mtu ambaye ni mbumbumbu mzungu wa reli dada wa watu kasoma anaelimu yake...big up Fancy tuko pamoja

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2010

    Kampeni za uchaguzi na kura za maoni zimetawaliwa na vitendo vya rushwa. Kwa mara ya kwanza naona TAKUKURU wanafanya kazi yao, lakini cha ajabu watuhumiwa wanaachiwa na ndivyo itakavyokuwa hawatafikishwa mbele ya sheria au kufunguliwa mashtaka. Wabunge waliupitisha mswada huu bungeni kwa kauli moja na Mhe. Rais akausaini kwa mbwembwe. Sasa sheria hii inawageukia na wanaiona TAKUKURU kuwa adui. Kweli hatuwezi kupata viongozi bora wenye mtizamo wa Utawala Bora, utetezi wa maslahi ya wanyonge na usawa mbele ya sheria. Nia yao kubwa ya kuchaguliwa ni kujinufaisha na siyo uwakilishi wa wananchi.

    ReplyDelete
  5. bila ufisadi maisha bora kwa wote yanawezekana, lakini ubinafsi wa viongozi, hembu tujiulize bongo kuna wabunge wangapi?

    ReplyDelete
  6. maskini kalivyo kazuri lazima katashinda afu ile mibaba ya vijicent inamsubiria kwa hamu wammege, Fancy pliz be yourself umesoma na mzuri, i see bright future without rushwa ya ngono.

    ReplyDelete
  7. Annon unayezungumzia uzuri wa Fancy umenigusa sana, maana hata mimi nimeguswa sana na uzuri wake! Ila ndio hivyo, inategemea na yeye mwenyewe ana mtazamo gani katika maisha na anataka nini toka kwa waheshimiwa sana wa mjengoni.

    All in all, mimi siipendi kabisa CCM, ila Fancy angeweza kunihadaa kwa sura yake na nikajikuta napigia kura CCM kama anagekuwa mgombea kwenye jimbo langu la Kawe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...