Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia na kumsikiliza msichana mlemavu Joyceline Paulo huko Rusahunga wakati mgombea huyo aliposimama kuwasalimia wananchi na kunadi ilani ya CCM.Dr.Kikwete aliahidi kumpatia mlemavu huyo baiskeli maalumu ya matairi matatu ili aweze kumudu shughuli zake kwa urahisi zaidi.Dr. alikuwa njiani akitokea Ngara mkoani Kagera kuelekea Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa barabara
Dr.Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijijini Rusahunga wakati aliposimama kuwasalimia na kunadi ilani ya CCM wakati alikuwa njiani akitokea Ngara mkoani Kagera kuelekea Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa barabara.
(Picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hiyo picha ya Ndugu Jakaya na mwanamke mwenye ulemavu inaonyesha UTU, HURUMA, UPENDO na UKARIMU alionao na kwamba anawajali watu. Mungu akulipe kwa kadri yako kwa sadaka uliyoitoa.

    ReplyDelete
  2. Siyo kebehi wala nini, Rais wetu ana moyo wa utu; tatizo ni uwezo wa kufanya makubwa ya kubadili nchi.

    ReplyDelete
  3. Mbona unaminya picha za vyama vingine? Biased or what?

    ReplyDelete
  4. walemavu kama hao wapo wengi sana !! si adi siku ya uchaguzi ndo kuwasaidia watu kama hao ni haki yao kusaidiwa na serekali. kweli tunashindwa kuwapatia hata basikeli how masikeli ya mlevavu ? mimi ningekuwa rahisi ninge ningesitisha hata marupurupu ya wabunge ya mwaka hili kuwasaidia walemavu !! Shame on US kweli tunashindwa kila kitu! what is there that we can do for our ppl !! hata misaada tukipewa mnatafuna kila kitu mnatafuna wenyewe, kweli hamna hata huruma!!

    ReplyDelete
  5. Hizi huruma ambazo hajaziona kabla, unakuja kuziona uchaguzi unaanza. Msitudanganye hana cha huruma wala nini!!!!!!!! Ni walemavu wangapi wamejaa Dar es Salaam. Anafanya hivi kwa sababu ya uchaguzi hana lolote.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  6. Basi angewaonea huruma wakina babu seya na watoto wake pia wanaokula life time jail sentence for nothing.

    ReplyDelete
  7. Naungana na mdau wa kwanza na wa pili katika safu hii. Hii ni picha inayogusa moyo sana!

    ReplyDelete
  8. wewe unaesema akina babu sea wanakula life time 4 nothing ni hakimu? unajua watoto wale wenye miaka kati ya 6 na 12 sasa hivi wana umri gani? unadhani mtoto wako wa kike aingiliwe kimapenzi na mwanaume ktk umri huo na unajua kabisa si lazima ushauri wa dr. kwani hata wewe ukimchungulia unaona alivyoharibiwa ungejisikiaje? maoni mengine ni hopeless sana

    ReplyDelete
  9. ninachotaka kusema ni kwamba kwenye sheria ushahidi ukithibitisha pasipo na shaka huruma inawekwa kando, hatutaki taifa la wabakaji,walawiti wala mafisadi. muhalifu hapaswi kuonewa huruma. so mdau unaehusisha huruma kwa mlemavu huyo na waharibifu wa watoto wetu wakike umenibore sana. KIKWETE OYEEEEEEEEEEEEEEEE,MI NAMFAGILIA SANA JK, BASI TU IMPLEMENTERS WANAMUANGUSHA

    ReplyDelete
  10. Picha inagusa moyo and then what...Kama inagusa moyo he is a leader...He can and he is able to help out. Tz tuna watu population gani na naamini hata kama tuna watu million 10 vilema serikali kama wanataka ina uwezo kabisa wa kumpatia kila kilema means of transportation. Kama ni wheelchair, magongo au tricycle serikali ina uwezo kabisa wa kutoka kwa watu hao. Na kuna wengine wanachohitaji ni miguu tu ya bandia sasa kwanini wasiweze kuwapa? Nchi nyingine vilema wanapewa nyumba ya kuishi, chakula na jinsi ya kumwezesha kufika kutoka point a to b. Sasa hao vilema wetu kama hatuwezi kuwatunza kwanini tushindwe tu kuwapa something to make them at least mobility able na mengine watajitafutia wenyewe. Kwa nini isie haki ya kilema kupatiwa njia ya kumwezesha kumudu maisha yao. Wengine wanashindwa kufanya chochote kwa kukosa tu miwani ya dola 100.

    Kama tunaweza kununua magari ya serikali ya nguvu hivyo na kuwalipa wabunge na watumishi waserikali vizuri hivyo kwanini washindwe kwa watu hawa?

    Upost usiposti lakini ukweli ndio huo kukaa hapo chini na huyo mtu hakutamsaidia huyo mtu chochote au kumpunguzia machungu ya maisha aliyo nayo

    ReplyDelete
  11. Hana lolote,hana cha huruma wala shangazi yake huruma.angekuwa na huruma nchi hii isingekuwa na ombaomba wala walemavu wasingetaabika ingawa asingeweza kuwasaidia wote lakini angalau angewaweka katika hali nzuri fulani hivi...anyway hapo ni katika kutafuta kula yake kwa wananchi ili baadaye akishapewa hiyo shibe siye tuendelee kutaabika huku ye ananeemeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...