wadau wakidadisi na kuperuzi katika internet cafe ya Stambuli millenium towers, Kijitonyama jijini Dar, ambayo imepata umaarufu mkubwa kwa kuwa na mtandao wa kasi usio na kwikwi na kwa bei poa. uzuri wa hapo huna haja ya kupanga foleni kungojea kompyuta. ukiwa na laptop yako unaifungua na kuunganishwa na wireless internet na unakaa popote maeneo hayo kama ambavyo wadau wanavyoonekana. mwenye kibandiko ni Shehe Hassan Chizenga, mmoja wa viongozi wa dini vijana wanaokwenda na wakati inapokuja swala la matumizi ya mtandao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. aaah nicheke mie,mtandao wenye kasi kwi kwi kwi ukiuliza unaambiwa 2Mbps.

    ReplyDelete
  2. Wadau nisaidieni,
    Hiyo speed kubwa ni ya kipimo gani? Hiyo bei rahisi ni sh. ngapi kwa saa


    Sony

    ReplyDelete
  3. Duh! Sio mchezo nimepamisi sana Millenium tower... Jack na wajomba wengine naona mnakula w.less kwa saana

    ReplyDelete
  4. Bwana,

    Nakubaliana na wewe kuwa hapo huna haja ya kupanga foleni, ila sikubaliani nawe juu ya spidi.

    Nikiwa nchini nakumbuka nilikaa hapo na wateja tulibaki kuchanganyikiwa hata ku-sign in kwenye email zetu ilichukua zaidi ya dk 10, na nilishindwa hata ku-download file langu. Lakini mwishowe walidai tulipe pesa kamili.

    Mimi, sina ujuzi wa IT, lakini kwa vile walivyoshindwa kutuomba radhi wateja, nilidhani labda wame-slow down mtandao makusudi ili watuibie wateja.

    Wazo la wireless ni zuri sana kwa mahali hapo, ila huduma yao si nzuri, hasa upande wa speed ya internet ina "kwi kwi bado".

    Mdau (Amsterdam)

    ReplyDelete
  5. Sasa jamani nyinyi mnasahau kama hapa ni bongo any way mtandao ni mzuri sana tu kwa sisi wabongo unatutosha ...

    ReplyDelete
  6. Naona huyu mdau wa amstadam amekuja siku nyingi sana mimi niko hapa sasa hivi kwa kweli speed inatisha kabisa kwa kuwa sijawahi kwenda kwenye net za uswahili nikakuta speed kama ya hapa. Kiukweli lazima tukubali kuwa net yao nzuri pamoja na huduma kwa kweli ni tofauti na internet nyingine za bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...