MICHUZI,
NIMEONA VEMA KUSEMEA HILI KWANI WATANGAZAJI WA 'POWER BREAKFAST' WANATUMIA MUDA MWINGI SANA KUFANYA UTANI HIVYO KUONDOA MAANA NA UZURI WA KIPINDI HICHO.

HALI HIYO INAJITOKEAZA SANA WAKATI WA MAWAJIANO NA 'BONGE 'NA PIA WAKATI WA 'KUPEZURI NA KUDADISI' MAGAZETI. UTANI WAO UMEFANYA VIPINDI KUWA VIFUPI SANA NA KUKERA ZAIDI KULIKO KUBURUDISHA WASIKILIZAJI.

IJULIKANE KWAMBA WENGI HUSIKILIZA VIPINDI HIVI KWENYE MAGARI WAKATI WA KWENDA MAKAZINI ASUBUHI
MDAU DAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 74 mpaka sasa

  1. Hapo naona mdau umechemka au una jambo.Umekiri kwamba watu wengi wanasikiliza kipindi hicho kwenye magari wanapoenda kazini ila hujasema kwanini wengi husikiliza....ni huo utani unaousema!.Ukiondoa huo utani hatutasikiliza!.Kweli kama hupendi utani ni vyema ubadilishe kituo waache wanaopenda utani waendelee kusikiliza!.

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na mtoa hoja ila nataka nimkumbushe kuwa hiyo ni namna yao ya kufikisha habari kwa watu husika.

    Kuna watu, mimi nikiwemo, tunapenda kupata habari kwa njia hiyo ya utani n.k.

    Pengine ndugu mtoa hoya hiyo si station yako ya habari na nakushauri u-tune RTD next time.

    Asante.

    ReplyDelete
  3. Yes Mdau umenena! Na pia wanapoteza muda kila siku wanakula dakika nyingi za kipindi cha Cha Leo Tena na Dinah, wanazidisha dakika 3 leo wamezidisha dakika 15. Mnaboa kinamna.

    ReplyDelete
  4. Mdau usisahau kwamba Clouds ni radio ya burudani kwa hiyo wanafanya vipindi vyao kiburudani na wengine tunapenda namna yao ya kuendesha vipindi. Ukitaka kusikiliza muhtasari wa magazeti kwa namna ambayo sio ya kuburudisha mbona karibu radio nyingine zote zinafanya hivyo na karibu muda ule ule? unaweza kusikiliza hao. Kila radio ina namna yake kwa mfano ukisikiliza kipindi cha michezo cha magic Fm ni tofauti kabisa na radio one na TBC!!!

    ReplyDelete
  5. BINAFSI NILIKUWA MPENZI MZURI TU WA KIPINDI HICHO. LAKINI NI MUDA SASA TOKA NIMESIGN OUT KUSIKILIZA KIPINDI HICHO. KIPINDI KIMEJAA MASKHARA NA UTANI KAMA ILIVYOELEZWA. SINA HAKIKA KAMA WAHUSIKA WANAFAHAMU KUNA HADHIRA KUBWA YA WATU TOFAUTITOFAUTI INAFUATILIA KIPINDI MIONGONI MWAO IKIJUMUISHA WATOA MAAMUZI(WAKURUGENZI N.K..) WAJIREKEBISHE NAAMINI HAWAJACHELEWA KUWEKA MAMBO SAWA.

    ReplyDelete
  6. jamani haters stop it:
    wenzenu ndo 2napenda hivyo hivyo kama hupendi wataka crious fungua redio tanzania au praise power au wapo radio acha sie 2jienjoy na utani we2
    yaani big up kwa saaaaaaaaaaanaaaaaa 2 its an entertainment radio so kama hutaki badilisha 2 station unachokitaka hakipo clouds ndio tazizo la vijana kuwa na mawazo ya ujima

    ReplyDelete
  7. kwa kweli binadamu tunatofautiana nimeamini, yaani mi navyopenda wanavyoendesha kile kipindi kwanza huchoki kukisikiliza, pili utani wanaoutumia na maneno yanaleta mafunzo na msisi mko kwa msikilizaji hivyo huwezi zama radio yako,kwani kupitia utani unapata elimu na mafunzo labda uniambie una uelewa mdogo wale utaniwao si wa pj,babra,gelard au bonge ni maneno ambayo huyatumia km wawakilishi so km mwelewa na mpembuzi yakinifu utapata ukweli uliopo
    kwa kumalizia kipindi ni kizuri tulio wengi tunakipenda nna uhakika na hilo kwani mi bila wao na wale wa jahazi siku haijaisha kwangu na nathibitisha hilo kutoka wengi

    so mdau uwe makini pindi usikilizapo kipindi utang'amua namaanisha nini upo hapo

    Regards,
    M.B

    ReplyDelete
  8. NI KWELI MICHUZI UNAVYOSEMA CLOUDS FM SIKU HIZI WAMEKUWA WANATUBOA SANA WANAONGEA SANA KULIKO BURUDANI WAAMBIE WASIJIFANYE MAARAFU KWA SABABU KUNA SASA HIVI KUNA VITUO VYA RADIO VINGI AMBAVYO HUTOA BURUDANI NZURI KWA WASIKILIZAJI KUZIDI WAO.

    ReplyDelete
  9. na matangazo ya biashara yamekuwa mengi mpaka kipindi kinaboa.

    hata wale zekomedi kule tbc matangazo yamekuwa mengi hadi kipindi kinaboa - sasa wamebakia jina. hakuna kichekesho chochote tana.

    ReplyDelete
  10. Asante kwa kuliona hilo kaka mi huwa ninapata shida wanapoweka utani na kutumia maneno kama upuuzi, wapuuzi, washenzi na maneno mengine ya kashfa na yasiyofaa katika kipindi. Hata kama ni utani kuna maneno ambayo hayafai kusikika redioni kwani moja ya kazi ya redio ni kufundisha. je watoto wanaosikiliza kipindi hicho wanajifunza nini? Sina uhakika wa viwango vya elimu vya watangazaji hawa ila nasahuri wawekekwe usimamizi wa karibu ili wafuate maadili.

    ReplyDelete
  11. MZEE WA BUNJUAugust 06, 2010

    HUNA LOLOTE ZAIDI YA HUSDA TU, CLOUDS SIO RTD BWANA, CLOUDS HIYO NDIO STIL YAO YA UTANGAZAJI NA KWA TAARIFA YAKO WENGI WANAIPENDA SANA NA HASA VIPINDI UNAVYOSEMA WEWE NA KINACHOISUKUMA KUPENDWA NI HIYO HIYO STAILI YA UTANGAZAJI, COMEDY KIAINA, MESSAGE HUWAFIKIA WALENGWA NA MAMBO MENGI YAMEBADILIKA SANA KWA AJILI YA VIPINDI HIVI, TATIZO LAKO HUJUI TAFSIDA, NA ISITNZAI NDO MAANA HUPENDI, KISWAHILI LUGHA PANA SANA , NDANI YA VIPINDI HIVI KUNA KEJELI, TAMBO, SIMAMGO, SUTA, ONYA, ELEKEZA, NA KWA KWELI KAMA WEWE NI MLENGWA FOR SURE UTATAMANI CLOUDS IFUNGWE, NI KWAMBIE WEWE KAMA UMETUMA NA RADIO NONIHINO WAMBIE WAPENZI WA CLOUDS NIMEKUTA HAWAPO.

    MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  12. Kaka ni kweli kabisa, hata mimi hua inaniboa sana, sitaki kuamini kua jamaa ni walevi wa kuamka nazo au walevi wa umaarufu, uzuri wa sisi watz hua hatusiti kukukacha ukituboa. Mbaya zaidi wanatumia radio ku'express their interests whether politically or any way kupata umaarufu, kitu ambacho ni mwiko ktk fani ya uandishi wa habari. Wanazidiwa ubunifu na watoto wadogo wa xxl. Nahisi kuwakumbuka Fina na Masoud wkt Gerard akiwa msom magazeti tu kipindi hicho nasasa ndio mboaji klk maelezo.

    ReplyDelete
  13. Mdau nakuunga mkono kabisa..!! kipindi ni kizuri sana na ujumbe ni mzuri lakini nahisi inabidi wapunguze matani au ku-balance vyote ili watu waweze kupata ujumbe kamili. zangu chache tu.

    ReplyDelete
  14. Nakubaliana na mchokoza mada kuwa kipindi hususan cha jioni kinachopitia magazeti ni 'boredom'. Ni bora wangesema wanapiga porojo zao kuliko kusikiliza mambo ya kitoto muda mrefu ambayo mengine ni aibu. Aidha unashindwa kama msikilizaji kufahamu ikiwa hayo ni mawazo binafsi au magazeti yameandika hivyo. CLOUDS ACHENI HIZOOOOOOO!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. kweli namuunga mkono mdau hapo juu,waedeshaji wa kipindi hiki wana mizaha sana hata radha ya kipindi haipo wanaboa kweli,mara nyigi nasikiliza ninapoelekea kazini asubuhi haileti raha kabisa.

    ReplyDelete
  16. Nami namuunga mkono mdau huyo hapo juu kwani kaongea UKWELI MTUPU ! Kwa muda huo wengi huwa tuko kwenye magari tukielekea makazini mwetu na hivyo kupata muda wa kusikiliza hiki kipindi cha PB. USHAURI WANGU BURE !!
    Ningeuomba UONGOZI wa RADIO CLOUDS ujaribu kuangalia kipindi cha PowerBreakfast (PB) kinachorushwa na CITIZEN TV ya Kenya, utagundua kuwa hawa vijana wanaoendesha kipindi cha PB cha Radio Clouds wanacheza !!!! Mantiki inakuwa hakuna na umaana wa POWERBREAKFAST unakuwa HAUPO kabisa !!! Na ushauri mwingine ni kuwapeleka au wakajifunza toka kwa CITIZEN TV (KENYA) mambo haswa yanayotakiwa kuongelewa ktk kipindi kama hicho !!! Kweli hawa vijana wanaoendesha huwa WANACHEMSHA muda mwingi na kupoteza maana halisi ya kipindi husika !!!!

    ReplyDelete
  17. Mdau Mkubwa wa Kipindi - DSMAugust 06, 2010

    Nami namuunga mkono mdau huyo hapo juu kwani kaongea UKWELI MTUPU ! Kwa muda huo wengi huwa tuko kwenye magari tukielekea makazini mwetu na hivyo kupata muda wa kusikiliza hiki kipindi cha PB. USHAURI WANGU BURE !!
    Ningeuomba UONGOZI wa RADIO CLOUDS ujaribu kuangalia kipindi cha PowerBreakfast (PB) kinachorushwa na CITIZEN TV ya Kenya, utagundua kuwa hawa vijana wanaoendesha kipindi cha PB cha Radio Clouds wanacheza !!!! Mantiki inakuwa hakuna na umaana wa POWERBREAKFAST unakuwa HAUPO kabisa !!! Na ushauri mwingine ni kuwapeleka au wakajifunza toka kwa CITIZEN TV (KENYA) mambo haswa yanayotakiwa kuongelewa ktk kipindi kama hicho !!! Kweli hawa vijana wanaoendesha huwa WANACHEMSHA muda mwingi na kupoteza maana halisi ya kipindi husika !!!!

    ReplyDelete
  18. I agree with the person aliyetuma ujumbe..I used to be a fan ila kikweli they joke tooo much while there is nothing to joke kama today morning something about **ilala mmelala ** it was boring and not fun cos they kept on talking the same thing all over and again, unafika at your place of work hujapata any habari ....its weird how they think too much joke makes good???....PLEASE CHANGE YOU ARE CHASING AWAY YOUR LISTENERS

    ReplyDelete
  19. Mimi naona aina yao ya upashaji habari kwa kutumia utani na kabehi ni MZURI SANA na watu wengi wanakipenda kipindi cha Power breakfast. Labda mlalamikaji yeye binafsi hapendi aina hiyo ya upashwaji habari.
    Kipindi kingine cha aina hiyo kipo Clouds FM pia,kinaitwa Jahazi, nacho ni kizuri sanaa.

    Ippy

    ReplyDelete
  20. MIJITU MINGINE AKILI ZAO HAZINA AKILI KABISA..CC TUNAIPENDA CLOUDS KWAAJILI YA HUO UTANI WAO NA VICHEKESHA NDO MAANA KAMA USEMAVYO MWENYEWE WATU KIBAO WANASIKILIZA CLOUDS WAKIWA WANAENDA KAZINI NA PIA JIONI WKT WA KUTOKA KAZINI KIBINDI CHA JAHAZI.

    NAOMBA NIKUULIZE SWALI MOJA; MBONA REDIO ZIKO NYINGI SASA WHY WATU WOTE WAPENDE CLOUDS WAKATI HABARI NI HIZO HIZO?? KAMA KUSOMA MAGAZETI NI YALE YALE SASA WHY WOTE WATAKEKUSIKILIZA MAGAZETI YAKISOMWA NA CLOUDS??

    HANDO, BABLA NA PJ TAFADHALINI ONGEZENI MBWEMBWE KWA KWENDA MBELE ILI MTUPE RAHA ZAIDI NA KUMBUKENI "MTI ULIO NA MATUNDA NDIO UPOPOLEWAO"

    MWISHO NAMSHAURI HUYU MWANDISHI KAMA ANAONA ANABOREKA BASI AWE ANAFUNGULIA RADIO STATION NYINGINE MAANA ZIPO ZA KUMWAGA

    ITS ME ASHA NGEDERE

    ReplyDelete
  21. NAFIKIRI HUYU MDAU HAFAHAMU OBJECTIVE YA PB. ULE UTANI MAANA YAKE NI KUBURUDISHA HASA KWA WALE WALIOAMKA ASUBUHI HAWAJUI SIKU ITAISHAJE NA PENGINE WAMETOKA HOME WAMENUNA HUO NI WAKATI WA KUVUNJA MBAVU NA KUSAHAU MATATIZO YENU. KILA RADIO INA UTARATIBU WAKE TENA MIMI HAPA NAONA HAWA JAMAA WAMEPUNGUZA UCHESHI KWANI BABRA ANAWAKATISHA KILA WAKATI KINA HANDO NA JP A.K.A NYANI MZEE WANAPOTAKA KUWABURUDISHA WANANCHI. KWA KIFUPI KILE NI KIPINDI CHA VICHEKESHO VIKIAMBATANA NA UJUMBE MZITO WA KUWAKUMBUSHA WATU WALIOJISAHAU KUWAJIBIKA KATIKA MAENEO YAO

    ReplyDelete
  22. we uliyetoa maoni yako naomba uelewe kwamba kila kitu kina swaga yake,basi wasipofanya utani huo sijui kama power breakfast itapendeza.Hiyo ndiyo swaga yake rafiki Vumilia tu.

    ReplyDelete
  23. Huo utani mwingi ndo tunaoupenda kwa sababu una kweli ndani yake.haupendi tune radio nyingine!!

    ReplyDelete
  24. MSG HIYO IWAFIKIE PIA WATANGAZAJI WA KIPINDI CHA JAHAZI KINACHORUSHWA KUANZIA SAA 1O ALASIRI cha radio hiyo hiyo!tunapenda hovyo vya jokes zao lakini visipitilize kwani too much of everything is harmful

    ReplyDelete
  25. mambo yenu hayo wala vumbi huko africa mtajua wenyewe..

    ReplyDelete
  26. NI BURUDANI YENYEWE HIYO ..KAMA HUTAKI SI UZIBE MASIKIO KAMA UKO KWENYE BASI?WENZAKO NDO TUNAVYOIJIO HIVYO YAN ...KILA MTU ANA KAREDIO KADOGO HAPA JOB KWA AJILI YA CLOUDS ..HUJUULIZI KWA NINI?...HAMA UTUACHIE RADIO YETU.....hinsy

    ReplyDelete
  27. Wewe mdau ukoje weweee? unataka kipindi kitangazwe kama matangazo ya vifo? Hili lidau lazima litakuwa ZEE, umetupiwa virago na vijana CCM sasa hivi unatufata kwenye redio zetu... TUPA KULE...CLOUDS OYEEEE

    mdau Ashkamatit

    ReplyDelete
  28. Hivi nini maana ya kusajili radio nyingi? Inalenga na kuwa na uhuru wa kuchagua, kwa nini huyo 'kikongwe' asichague redio nyingine kama hiyo inamshinda, au ana redio ya mkulima isiyobadilisha bendi hadi irudishwe kiwandani!!!!! Nafikiri huwezi kuwa na redio ya kuridhisha matakwa ya kila mtu. Please maintain our 'status quo'

    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  29. Wote wanaolalamikia utani they are not target market,hiyo redio imepata umaarufu kupitia utani huo huo na wao ndio waanzilishi wa utani redioni, wengine wote wameiga. Mdau wa 12:55pm pole sana, Africa siku hizi ni kula kuku tu, vumbi unalo wewe mbeba mabox huko porini ulipo

    ReplyDelete
  30. Tatizo la hawa watu ni ujinga walio nao. Utakuta wanapoteza hata point zenyewe kwa kujitahidi kuongea broken english. Wewe huko TZ unamuongelea english nani? Na hili si kwa Power Breakfast tu, yaani karibia kila mtangazaji wa Clouds yuko feki pamoja na miziki yao ya kibongo fleva wanayoipromote yote feki. Yaani Clouds ina boa sana.

    ReplyDelete
  31. BINAFSI SINA TATIZO NA UTANI WANAOUFANYA WATANGAZAJI HAO. HOJA YANGU NI KUHUSU COVARAGE YAO YA MAGAZETI NAONA INAKUWA NDOGO KADRI SIKU ZINAVYOENDELEA. WENGI TUNAKIPENDA KIPINDI HIKI NI KWA SABABU YA KUPATA HABARI TOFAUTI ZA KILA SIKU.NADHANI WINGI WA MATANGAZO NAO UNACHANGIA KUFANYA KIPINDI KUBOA SOMETIMES. MIMI NAWAOMBA WATAFUTE JINSI YA KUBORESHA TUFURAHIE KIPINDI KAMA MWANZO.KWANI HATA MIMI NIMEANZA KULOOSE INTEREST KUWASIKILIZA. NAVIZIA PART YA KUPEROOSE NA KUDADIS TU KISHA NA SWITCH TO ANOTHER SERVICE PROVIDER.

    MDAU PB LEO TENA AND JAHAZI

    ReplyDelete
  32. KWANI KUNA MTU AMEKULAZIMISHA KUSIKILIZA CLOUDS??? SISI HUO UTANI UTANI NDIO TUNAPENDA NA KUFANYA TUSAHAU SHIDA YA FOLENI. WEWE KAMA HUIPENDI TUNE RADIO NYINGINE!!

    ReplyDelete
  33. NIMESOMA COMMENTS ZA WADAU MBALIMBALI NAMI NAONGEZEA HIVI

    NI KWELI MATANGAZO YAMEZIDI LAKINI MKUMBUKE KUWA NYIE WASIKILIZAJI MNABURUDIKA BUREEEEEEEEEE ILA NI KUPITIA HAYO MATANGAZO MNAPATA BURUDANI NA WAO KAMA KAMPUNI WANAWEZA KUPATA FEDHA ZA KUJIENDESHA

    PILI NI KUWA HII SWAGA YAO PAMOJA NA ILE YA JAHAZI JIONI NDO INAYOUZA KULIKO HATA VIPINDI VINGINE VYOTE. UKITAKA KUJUA KIPINDI NI KIZURI ANGALIA AU SIKILIZA IDADI YA MATANGAZO YA BIASHARA. HIVI VIPINDI MBALI YA KUBURUDISHA PIA VINAREKEBISHA TABIA ZA WATU. MFANO TANGU KIBONDE ASEME KWENYE JAHAZI KUWA WATU WOTE WANAOENDESHA MAGARI KWA KUTANUA BARABARA ZA PEMBEZONI WANAITWA "PANUA" TANGU SIKU HIYO NIMEACHA KUTANUA NA NIKIMWONA ANAYETANUA NAMWITA WEEEE PANUA KUUUUBWA

    ReplyDelete
  34. Mimi naipenda PB maana inanifurahisha. Kipindi ambacho inabidi wabadili mtazamo ni kile cha Jahazi, kwani baada ya kusoma magazeti wanapoweka tafsiri zao kwenye issue seriuos unaweza tamani kuwachapa. Ushauri wangu issue zote ambazo zinahitaji ufafanuzi wa kitaalamu musiwe mnazichambua maana mko watupu mno vichwani. Nadhani deal zenu ni kama zile mama kapelekwa mahakani kwa kumtusi mwenzie hapo nawapa mia kwa mia, mambo mengine muwe mnamezea.

    ReplyDelete
  35. Leo tena ni kipindi kizuri sana kwani kinatupa picha ya maisha halisia ya wanajamii. Big Up Dina Marios and the crew.

    ReplyDelete
  36. Jamani Power breakfast ilikuwa enzi za Kipanya, Hando na Fina bana

    acheni nyie minashangaaa sikuhizi sijui hakuna mtu wa kuwa evaluate khaaaaaaaaaaa.....

    ReplyDelete
  37. Mimi nafikiri hakuna cha kumbisha hapa wala malumbano.....cha muhimu ni kwa wale amabo hawapendi kusikiliza PB basu sikiliza radio ingine na kwa wale ambao wanaona sawa endelee kusikiliza...haina haja ya kuendelea kusema kinaboa wakati hulazimishwi kusikiliza kama kinaboa sikiliza radio one, free afrika,east afrika, times, na nyinginezo nyingi


    Kunta

    ReplyDelete
  38. Mikausho MikaliAugust 06, 2010

    Wanaolalamika siwaelewi kwa kweli kwani tunasahau kwamba wengi wa Watanzania wanapenda mambo ya utani na vitu vya msingi vyenye kuleta maendeleo hawana habari navyo kabisa.Ndo maana utakuta magazeti yale yenye habari kama "AFUMWA AKIJAMBA HADHARANI" yananunuliwa sana kuliko magazeti makini

    ReplyDelete
  39. USHAURI WA BURE KWA GERALD HANDO! WAKATI WA PJ aka NYANI MZEE AKIPERUZI ANATAKIWA AMPE NAFASI PJ NA SIO KUA KINARA WA KILA JAMBO!
    PINDI AMALIZAPO MAGAZETI NDIO AENDELEE NA VURUGU ZAKE!PJ NA BABRA NI WATULIVU SANAAAA!!
    PDG MUNENE

    ReplyDelete
  40. Watu mnashangaza sana na kutia kinyaa. IS IT A MUST KUSIKILIZA CLOUDS? THE ANSWER IS DEFINITELY ‘’BIG’’ NO. Sasa kama unaona kuna masihara mengi tune another radio, zipo za kumwanga nowdays. Ooh nafika hadi ofisini bila kupata news, nani kakulazimisha wewe nyambafuuu!!
    Naona wanaolalamika hawaijui fasihi au lugha ya Kiswahili barabara na si-wafuatiliaji wa mambo..vipindi vya clouds ni kama SERIES, kama season one hukuchek na kichwa chako cha maji kama jamaa anayelalamika hapo juu you will obviously be out of the circle. Wachen watu tujipanguse na CLOUDS yetu..raaaaaaaaaaah! Big up Hando and the crew. A bottle of JD from me..Peace

    Mdau wa burudani Babati

    ReplyDelete
  41. kwa kweli mimi sina tatizo kubwa na utani wao, tatizo langu kubwa ni wao kutojua kuwa radio yao inasikilizwa na kila mtu, umri wowote, but sometimes wanaongea mambo ambayo watoto wetu wanakuwa kwenye magari wakienda au kurudi shule au hata nyumbani wanasikia, mambo yasiyofaa kuwekwa public. eti uhuru wa habari, je kuna uhuru wa habari unaovunja maadili? leave alone kuongea hata nyimbo wanazopiga, si radio wala TV yao hazifai for public viewing. Ndio maana wenzetu huwa wanatoa version mbili, radio/TV version na public version. Wakati wakiwa kwenye test signal nilifikiri the so called TCRA wangesema kitu, lakini they ended up getting a full kibali. TCRA TCRA TCRA.... Michuzi na hii ibanie, manake sio lazima wafungiwe no, bali wakumbushwe kuwa sisi bado ni Watanzania wenye maadili yetu

    ReplyDelete
  42. we mdau ni mstaafu nini kwa taarifa yako tanzania nzima hakuna radio kama clouds unachotaka wewe nini vile vionjo ndo vizuri kama hutaki basi hayo matangazo futa kabisa maana unatukera we nenda tuachie radio yetu kwanza we nani kwenye radio hii clouds funika bovu africa africa bambata au uliomba upaiswe ukapigwa chini kama unataka kupaishwa nenda mashujaa bendi nenda bana sisi bia hindi penda sana sikiliza radio ya watuiko sef che iko balabala che 24 pasikala ba

    ReplyDelete
  43. just tune to other radio you idiots! Clouds kipindi kiko poa, kinatuhabarisha na kinatuchangamsha asubuhi + kufurahisha. Washasema sikilizeni RTD kama mnataka kusikiliza habari kama risala..! JIPANGUSE.... RAAAA RAAAAA

    ReplyDelete
  44. CHANGE WE NEED!August 06, 2010

    JAMANI MI WENZENU NAMKUMBUKA FIRST LADY FINA MANGO NA MASOUD KIPANYA,PIA PAMOJA NA BONGE WAO HAPA NAMAANISHA BONGE YULE ORIGINAL WA ZAMANI.NI HILO TU KWA LEO.

    ReplyDelete
  45. utani sio mbaya.
    lakini yale matangazo sijui ndo mnawaita wadhamini wenu, yamekuwa mengi sana.
    punguzeni matangazo halafu wale wachache watakaotangaza air time iwe a bit expensive.

    ReplyDelete
  46. MIMI NAMSHAURI HUYO MTOA MADA KAMA YEYE HAPENDI UTANI ATAFUTE RADIO NYINGINE YA KUSIKILIZA. SI WENGINE TUNAUPENDA HUO UTANI KWA HIYO USITUBOE. GERARD, BABRA NA PJ HONGERENI SANA NA KAZENI MWENDO.

    ReplyDelete
  47. NGOJA NIFAFANUE KISOMI SASA, HUYU JAMAA ANA VARIED POINT ILA KASHINDWA KUIFAFANUA VIZURI.
    HIKI KIPINDI KIPO MUDA MREFU NA KILIPATA UMAARUFU SANA ALIPOKUWA FINA NA KP JAMAA WALIKUWA VERY SERIOUS NA WALICHOKUWA WANAFANYA.

    fINA NA KP WAKAENDA ZAO WAKAJA HAWA JAMAA WAPYA SASA HAPA NDIPO HALI YA HEWA IKAANZA KUCHAFUKA. MAANA WAMEONDOA KABISA ULE MPANGO MZIMA WA FINA NA KP WALIOKUWA WANAUTUMIA NA KUBAMBA WATU WENGI MNO MITAANI. SI WALE WANAOENDA MAKAZINI TU HATA KWA WALE WALALA MCHANA WALIJARIBU KUUCHELEWESHA USINGIZI ILI MRADI WASIKIE FINA NA KP WANAONGELEA NINI.

    HUYU JAMAA ALIYELETA HII HABARI INAELEKEA NI MPENZI MKUBWA WA HIKI KIPINDI NA NI KWA MUDA MREFU. SASA SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA ANAONA MAMBO SIYO SAWA NDIYO MAANA LEO KALETA DUDU LAKE.

    ILA REDIO NI BIASHARA NA NI JUKUMU LA CLOUDS MANAGEMENT KUFANYA MCHAKATO UTAKAOWAWEZESHA KUJUA TOFAUTI KATIKA KIPINDI WAKATI WAPO WAKINA FINA NA KP NA HAWA WA SASA. ILI KUWEZA KUJUA JE WASIKILIZAJI WAMEPUNGUA AU WAMEONGEZEKA? WAZIKILIZAJI WANA MAONI AU MTAZAMO GANI KUHUSU MFUMO WA UTANGAZAJI UNAOTUMIWA NA HAWA JAMAA NA ULE WAKINA FINA NI UPI WANAUPENDA?, THEN NAAMINI WATAFANYA MAAMUZI MUAFAKA ILI KUPATA UFUMBUZI WA HILI JAMBO.

    NI HILO TU NA TUSIPENDE KUTUMIA JAZBA SANA TUNAPOTAKA KUJIBU HOJA AU LUGHA ZENYE MAPUNGUFU YA HEKIMA, KWENYE KUJIBU HOJA AU MADA YA MWANAJAMII YOYOTE YULE BILA KUJALI RANGI,KABILA, DINI.

    MDAU UK HAPA

    ReplyDelete
  48. waacheni jamani watangazaji wa radio ya watu sa ka unaamka asubuhi umenuna nani sa akuchekeshe ka sio wana breakfast!!
    keep it on and keep it up guys!

    ReplyDelete
  49. wadau acheni chuki binafsi

    ReplyDelete
  50. Mdau acha chuki binafsi lol
    Hicho kipindi sisi tunakipenda kusikiliza kama kilivyo..kwani lazima usikilize power breakfast???ndo maana kuna radio station nyingi.tafuta inayokufaa usikilize tuache sisi wapenda utani tuwasikilize..

    usipenda kusemea moyo wa watu

    ReplyDelete
  51. NAFIKIRI WOTE TUNA LENGO ZURI TU LA KUWEKA MAMBO SAWA SIONI HAJA YA BAADHI YA WADAU KUTUMIA LUGHA ZA JAZBA 'TUHESHIMU MAWAZO YA KILA MDAU KWA KUJENGA HOJA' KUBWA JAMAA WAPUNGUZE MUDA WA KUFANYA MASKHARA NA MBWEMBWE NYINGI UKIZINGATIA WANA MATANGAZO YA BIASHARA LUKUKI HAITAKUWA NA MAANA KM KILA LEO WATAISHIA KUSOMA HEADING MOJA NA VICHEKO TELE AF KIPINDI KIMEISHA!!!

    ReplyDelete
  52. Ni hivi utani si mbaya makes the world moving lakini pia uwe na kipimo chake usivuke mipaka especially kama you are trying to convey a message to a particular group of people.
    PB wamezidisha utani sana kwa kweli hata mimi hilo naliafiki 100%. it will reach a time nyie mnao-support hu utani uliozidi mkauchoka pia hakuna binadamu anayependa kitu kizidi kiwango ina-bore sana tu.
    Kwa hiyo Gerald, Bonge, Barbara na Paul punguzeni matani kidogo mrudishe watu kundini maana ndo washaanza kuwachoka.

    ReplyDelete
  53. Spot on!

    Tatizo ni kurithi ubunifu, waanzilishi wa style hii ni KP na Fina, baadae akaja Gerald Hando, but walipoondoka KP na Fina, naona mngment ikaamua badala ya kubadili kipindi wakareplace watu (PJ na Barbara). It was wrong, maana wao wali concentrate kuwaigiza Fina na KP, kitu ambacho si rahisi, mara mia wengepewa tak ya kuja na style yao. Infact sio klaudis tu, FM redio nyingi sasa wanaiga huo mtindo wa Fina na KP.

    Mbona JAHAZI la kapiteeeeein na Kibonde linakuwa poa tu! infact mimi nilihama BP nikarudi Jahazi, na kapiteeeni na Kibonde wanakijulia kuendesha, in their own way. Akiwapo nanii yule Anthonio, aah huwa nachoka kabisa. Some radio program zina utamu wa mwanzilishi, Rejea Kiti moto ( pascal Mayala hadi Adam), Generali On Monday, Lary king live, Hardtal ya Sebastian na ya huyu mama wa sasa, Doha debate ya Sebastian etc

    Mdau Kiwoso
    Ukerewe

    ReplyDelete
  54. ........Mle kuna kejeli na madongo yanatupwa kwa wahusika (wafanya maamuzi) na ikisikia mtu kalia...yallah.....!!! ujue dongo limempita. Hiyo ndio staili yao. Kule kwa watani wa jadi kuna kipindi kinaendeshwa pamoja na yule "MWALA" wa vitimbi. humo ni burudani tupu utasahau stress zako zote! BABRA HASSAN unanimaliza sana ukiigiza "SHENG" za watadi wa jadi, yani Raha Tupu!!!!!
    Shemeji yake Kamau

    ReplyDelete
  55. sisi nataka cheka cheka wakati kwenda kazini.naliyaliya tu kilasiku.CLOUDS ZURI SANA TENA SAAAAANA

    ReplyDelete
  56. HEE!! JAMANI HIVI HIYO REDIO YAKO INASHIKA CLOUDS PEKE YAKE, MBONA REDIO HUMU DUNIANI ZIKO NYINGI SANA, KAMA WANAKUBOA SI UTYUNI NYINGINE, POLE SANA SIDHANI KAMA WATAKUSIKILIZA MAANA WADAU WENGI TUNAPENDA HIYO STYLE

    ReplyDelete
  57. JAMANI TANZANIA KUNA RADIO STESHENI NYINGI SNA KAMA MTU HUPENDI KUSIKILIZA KIPINDI FULANI TAFUTA STESHENI NYINGINE. KAMA UNATAKA WAKUSOMEE MAGAZETI BASI HATA RADIO NYINGINE PIA WANASOMA MAGAZETI MIDA YA ASUBUHI. HUYO ANAYELALAMIKA ATAKUWA MZEE ALIYETUPWA KWENYE KURA ZA MAONI YA CCM SASA HUWA KUNA MANENO YANAMUUMA SANA!!!! HAO WANAOZUNGUMZIA CITIZEN TV NAO WANA UPEO MDOGO SANA. CLOUDS NAOMBA SANA MKURUGENZI AKIWAAMBIA AWAPELEKE KENYA MKAJIFUNZE KATAENI BALI TUMIENI UBUNIFU WENU HUO HUO, KWANINI MUENDE MKAJIFUNZE NJE WAKATI CLOUDS MKO JUUUUUUUUUUUU SAAAAAAANNAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  58. ...Raia wana haki ya ku-criticize PB, Jahazi etc, kama ambavyo wao wanavyo-criticize institutions, individuals etc.
    Mfano...website ya clouds ipo under construction toka ujenzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni (km 127) hujaanza, barabara imeisha clouds bado wanajenga website.
    Watu wamelipia matangazo wakati wa PB sasa inabidi wawajibike sio kukata viuno na matani ya bei rahisi.

    ReplyDelete
  59. Hatukatai utani, Lakini usizidi mpaka kuharibu maana halisi ya kipindi, then Maneno ya kishenzi yasitumike, wajitahidi kutumia tafsida.....kiswahili mbona kipana tu siku hizi. Nimepunguza sana kuwasilikiza coz ya hivyo vijimambo. Ahsante mdau kwa kutoa hoja ya ukweli

    Mdau

    ReplyDelete
  60. SWALI MOJA TU KWANI DAR RADIO STATION MOJA TU??? TUNE THE ONE YOU LIKE

    ReplyDelete
  61. Yaani Clouds ni utamu kunoga!
    Bugando hospital kina mama hakuna kuvaa basuruareeee!Yaani ile topic naomba irudiwe!

    ReplyDelete
  62. Mdau uliye lalamika unatakiwa kuelewa kuwa wanacho tumia PB ni ubunifu wa aina ya kufikisha ujumbe na kwa hilo wamefanikiwa kwa 100% na ndio maana utaona baazi ya radio station zimeiga staili ya bonge kwa kuongea na matrafiki hasubui pia staili nzima ya PB inaigwa na baazi ya radio nawapongeza PB endeleeni ujumbe unafika,HANDO,PJ,BABLA HANS,MH.BONGE TUNAWASIKILIZA,TUMEWAKUBARI NA TUPO PAMOJA nazani mngekuwa ni watu wa utani MH.WA TAKUKURU ASINGEFIKA KUHOJIWA KWENU.

    ReplyDelete
  63. KUHUSU UTANI NA MASIKHARA SAWA TUNAPENDA LAKINI KUNA SEHEMU AMBAYO UNAKUTA WANAINGIZIA UTANI AMBAO HAUFURAHISHI BASI TU WANAJICHEKESHA YAANI INAKUA BORED SIO SIRI KIPINDI CHA MASOUD NA FINA WALIKUA NA UTANI NA MASIKHARA AMBAYO YALIKUA YANABURUDISHA NA UJUMBE YANAAFIKISHA VILE VILE, WENGI WANAPENDA KUKISIKILIZA HIKO KIPINDI KUTOKANA NA LADHA WALIOIACHA KINA MASOUD AMBAYO KWA SASA BABRA NA WENZAKE WANAIAHARIBU

    ReplyDelete
  64. Umenikumbusha JAHAZI burudani ya ukweli. Jamaa anayesoma zile habari za magazeti utadhani anajua hisia za mwandishi anailezea kama inavyopasa.

    Nikihitaji jokes especially mida jioni nawa-tune mabingwa, poa tu.

    ReplyDelete
  65. mtoa maoni umenena sawa kabisa. Kuna mtu mwingine anafanya kosa kama hilo pale clouds Fm... Huyu ni Ephraim Kibonde katika kipindi cha Jahazi cha Gadner Habash. Nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa jahazi lakini kwa sasa nimeacha kabisa kusikiliza hicho kipindi, hii ni sababu ya utani , mizaha iliyopitiliza kiasi ya huyu ndugu mpendwa Kibonde. Anafanya utani ambao wakati mwingine unakuwa ni wa kitoto na unaudhi na kuwa kejeli. Pili anatakiwa asituonyeshe msimamo wake wa kisiasa kuwa anaegemea wapi maana kila wakati anashambulia upande mmoja tu wa kisiasa, tunajua kuwa yeye anapenda chama gani lakini akiwa pale studio anatakiwa awe neutral! Pia katika mambo ya mpira , mjifunze kwa watangazaji wenzenu wa supersport , CNN , BBC sport n.k sio lazima sisi tujue kuwa Kibonde ni shabiki wa man united au arsenal , tunataka awe neutral akiwa studio ili achambue mambo mbalimbali ya kimichezo bila kuegemea upande wowote. Mnatakiwa kuwa professional sio kuonyesha unazi ambao haumsaidii msikilizaji.
    Kitu kingine ni kuwa hautakiwi ukiwa mtangazi kujionyesha kuwa wewe unajua kila kitu ..unatakiwa kuacha uwanja wazi wa kupokea maoni tofauti ya wasikilizaji wako na pia kuheshimu maoni yao na pia kujifunza kwao kwa kuwa hamna mtu ajuaye kila kitu.
    Sio kila mtu anayekukosoa au kukushauri ana nia mbaya na wewe au anakuchukia ..Hapana ! jamani watanzania tujifunze kuishi katika mazingira ya kukubali kukosolewa na maoni tofauti na yenu. Kuna mtu alisema siku za nyuma ..nadhani ni Chancellor wa zamani wa ujerumani Helmut Kohl: " we must live with criticism just as we live with different weather conditions"
    Nampenda sana Ephraim Kibonde katika style yake ya utangazaji na jinsi anavyopenda kutafiti mamnbo lakini namuomba arekebishe mambo kadhaa machache . Ana uwezo wa kuwa mtangazaji wa kimataifa asiridhike na hapo alipofikia.
    ni mimi mshika dau wa Segerea

    ReplyDelete
  66. mdau unaeboreka si u-tune redio One tu kwa wazee wenzio :-)

    ReplyDelete
  67. ANKAL, MAONI YA WATU WENGI YANAONESHA NI KWA KIASI GANI WATU WANAPENDA AU WANALZIMIKA KUSIKILIZA PB NA JAHAZI. (PENGINE NI BORA ZAIDI KULIKO VIPINDI VINGINE KATIKA RADIO KWA WAKATI HUO AU WANASIKILIZA KWA SABABU WATAFANYAJE/HAKUNA MBADALA)

    TUKIPENDA PIA TUSIWE VIPOFU WA KUONA VITU AMBAVYO VIKO WAZI. BAADHI YA MANENO HAYAFAI. SIO MAADILI YA UTANGAZAJI. KAMA MATERIAL IPO YA KUTOSHA KIPINDI MASKHARA YA NINI?
    PAMOJA NA HAYO, CLOUDS IPOKEE MAWAZO NA MAONI YA WATU WAKAOWAKOSOA NA KUYAFANYIA KAZI BADALA YA KULEWA SIFA ZA WANAOWASIFIA. WANAOWASIFU HAWAWATAKII MEMA. (MSILEWE SIFA. SASA HIVI MJILINGANISHE NA RADIO ZA KIMATAIFA) HAPA HAKUNA CHA CHUKI BINAFSI WALA CHOCHOTE. NI MAWAZO YA WATU WALA SIO HOJA YA MICHUZI INGAWA WENGINE MMESHAIPACHIKA ANUANI HIYO. WABONGO TUONE MAMBO KWA UPANA.

    ReplyDelete
  68. wadau walio toa critic ni wakuwasikiliza hao wanaosema badilini stesheni bila sababu hawana hoja. kama producer upo na umesoma haya take action it all lies on the producer kwasababu anatakiwa kufanya moderation ya kipindi na kutengeneza mwelekeo. as it is now kipindi hakina dira presenters grab what comes their way and sometimes wakifika njiani wanakwama matokeo wanaleta utani wa kuchusha. this also applies to JAHAZI kwani wao hata segments zao hazieleweki hawana script they say what comes first in their minds. nadhani tunakiwa kuacha ushabiki au kupenda personalities let us work on the facts and make the show more lively in a creative way.

    ReplyDelete
  69. Nimegundua kwamba wafanyakazi wa Clouds FM ndio wanajibu comment za watu humu ndani!

    Jamaa katoa constructive idea or argument, badala ya kupokea na kuifanyia kazi, nyie mnakaa na kumponda kwa kujibu comment za watu! Hamtaendelea kabisa, Radio au biashara ni watu ata kama ni mtu mmoja anatoa maoni, mnabidi mkae chini na kusikiliza kero zote na kuzifanyia kazi na mtaendelea.

    Kusaga na wengine wote mnao husika mnabidi muliangalie ili swala la sivyo mtakosa watu, kwa mara ya mwisho kuangalia nilikuwa najua clouds fm ni the people's station, then prove it.

    謝謝.

    ReplyDelete
  70. mi kwa mtazamo wangu clouds ni ya vijana na its time sasa hando akae pembeni kwani umri wa ujana umeshampita...kwa radio one wakina kitenge bado ni vijana wahamie clouds sasa

    ReplyDelete
  71. uongozi wa clouds waliangalie kivipi ? kwani ni lazima nyie msikilize habari kupitia clouds ? sikilizeni wapo radio,radio uhuru, tbc, na nyingine nyingi tu !!!
    wengine sisi ndio tunapenda utani huo kwenye habari heeh !! watu wengine bwana ..kwani mmelazimishwa kufungua CLOUDSSSSS !!!

    ReplyDelete
  72. Hivyo hivyo Power Breakfast and Jahazi kaza buti - umeona siku hizi watu wamevaa ear phones barabarani na kwenye daladala- wanasikiliza. huo utani ndio furaha ya wengi. KAAAAAAZAAA BUUTIIII. Badili stesheni kama hupendi.

    ReplyDelete
  73. Mtu anayejidai mjanja hata siku moja huwezi kumshauri. kama anavyosema mdau opposing comments zinatoka kwao wenyewe clouds. cha kufanya ni kuwaachia WAMESHASIKIA KUWA BOTH PB NA JAHAZI sasa hivi hawana substance WANABOA, but iam sure watajirekebisha kiaina.

    ReplyDelete
  74. Clouds ilikuwa inapatikana online bongo5 lakini siku hivi haipatikani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...