Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mmoja wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Visiwa vya Ushelisheli walipokutana kwenye Kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay wakati Makamu wa Rais alipokuja kupiga kura. wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ndg. Jordan Rugimbana akisikiliza mazungumzo hayo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Dr. Shein anagombea uaris Zenji why anapiga kura Osterbay?

    Naomba majibu?

    ReplyDelete
  2. sasa Dr shein atachagua mwakilishi na mbunge wa wapi?na atajipigia kura mwenyewe ya urais? MAANA YUPO BARA NA RAIS WA ZANZIBAR KWA WAZANZIBARI TU HAPA NAUMIZA KICHWA

    ReplyDelete
  3. kwa kweli mdau wa hapo juu nami ninakuunga mkono, maana kichwa yangu inaumia pia, huyo Shein inakaaje kwa kupigia kura BARA wakati bara hatuchaguwi watu wa Zenj?? so inamaana yeye hakuchaguwa au hajahusika kabisa na uchaguzi wa Zenj?huo si ni usanii jamani? mnamchaguwa mtu ambaye yeye hata hahusiki kwenu?

    ReplyDelete
  4. Anon wa kwanza na wapili, Dr.Sheni nimakamu wa raisi na makazi yake ni Dar. Kama ulijiandikisha kupiga kura, utajua kuwa kituo chako cha kupigia kura ni eneo la makazi yako.

    ReplyDelete
  5. hapa ndo unapochoka na siasa za bongo..maana haileti maana kama mgombea mwenyewe hajipiigii kura..iweje sisi tumpigie? kweli bongo tambalale..au kuna taratibu tofauti ati yakhe? twambiane....kama nataka kuamini ule usemi wa wapinzani ati bongo tumepotea njia

    ReplyDelete
  6. dr shein hakuwa amejiandikisha kule zenji -NADHANI HAKUJUA KA ATAGOMBEA KULE

    ReplyDelete
  7. Dr. Shein alijiandikisha kupiga kura hapo Osterbay kabla hajajua kama atagombea Uraisi wa Zanzibar. Wazee wa CCM walivyotaka agombee akachukua form za kugombea Uraisi Zenji ila alishajiandisha kupiga kura bara. Kwa hiyo Huwezi badilisha unapopiga kura, unapiga kura pale ulipojiandikisha kupiga kura. Ndio, maana Dr. Shein anapiga kura yake shule msingi Osterbay leo.

    Hawezi kwenda Zenji kupiga kura kwani hakujiandikisha kulee. Halafu sheria ya Zenji inasema lazima uwe mkazi wa miaka 7 kujiandikisha kupiga kura. Dr. Shein alikuwa naishi bara baada ya kuteuliwa kuwa makamu wa Raisi. Ila sijui sheria inasemaje kuhusu mgombea na makazi yake. Ila inaonekana unaweza kuishi sehemu ingine na ukaruhusiwa kugombea ila huwezi kuishi nje ya Zenji na ukaruhusiwa kupiga kura huko lazima uwe unaishi zenji.

    ReplyDelete
  8. kwa kweli tunahitaji majibu hapa yeye anagobea uraisi zanzibar halafu an piga kura dar ya nini? au alipiga kama raia wa tanzania kupiga kura ya raisi wa tanzania halafu akaenda zanzibar kupiga kura ya raisi wa zanzibar.....? please we need to know

    ReplyDelete
  9. Haya tukubaliane na nyie mnaosema alishajiandikisha kabla hajajua kuwa atagombea Urais zenji ina maana hakujipigia kura Zenji?
    Maana navyojua mimi Wazenji wanapiga kura kumchagua rais wao na sio rais wa Jamhuri,kwa mantiki hiyo Shein hakujipigia kura kule zenji.Ipo shughuli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...