Boda boda wa mjini Songea wakimsindikiza JK kuingia uwanja wa Majimaji leo
JK akiingia kwa mbwembwe uwanja wa Majimaji, Songea, leo

JK akimnadi Dr. Emmanuel Nchimbi, Mgombea ubunge jimbo la Songea Mjini leo

Dk. Emmanuel Nchimbi akimhakikishia JK kura za wana Songea mjini
JK akihutubia wana Songea uwanja wa Majimaji leo
JK na wana CCM, akiwemo Mzee Mustafa Songambele (mwenye baraghashia) na Mh. Paul Kimiti (mwenye kapelo), wakisakata rhumba baada ya mkutano huo wa kampeni uwanja wa Majimaji
Uwanja wa Majimaji mjini Songea ulifurika leo
Wana CCM wakimlaki JK uwanja wa Majimaji leo
Sehemu ya umati wa wana Songea leo
Nyomi uwanja wa Majimaji leo










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Dk Kikwete na Dk Nchimbi tehee hee. Safi sana.
    Hao boda boda vipi, hawavunji sheria kwa kupiga misele na tuktuk bila kuvaa kofia za usalama? Trafiki hawakuona hiyo? Ukipita hivyo mtaani lazima udaiwe takrima.

    ReplyDelete
  2. MAKAMPENI YA NINI NA UTASHINDA...SASA INABOA

    ReplyDelete
  3. Jakaya mwana wa Kaya nenda baba usiogope Mungu yuko nawe kura tutakupa baba.

    ReplyDelete
  4. Kweli kabisa, Kampeni ya nini wakati mshindi tunamjua.
    Lakini, kama asipotembelea wananchi majimboni sasa atawatembelea lini?

    Wacha atembelee wadanganyika wamwone Raisi wao.

    ReplyDelete
  5. Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Tanzania utakuwa 2020, tukisharekebisha katiba.
    Katiba ya Sasa inakilinda sana Chama tawala.
    Na swala la kuviita vyama vingine vyama vya upinzani, itabidi tuache.
    Neno upinzani limekaa kinyume nume, kwani lengo la vyama vingine si tu kupindana na Chama Tawala(CCM)
    Mimi nasubiri siku Chama kingine kikichukua utawala wa nchi, je CCM nayo itawekwa kwenye list ya vyama vya Upinzani?

    ReplyDelete
  6. ILI MAANDIKO YATIMIE, NI LAZIMA JK ASHINDE. ATAIFIKISHA SISIEM MAHALI AMBAPO ITASHINDWA KIULAINI TU. HAPATAKUWA NA JESHI WALA REDET SIKU HIYO.

    ReplyDelete
  7. Absolutely BEautiful....Go Kikwete Go.....

    ReplyDelete
  8. Hadj Drogba "mwana chelsea"October 11, 2010

    Aaaah!mzee SONGAMBELE A.k.a. DOCTOR OF MINI SKIRT,huyu mzee bandugu mliokuja dar baadae sana au mliokuwa hamjazaliwa alikua ndio mkuu wetu wa mkoa hapo dar,mzee alikua mbabe huyu,aliitwa doctor of mini skirt kutokana na kupiga marufuku kivazi hicho na yeyote aliekaidi alikiona cha mtema kuni,waulizeni masister duu wa zamani watawaambia habari zake,kumbe yuko songea sasa?nimefurahi kumuona mzee huyu.Alipata kazi hiyo kama shukrani toka kwa nyerere nasikia enzi hizo alimpa nyerere lifti kwenye lori la mchanga alilokuwa akiendesha enzi hizo nyerere akiwa mwalimu pugu.

    ReplyDelete
  9. Gharama ya Tisheti,skafu,kofia,
    vibendera,vipeperushi,kanga n.k
    sibora angeweka bombi nyumba
    nchi nzima.
    Maana kushinda kashashinda ,sasa
    anaingia maghara yooote haya yanini?

    ReplyDelete
  10. Mwenyekiti habari za bongo!

    Juzi niliona mama Kikwete aliongelea kuhusu udini kwa uchaguzi, leo nimeona kwenye gazeti hili la mwananchi kwa kweli ni nimeshangaa hawa ni viongozi wa dini http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/5454-dk-slaa-awachanganya-masheikh-maimamu
    Sasa nani ni mdini hapa?

    ReplyDelete
  11. Raisi Kikwete ameshaahidi mambo lukuki.Naomba niyataje halafu wengine mtaongezea kwa ahadi nilizosahau na kufanya uchambuzi yakinifu
    1: Bajaji 400 - Mbeya
    2: Meli kubwa 1- Kagera
    3: Trekta 1 -kijiji sikumbuki
    4:Mradi mkubwa wa umeme(US $1.6
    billion)- Morogoro
    5:Kujenga uwanja wa ndege -
    Kagera,Bukoba mjini
    6:Kulipa madeni chama cha ushirika cha Nyanza(5 billions Tsh) - Mwanza
    7: Kukamilisha uwanja wa Ndege Songwe - Mbeya
    8: Kujenga nyumba kwa Kila mwalimu - Iringa
    9: Kuwajengea nyumba waathirika wa
    mafuriko Kilosa- Kilosa ,Morogro
    10:Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Nyasa
    11: Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi
    12: Kujenga uwanja wa ndege mkubwa
    Kigoma
    13: Kila mwanafunzi kuwa na laptop yake (wanafunzi kufundishwa online)
    14: Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam
    15: Kigamboni kuwa mji wa
    kibiashara(Dubai)- Kigamboni-DSM
    16:.......

    mwendo mdundo ahadi mradi siku zinakwenda CCM oyeee!!!????

    ReplyDelete
  12. Wewe Anonymous wa Monday Oct 11, 2010 ni muongon sana,kwa sababu ahadi no. 13 JK hajawahi kuahidi hicho kitu. ahadi no. 15 hiyo ipo kabla hata mwaka huu kuanza, na itakuwa kwa hisani ya watu wa Marekani na wala sio hela za Serikali yetu ya TZ,pia huo mji utakuwa kweli kama wa Dubai tumeshaona hizo picha.ahadi ya 1 bajaji 400 mbeya, haiwezekani hilo, kama una mpango wa kungoja bajaji ya JK umeulawa chuya,nunua yako ndugu. ahadi zingine ni kama wagombea wengine wanazitoa tu, nahakika JK atazitimiza zote hizo kupitia chama chenye nguvu zaidi CCM. CCM OYEEEEEEEEEE, CCM JUUUUUUUUUU.

    ReplyDelete
  13. hi!JK2010 namkubali,kama walijisemea ffu...wembe ule ule..nyoa nyoa

    ReplyDelete
  14. Hivi Chadema hawatupa taulo ndani ya uwanja wa mapambano?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...