Pichani Dk. Slaa akihutubia maelefu ya wananchi wa mji wa Mwanza siku ya Jumatano

Na Mwandishi Wetu.

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa endapo wapiga kura watamchagua kuwa Rais wao basi atawatumikia kwa kipindi kimoja na hatogombea tena mwaka 2015. Dr. Slaa ametoa ahadi hiyo alipozungumza na kijarida hiki mapema wiki hii katika mazungumzo ya kina yaliyohusu kampeni yake,mipango yake na mwelekeo wa chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuwa tangu mwanzo alipoombwa kuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi huu alishaamua kuwa akipata nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa kisiasa nchini basi hatotaka kugombea tena kipindi cha pili akimaliza muda wake wa Urais. Dk. Slaa alirejea maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere Ikulu “siyo mahali pa kukimbilia” na kuwa yeye hakuwahi katika maisha yake kuwazia wala kutamani cheo hicho, hivyo anataka kuingia kufanya aliyoahidi kufanya na kutoka kuwaachia wengine.

“Tangu mwanzo waliponiomba nilikubali nikiwa na nia ya kuwa Rais kwa awamu moja tu na kinyume na wengine sitoingia ili nitumie miaka miwili au mitatu kujifunza halafu nirudi kuomba niongezewe muda, mimi ninaingia tayari kufanya kazi kwani Urais hauna chuo” amesema Dk Slaa mara baada ya kumaliza mkutano wake mkubwa wa kampeni huko Shinyanga na akiwa anajiandaa na mikutano ya Mwanza na maeneo mengine nchini huku siku zikiwa zinakimbia kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31 mwaka huu.

Akizungumzia kwa kina uamuzi wake huo Dr. Slaa amesema kuwa pamoja na kuzingatia usia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere yeye mwenyewe alikuwa na sababu zake nyingine za kutotaka kugombea tena kipindi cha pili. “Kwanza, kiumri nitakuwa nakaribia miaka sabini ifikapo mwaka 2015 (Dr. Slaa anatimiza miaka 62 Oktoba 29) sasa heka heka za kampeni tena na mambo ya kisiasa nataka niwaachie wengine ili na mimi nifurahie maisha ya kustaafu” ameelezea.

Pamoja na sababu hiyo Dr. Slaa ameelezea vile vile nia yake ya kuhakikisha kuwa utakapofika mwaka 2015 serikali ya Chadema na chama vitakuwa vimeandaa watu wa kutosha na wenye uzoefu wa kutosha kiuongozi ili waweze kuchukua nafasi baada yake.

“Unajua CCM wamewaandaa watu wao mbalimbali kiasi kwamba wana wigo mkubwa sana wa kupata viongozi wa serikali kwani wengi wamepata uzoefu wa aina mbalimbali kwa muda mrefu.

Kwa upande wetu ninataka tutumie miaka hiyo mitano kuandaa viongozi wapya kabisa wa kisiasa nchini nje ya wale walioko CCM ambao wanaweza kuiongoza serikali.”

Pamoja na sababu hiyo Dk. Slaa amesema kuwa lengo lake ni kuanzisha mabadiliko makubwa nchini ya kusahihisha makosa ya utawala wa CCM yaliyodumu kwa miaka 49. “Ni lazima tusahihishe makosa haya,hatuwezi kuendelea na njia ambayo tunajua tayari tumepotea.

Tutakuwa ni watu wa ajabu kama pamoja na kujua tumepotea tutaendelea kwa hiari yetu kuchagua kupotea miaka na miaka, hivyo nataka niweke msingi wa mageuzi makubwa ya utendaji kazi na utawala nchini ili tuweze kuwarithisha watoto wetu na watoto wa watoto wetu taifa bora zaidi lenye mafanikio na maendeleo zaidi”

Akizungumzia mwelekeo wa kampeni yake ambayo kwa maoni ya watu wengi inaonekana kuwa na uhai wa aina yake Dk Slaa amesema kuwa kama kuna watu walifikiri ameingia katika kinyang’anyiro hicho ili kubahatisha basi wamefanya makosa.

“Tumeingia kwa lengo la kushinda na siyo kusindikiza na kinachosimama kati yetu na ushindi ni wapiga kura!” Alisema kwa kujiamini.

Akijibu swali la ni kitu gani kimemgusa hasa katika kampeni zake zilizomchukua katika kona mbalimbali za nchi yetu Dk. Slaa amesema kuwa kati ya mambo ambayo yamemgusa zaidi na kumfanya awe shime zaidi ya kuwatumikia Watanzania kama Rais wao ni hali ya makazi ya wananchi wengi kijijini.

“Wananchi wetu wengi wanaishi katika nyumba ambazo kwa kweli kabisa hazistahili kuishi wanadamu.

Yaani miaka 49 ya uhuru bado watu wanaishi kama walivyoishi kabla ya uhuru na kabla ya kuja wakoloni!,hii ni dhambi ya taifa na ni aibu” alisema Dr. Slaa.

Katika mazungumzo hayo Dr. Slaa amewataka Watanzania kumchagua kwa kura nyingi na wasitishwe na kauli zenye kuwafanya wahofie kupiga kura au kutoona umuhimu wa kura bali wajitokeze kwa maelfu,wakishikana mikono katika familia kwenda kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa Ubunge na Udiwani ili aweze kweli kupata watu wa kushirikiana nao na wenye mtazamo mmoja.

Dr. Slaa amezungumzia mambo mengine mengi kuhusu kampeni yake, ajenda yake na malengo yake kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mazungumzo hayo na Dr. Slaa yatarushwa siku ya Jumamosi asubuhi (saa za Marekani) kupitia mtandao wa http://www.bongoradio.com na baadaye yatapatikana kwa njia ya mtandao na Cds yakijumuisha mahojiano na wagombea wengine wa Uchaguzi huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ni dhahiri kinachompeleka sio njaa bali nia ya dhati ya ukombozi wa mtanzania. Tumeshuhudia udhati huo katika kipindi ambacho ameshiriki siasa tangu 1995.

    ReplyDelete
  2. kumbe ni mfanyi biashara wa miaka mitato tuuu!kwa maana hii tukimchagua lazima afanikishe biashara zake kwa haraka haraka ya miaka mitano,hana dili

    ReplyDelete
  3. WATU HEEEE,MICHUZI KAWEKA LOL

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuziiiiiii, amechukua, ameweka waaaaaaaaa!!!!CCM ooooohhhh, shangilia msiba unakujaaaaaaaaaaaaaa!!!! Jamani mnataka msikie nini tena? Tamko hili la Slaa, ni tamko ambalo si rahisi kutoka kwa kiongozi wa siasa Afrika......Mandela wetu si ndio huyu sasa, kilichobaki watanzania ni kufanya kweli tu hapo October 31!

    ReplyDelete
  5. G M NhigulaOctober 23, 2010

    Come on Dr Slaa. Ikulu siyo mahali pa kukimbilia? Hiyo mizunguko unayoifanya nchi nzima ni nini? Siyo mbio za kukimbilia Ikulu hizo baba paroko? Porojo asubuhi, porojo mchana na porojo usiku. Mbona yuko JK ndiye mpangaji mpaka 2015? VOTE JK VOTE CCM

    ReplyDelete
  6. SLAA ndio kiongozi wa kweli,NELSON MANDELA WA TZ!!Hivi watanzania tunataka tupewe nini tena zaidi ya huyu mwanafalsafa?

    ReplyDelete
  7. Tuliowaamini wametupoteza tena sana! Ni bora tuendelee kubahatisha kwa kumwamini mtu mwingine labda ataturudisha kwenye njia, hata akitupoteza naye poa. Watanzania wanaumia sana na viongozi wa ccm. 'Wafanya kazi wako laki 3 basi kura zao tumezikosa' haya kumbe wafanya biashara na wakulima ni wangapi. Mwaka huu kura hazitatosha.

    ReplyDelete
  8. for once tanzanians lets do changes we can make it if americas did it, why not us africans... use your card well on 31st october

    ReplyDelete
  9. Michuzi nakupa pongezi kwa kutoa coverage ya chama tofauti na chama fulani kwa kina namna hii. Endelea kufanya hivyo na kwa vyama vingine ili wadau ambao pia ni wapiga kura waweze kuchambua mbichi na mbivu kwa urahisi.

    ReplyDelete
  10. Dk si raha anagombea ili amkomoe JK kwa kuwa JK aliyekuwa chaguo la Mungu la Kanisa Tanzania amewageuka kwenye ile issue ya memmorandum of understanding bth Christian Church and Govt of United Rep of TZ,na hii inatokana na JK kuwa mtoto wa Saigoni hivyo ni npigo kwa wenzetu na sie na ndio maana mpaka leo hakuna Mkapa,Sumaye,Warioba,Butiku,Malachela wala yeyote aliyesimama jukwaani kumpigia debe la wazi JK,enyi Christian Churchies hebu kuweni na subra bas mpaka 2015 akija Membe mnamteua huyu Dk Si:raha kwa udini?
    Wallahi Michuzi ukibania comment hii nakupiga albadir na utakuwa unausaliti uislam kwa kutoujulisha umma.

    ZAUNUNU AMSTERDAM

    ReplyDelete
  11. hilo jina tu mtu antambua ni mnafiki, mpangaji mpaka 2015? si mpaka wajukuu wataanza nao kufanya biashara ikulu kama Ridh,,, salm,,Mir,,

    ReplyDelete
  12. Msikilize Dr. Slaa Ph.D akiongea ktk mdahalo uliorushwa na kituo cha ITV siku ya jumamosi tarehe 23/10/2010 katika linki hii hapa:
    http://www.chirbit.com/mambo

    ReplyDelete
  13. Michuzi you are a SISSY! Unajua kabisa Dr. Slaa hajasema hivyo lakini unaweka kwenye mtandao wako wa kike> Yaani sikujua kama na wewe ni shoga. What a whore!!!Ungekuwa karibu yangu ningekutemea mate mbwa we!!

    ReplyDelete
  14. we zaununu hata hk amsterdam nahisi waishi kimazali, ama kwa msaada. Huna kitu kichwani, in short, MBUMBUMBU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...