Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame amkikabidhi cheti Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame akimpongeza JK muda mfupi baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha cheti cha ushindi katika mbio za urais mwaka 2010 muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kumtangaza Dr.Jakaya Kikwete kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010.
Rais wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya tume ya Uchaguzi kutmangaza Rais Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka huu 2010 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo mchana. Picha na Freddy Maro.

MATOKEO RASMI YALIYOTANGAZWA LEO
1. KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO: 96, 933 (1.12%)

2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%)

3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%)

4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%)

5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%)

6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%)

7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP: 13,176 (0.15%)
----------------------------------------------
WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303

WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)

KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394

KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Lewis Makame leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2010 kuwa ni Ndugu Jakaya Kikwete kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).

Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yalitangazwa leo majira ya saa kumi jioni na Mwenyekiti huyo katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu , Makame alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.

Aidha Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basin a mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.

“Kwa kuwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2010.

“Mheshimiwa Kikwete Jakaya Mrisho amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Bilal Mohammed Gharib amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 20,137,303, waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha, zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64 ya kura zilizopigwa.

Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36 ya kura zote zilizopigwa, hivyo Kikwete amepata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali.

Wagombea waliofuatia ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye ni Slaa Willibrod Peter amepata kuwa 2,271,941 ambazi ni sawa na silimia 26.34 ya kura zote halali, Lipumba Ibrahim Haruna wa chama cha CUF, amepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali, Mziray Kuga Peter wa APPT – Maendeleo amepata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12 ya kura zote halali.

Wengine ni Rungwe Hashim Spunda wa NCCR- MAGEUZI amepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31 ya kura zote halali, Mgaywa Muttamwega Bhatt wa TLP amepata kura 17,482 sawa na silimia 0.20 na Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa wa UPDP amepata kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali.

Akitoa salamu kwa niaba ya wenzake badala ya Slaa ambaye hakuwepo uwanjani hapo, Lipumba alimpongeza Kikwete na Makamu huku akisisitiza suala ya ushiriki wa watu katika kupiga kura liangaliwe na kusema Rais aliyeshinda ni Watanzania wote.

Alisisitiza suala la elimu bora , ajira, ujengaji wa miundombinu na uvumulivu wa kisiasa ni muhimu, hivyo alimshauri Rais Mteule Kikwete kujiwekea malengo katika kipindi cha miaka 5 ijayo, ambayo ni uongozi wa demokrasi, ujenzi wa uchumi ajira kuboresha miunbombinu, utawala na kupamban na rushwa.

Pia alimkabidhi Rais Mteule Kikwete Ilani ya chama chake kwa ajali ya kusaidia katika utendaji wake wa kazi.


Kwa Upande wake Rais Mteule Kikwete, alitoa shukura za ushindi alioupata na kusema watazifanyia kazi changamoto zilizibuliwa wakti wa kampeni yakiwemo mawazo ya Lipimba.

Alivishukuru vyombo vya habari kwa tendaji wao wa kazi , lakini aliviomba kufanmya kazi zaidi ya kusaidia kutibu majeraha ya nchi ili kurejesha umoja na amani badala ya kuongeza chumvi.

Naye Dovutwa alisema sasa ni wakti wa kumsaidia Rais Mteule kujenga nchi malumbano yamekisha.

Mziray amesema hajakata tama ananjiandaa kwa baade , huku Muttamwega alisema matokeo yameenda vizuri.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 50 mpaka sasa

  1. Yaani na kuchakachuliwa kote huko bado asilimia ndiyo hiyo. Mhh ama kweli mwaka huu kazi ilikuwepo, ndio maana hata wale waliokuwa wanayasoma, nyuso zao zilionesha kabisa nafsi zao zinawasuta, kwa maana nyingine, nafsi, nyuso na midomo yao vilikosa ushirikiano. All the best najuo utaitia kapuni lakini message sent and delivered maana najua ili itiwe kapuni lazima isomwe kwanza

    ReplyDelete
  2. Toka Asilimia 80% mpaka asilimia 60% naona tumeenda nyuma hatua tano. Mkapa alianza na asilimia 56% mwaka 1995 akapanda mpaka 75% mwaka 2000. Hapa tumeenda nyuma tena sana. Somo la kujifunza kwa chama Changu cha Mapinduzi. Bila CCM Madhubuti nchi itayumba, hayo ni maneno ya Mwalimu Julius Nyerere.

    ReplyDelete
  3. KURA ZIMEIBIWA SANA. KWA MTAZAMO WANGU NA NILIVYOKUWA NAFUATILIA CCM HAKUPATA ZAIDI YA 51% CHADEMA SIO ZAIDI YA 38% LIPUMBA SIO ZAIDI YA 8% ZILIZOBAKI NI ZA VYAMA VILIVYOBAKI.HUO NDIO UKWELI

    ReplyDelete
  4. ONGERA MH.JAKAYA MLISHO KIKWETE KWA KUTEULIWA KUWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.

    ReplyDelete
  5. Yay!!!CCM oyeeeeeeeee!!!Kila la kheri Rais Kikwete kwa miaka 5 ijayo.

    ReplyDelete
  6. CCM.CCM,CCM JUU.ONGERA MH.KWIKWETE WASEMA OVYO NA WAENDELEE KUSEMA.UKWELI NDIO HUO NA RAIS LEO NDIO TUMEMJUA ONGERA BAB KAZA BUTI KATIKA KUTUONGOZA,TANZANIA SIKU ZOTE NI KISIWA CHA AMANI.MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA.ALL THE BEST

    ReplyDelete
  7. nani ajuaye Kikwete yu mwene.ALL THE BEST atatukisema ukweli utabaki kuwa ndio huo huo,Uchaguzi umekwisha salama so tofauti zetu tuziache na tusonge mbele.Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Africa.

    ReplyDelete
  8. Habari ndiyo hiyooooooooooooooooo.Hakuna zaidi ya KIKWETE CCM JUUUUUUUUUUUUU,KIKWETE JUUUUUUUUUUUUU.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA

    ReplyDelete
  9. Watu wenye thinking capacity ndogo huzungumza mambo ambayo hawatotoa ushahidi wakitakiwa kufanya hivyo. Suala la kujiuliza ni kwa nini idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni ndogo kuliko waliojiandikisha? kwa nini nchi inao zaidi ya watu milioni 25 wenye sifa za kupiga kura lakini hawakujiandikisha? sio kuleta propaganda za Dr Silaha katika kila jambo, tutulie tuangalie miaka 5 ijayo tufanye nini?

    KK
    Magamba Coast.

    ReplyDelete
  10. MATOKEO NDIO HAYO ASIYEKUBALI KUSHINDWA SI MSHINDANI CONGRATUATION HON.JAKAYA.MUNGU IBARIKI AFRICA,MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  11. Hongeraa Dr. Slaa! mwaka 2015 kazi ni kulinda kura za majimbo yote

    ReplyDelete
  12. WATANZANI SASA TUMALIZE TOFAUTI ZA VYAMA NA TUNACHOTAKIWA TUENDELEE NA YANAYOKUJA MBELE YETU.TUMELIDHIKA NA MATOKEO TULIYOSOMEWA MUDA MFUPI ULIYOPITA.HATA TUKIBISHA HABARI NDO HIYO.TUNAIOMBEA NCHI YETU AMANI NA UPENDO DAIMA .MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA

    ReplyDelete
  13. Ehee hasira itakayotoka hapo tutajitu. watu wengine kisasi ni nje nje!

    ReplyDelete
  14. CCM OYEEEEEEEEE KIKWETE KAZA BUTI TUNATAKA MAENDELEO NDANI YA MIAKA MITANO

    ReplyDelete
  15. Duh tumesubiri wee utafikiri uzazi wa mimba ya kwanza, lakini hatimaye matokeo yametolewa na mshindi amejulikana.

    Hongera sana JK mungu akulinde na husda na roho mbaya zao. Akujaalie afya njema na umuri ili uweze kutekeleza yale uliyoyaahidi. Na hiyo mwaka 2015 tunamsubiri mwingine tena agalagazwe kama alivyogalagazwa mchangani Dr Slaa, tofauti ya kura ni kubwa sana. JK umeshinda kwa nguvu na uwezo wake manani, maana alikupangia Mola mwanadamu hawezi kulifuta. Tunajua unapigwa vita hata ndani ya CCM na wengine walikuwa wanaombea miaka mitano hii usipate lakini wa mbili havai moja na muungwana haumbuki siku zote.

    Kama wanaweza wapande juu waende wakazibe!

    Hongera JK Hongera CCM!

    ReplyDelete
  16. Kuipindua CCM ni kuungana kwa
    vyama Pinzani.
    Vyama vingine vinajua kabisa kama
    Havitashinda lakini bado vinagombea.
    sasa si uharibifu wa kula tu.

    ReplyDelete
  17. where r other WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303

    WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
    less than nusu ndio wamepiga kura.....cant be serious

    ReplyDelete
  18. Hongera Mh.JK iliyobaki sasa ni kumwomba mungu akusaidie kutekeleza yale yote uliyo waahidi watanzania wenzako wakati wa kuomba ridhaa ya kubaki hapo kwenye nyumba nyeupe.Nawapongeza wapinzani kwa changamoto zao kubwa kwa chama chetu tawala,kwani wametusaidia kujua watanzania wa leo wanahitaji nini.CCM OYEEEEEE!!!!

    ReplyDelete
  19. Kura Milion 9 mpaka milion 5? asilimia 80 mpaka 61??
    kuna maswali mengi. Japo ushindi ni ushindi lakini huu kwa watu makini si wakushangilia.

    ReplyDelete
  20. HONGERA JK, HONGERA CCM.

    ReplyDelete
  21. NGUVU UNAYO NA NIA UNAYOO JK...KAZA BUTI MHE,,
    KIDUMU CHAMA TAWALA.....
    AKSANTE SANA ANKOL KWA KUTUJUZA KILICHOJIRI NA KINACHOJIRI JIJINI....MUNGU AKUJALIE NGUVU ZAIDI....

    NANA

    ReplyDelete
  22. Asante sana Slaa, Lipumba na wengine kwa kuchangia kupunguza kura za ushindi!

    Ndio demokrasia, yakhe!

    Na wewe Mrisho, HONGERA!

    ReplyDelete
  23. Baada ya kupata wabunge wengi zaidi CHADEMA sasa kiwango cha ruzuku kitaongezwa tumieni at least 70% kujenga chama vijijini na mikoani na kuwezesha makada. Tumieni pia wabunge wenu wengi vijana kusaka wanachama wengi kwenye vyuo vya juu na High schools. Strategies za operation sangara ziendelezwe.

    Keep it up!

    ReplyDelete
  24. hongera ndugu kikwete(samahani situmii muheshimiwa kwani siyo jadi ya watanzania ,Baba wa taifa alisema wote ni ndugu,hayo mambo ya muheshimiwa siyajui yametoka wapi),jitahidi kutimiza ahadi ulizotoa kwenye kampeni ,na ujue usipotimiza mgombea wa ccm 2015 tutamuulizia hizo ahadi,umeona mwenyewe ccm ilivyo,umeona mwenyewe ulivyohangaika peke yako kwenye kampeni,umeona mwenyewe chama kilivyo na makundi,umeona mwenyewe tulivyo POKWA na wapinzani majimbo zaidi ya hamsini(mengine yalikuwa ngome ya ccm)umeona hata huo ushindi wako si wakishindo kama 2005,sasa timiza ahadi ili umpe urahisi mgombea ajae,USANII haufai ktk mambo ya utawala hasa kwa mtu kama RAIS
    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  25. Mungu ni Mwema kwa kutupa rais tukiwa na amani. Poleni mliofiwa na ndugu zenu katika fujo mbalimbali. Hongera Kikwete rais wetu. Tuanze kazi ya kujenga taifa. Ninakuombea uchague wachapa kazi na Roho Mtakatifu akuongoze. Asilimia ya kura si hoja hoja ni kujenga nchi yetu na chama chetu CCM. Mwenyezi Mungu akubariki na aibariki Tanzania na watu wake

    ReplyDelete
  26. Hongereni washiriki wote wa ugombea wa uraisi kwa kuunga mkono Kikwete.
    Nchi ni yetu wote bwana yeye nyie sisi msiwe na kinyongo chochote ili mradi mpate saidia kwa mambo mhimu.
    Leo yeye kesho nyie na mungu anawaona acheni wenye kuumbiwa roho za chuki.
    Asusa Mwenzio atangazwa helo helo helo helo.
    Yaani alikuwa na imani kabisa atashinda? basi angetangaza tangu mwanzo kusiwe na uchaguzi aapishwe tu. Sie wananchi hatujachagua chama wajua tumechagua watu wanaofaa

    ReplyDelete
  27. Lo!Hata Jaji Makame anampongeza kwaq aibu kwani anajua kilichotendeka.
    SASA HATA MAJAJI WAKITETEA UCHAKACHULIWAJI WA KURA na watu wa kawaida watafanyaje? NI AIBU TUPU!

    ReplyDelete
  28. JK aliniacha hoi na ule wimbo wake rumba Jaka kikwete 2010,kampeni kweli anaiweza mziki wake ukiwa Ngara unausikia uipigwa kutoka redio za Burundi,si mchezo JK kiboko yao
    Ongera sana Rais Kikwete

    ReplyDelete
  29. CCM bora tu mngelikubali kilichokuwa haki yenu kutoka kwa Wananchi kuliko uhuni wa kuiba kura mlioufanya hadi mnaona hata haya ya kuendelea kutangaza huo ushindi feki katika Majimbo mengine.YOU WILL SUFFER FROM GUILTY FOR THE REST OF YOUR LIFE!

    ReplyDelete
  30. Prof LIPUMBA WEWE UMEAHIDIWA NINI NDUGU YANG!MBONA UMECHEKELEA SANA KINYUME NA MIAKA MINGINE? UNAFIKI/UDINI MTUPU!

    ReplyDelete
  31. yaani bwana siasa ni kitu cha ajabu sana eti mkapa leo anafurahia ushindi wa Kikwete haitaji mtu kuwa mjumbe wa NEC kujua kwamba hao jamaa wawili ni maadui kinoma juzi kufunga kampeni ati aliimba wimbo kumsifu ......dah jamani.The reason behind i think alijua kwamba kama slaa atakwenda ikulu wangetafutana vigogo so the only way out ni kujaribu kumsupport and i think he is pretending ili jamaa amsafishe his public image in the next five years.kwakifupi MKAPA-intelligent but also very arrogant,mbinafsi na conservative hana busara hata chembe

    ReplyDelete
  32. mafisadi oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  33. Wee anonymous wa mwisho, usimhusishe Roho mtakatifu hapa. Roho mtakatifu hashiriki kwenye uchakachuaji!

    Usimkufuru Roho Mtakatifu ni dhambi isiyosamehewa.

    ReplyDelete
  34. Hongera Chadema kwa kufurukuta kiivyo. Sasa angalieni msije kuparurana kwa hiyo Ruzuku. Mkiwacheleweshea akina nanihii mgao wao tu, mtajiju!

    ReplyDelete
  35. Dr. Slaa is to join and help wholeheartedly president Jakaya Mrisho Kikwete, for Kikwete's success is the success of Tanzanian people...Safi sana Dr. Slaa!

    ReplyDelete
  36. Hongera Dr.Slaa kwa kazi kubwa, na pole sana kwa kuibiwa. Sasa kazi iliyopo ni kudai TUME HURU mapema iwezekanavyo na KATIBA MPYA. Hapo ndio tutapata mchaguliwa halali wa wananchi.

    ReplyDelete
  37. HONGERA MHESHIMIWA RAIS. KWA SABABU YA SERA YAKO YA KUKUZA DEMOKRASIA NDIYO MAANA KURA ZIMEPUNGUA NA WALA SI UMESHINDWA!!! NDIYO MAANA TANZANIA NI MFANO WA UTAWALA BORA AFRIKA. INASIKITISHA DK SLAA HAKUONYESHA UKOMAVU KWA KUKUBALI KUSHINDWA KISTAARABU. HIVI ANGESHINDAJE WAKATI CHAMA CHAKE HAKIJAWEZA KWENDA NCHI NJZIMA? SHAME ON YOU!! HATA ILE HESHIMA NDOGO ULIYOKUWA NAYO UMESHAISQUANDER. ILIYOBAKI RAIS WETU AAPISHWE AANZE KUTUONGOZA KUIJENGA NCHI YETU NA MUNGU AMUIMARISHE. CCM HOYEEEE!

    ReplyDelete
  38. Mambo ya kufanya kwa vyama vya upinzani ni kuweka mkakati wa ushindi.

    Kuweka mgombea mmoja na si kila chama kuwa na mgombea wake, kudai tume huru, katiba kuangaliwa upya kuona kama inakidhi mahitaji ya sasa na ya baadae. Kushindwa kwa wabunge wa sisiem katika maeneo mengi ya mijini ni wananchi wenye uelewa kukataa porojo za ccm na si tu kukimbilia kusema ni kukua kwa demokrasia.

    ReplyDelete
  39. NDUGU ZANGU USHINDI WA CCM ULIKUA NI WA VEMA NA HAKI MAANA PIA SOTE TUNAKUBARI YA KUWA CCM NI ZAIDI YA KILA KITU,....HAWAKUCHAKACHUA POPOTE PALE MAANA WATU WENGI WANALAUMU SANA JUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI JAMANI VYAMA VINGINE PENGINE HAVINA SELA ZA KUWAKONGA WANANCHI......CCM NI CHAMA BORA NA WANANCHI WANAIKUBARI KWA KILA KITU....NAUNGANA NA WATANZANIA WENZANGU KUMPONGEZA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE CCM HOYEEEEEE

    ReplyDelete
  40. chadema mmejipotezea umaarufu sana kwa kuropoka kwenu na kujifanya wajuaji na kuleta mgawanyo wa kidini katika jkamii,watanzania sio wajinga hawawezi kugawa nchi kwa watu wenye udini na ukabila hatujazoea hivyo na wala hatujalelewa na kilichowadanganya ni washabiki wasio hata na card za kupigia kura.halafu wenyewe mnajipanga kuna kundi la walaji na la wasotaji so hamna msimamo,na slaa hii ndi bye bye yako nimekudharau sana na speeches zako

    ReplyDelete
  41. kuna watu kadhaa wamejiandikisha ili watumie vitambulisho kwenye mabenki na taasisi kadhaa kwa manufaa yao na sio kupiga kura,,

    hata kama Dr.Slaa ningekuwa nampenda, kutotokea kwenye kutangazwa washindi inaonesha ukosefu wa maturity, politics is a game. you win or loose, halafu hakuna chaguzi saafi; juzi juzi UK kuna wanancki wengi zaid ya millions hawakupiga kura, sometimes wamekuwa wakipiga kura watu ambao co wa UK, think about US, Canada hata france?? kote huku kuchafu.. so wabongo tujisifu kwa chakwetu sio kuendeleza utumwa wa mawazo kwamba kila kizuri lazima kipo abroad.
    G7

    ReplyDelete
  42. MUNGU IBARIKI AFRICA MUNGU IBARIKI TANZANIA.KILICHOPANGWA NA MUNGU BINADAMU AWEZI KIZUIA.TUMALIZE TOFAUTI ZETU ZA KIASIASA NA SASA TUNATAKIWA TUANGALIE TUTAFANYA NINI KWA MIAKA MITANO IJAYO.HONGERA SANA MH.JAKAYA MRISHO KIKWETE TUNAKUOMBEA AFYA NJEMA,UPENDO NA AMANI KATKA KUIONGOZA NCHI YETU.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.

    ReplyDelete
  43. MH.USIBWETEKE NA USHINDI ULIOUPATA WA KUIONGOZA NCHI TENA KWA MARA NYINGINE,USHINDI ULIYOUPATA UMESHUKA KWA ASLIMIA KADHAA UKILINGANISHA NA USHINDI ULIYOUPATA MWAKA 2005.HII INAONYESHA KUWA UTENDAJI WAKO WA KAZI ULIPUNGUA.TUNAWASHUKURU WA PINZANI KWA CHALLENGE WALIZOTOA NA NADHANI SASA UTAONA KUWA KAMA UTACHEZA TENA KWA MIAKA HII MITANO KUNAUWEZEKANO MKUBWA SANA KWA MWAKA 2015 CHAMA CHA MAPINDUZI KIKAPUNGUZA KUWA NA WABUNGE WENGI NA MADIWANI NA VYAMA VYA UPINZANI VIKAWA NA ONGEZEKO LA WABUNGE NA MADIWANI.HII HIWE NI FUNDISHO TOSHA KWA CCM NA MNATAKIWA MJIPANGE KWA MIAKA MITANO IJAYO.MH J.K Hongera kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamuhuri ya tanzania.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.

    ReplyDelete
  44. MH.USIBWETEKE NA USHINDI ULIOUPATA WA KUIONGOZA NCHI TENA KWA MARA NYINGINE,USHINDI ULIYOUPATA UMESHUKA KWA ASLIMIA KADHAA UKILINGANISHA NA USHINDI ULIYOUPATA MWAKA 2005.HII INAONYESHA KUWA UTENDAJI WAKO WA KAZI ULIPUNGUA.TUNAWASHUKURU WA PINZANI KWA CHALLENGE WALIZOTOA NA NADHANI SASA UTAONA KUWA KAMA UTACHEZA TENA KWA MIAKA HII MITANO KUNAUWEZEKANO MKUBWA SANA KWA MWAKA 2015 CHAMA CHA MAPINDUZI KIKAPUNGUZA KUWA NA WABUNGE WENGI NA MADIWANI NA VYAMA VYA UPINZANI VIKAWA NA ONGEZEKO LA WABUNGE NA MADIWANI.HII HIWE NI FUNDISHO TOSHA KWA CCM NA MNATAKIWA MJIPANGE KWA MIAKA MITANO IJAYO.MH J.K Hongera kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamuhuri ya tanzania.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.

    ReplyDelete
  45. Binafsi nimeridhika! nilitamani icheze kwenye 51% au kama ile ya Shein! sijui mheshimiwa ujumbe ameupata! au itakua yale yale!

    ReplyDelete
  46. NYIE MNAOZUNGUMZIA UDINI NA UKABILA WOTE NI WAPUMBAVU. HAMNA CHA UDINI WALA UKABILA HAPA.

    CUF INA WAISLAM WENGI KWAKUA IMENZIA ZANZIBAR NA CHADEMA WACHAGGA WENGI KWAKUA MWANZILISHI NI WA HUKU, UNATEGEMEA NINI?

    TANZANIA HAINA UKABILA WALA UDINI, MNAO SEMA SEMA KUHUSU UKABILA MNACHAFUA SURA YA NCHI YETU. SHINDWENI NA MASHETANI YENU HUKU.

    MNATUMIA HIO LUGHA YA UKABILA NA UDINI ILI WATU WAPATE HOFU TU. JAMANI WE ARE ONE,NA SASA KWAKUA RAIS KISHACHAGULIWA, TURIDI KATIKA UJENZI WA TAIFA,NA RAISI WETU JK MUNGU AMJAALIE AFYA NA UWEZO WA KUTIMIZA AHADI.

    VYAMA VINGI NDO MAENDELEO ANAE LALA ANAAMSHWA SIO KUNG'ANG'ANIA CHAMA KIMOJA TU.

    HONGERA JK, WE NDO UMESHINDA, SO KEEP THE BALL ROLLING

    ReplyDelete
  47. Prof. Lipumba...next time gombea japo ubunge/uwakilisji manake tumechoka kuona jina lako katika kugombea urais.

    ReplyDelete
  48. Huu ukabila na udini umeanza lini? JK alipoingia Ikulu na asilimia 80 ya kura alizipata kwa watu wa dini moja au wa kabila moja?
    Nani aliyeingiza mambo ya dini au kabila kwenye uchaguzi huu?
    Mbegu ya siasa za makundi za CCM imeanza kupandikizwa kwenye ngazi ya taifa. Watanzania mnachotakiwa kufanya ni kumkataa shetani, na nguvu zake zote na kazi zake zote!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...