Kaka,

Kuna huyu jamaa yetu mjasiliamali akiitangaza utalii na vivutio vyote muhimu vya Zanzibar kwa Wataliano.

Ni vizuri kutumia mikakati kama hii na hata kumpatia kijana huyu tenda ya kuvutia watalii toka Italia na kama kuna wengine wajuao Kijerumani, Kijapani, Kichina, Kispaniola n.k pia wapatiwe tenda na TTB, Precisionair, Speedbots n.k.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Mume Wangu, Mikanjuni TangaNovember 24, 2010

    Mshikaji kwa hivyo unavyokitafuna kiitaliano, mademu wa kitaliano lazima watakuwa wanakuzimia sana.
    Ukiwapatia nafasi usiwaache, wanajua killlla kitu kwenye malavi davi na wanatuzimia wamatumbi.

    ReplyDelete
  2. Safi Sana Kaka!!! Kamua ila Mwana Ukipita mtoto wa kitaliano ndani ya 18 yako ahhh nenda kachukue Passport YA EU mbele ya safari...

    ReplyDelete
  3. Nimecheka sanaaaa, lo! jamaa ni muongo, haongei kitaliano, Nimecheka sanaa, mimi ninaishi hapa Italy na hakuna ambaye amemwelewa. hahahaaaa

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa Wed Nov 24, 09:46:00 AM wewe ni Mnafiki. Hicho ni Kitaliano na kila mwenye kuongea kitaliano anamuelewa vizuri sana jamaa anazungumza nini. Fitna hazijengi. Huo ni Ushoga.

    ReplyDelete
  5. Hii inatia moyo, ni vizuri pia watanagze kipare, kingoni, kindengereko ili kutuvutia na sisi au hawataki watalii toka Tanganyika?

    ReplyDelete
  6. anon-094600am
    sasa jamaa kama haongei kiitaliano anaongea nini, mshikaji yuo fit. ila kama anongea kindengeleko cile. yaangi wakati anataja email nimesikia yahoo punto com, duuuu safiiiii

    ReplyDelete
  7. Nimeisikia Fiorentina mara kadhaa..halafu na Katoliko na Anglicano..then nikainyaka presso..amenimaliza hapo kwenye kutaja namba za telefone..very interesting. Tatizo serikali haithamini vipaji na juhudi binafsi za kuliletea taifa maendeleo.

    ReplyDelete
  8. HALAFU WATU WENGINE FITNA SANA NA ROHO MBAYA..WEWE FALA WA HAPO JUU UNAYESEMA HAONGEI KITALIANO ,ANAONGEA NINI SASA,MBONA UNAKUWA KAMA MWANAMKE ALIYEKOSA BWANA WA KUOLEWA NAYE....ACHA HIZO NDUGU YANGU FITNA HAZIJENGI WALA NINI,TUNATEGEMEA NYINYI WA NJE MJENGE KUMBE MNABOMOA...NIMESIKITISHWA SANA NA COMMENT YAKO..AU KWA SABABU HUONGEI KITALIANO KAMA YEYE....DAAA KAMA NI MWANAUME BASI UNAHITAJI UKAKAE LAMU,MAANA HUKO WENZAKO KAMA WEWE NDIO WANAPELEKWA.

    ReplyDelete
  9. haya ni Maoni tu: Ingekuwa vizuri kama kungekuwa na tafsri yake katika lugha nyingine haswa Kiingereza (kimaandishi) ili kuvutia watalii wengine wa bara hilo la Ulaya.

    ReplyDelete
  10. Buorgiorno! Habari gani!
    Du huyu jamaa anaongea kile kitaliano cha fierontina.

    Haya kazi kuitangaza Tanzania kwa youtube kwa ligha zote kama Juma Mauno. Mkiwa huko China, Japani, Korea, Spain mjifuze lugha kwa bidii na kuposti clips fupi kuelezea utajiri wa sekta ya kitalii Tanganyika na Zanzibar.

    ReplyDelete
  11. Huyu jamaa hapa kangangania tu kuhusu Bara mara Tanganyika utamjuwa mtu tu akitaka kuharibu Rumu? Jamaa anaongea kitaliano sema broken Italy, ZNZ nimeenda watoto wengi pia sehemu za Beach wanaongea kitaliano.

    ZNZ kitu kimoja hawajui wataliano sizani kama watalii wengi wana ma hotel na makazi yao wanatumia Kuingiza UNga ndomana znz vijana wengi mateja. na historia ya hawa jamaa walifukuzwa Mombasa baada kufatiliwa na FBI wengine.

    Wewe unaoongelea avutie watu bara kwani si hapo tu nenda mbona mie naenda wewe basi wavutie na wao waje kwako. KK

    ReplyDelete
  12. Jamaa naamini anaongea Kitaliano ila mzizi wa fitna utakatwa tumtafute jamaa wa michuzi yule mwenye jina la kimakonde atakuja kutumalizia kaka tafsiri msimuonee wivu jamaa. no problemo mtapata tu kula Red lobster.

    wacheni wataliano walete White Lobster tu.

    ReplyDelete
  13. je huyu jamaa anafanya kazi kwa niaba ya zanzibar?au ni mkenya huyu?mlima kilimanjaro mara nyingi kama ni wao.kwa kila hicho kiluga anacholonga sina aidia nacho muhimu nani kamtuma kama sisi wabongo ni sawa kama katumwa na mtu mwingine basi sisi tuendelee kulala tubaki kama watoto gari la baba lileeeeeee wakati baba hata baiskeli hana.na wale wanaoshangalia uzinzi je watafurahia kwa mama zao,dada zao au jamaa zao uki,kimwi tuogope

    ReplyDelete
  14. mbona arusha watu wanaongea kila lugha huku duniani mpaka kimongolia

    ReplyDelete
  15. Mimi nawahakikishieni kabisa, kuwa jamaa ana ongea vizuri kabisa,kushinda hata wengine wameenda shule ya lugha hii, lakini hawamfikii kabisa, na wengi tu nawajua wamesoma kabisa darasani lakini wameambulia hola...lakini hawaongei vizuri lugha hii, ila sema rafuzi yake ya kikabira cha watu wa mkoa wa Toscana,kama vile kwetu wasukuma au wamasai wakiongea kiswahili lazima tu! ucheke ile mbaya. Kama kweli amejifunza hivi hivi kisela basi nampa hongera sana. Ila nimecheka sana tena sanaaaaa.....!!!!! Pia anaonekana ni msanii sana huyu jamaa. Hongera sana mshikaji.

    CHIBIRITI.

    ReplyDelete
  16. MBONGO MFUNDISHE LUGHA YOYOTE ILE ATAIMASTER IN A SHORT OF PERIOD TIME NA ATAIONGEA KWA MBWEMBWE NA KUSIMAMIA.
    EXCEPT ENGLISH. WE ARE ALLERGIC TO IT.
    teh teh teh

    ReplyDelete
  17. Ivi anajua kiswaha?

    ReplyDelete
  18. http://www.youtube.com/watch?v=8StD-PfxPMM&feature=related

    ReplyDelete
  19. acheni wivu jamaa anaongea kitaliano safi kabisa na kinaeleweka kabisa, znz vijana wengi sana wanaongea kitaliano,french, kijerumani, kispain, na lugha tafauti nyengine, unaweza kumkuta mtu anaongea lugha zote izo kwa pamoja na sawasawa kabisa kama wanavyoongea wenyeji wa lugha hizo, swali langu ni inakuwaje wenye izo lugha zao wanawaelewa kisha nyinyi wengine mseme hawaeleweki? izo ni chuki binafsi na hazifai, hakuna kisowezekana ulimwengu huu, jifunze tu utaelewa.

    ReplyDelete
  20. Jibu la kwa nini huyo mnoko haelewi anachoongea mjasiriamali ni veeere simpooo, ni kuwa yeye haelewi kabisa kiitaliano. Kuishi italia haimaanishi kuwa ni lazima anaijua lugha ya italiano.

    Wapo wabongo wanaishi ughaibuni na hujikusanya na wamatumbi wenzao popote na kokote waendako na lolote wafanyalo miaka na miaka. Wanaongea kimatumbiii, wanasikiliza muziki za kimatumbii, n.k, n.k. Tofauti kubwa ni kuwa tu yupo nchi au bara nyingine/lingine, lakini kila kitu chaenda kimatumbi matumbi tu. [Sina maana kuwa kimatumbi ni mbaya, kamwe sikandii]. Kwa hiyo huyo mjamaa asijifanye jaji wa hiyo lugha wakati hainyaki.

    ReplyDelete
  21. Waosha vinywa pigeni kelele, lakini huyu Hamisi Mauno Mtaliano ameshapata hits karibu 10,000 ktk Youtube.

    Sasa lazima tumpongeze kwa kutangaza utalii wa Zanzibar kote duniani kupitia youtube na siyo kama wengine wanajulikana mitaani kwao Arusha, Lamu au Zanzibar tu.

    Hapa huyu jamaa lazima tumkubali kwa kwenda hatua moja zaidi mbele kuifanya kazi yake kama guide wa watalii/beachboy kwa kutumia teknohama. Ujumbe siyo kwa mdomo tu bali hata kutumia youtube ya buree.

    Watanzania wengine wenye vipaji vya lugha za kigeni, tumieni teknohama kujiongezea kipato cha ujasiriamali na pia pato la nchi yenu tu, siyo oh mi najua sana kiingereza, kichina, kihispaniola, kigiriki n.k lakini tunashindwa kuitangaza ipasavyo Tanzania.

    Pia asante Chibiriti wa Cesena Italia kutufafanulia kuwa kama ilivyo kiswahili cha Umasaini, Usukumani, Kisiwa Panza, Ntwara, Karagwe, Kasulu n.k pia hata lugha ya Kitaliano kina lafudhi mbalimbali.

    ReplyDelete
  22. Ni kweli mtanzania na kiingereza chako ukishuka Liverpool, England ukaingia mitaani utatoka kapa na Kiingereza chako.

    Hivyo huyo jamaa anayesema anaishi Italia lakini hamuelewi mjasiriamali Hamisi Mauno, ni kwa vile bado ki-taliano chake siyo kama cha wenyewe Wataliano.

    ReplyDelete
  23. its good anavyo advertise kwa rugha ya italiano,but nafikiri wakati anaongea angejaribu kuonyesha na sehemu yenyewe artilist some of it,kusudi waamini what hes trying to sell.

    ReplyDelete
  24. Nendeni mkaitangaze Tanzania kwa ligha zote duniani kupitia huduma ya bureeee ya youtube.

    Hongera mjasiriamali kwa kuanza kampeni hiyo, wengine tutafuata kwa Kiswidishi, Kifinishi, Kidenishi, Kijerumani, Kipolishi, Kiarabu, KiFarsi, Kichina, Kikorea, Kimandarini, Kipotugizi, Kifaransa na kieskimo.

    ReplyDelete
  25. we anony wa nov 24, 12:45 fala sana. sasa umemshushua mwenzio nini na wewe unaongea nini kifalafala hvyo? una mama wewe? umemtusi naye hapo

    ReplyDelete
  26. artilist??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...