Profesa Alec Chemponda na mai waifu
wake Mama Rita Chemponda.
Mhadhiri mstaafu huyu wa chuo kikuu cha Dar es salaam University na mwanasiasa wa siku nyingi muda mfupi uliopita amechukua fomu za kuwania Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutimiza idadi ya wagombea kuwa 13.

Wengine ni Spika anaemaliza muda wake Mh. Samuel Sitta, Naibu Spika anayemaliza muda wake, Mama Anne Makinda, Mbunge-mteule wa Bariadi-Mashariki, Mh. Andrew Chenge, Mbunge-mteule wa Kongwa, Mh. Job Ndugai, Mbunge wa Afrika Mashariki Mama Kate Kamba, Mbunge wa Viti Maalumu Mama Anna Abdallah na Luteni Mstaafu Benedict Lukwembe.

Wengine ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Saint Augustine University (SAUTI), Bw. Stephen Deya, Mjumbe wa Baraza la vijana mkoa wa Pwani Bw. Mohammed Nyundo, Kada wa CCM Bw. Kazimbaya Makwega, Kepteni Mstaafu Peter Nyalali na Mwalimu wa Shyule ya Sekondari ya Tambaza, Mwl. Salum Kungulilo.


ha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. duuuuuuuuuuuuuuuu ile picha ya kwanza ilikuwa noma bora umewahi kitoa wangeosha sana vinywa wadau

    ReplyDelete
  2. All the best Dr Che-Mponda.

    Mwanaharakati

    ReplyDelete
  3. sorry ni spika wa Bunbge la muungano au wa CCM?Maana naona sioni mzanzibari hawana sifa au wamesusia,hebu tuwekeni sawa hapa kama kweli kuna uwiyano wa Muungano,naomba isibanwe hii

    ReplyDelete
  4. Dokta....Kila la kheri.....Tunaamini ukipewa unaweza...na hutakuwa biased

    ReplyDelete
  5. Let Tanzania get something right for the change. Dr. Che-mponda anafaa kuwa spika. Lakini siasa zetu mmmmhhh!

    ReplyDelete
  6. All the best Dr. Chemponda.

    Nice pic.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. I am impressed! He can do the job! Best Wishes Dr. Aleck Che-Mponda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...