Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania LTD,Mama Rahma Al. Kharoos akizungumza leo wakati akitangaza kuisaidia Taasisi ya Popular Sports and Entertainment ambayo imeandaa Bonanza la watoto wapatao 600 toka katika vituo 10 vya kulelea watoto yatima vya jijini Dar.Mama Rahma Al-Kharoos ametoa kiasi cha sh. Milioni 4 taslimu kwa ajili ya kuwezesha kufanyika kwa tamasha hilo siku ya jumapili,Novemba 21 katika viwanja vya Lidaz Klabu.
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania LTD,Mama Rahma Al. Kharoos akimkabidhi kitita cha sh. milioni 4, Mkurugenzi wa Taasisi ya Popular Sports and Entertainment Tanzania ambao ndio waratibu wa Bonanza hilo,Osman Kazi katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Coco Beach,jijini Dar.
Timu nzima ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania LTD ikiongozwa na Mama Rahma Al-Kharoos (kati) wakiwa na baadhi ya viongozi wa vituo vya kulea watoto yatima pamoja na baadhi ya watoto hao walioweza kuhudhulia hafla hiyo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. hivi kwanini watu wanaotowa misaada huwa wanataja kiwango cha pesa au garama wanazotumia kwenye misaada hiyo? tena ukizingatia wengi wao ni waislam kama hawaelewi sadaka haitakiwi hata mkono wa kulia au wa kushoto ujue ni kiasi gani unagharamia.wanapotaja inakuwa kama showoof au propergander fulani.
    wangesema tuu tamasha la watoto ......leaders club mdhamini wamtaje lakini garama iwe siri how abt that?

    ReplyDelete
  2. Jamani wewe mwanamama ni mzuri...sitasema zaidi...!!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza nakuunga kwa sana, hiyo ni sadaka sioni sababu ya kuitangazia dunia, Mungu atakupa thawabu na sio binadamu!

    ReplyDelete
  4. Wee sifia wanawake za watu utanyofolewa macho au unataka kwenda kufia Segerea!nawasilisha

    ReplyDelete
  5. Mi naona huyo jamaa anataka kufia segerea..we una sifia sifia tuuuu..wengne wana wivu sana jamamn angalien msije ripotiwa.!

    ReplyDelete
  6. Tooba hajui mwenzenu msaidieni....kaka kabla ya kusifia chunguza mjomba utabaini sio kusifia tu...utafia segerea kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...