Habar za kazi kaka michuzi.hongera kwa kazi nzuri ya kutupa taarifa mbalimbali ktk blog yetu ya jamii.
Naomba msaada,uniwekee post yangu hii katika blog yetu pls!

mimi ni msichana,umri wangu ni miaka 26.elimu yangu ni form 4,na kwa sasa nafanya kazi ya ualimu huku kilimanjaro. nimekuwa ktk relation mara 2 kwa wakati tofauti ila tatizo ni kuwa najihis nina bahati mbaya,bcoz kila niliyedate nae alikuwa tayar ktk uhusiano. so mimi nimechoka kuwa mtu wa ziada.ndio maana natafuta mtu aliye serious ili tufanye maisha.nipo tayar kupima HIV,na hata kama atahitaji tuchunguzane kwa muda nipo tayari kwa aliye muaminifu.
weka email yangu,ili kwa atakae kuwa tayari tuwasiliane,
na endapo kuna maswali nitayajibu.
Thanx!
marryjoseph84@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Mdogo wangu Mary, you want to get married on your time, and you have been trying to find the right person because you want to certify your will, but Nakushauri to wait on GOD'S WILL, atakapokuwa tayari atakushushia Mume aliye mwema. Ukiona relationship hazi-work out, maybe there something you need to finish before you get married. Chunguza familia yako kama kuna kazi ya kufanya na kumaimaliza malizia kwanza kwa marriage ni kazi nyingine, hutapata muda wa kurudi nyuma.

    ReplyDelete
  2. Binti, najua societal pressure ya kuolewa kwa mwanamke Afrika ni kubwa mno. Shangazi anauliza, wazazi wanauliza, ukienda likizo kwa bibi na babu wanauliza kwamba kwa nini hujaolewa - pressure inakuwa kubwa mno. Matokeo yake watu huishia katika mahusiano yasiyokuwa mazuri na ndoa zao kushindwa kudumu. Ukitaka kujua kuwa ni societal pressure tu, njoo huku Marekani utaona kuwa binti wa miaka 26 wala hafikirii habari ya kuolewa na jamii haioni ajabu.

    Sasa utamchunguza vipi mtu ambaye yuko Dar au Ulaya au Marekani kama mimi wakati wewe uko Kilimanjaro? mary, kuwa mwangalifu usije ukajikuta unaongeza wanaume wengine kwenye list hiyo ya wawili. Hata ukiwapata kwa tangazo hili, uwe makini mno na wanaume wanaotaka kulala na wewe kabla ya ndoa.

    Ni mimi kaka yako,

    Kalikali

    ReplyDelete
  3. Anony hao juu ushauri wako nimeukubali.Ni kama vile sauti kutoka kwa Mungu!

    ReplyDelete
  4. wewe mdau wa mwanzo una maana gani unaposema Ukiona relationship hazi-work out, maybe there something you need to finish before you get married. Chunguza familia yako kama kuna kazi ya kufanya na kumaimaliza malizia kwanza kwa marriage ni kazi nyingine,?

    Are you for real? unaishi karne gani mwenzetu?

    ReplyDelete
  5. Wee anon wa hapo juu, nawe msaidie kumuombea mwenzako anaitaji mwenza, hayo maswala y familia yapo pale, muoombe mwenzako apate mume nae awe na familia yake, ndivyo generation inavyoenda majukumu yapo muda wote.

    ReplyDelete
  6. Si mnataka wanaume wenye pesa zao tayari? sasa unategemea nini? mtaendelea kuwa watu wa ziada tuu kwa mustakabali huo.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa kwanza mary mwenyewe, ameandika ishu yake kwa kiswahili, sasa wewe kutujia na kiswanglish inahusu? Mary mwenzangu ebu tafuta kwanza kozi fulani manake kidato cha nne peke yake mh, na hakika ukiwa chuoni utakutana na mtu wa ukweli.

    ReplyDelete
  8. Mary nakushauri usubiri, Kama anonymous happ juu alivyoshauri. Mimi mi mwanaume na sijaoa lkn bado nakubaliana naye wa hapo juu. 9 ya mwanadamu 10 ya Mungu. Subiri, mwanamke kamili silo ndoa Bali uwezo wa kujitengenezea maisha. Olewa ukiwa na miaka 28 jipe hui miwili kujitafutia msingi. Wanaume wa sasa hutaka Demu mchanga Kama wewe wakuchezee ktk ndoa wakuache. Tulia.

    ReplyDelete
  9. Dada bado ungali binti mdogo sana, angalia uwezekano wa kuendelea na masomo yako. Then kama siyo riziki unaweza kuwa na maisha yako tena mazuri tu. Kuolewa ni bahati tu. Weka mambo sawa kwanza.

    ReplyDelete
  10. Mary, umepewa ushauri wa kutosha, hivyo fanyia kazi. Watu wengi hupata marafiki / wenzi shuleni lakini zaidi vyuoni, kama una UWEZO wa kiuchumi, weka azma ya kusoma, soma sana na kwa vile miaka ya kusoma si michache katika wakati huo wapo watakaokuwa na nia nawe, utakuwa na muda mzuri wa kuona kama ni chguo la Mungu kwako au la. Katika karne tuliyonanyo pamoja na mapenzi Wanaume wanavutika katika mahusiano na Wanawake WEPESI amabao kwao si mzigo, sasa fanya tafakari je, ushakuwa MWEPESI , njia ya kuwa mwepesi ni KUSOMA na kujiimarisha. Ndipo unaweza kushauriana na mwenzako bila kubezwa na kuonekana huna mchango wa maana.
    Lakini pia usitumie TEKNOHAMA kupata mwenza wa maisha, nachelea kusema hatari ni kubwa kuliko faida.

    ReplyDelete
  11. Njoo Marekani ndo utajua maana ya kuolewa ni nini!! Miaka 26 tu unaona umechelewa. Hao wanaume kama walikukimbia usilalamike ni kwamba Mungu alikuwa anakuepusha kitu fulani katika maisha yako. Kwa hiyo anao mpango mwingine kwa ajili ya maisha yako ya baadae. Mimi nina miaka 36 lakini sifirii cha kuelewa leo wala kesho kutwa na subiri tu mpango wa Mungu. Naamini siku moja itatokea haki yangu kutoka kwa Mungu.
    Kwa hiyo vuta subira umri wako bado mdogo sana mdogo wangu.

    Mdau Dodoma.

    ReplyDelete
  12. WASHAURI WAZURI WATAMPELEKEA USHAURI KUPITIA ANUANIA YAKE YA E-MAIL NA SIYO HAPA. YEYE AMEWEKA ANUANI HIYO ILI APATE USHAURI AMBAO ATAUPIMA NA SI KUANZA KUMFEDHEHESHA KAMA WENGINE WANAVYOJARIBU KUFANYA KUTOKANA NA KUTOKUWA NA ELIMU YA URAIA INAYOWAFANYA WATU WAHESHIMIANE.

    ReplyDelete
  13. We anon hapo juu elewa swali, ameweka email kwa jamaa aliye tayari kuwasiliana naye na sio kuwa tumjibie kwa email yake, hapa anapata ushauri tu ambaye yuko tayari ndo amwandikie kupitia email yake full stop!

    ReplyDelete
  14. Dada Mary, pole sana. Nafahamu kiu ya ndoa. Lakini dada yangu nakushauri, tulia. Halafu ushauri wangu zaidi ni kwamba, hao wawili tayari wamekwisha kuwa kipimo tosha kwako kwamba hakuna ambaye alikuwa na nia ya ndoa na wewe bali kukuchezea tu. Hebu subiri.

    Mimi ni mwanmme ninayekushauri dada yangu, nasikia uchungu sana kwa umri wako huo kulilia kuolewa. Tulia, omba msaada wa kujiendeleza, na siyo kupata ndoa. Ndoa huja miongoni mwa maisha.

    Sasa basi, nakupa ushauri, kuanzia sasa, tulia, usijitoe mwanaume yeyote akujaribu, wewe siyo mbiga ili kujua chumvi imekolea au la. Na angalia sana, watakuja wengi sana kwa sasa, lakini wengi wao watakuwa kama wale wa wawili wa mwanzo. Ukiwa na papara ya kuolewa nahofia utaishia kupata homa mbaya.

    Kama ni wa kuolewa dada, utaolewa. Mume wako Mungu anakutengenezea. Tulia binti, usione watu wanaishi, kuna magumu humo kwenye ndoa, hata unaweza kuja kujuta kwa nini ulilia.

    TULIA, MUME MWEMA ANAKUJA ATOKA KWA BWANA. USIMTAFUTE KWENYE MITANDAO, UTAPATA HOMA.

    ReplyDelete
  15. Why not, bahati ilioje - inawezekana ndugu yangu. Nimeshatanguliza email, nichekie.

    ReplyDelete
  16. 26 MBONA BADO MDOGO WEE...POOZA PRESSURE ZA BONGO ZITAKUFANYA UPATE MWANAUME ASIYE NA MBELE WALA NYUMA....WEE MUACHIE MUNGU ULIMWENGU WA SASA WATU WAKO 38 NDIO WANAANZA KUCHANGANYIKIWA. ACHANA NA MAMBO YA PRESSURE ZA KIZAMANI. SIKU HIZI NDUGU YANGU TAKE YOUR TIME UTAPATA TU LAKINI UKIKIMBILIA MWANAUME KWA AJILI YA PRESSURE ZA WATU UTAPATA MWANAUME LAKINI UNAWEZA KUPATA BOMU UKAISHIA KUTESEKA MAISHA YAKO YOTE IMAGINE UTESEKE ANZIA UMRI HUO MPAKA UZEEKE...SUBIRI SUBIRI UKIPATA MWANAUME SIKU HIZI 30 IS THE NEW 20S....

    ReplyDelete
  17. Mary wee baado mdogo sana

    Miaka ya zamani ilikua kuolewa ni 16, halafu ikaja 23, ikaja 28 sasa hivi average ni 34 tulia tu bado hujachelwa kabisa...

    Njoo USA uone dada zako wapo mtaani happy bila wasiwasi.

    Bongo wameshachoka na mafumbo yao. Ulimwengu wa leo ukiolewa ni wewe kwa hiyo pressure za watu zisikulaze macho

    ReplyDelete
  18. mimi nimeoa nikiwa na miaka 36, na nimejariwa kupata mtoto wa kwanza na mke wangu mwaka huu..kwa kweli kuwahi kuoa au kuolewa kwa dunia ya sasa sio deal tena, sasa sana ukiwa na papala wanaume watakuwa wanakuchezea na kukuacha kwenye mataa , kuna methali ya kiswahili isemayo " chema chajiuza kibaya chajitembeza" jaribu kuwa " chema" na sio"kibaya" nafiri umenielewa nina maana gani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...