Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa shambani kwake Kibaoni kwa maandalizi ya kupanda mahindi mh yupo nyumbani kwao kwa mapumziko ya Krismasi na Mwaka Mpya. Picha na mdau Chris Mfinanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Rais wetu 2015.

    ReplyDelete
  2. Kweli unamuenzi Baba wa taifa. Ungekuwa mkali kidogo tungekupa urais ujao,lakini bwana wewe mpole sana itabidi apewe Magufuli ili asiwe na mpinzania.Hongera mtoto wa mkulima kwa kuonyesha vitendo kilimo kwanza.

    ReplyDelete
  3. Naona ameamua kupromote Tusker...hivi hakuna Tshirt za Kilimo Kwanza?

    ReplyDelete
  4. mdau hapo juu, unamjua waziri wa ulinzi? huyo ndo raisi wetu 2015 piga ua!

    ReplyDelete
  5. MGUMU ASILIA!SURA YAKE INAONYESHA!! SAFI SANA!!

    ReplyDelete
  6. SAFI MH WAZIRI MKUU
    WEWE NA WACHACHE KAMA WEWE
    ONYESHENI NJIA NA NYINYI WENGINE
    MFUATIE
    MLIMGOTINI..MWENYE KIJIJI CHAKE

    ReplyDelete
  7. mtoto wa mkulima naona unawajibika, mambo ya kilimo kwanza

    ReplyDelete
  8. mheshimiwa ni mtu mchapakazi. ni mfni mzuri sana anaotoa sio kama waheshimiwa wengine.ukali kama huna busara haufai.

    ReplyDelete
  9. THAT'S THE WAY WE LIKE IT.MAKES ME PROUD AFTER A VERY LONG TIME.MAY YOU BE BLESSED.

    ReplyDelete
  10. watanzania huwa hatuna fikra pana na kuona mbali, mtu anakuwaje mchapakazi wakati ananyamazia masuala nyeti ya rushwa na kujiweka kando na vita ya mafisadi? kama mtoto wa mkulima angekuwa na uchungu basi na nchi, siyo kuwa yes man,
    hii picha ni kujitafutia umaarufu tu, siyo sign ya kiongozi bora hiyo.

    ReplyDelete
  11. Ama kweli si tu ni mtoto wa mkulima bali yeye pia ni mkulima. Analima huku anatangaza tusker!! Mdau wa hapo juu waziri wa ulinzi atakuwa rais wa Visiwani sio Bara!

    ReplyDelete
  12. Mkulima wa Tanzania anavaa nguo mbovu na zenye madoa ya mazao anayolima, hana viatu, na anatumia jembe la mkono.

    ReplyDelete
  13. Nadhani ni vizuri kuonyesha kuwa unajali na kwamba maisha ya mtanzania yanatakiwa kuwa simple to the earth. Lakini mimi nalipinga hili. Mfano anaouonyesha WM wetu siyo sahihi, siyo sahihi kwa sababu, anachoonyesha ni kilimo cha jembe la mkono jambo ambalo halitakiwi kufikirika hata kidogo. Kiongozi wetu atuonyeshe mambo makubwa, kwa kuwa na eneo kubwa, machine za kilimo, ma meneja kilimo na atueleza kuwa kilimo anachofanya ni cha kiviwanda, amekopa kiasi kadhaa (Kwa sababu huwezi kushiriki kilimo cha biashara kweli kwa fedha zako), ameweka bima (Na atuambie shirika lilomwekea bima ya shamba lake), na atuambie soko la mazao yake. Suala la 2015 siyo mahala pake hapa. Najua mh. WM ni muadilifu, hilo halina ubishi lakini nadhani abadili gia ya hizi stori nyepesi nyepesi.

    Happy Holidays Season.

    ReplyDelete
  14. Mdau hapo juu nakwambia tena waziri wa ulinzi ndiye kidedea 2015 tuombe uzima uone mambo, usilolijua litakusumbua!! wakati vuguvugu la kumchagua mgombea likianza ntakukumbusha urudi nyuma kwenye hii picha ya mtoto wa mkulima ndiyo ujue nani kajura!
    christmas njema

    ReplyDelete
  15. Mifano ya kila namna ipo. Mdau unayetaka kiongozi atoe mfano kwa kuwa na mambo makubwa kama eneo kubwa, mameneja kilimo nk usiwe na shaka maana mfano huo upo. JK kwenye kampeni zake alituambia kwamba katika ushiriki wake yeye wa kilimo ana mijing'ombe lukuki katika eneo kubwa.
    Mizengo bado hajapiga hatua unayoitaka mdau lakini kutopiga hiyo hatua si sababu ya kumzuia kushiriki katika kilimo kwa kadri ya uwezo wake yaani kwa kutumia zana za mkono. Inawezekana kipato chake hakitoshelezi kukopa hela benki au kwenye mfuko wa pensheni. Tusimlaani kwa hili. Mtu hujikuna anapofikia.

    ReplyDelete
  16. kajimegea pande la nguvu!!!lima mkuu tuje kukusaidia kuvuna.

    ReplyDelete
  17. Kweli amekaa kikulima. Kazi za ofisi hazimfai!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...