In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for February 2010

babu njenje hajambo baada ya kuteguka mguu

Kinyaunyau
Mwanamuziki mkongwe wa Kilimanjaro Band "Wana Njenje" Mabrouk Omar amepata mstuko katika enka ya mguu wake wa kushoto baada kuteleza na kuanguka kwenye ngazi za kupandia jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cho kipya cha maraha wanapotumbuiza siku hizi kila Jumamosi cha Salender Bridge Club maarufu siku hizi kama daraja la manyoya....
Kiongozi wa bendi hiyo maarufu, Waziri Ally, kaiambia Globu ya Jamii sasa hivi kwamba Babu Njenje hivi sasa yuko nyumbani kwake akipumzika baada ya kuruhusiwa na madaktari ambao wamempima na kukuta hana madhara makubwa isipokuwa enka yake hiyo imepata mstuko katika ligamenti baada ya kuteleza na kuanguka.
"Babu Njenje hajambo na kwa kweli tunawashukuru mno wapenzi wetu kibao ambao wamekuwa wakifuatilia hali yake kwa njia ya simu ndani na nje ya nchi" amesema Waziri, akiongezea kuwa Babu Njenje hajambo na hamna haja ya kuwa na wasiwasi wote na kwamba Jumamosi ataonekana Jukwaani kama kawa hapo Salender Bridge club.
Zaidi


mashujaa music band yazinduliwa kwa kishindo

Mpiga mpini mahiri Elystone Angai ambaye ni kiongozi wa bendi ya Mashujaa Music Band akiwa jukwaani na wenzie wakati bendi hiyo ilipofanya onyesho lake la kwanza kwenye Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, jijini Dar na kukonga nyoyo za wadau. Ukumbi wa Makumbusho awali ulikuwa unatumiwa na bendi ya FM academia, lakini sasa ni zamu ya wana Mashujaa Music Band kutesa hapo kila Jumamosi.
wanenguaji wa Mashujaa Music Band



NEWS ALERT: Ramadhani Nasibu anyakua tena kiti chake cha makamu wa Rais TFF

Ramadhani Nasibu akionekana mtu mwenye furaha usiku huu katika hoteli ya Travertine alikokwenda kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF waliofikia hapo, baada ya ngwe nzito ya kinyang'anyiro cha Umakamu wa Urais wa TFF jana ambapo alimshinda John Nchimbi.
Ramadhani Nasibu akipongezwa usiku huu
Makamu wa Pili wa Rais wa TFF akipiga stori na mashabiki wake usiku huu
Ramadhani Nasibu (kulia) akiwa na Jamal Malinzi wakati wa uchaguzi mkuu wa TFF uliopita ambapo Malinzi alikuwa anagombea urais na Sir Leodegar Chilla Tenga na Nasibu Umakamu wa Pili wa Urais. Malinzi alishindwa na Nasibu alipeta. Tenga alifanikiwa kunyakua kiti cha Urais nwa TFF na anapeta hadi leo.

Mgombea Ramadhani Nasibu leo amekibeba tena kiti cha Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa nafasi hiyo iliyokuwa inagombewa pia John Nchimbi. Kapata kura 54 dhidi ya 47 alizopata mpinzani wake.

Nafasi ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji Nyanda za Juu Kusini imenyakuliwa na Bras Kiondo aliyepata kura 63, ambapo wagombea wengine Samson Mkisi aliambulia kura 29 na Gwamaka Mwaihojo 9. nafasi hii imejazwa baada ya aliyekuwa akiishikilia Theophil Sikazwe kufariki dunia.

Nasibu kaijaza nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais aliyoipoteza baada ya klabu ya Villa Squad ambayo ndiyo iliyomdhamini kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita wa TFF kushuka daraja msimu uliopita .

Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo, ikitokea timu iliyomdhamini kiongozi inashuka daraja basi nafasi hiyo itajazwa kwenye mkutano unaofuata wa TFF. Safari hii Nasibu alikuja kwa udhamini wa Mtibwa Sugar FC.

















salamu za pole kwa ramsey toka kwa wadau wa arsenal uturuki

Ramsey akilia kwa uchungu
baada ya kuvunjwa mguu
Ankal pole sana na kazi na tunakupa heshima zote kwa kutuwezesha kutupa habari mbali mbali za ndani na zile zinazowahusu watanzania ambao wapo nje ya nchi.
Mie leo ningependa kuwawakilisha wadau wanaoishi Uturuki na ambao ni wapenzi wa ARSENAL kutoa pole kwa wapenzi wote wa ARSENAL na wale ambao wapenzi wa soka kwa ujumla kutokana na striker chipukizi na machachali wa ARSENAL (RAMSEY) kuvunjika mguu.
Mungu amsaidie apone ndani ya kipindi kifupi na amjaalie arudi ktk kiwango chake kile kile. Jeraha alilopata isiwe sababu ya kushuka kiwango chake cha mpira atakaporudi dimbani. mungu mjaalie Ramsey afya njema na matibabu mema... Aaamin
From: Bab Tid, Turkey


kilimanjaro marathon 2010 yafana, ushindi waenda kenya

Wakimbiaji wa mbio za kilomita 42 za Kilimanjaro Marathon 2010 wakiwaanza mbio hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo Kiuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro leo
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi mshindi wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni za kiliomita 42 upande wa wanaume, Steven Chebogout.
Wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Vodacom za Kilomita tano wakikimbia wakati wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2010zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjar jana.
Mzee wa mika 67 kutoka moani Arusha, Ake Lingstone akimaliza mbio za kilomita 21 wakati wa Kukimbia Mbio za Kilimanjaro Marathoni zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana
Mmoja wa wakiambiaji wazee raia wanje kutoka San Diego,
Marekani, Cath Loper akimaliza mbioza Kilomita 21
Mshindi wa Mbio za Kilomita 21 za Kilimanjaro Marathoni 2010,Fabian Joseph Mtanzania akimaliaza mbio zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoaniKilimanjaro jana.

Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi






CCM london

Shoto ni katibu siasa na uenezi Bw. M Katega akiwakabidhi katiba ya chama cha Mapinduzi viongozi wa tawi la South London Mwenyekiti Bw. Kassim Hassan na katikati mjumbe wa tawi hilo Bw. Seth Mdendemi
katibu siasa na uenezi Bw. M Katega akiwakabidhi katiba ya chama cha Mapinduzi viongozi wa tawi la East london Katibu wa tawi Bi Mariamu Mungula na Mjumbe Bw. Iddy Mwanga

kushoto Bw. Frank Mukiza, Kassim Hassan, Mariamu Mungula, M Katega, Seth Mdendeni na aliyekaa ni Pashency Linus
kutoka shoto ni Neema Kumba, mwandishi wa Tanzaniaone UK Bw. Ally Muhdin na Katibu wa tawi la East London Bi. Mariamu Mungula

Chama cha Mapinduzi CCM jana jumamosi ya tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2010 kilifungua mashina mawili na kuchagua viongozi wa kuongoza mashina hayo jijini London Uingereza. Mashina hayo yalifunguliwa na katibu siasa na uenezi Bw. Katega. Mashina yaliyofunguliwa ni sina la South London na Shina la East London.







shukurani ya familia ya samike

Tunatoa shukrani za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha mazishi ya Baba yetu Mpendwa Mzee Samike wa Samike aliyefariki dunia Februari 15, mwaka huu.
Tumefarijika sana kwani wengi walitufariji (kwa kutupa maneno ya faraja) na tulikuwa nao pamoja katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na baba yetu kipenzi.

Tunamshukuru Mungu kwani shughuli zote za mazishi zilikwenda salama hadi tulipompunzisha baba yetu katika nyumba yake ya milele. Bwana ametoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe.
Amina

Leah Samike


mufti mkuu ahitimisha ziara yake nchini misri

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaabani Simba akiwa jijini Cairo, Misri, muda mfupi kabla ya kurejea Tanzania baada ya kumalizika Mkutano Mkuu wa 22 (The 22nd General Conference Under the Title The Objectives of Shariah(Islamic Law And Issues of the Contemporary Age).

Mkutano huo ambao ulianza siku ya 22-25 February 2010 sawa na 8-11 Rabi Al-awwal 1431H.
Mkutano huo ulifanyika Katika Hoteli ya Conrad jijini Cairo ambao ulijumuusha Masheikh na Viongozi wa Wakuu wa Nchi mbalimbali. Mkutano huo ambao ulianza siku ya 22 na kuisha 25 February 2010 sawa na 8-11 Rabi Al-awwal 1431H.
Vivile Mufti Mkuu alitumia nafasi hiyo kwa kukutana na kusalimiana na Wanafunzi na Wataanzania mbalimbali ambao wanaaishi Nchini humo
Mufti akisindikizwa na baadhi ya wanafunzi wanaosoma Misri

Mufti akiwa na baadhi ya wanafunzi aliokutana nao Misri


Mbio za kilometa 5 za Vodacom Fun Run zanoga leo moshi

Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini Musa Samizi wa pili toka kushoto akimpatia zawadi yake mshindi wa kwanza wa mbio za kujifurahisha za 5 kilometa Vodacom Fun run Bw.Wilbrodi Kidaga aliyejinyakulia simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi elfu 60 pamoja na fedha alizopewa kwa njia ya M pesa shilingi Elfu 70 asubuhi hii mjini Moshi. Kushoto ni katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru.
Naibu Waziri wa Habari na Michezo Joel Bendera na Mkurugenzi Mkuu wa wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Nector Foya kushoto wakiwa tayari kwa kuanza mbio za 5 kilometa Vodacom Fun run zilizofanyika mjini Moshi leo
washiriki wa mbio hizo wakikata mbuga leo Moshi

washiriki wakichuana mjini Moshi leo

WANARIADHA kutoka Kenya leo wamedhihirisha umahiri wao baada ya kufanya kweli kwa kunyakua nafasi za juu katika mbio za nane za marathoni za Kilimanjaro zilizofanyika jana mkoani Kilimanjaro na kushuhudiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCoBS) mjini Moshi.

Lakini pamoja na hayo Mtanzani Fabian Joseph aliiweza kuing’arisha Tanzania katika mbio za nusu marathoni baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza akiwa amevunja rekodi ya mbio hizo akiwa ametumia muda 1:03:59.

Rekodi ya iliyokuwa inatamba yam bio hizo ilikuwa ni saa 1:o4:15 ambayo ilivunja hiyo jana na bingwa wa zamani wa mbio za nusu marathoni za dunia Joseph kwa kuweka rekodi hiyo mpya baada ya kuwaacha mbali wapinzani wake katika kitimtim hicho na kujinyakulia medali na Sh milioni 1.5.

Nafasi ya pili katika mbio hizo ilichukuliwa pia na Mtanzania mwingine Dickson Marwa ambaye alikimbia kwa muda wa saa 1:04:19 na kujinyakulia kitita cha Sh. 750,000 wakati nafasi ya tatu nayo ilikwenda kwa mwanariadha kutoka Jehi la kujenga Taifa (JKT),Damian Chopa ambaye alitumia muda wa saa 1:04:26 akifuatiwa na Mkenya Mgundu Sagwa alitumia muda wa saa 1:04:28.

Na kuanzia nafasi ya tano hadi kumi zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya ambao walionekana kutamba katika mbio za mwaka huu na kuwafunika wenyeji.

Kwa upande wa wanawake kwenye mbio hizo washindi walikuwa ni Naomi Maiyo kutoka Kenya ambaye alitumia muda wa saa 1:16:26 akifuatiwa na Mkenya mwenzie , Beatrice Ruto aliyetumia muda wa saa 1:16:34 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mtanzania Restituta Joseph aliyetumia muda wa saa 1:16:47.

Lucy Kirimi kutoka Kenya alishika nafasi ya nne akifuatiwa na mshindi wa pili wa mbio hizo kwa mwaka jana ambaye pia alikuwa mwanamichezo bora wa mwaka jana aliyechaguliwa na Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) , Mary Naali aliyeshika nafasi ya tano.

Katika mbio kamili za marathoni za kilometa 42 , nafasi zote tatu za juu kwa upande wa wanaume na wanawake zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya ambapo Steven Chebosus aliyetumia muda wa saa 2:15:32 akifuatiwa na David Kiprono aliyetumia saa 2:16:46 na Julius Tumakar alishika nafasi ya tatu akitumia 2:16:56.

Nafasi za nne na tano zilichukuliwa na wenyeji Tanzania ambapo Ali Juma alishika nafasi ya nne akitumia muda wa saa 2:19:16 na Daud Joseph alinyakua nafasi ya tano na nasi za 6 hadi kumi zilichukuliwa na wanariadha kutoka Kenya.

Kwa upande wa wanawake Frida Lodepha ndie alikuwa mshindi wa kwanza akitumia muda wa 2:40:22 akifuatiwa na Evelyn Nyamu aliyetumia saa 2:40:26 na Leah Kusara 2:42:23 akifuatiwa na Truphema kuraui . mbio za hizo kwa wanawake zilitawaliwa na wanariadha kutoka Kenya ambao walishika nafasi zote 10 za juu.

Washindi wa kwanza wa mbio kwa upande wa wanawaume na wanawake walijinyakulia medali na pamoja na Sh milioni tatu kila mmoja .

Katika mbio za kujifurahisha za kilometa tano maarufu kama ‘Vodacom Fun Race’ ambazo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alishiriki pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali,Wilbroad Kidaga aliibuka mshindi wa kwanza na kuzawadiwa simu ya mkononi pamoja na muda wa maongezi wa Sh 20,000 na fedha Sh 70,000 kupitia huduma ya M-Pesa .

Wakati Paulo Kalera alishika nafasi ya pili na kujishindia simu pia pamoja na muda wa maongezi wa Sh 20,000 na fedha Sh 50,000 kupitia huduma ya M-Pesa na Doto Ramadhan alishika nafasi ya tatu na ye alizawadiwa simu, muda wa maongezi pamoja na fedha taslimu.






nondozzz chuo cha uandishi morogoro

Wadau John Nditi ( kulia) Grece Msovela ( kati kati) na Halfan Diyu ,wakijiandaa kuingia kubwia nondozzz zao katika ukumbi wa mahafali ya 13 ya Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro juzi mjini hapa
Mwalimu wa Chuo MSJ , Alhaji Ahmed Zidadu ( kushoto) , Jimmy Mengere na John Nditi baada ya kutunukiwa stashahada ya Uandishi wa habari wikiendi hii mji kasoro bahari

Mzee ...umependeza ..ni wapambe wakitoa pongezi zao kwa muhimitu wa Diploma ya Uandishi wa Habari na mwandishi na mpiga picha wa Globu ya Jamii wa Mji Kasoro Bahari John Nditi wikiendi hii
Baadhi ya wahitimu wa Diploma ya Uandishi wa Habari Chuo cha MSJ wakiwa na Mwalimu wao , Wilson Karuwesa mwenye kaunda suti baada ya kulamba nondozzz zao wikiendi hii.



AddThis Toolbar for Internet Explorer


“I AM STILL GOOD AND WILL BE BACK SOON” - HASHEEM THABEET

Hasheem with his Dakota Wizards team mates
When news surfaced that Hasheem Thabeet is headed to the Development League (D-League), the reaction among Tanzanians especially the users of social networks such as Facebook and blogs were overwhelming.
I guess the big question in lots of folk’s minds was; what is a D-League? Does it suggest that he is no longer going to be playing in the usual NBA league? Well, it depends on a lot of things. You can read more about the D-League and its implications or benefits to Hasheem career by clicking here and also here.

The social networks such as Facebook and blogs were immediately stuffed with comments and opinions. Some were wishing him a “quick comeback “to the NBA, while some couldn’t hesitate to throw jabs on him in the sentiment of “we told you”.

The Memphis Grizzlies have just assigned center Hasheem Thabeet to the Dakota Wizards, Memphis’ NBA D-League affiliate. The assignment is the 23rd time an NBA player has been assigned to an NBA D-League affiliate this season.

Thabeet, the second overall selection in the 2009 NBA Draft, becomes the highest-drafted NBA player to join an NBA D-League roster. In 50 games for Memphis this season, he averaged 2.5 points, 2.9 rebounds and 10.3 minutes.

A 7-3 native of Tanzania, Thabeet played three seasons at the University of Connecticut, averaging 10.3 points and 8.5 rebounds in 100 career NCAA games. Named the Big East Co-Player of the Year and the Big East Defensive Player of the year in 2009, Thabeet was also a two-time NABC National Defensive Player of the Year. During his final campaign at UConn, Thabeet averaged 13.6 points, 20.8 rebounds and 4.2 blocks (second in the nation).

I guess the news was “worth the talk”, because not only Hasheem is the first Tanzanian ever to play in the NBA, but also the highest draft pick ever to go to the D-League.
Thabeet, who has played sparingly in his rookie season, averaging 2.5 points in 10.3 minutes over 50 games, has been optioned to the Dakota Wizards. He made his debut yesterday when Dakota Wizards played Erie Bayhawks. Dakota Wizards won 108-103.

Before his debut in the D-League, www.bongocelebrity.com had caught up with Hasheem with only one question my mind; his reaction following the demotion to the D-League. This is how it went;

BC: Hasheem, what is your reaction to
this whole thing of moving to the D-League?

HASHEEM THABEET: "My reaction about D-League…Uhmmm… well I’m excited to participate in the D-League. I’m looking forward to playing and maximizing this opportunity to be on court and use the skills that I have developed thus far rather than to be on the bench.

"Right now the key for me is consistency court time as I am still learning the Pro Game. I know Coach Hollins has my best interest at heart so I’m happy with his decision which I believe is to make sure that I stay active.

"Now I know this is the time for the haters and all the doubters to talk and say whatever they have because they have been waiting to bring me down for a minute. So it’s my downtime and I promise I’m not backing back.
"It’s a new saga that has started. Plus I’m still be getting the same cheque… it’s not like they are not gonna pay me the usual.
"So I’m still good and soon I’ll be back!!! And oh by the way, I’m only going there for 6 games. So I will be back sooner than they are thinking" says the towering Hasheem.


yanga mdebwedo klabu bingwa afrika, yachapwa 1-0 na FC Lupopo

Yanga imeaga mashindano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufungwa goli moja na timu ya FC Lupopo katika mchezo uliochezwa katika jimbo la Katanga nchini DRC.
Goli lilifungwa na mabeki wa Yanga baada ya kubabatizwa na washambuliaji wa FC Lupopo katika Dakika ya 89 ya mchezo hivyo Yanga imetolewa kwa magoli 4-2 ya agrigeti.


taswira

hapa ni ufukwe wa hoteli ya kunduchi jijini dar jumamosi saa za magharibi
mhudumu akiwahisha oda



WAPi Zenj Jumapili hii

WAPI ZANZIBAR
Presents
MKALI WA FREESTYLE (BATTLE OF MCs)
Judges will be the audience!!!

Performances by:
BLACK ROOTS, SWAHILI VIBE, MARCUS ALPHA, ORIGINAL SHAKE AND MANY MORE....

LIVE @ Ngome Kongwe, Zanzibar
Sunday, February 28th, 2010, 3pm-9pm

fashion show by local up and coming designers & models..coordinated by Kemi Kalikawe

Visual art corner will activated by lots of new talents

LADIES & GENTS- Free Entry

KARIBUNI WOOOTE

WAPI, which stands for Words and Pictures, is a British Council initiative that was launched in Nairobi, Kenya, in 2006 and now operates in Nigeria, Ethiopia, Ghana, Uganda and Tanzania too. It’s a platform for underground artists – whatever their medium – to meet and compete and show what they can do.


msaada tutani

Mjomba naomba nafasi kurusha shida yangu kwa wanaglobu!
Mimi ni mpenzi wa mbwa sana tu, natafuta DOBERMAN PINCHER (JIKE) na ROTWEILLER (DUME) puppies kwa ajili ya kufuga.
Aliyenao, au anayefahamu nitakapowapata naomba awasiliane nami kwa barua pepe
Angalizo; “wawe pure breed” tafadhali
Weekend njema
Mdau Semesozi


balozi daudi mwakawago azikwa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Balozi Daudi Mwakawago wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo mkongwe yaliyofanyika katika makaburi ya kisutu jijini Dar leo
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Seif Shariff Hamad wakati wa mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia Marehemu Balozi Daudi Mwakawago yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar leo jioni.Katikati ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Mh. Benjamin William Mkapa.



MCT yazindua jarida la 'Scribes'

Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (SJMC) Dkt Bernadeta Killian ( katikati) akisisitiza jambo leo jijini Dar kwa waandishi wa habari huku akiwa ameshika chapisho la jarida la kitaalum la Scribes liloandaliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) . Kushoto ni Rais wa MCT Jaji Robert Kisanga na kulia ni Meneja mapachisho wa MCT John Mireny.
Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (SJMC) Dkt Bernadeta Killian ( kulia) akizundua jana jijini Dar es salaam jarida la kitaalum la Scribes liloandaliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) . Katikati ni Rais wa MCT Jaji Robert Kisanga na kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga.
Mkuu wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (SJMC) Dkt Bernadeta Killian ( kulia) akionyesha machapisho ya majarida mbalimbali baada ya kuyazindua jana jijini Dar es salaam yanayohusu tasnia ya uandishi wa habari ambayo yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania(MCT) . Katikati ni Rais wa MCT Jaji Robert Kisanga na kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga



arobaini ya simba wa vita yafanyika dar leo

JK akisamiliana jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Captain John Chiligati na Mzee Kingunge Gombale Mwiru katika Arobaini ya Simba wa Vita Mzee Rashid Kawawa nyumbani kwake Madale jijini Dar leo
JK akiwa kwenye hitma ya Simba wa Vita Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa jana jijini Dar. Wengine ni Mtoto wa Marehemu Vita Kawawa (kulia) na kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Mussa Salum.

Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria Arobaini ya Simba wa Vita Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika jana jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali Baadhi ya wakina mama wakiwa katika hitma ya hitma ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa iliyofanyika jana jijini Dar leo



WAMA yapokea msaada, shule yake rufiji kuanza jumatatu

Mwenyekiti wa Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Akipokea hundi ya Tsh 6,200,000 kutoka kwa Chama Cha Wachapishaji Vitabu Tanzania(PATA) Kutoka kwa Mwenyekiti wao Bw. Ian Moshi. Makabidhiano yalifanyika katika Ofisi ya WAMA Jijini Dar
Mwenyekiti wa Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Akiwajulisha wananchi wa wiliya ya Rufiji, kuhusu Wanafunzi wataoanza masomo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana iliyojengwa katika wilaya ya Rufiji ijulikanayo kama, WAMA-NAKAYAMA. Shule hiyo inapokea Wanafunzi wa kike yatima pia na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Pia Shule hiyo inapokea wanafunzi waliochaguliwa kutoka mikoa yote ya Tanzania. Shule hiyo inafunguliwa jumatatu tarehe 1 mwezi Machi 2010. Katika picha, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajat Amina Mrisho Said, Na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Mhe. Mwamtumu Mahiza. Shughuli hiyo ilifanyika katika shule hiyo jana.

watoto watakaoanza masomo katika shule
mpya ya WAMA-NAKAYAMA Wilayani Rufiji jumatatu.
Picha na Anna Itenda wa MAELEZO





Ban Ki Moon aomboleza kifo cha balozi daudi mwakawago

Na Mwandishi Maalum

Umoja wa Mataifa - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema ,amepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kufariki kwa aliyewahi kuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nchini Sierra Leone, Balozi Daudi Ngalautwa Mwakawago.

Ban Ki Moon ameyasema hayo katika salamu zake za rambirambi ambazo amemtumia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard Membe kufuatia kifo cha Balozi Mstaafu Daudi Mwakawago.

Katika salamu zake , Katibu Mkuu , amemuelezea Balozi Mwakawago kama mtumishi na kiongozi aliyetoa mchango mkubwa sana katika mchakato wa kutafuta maridhiano nchini Sierra Leone.

Aidha Ban Ki Moon anasema, Balozi Mwakawago wakati wa uhai wake aliyatekeleza majukumu yake kwa umakini na uhodari mkubwa. Na kwamba aliitumikia nchi yake Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jumuia ya Kimataifa kwa heshima kubwa.

“Wakati tunapotafakari utumishi wa kutukuka wa marehemu Balozi Daudi Mwakawago kwa nchi yake na kwa Jumuia ya Kimataifa , tuna kila sababu ya kuwa na shukrani, si kwaajili ya yale aliyoifanyika nchi yake lakini pia kwa aliyoufanyia Umoja wa Mataifa. Kuondoka kwake kumeacha pengo kwa familia yake na halikadhalika kwa wale wote waliomfahamu. Tafadhali pokea salamu zangu za rambirambi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Familia ya Marehemu Balozi Daudi Ngalautwa Mwakawago”.


globu ya jamii kumwaga ze fulanazzz 100 kwa wadu wa milioni 8

Globu ya Jamii itatoa ze fulanazzz 100 kwa wadau mia wa mwanzo watakaokuwa katika ulingo wa wadau wa milioni 8, hesabu ambayo itatimia muda si mrefu ujao (angalia takwimu chini kabisa kuumeni kwako).
Hii ni badala ya kumzawadia mdau mmoja mmoja. Hivyo mdau kaa chonjo mara tu hesabu itapogota 8,000,000 lete haraka jina na anuwani yako utumiwe ze fulanazzz ya Globu ya Jamii kama inavyoonekana hapo juu. Hakuna malipo na utapoleta jina na anuani utatumiwa popote ulipo ulimwnguni...
Sina uwezo kwa kumshukuru mdau mmoja mmoja kwa kampani baab'kubwa mnayotoa kwa Globu ya Jamii, ingawa iko siku panapo Majaaliwa kila mdau atapata zawadi.
Hao wataobahatika naomba wajione na wajulikana kuwa ndio wawakilishi wa wadau wote ambao nawapenda na kuwaheshimu sana kwa kutembelea Globu ya Jamii kila kukicha.
Bila ninyi nyote Libeneke hili lisingefika hapa.
Asanteni sana sana sana....
-Michuzi


pinda ziarani tabora

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Mtendaji wa Kata ya Urambo Mjini, Stella Riwa Pikpiki ili aweze kufanya kazi yake vizuri, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Urambo akiwa katika ziara ya mkoa wa Tabora, Februari 26, 2010. Kuahoto ni mkewe Tunu na watatu kushoto ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Urambo, Samwel Sitta.
Wasanii wa kikunid cha ngoma ya kisukuma ya Bugobogobo kutoka kijiji cha Muungano wilayani Urambo, wakitoa burudani uwanjani katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkkuu, Mizengo Pinda Mjini Urambo leo

Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo kutoka kijiji cha Muungano wilayani Urambo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Urambo akiwa katika ziara ya mkoa wa Tabora,




USIKU WA MAVAZI( STYLE AND SWAGG NITE) HOUSTON TX @ CLUB SAFARI


MARCH 6 STYLE N SWAGGA ALL LADIES GET UR BEST OUTFIT N WIN $200 FIRST PLACE $100 SECOND PLACE $50 THIRD PLACE
@CLUB SAFARI
SPECIAL LIVE PERFORMANCE FROM LBT(BONGO FINEST).
AB(BLACK SENSATION).
GIE MANIE(TZ FINEST)


mwanajeshi aliyeuwa wenzake akamatwa kigoma

Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi

Polisi mkoani Kigoma wamefanikiwa kumkamata askari Jeshi anayetuhumiwa kuhusika katika tukio la kuwaua wenzake wawili kwa kuwapiga risasi mkoani humo.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Twaha Ramadhani, amesema leo kuwa mtuhumiwa huyo mwenye namba MT.81071 Pte Yusuf Haji Hussein (30) amabaye ni mzaliwa wa Zanzibar kijiji cha Mamba Unguja Kaskazini alikamatwa na Polisi jana usiku huko kwenye eneo la Ilagala wilaya ya Kigoma vijijini kiasi cha kilometa 30 kutoka Kigoma mjini na kilometa 70 kutoka eneo alikofanyia tukio hilo.
Kamanda Ramadhani amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa wakati wa operesheni ya kumsaka iliyoendeshwa na Polisi kwa kushirikiana na Askari wa JWTZ waliosambaa katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Amesema makachero wa Polisi wanaendele kumhoji mtuhumiwa huyo na anategemewa kufikishwa mahakamani mara baada ya kumalizika kwa mahojiano ya kina.
Usiku wa kuamkia Novemba 23, 2009 mtuhumiwa huyo akiwa kwenye Kambi ya JWTZ Manyovu katika wilayani Kasulu mkoani Kigoma anatuhumiwa kuwauwa enzake kwa kuwapiga risasi akitumia silaha aina ya SMG.

Askari waliouawa ni MT.84720 Pte Hildefonce Burunja Masanja(35) na MT.8528 Pte Rashid Hassan Nawawi (25) na mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alikimbia na kutokomea msituni.


Dekula kahanga amwaga vumbi na kitu kipya

Kitu kipya cha Dekula Kahanga kilichotoka 23/02/2010. Dekula Vumbi Kahanga wa Maquiz Original Video yake ktk HD title: God is One by Dekula Kahanga.


NOW, THIS IS WHAT I CALL CULTURE.....

Kaka pole na majukumu ya libeneke lako.
Naomba kuuliza kwa wadau hawa ni jamii ya kabila gani?
na wanapatikana nchi au mkoa gani.?
nawasilisha
Mdau CM







Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker