





Archive for March 2010
Wednesday, March 31, 2010
ngumi mkononi ni kitu cha kawaida kwenye mabunge ya wenzetu...
Wednesday, March 31, 2010
udzungwa mountains national park
Udzungwa Mountains National park sio hifadhi maarufu kwa wengi kama zilivyo Serengeti, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na nyinginezo. Kikubwa kinachofanya wengi tusiifahamu yawezekana kuwa ni kutokana na kutokuwepo kwa wanyama wengi ambao ndio huwa kivutio kikubwa kwa wazalendo wengi. Ukweli unabaki kuwa Udzungwa Mountain National park ni hifadhi ya kipekee ambayo ni mahususi kwa wale wanopenda kwenda kuona miti, Viumbe hai wadogo na wa kati ambao hustawi ktk misitu ya ki-tropiki. Hii hifadhi ipo mkoani Morogoro. Kufika huku unapita bwawa la Kidatu. Mambo haya na mengine mengi kuhusu utalii na hifadhi zetu nenda:
http://tembeatz.blogspot.com/
http://tembeatz.blogspot.com/
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 2
Wednesday, March 31, 2010
mashindano ya kili taifa cup 2010 yazinduliwa rasmi
Mkurugenzi wa Masoko Bw. David Minja akizindua rasmi udhamini wa TBL kwa Kili Taifa Cup 2010 huku Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe akishuhudiaKILI TAIFA CUP 2010 LAZINDULIWA RASMI
Mashindano ya Kombe la Taifa (Kili Taifa Cup 2010) yamezinduliwa rasmi katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wafanyakazi wa TBL na waandishi wa habari wakishuhudia.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kilimanjaro Premium Lager, moja ya aina za bia za TBL kudhamini mashindano hayo yanayosaidia kung’amua na kukuza vipaji mbalimbali kuanzia ngazi za chini hadi timu ya taifa na kwenye klabu kubwa za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo ni mara ya nne kwa kampuni ya TBL kudhamini mashindano haya.“Tunajivunia kufadhili mashindano makubwa kama haya ambayo si tu yataleta shamrashamra miongoni mwa washabiki wa soka kote nchini, lakini pia yatasaidia kung’amua vipaji vipya na labda kuwaingiza baadhi ya wachezaji hao kwenye timu za taifa au kwenye klabu zinazoongoza,” anasema David Minja, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL.
Alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yanafanyika chini ya dhima: ‘Kufikisha Soka ya Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,’ yatajumuisha timu 24 zitakazocheza katika vituo sita, ambapo inatarajiwa kwamba mashindano hayo yataanza Mei 8, 2010 hadi Mei 15, 2010 katika vituo vyote hivyo, ambapo kila timu itacheza na mwenzake kwenye ngazi za mzunguko kisha zitakazopata pointi nyingi zaidi zitaingia kwenye hatua ya robo fainali.
Kwa mujibu wa Minja, robo fainali hizo zitachezwa Mei 22, 2010 na fainali zitakuwa Mei 30, 2010, na kwamba vituo hivyo sita ni pamoja na Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga.
“Ufadhili kwa mashindano yote ni Tsh milioni 850 na kila timu itapokea fedha za maandalizi, usafiri na malazi pamoja na seti za sare za michezo kwa ajili ya mashindano hayo,” alisema Mkurugenzi huyo wa TBL.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema; “Tuna furaha kwa kuwa mashindano ya mwaka huu pia yatahusisha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 lakini watakaocheza ni wale waliozidi miaka 18.
Timu zote zimejiandaa kwa ajili ya mashindano haya, hivyo tunawaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi kuunga mkono timu zao.” Kwa muda mrefu TBL imekuwa ikijifungamanisha na Kabumbu na kwa hakika inafurahia hali ya uhuishwaji wa ufadhili katika Soka.
Tanzania Breweries Limited (TBL) huzalisha, kuuza na kusambaza bia safi, vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL ina maslahi ndani ya Tanzania Distilleries Limited, na kampuni zinazohusiana nayo, Mountainside Farms Limited.
Bia za TBL zenye umaarufu zaidi ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt na Castle Lager. Vinywaji vya aina nyingine vinavyohusiana na kundi la TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds na Premium Cold.
Kundi la TBL limeorodheshwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na imeajiri karibu watu 1,300 na inawakilishwa kote nchini na viwanda vitatu vya bia, distillery, a maltings facility na depo nane za usambazaji.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 10
Wednesday, March 31, 2010
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 122 wa IPU wampongeza Balozi Sisco kwa mapokezi mazuri Thailand
Spika wa Bunge.
Mhe. Dr. Christene Ishengoma naye akitoa Salam za Pongezi kwa mapokezi mazuri kwa balozi Cisco (mwisho kulia) kwa kipindi chote ambacho wamekua nae hapa Bangkok, Thailand kuhudhuria mkutano wa 122 wa IPU. Katikati ni Mhe. Prof. Idris Mtulia (Mb)
Mhe. Balozi Sisco Mtiro akitoka nje ya Hotel ya Conrad, Mjini Bangkok Thailand, mara baada ya chakula cha usiku na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano wa 122 wa IPU katika hotel ya Conrad, kulia kwake ni Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumba akimsindikiza.
Juu na chini Spika wa Bunge Mh. Samwel Sitta, akifurahia zawadi ya Track suit zenye nembo na rangi ya CCM ambazo zimetengenezwa na Mtanzania anayefanya shughuli zake hapa Bangkok Thailand, Bwana Nicholaus Kipalanga (shoto) alipomtembelea katika Hotel ya Conrad usiku kuamkia leo. Bwana kapalanga ana kampuni yake inayojishughilisha na uuzaji madini iitwayo Asili Germs International Co. Ltd ambapo pamoja na madini anafanya biashara za kutengeneza nguo za sare kwa order Maalumu kama vile sare za makampuni, Tshirt na truck suit kwa ajili vyama na kampeni mbalimbali.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 11
Wednesday, March 31, 2010
taarifa ya msiba
Marehemu Martha Alu Alute enzi za uhai wakeFamilia ya Mzee Augostino Lissu Mughwai wa Mahambe, Singida inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa,Martha Alu Alute kilichotokea tarehe 30 Machi, 2010 huko Dar es Salaam, Tanzania.
Maandalizi yanafanywa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Mahambe, Singida kwa mazishi.
Marehemu alizaliwa mwaka 1932 Ighuka, Singida. Ameacha mume na watoto nane: Alute Mughwai wa Arusha, Tundu Lissu, Mjengi Lissu na Christina Lissu wa Dar es Salaam, Rose Masesa wa Songea, Peter Muro Mughwai wa Kondoa, Mateo Mughwai wa Singida na Vincent Lissu Mughwai wa Connecticut, Marekani.
Vile vile marehemu ameacha wajukuu 20, na vitukuu 6.
Kwa marafiki wa wafiwa wanaokaa nje ya Tanzania (Marekani, Uingereza n.k) unaweza kutuma rambirambi zako kwenye
accnt # 1259458568,
routing #221172610.
Au
kwenye anwani ifuatayo:
Vincent Mughwai
370 Huntington Road
2F Bridgeport
CT 06608
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 5
Wednesday, March 31, 2010
mdau wa mwanza achomoka na pikipiki ya zantel

MENEJA MAUZO WA ZANTEL MKOA WA MWANZA BW. KENNEDY NDONONDO AKIMKABIDHI MSHIDI WA PROMOSHENI YA CHOMOKA NA PIKPIKI BW. FRED KISSAKA TOKA MWANZA ALIYEJISHINDIA PIPIKI. ZANTEL INAENDESHA PROMOSHENI KABAMBE KWA WAKAZI WA MWANZA NA MARA TU. ILI KUSHIRIKI TUMA NENO PIKIPIKI KWENDA 15583 NA UJISHINDIE ZAWADI KIBAO.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 0
Wednesday, March 31, 2010
JK akabidhiwa ripoti ya ukaguzi na matumizi ya serikali
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti za ukaguzi wa matumizi ya Fedha za Serikali na Taasisi zake Ikulu jijini Dar leo mchana. Kushoto ni Msaidizi wa mkaguzi mkuu Bwana Atanas Tarimo.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 13
Wednesday, March 31, 2010
korea yaweka mktaba wa uzalishaji wa nishati ya taka
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ruth Mollel (Katikati) na ujumbe kutoka Serikali ya Korea, wakitia saini Mkataba wa Usimamizi wa taka na uzalishaji wa nishati itokanayo na taka, katika Hotel ya kempinski jiijini leo. Wanaoshuhudia mkataba huo ni Dr. Batilda Burian Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Bw. Joon-Seok Hong, Makamu Waziri wa Mazingira – Korea.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 2
Wednesday, March 31, 2010
TANGAZO LA MSIBA TABATA, DAR
BOSCO SAFARI MOSHA WA GLASGOW, SCOTLAND, ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MDOGO ABOUD NDESAMOKE MSOKE ILICHOTOKEA HUKO DAR-ES-SALAAM TANZANIA ANA MCHANA.
MIPANGO YA MAZISHI YA INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA JIJINI DAR. HABARI HIZI ZIWAFIKIE UKOO WA MSHA WA MAREKANI, FAMILIA YA DR MOSHA WA SAVANA-LA-MAR, UKOO WA MOSHA POPOTE PALE WALIPO.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 1
Wednesday, March 31, 2010
tatiana atua dar
Picha zote na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 11
Wednesday, March 31, 2010
JK na balozi wa China waweka jiwe la msingi wa jengo la taasisi ya ugonjwa wa moyo muhimbili
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 7
Wednesday, March 31, 2010
Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) yatoa kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha ujenzi wa barabara na reli nchini
Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jana mjini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt. Sipho Moyo.
Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akisaini ya makubaliano ya kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini . Kushoto anyeshuhudia ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt. Sipho Moyo.
Katibu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano ya msaada wa kifedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ya kiasi cha bilioni 322.5 kwa ajili ya kuimarisha barabara na reli nchini. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa ADB nchini Dkt. Sipho Moyo.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 0
Wednesday, March 31, 2010
Easter Eve Bash in New England
Easter Eve Bash in New England
The African Nite is inviting you to join us on Saturday the 3rd for an Easter Eve Bash.
That African groove and best African mix vibes will be on all night long...
Enjoy the Bolingo, Bongo Flava, Taarab, Kwaito, Mapouka, Reggae, hip-hop and many more…..
Location: Charlie’s Pub, 14 Cabot St, Lowell, MA, 01854
Door s Open: 8pm till 2am
Cover: $10
Cash BAR
Door s Open: 8pm till 2am
Cover: $10
Cash BAR
Party will be hosted by DJ Paff, DJ Sam and as always many guest DJ’s
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 0
Wednesday, March 31, 2010
Maofisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) wahitimu mafunzo yao
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ( Utafiti) Adam Mambi akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake kutoa shukrani kwa kupatiwa mafunzo ya Uandishi wa Sheria, aliyekaa ni Ofisa Sheria wa Tume hiyo Andisya Nalingigwa.
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 1
Wednesday, March 31, 2010
Ibada ya kiswahili Columbus Ohio
Swahili Service
for the Columbus Community
for the Columbus Community
Sunday, April 4, 2010, 3:30pm
Gethsemane Lutheran Church
Pastor Karen Asmus-Alsnauer
mchungaji@gethsemane.org
(A joint ministry of Gethsemane and Ascension Lutheran Churches)
Amefufuka kweli kweli
Please join us on Sunday, April 4, 2010, for Easter Eucharist Service in Swahili. The service begins at 3:30pm with African Christian music.
Holy Communion will be served and all baptized and believing Christians are invited to the Lord’s Table to share in this meal. After the service, there will be fellowship time to greet one another and enjoy delicious food prepared by Tanzanian women in Columbus to celebrate Easter.
The service is at Gethsemane Lutheran Church,
35 E. Stanton Ave.,
¼ mile off North High Street behind Tim Horton’s.
If you have any questions or would like more information,
please call the church at 614-885-4319
or
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 1
Wednesday, March 31, 2010
Afisa wa ubalozi kuwa mgeni rasmi katika mtanange wa Simba na Yanga,Ughaibuni
kikosi cha SimbaAfisa ubalozi amekubali mualiko kuwa mgeni rasmi kwenye kindumbwe dumbwe cha Simba na Yanga,mechi inayozungumziwa mjini Washinngton na vitongoji vyake,
Mpambano huo wa kukata na shoka utachezwa jumapili April 4 kwenye wanja jipya la 1417 Kalmia St,Nw,Washington Dc,kambi zote zipo shwari na zinaendelea vizuri na mazoezi.
Mpambano huo wa kukata na shoka utachezwa jumapili April 4 kwenye wanja jipya la 1417 Kalmia St,Nw,Washington Dc,kambi zote zipo shwari na zinaendelea vizuri na mazoezi.
Simba inaonekana imejiimarisha zaidi baada ya wachezaji wengi wa mikoani akiwemo Francis Makalaa aliyewahi kuichezea Simba miaka ya Nyuma kuthibitisha kuwepo kwenye mpambano huo,Kuhusu Nteze John bado viongozi wa Simba wanaendelea kumtafuta kwa udi na uvumba,Nteze anaishi Washington State alisahawahi kua mchezaji wa kutumainiwa Simba na Timu ya Taifa.kabla hajajiunga na Simba,alikua mchezaji wa Pamba ya Mwanza.
Kambi ya Yanga imekua kimya Kocha Yasini Randi amesema Simba wacha waongee,msema ukweli dakika 90,sisi bwana tupo tunaendelea vizuri na kambi yetu,sisi tunaingia uwanjani kama YANGA IMARA KUFUNGWA DAIMA MWIKO.
Jumamosi April 3 kutakua na mechi nyingine ya Stars na Maryland untd,itakayochezewa 18031 central park circle,Boyds,Md,20841,uwanja # 20
mechi hii ni moja ya mechi za kujinoa ya Stars kwa safari ya kuelekea Sweden july mwaka huu,mechi nyingine ya Stars ni April 24 mjini Boston itapambana na Zambia
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 5
Wednesday, March 31, 2010
Gavana wa China kujenga kituo Muhimbili
Waziri wa afya na ustawi wa jamii Profesa David Mwakyusa akipokea zawadi toka kwa gavana huyo Sun Liang wa Jimbo la Zhangdong ,Nchini China
Gavana wa Jimbo la Zhangdong,nchini China bw.Sun Liang akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.Mgeni huyo pamoja na ujumbe wake walifika Wizarani hapo kwa mazungumzo mafupi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa juu ya mkakati wao wa kujitolea kujenga kituo cha kutibu magonjwa ya moyo na upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Gavana Sun Liang (kushoto) akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa mara baada ya mazungumzo mafupi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo
Wednesday, March 31, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 5
Tuesday, March 30, 2010
ankal akagua ofisi za bonge mjini kusoma leo
ankal akiwa katika ofisi za Quality Machinery and Truck Commercial Ltd ya mji wa kusoma ambako alikutana wakurugenzi wake Mohamed Hijja (aliyekaa) na Athumani Mloka (kuume). Shoto ni mdau Gardol. hawa wadau ni mabingwa wa kusafirisha aina yoyote ya magari makubwa na matrekta na magreda na hata meli na treni popote duniani. wanapatikana katika email ya qmtcommercial@bconnect.com na namba ya simu ya chap chap ni +441 1895 98614
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 22
Tuesday, March 30, 2010
swali la kizushi
ankal eeee...
baada ya kumaliza kukagua miradi ya maendeleo ya libeneke na wadau wa globu ya jamii naomba msaada tutani kwa hao wataalamu wa kusafirisha mizigo. kila mara nikisafirisha mizigo naulizwa dokumaa ya bill of lading iko wapi? mie nachanganyikiwa. hivi ni bill of landing ama lading na kwa nini.
mdau Ukerewe
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 8
Tuesday, March 30, 2010
nakaaya sumari aanzisha libeneke
Tuesday, March 30, 2010
msaada tutani
Habari ya vekesheni ankal, hongera sana ten asana kwa burudani na habari za hapa na pale kupitia mtandao huu wa jamii. Mi naomba msaada wa kujua, eti, MAJI YA DAFU NA DAFU LAKE yanaitwaje kwa kizungu.
Mdau Pamoko!!!
Mdau Pamoko!!!
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 14
Tuesday, March 30, 2010
NDANI YA READING WADAU WANA DUKALAO
Wadau wakiwa mbele ya duka la wabongo lililopo 0xford road mji wa Kusoma liitwalo Bongo Flavour. Toka shoto ni mdau Gardol, mkurugenzi wa duka hilo Dixon, Mahamudu na Mdau Banduka. Hii inadhihirisha kwamba si kweli kwamba wadau wote huku ughaibuni ni wabeba maboxi. wengi wao ni wajasiriamali wa nguvu...
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 25
Tuesday, March 30, 2010
ankal ziarani slough
ankal ambaye yuko ziarani ukerewe kukagua miradi ya maendeleo ya libeneke na kuzindua matawi mapya ya ze fulanazzzz akiwa na mdau katika mjini wa slough jioni hii, Slough ni mji ulio takriban katikati ya london na mji wa kusoma. Mdau Juma Pinto aliishi hapa. kesho ankal anaendelea na ziara hiyo sehemu za oxford
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 7
Tuesday, March 30, 2010
new vincent restaurant ya mji wa kusoma
Tuesday, March 30, 2010
msaada tutani
Assalam aleyqum Ankal.
pole na majukumu ya kila siku kaka,
pole na majukumu ya kila siku kaka,
Mimi ni Kijana wa Kitanzania niitwae Khamis Kasim Ruhabaye (Kigoma ndo Home) ni mwajiriwa wa Tanesco na ni Engineer niligraduate 2007 hapo Udsm. Nimefanya kazi Tanesco for two years, then kupitia wizara ya elimu ya juu na.... kuna tangazo walitoa la scholarship za kusoma China nikaaplay nikapata, though mke wangu hakupata japo tuliomba wote wawili ( Mke wangu alimaliza Muhimbili) So katika kuja huku nae alinifuata baadae kaka. so nipo nae. Am sorry for kwa hii story ndefu ila ina maana hapa kama ifuatavyo.
Mara baada ya kufika China, nikaanza kukamua kama kawaida lakini nikiwa na malengo ya kubadili koz na kusoma Umeme kitu niliyofanyia degree ya kwanza lakini kwa bahati mbaya jamaa wamechomoa kubadili kaka so nasoma SIGNAL AND INFORMATION HANDLER kaka....so mbaya ila siipendi so sikuchoka kutafuta kwingineko huku nakomaa na hapa nilipo.
One day katika kupitia Blog yako though huku tunaifungua kwa shida mpk tutumie VPN na PROXY ndo inakua poa otherwise hakuna BLOG huku. Niliona umepost kitu flani kuwa kama unataka kuwork au kusoma kwenye scandivia Countries then uandike mail kwa Gloria Boiko mail ilikua gloriaboiko@ymail.com so kama kawa nikaaplay mie na yf wangu as per your post....
Its just last week jamaa wamenijibu kuwa nimepata hiyo chance nami nikawachana kuwa mie nina mke so itakua vp?? wakaniambia kuwa haina kwere.. niwapostie doc za yf na watamconsider.
Its just last week jamaa wamenijibu kuwa nimepata hiyo chance nami nikawachana kuwa mie nina mke so itakua vp?? wakaniambia kuwa haina kwere.. niwapostie doc za yf na watamconsider.
(Nshawapostia)...ila kuna malipo ya USD 350 each so kwa mtu mbili USD 700 sio shida kuitoa hiyo pesa kwa kupata shule au kazi ila kuingizwa kingi nayo sio poa...koz nimewaomba jamaa hata namba yao ya simu ila sijui inakua vp hiki kipengele kinakua kigumu kwao.... SO MI NAKUOMBA MSAADA KAKA NI KUJUA HAWA WATU UHAKIKA AU NDO CHANGA???
Am not sure kama unamkumbuka mtu aliekutumia hii kitu. ila kama unamkumbuka naomba contacts zake ili kucomfirm zaidi hii issue isije tukawa tualipa pesa kwa empty thing.. PLEASE HELP ME ......JUST KUJUA NI UKWELI AU LA....
Msaada wako unahusika.
Khamis.
Msaada wako unahusika.
Khamis.
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 16
Tuesday, March 30, 2010
CHUNYA YATOA MSHINDI WA NITASOMA MOBILE 2

Wiki ya pili ya shindano la kitaaluma NITASOMA SCHOLARSHIP Promotionyapata mshindi Bwana Boniface Peter Mwaipopo, kutoka Chunya Mbeya.
Mshindi huyo wapili toka shindano lilipanza rasmi 15.03.2010 alipatikanana kutanganzwa jana asubuhi.Mshindi wa kwanza Bwana Witnes Lucas toka Iringa (Tumaini University).Washindi hao wanaombwa kufika ofisi za 4Layers (T) ltd. zilizoko MsasaniDar es salaam kujichukulia zawadi zao.Au wapige simu 0765 232383 wawasiliane na meneja masoko wa 4layers (T)ltd.
Zawadi nyingine kama vitabu va masomo, Laptop na scholarships ambazounaweza kujishindia kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno NITASOMA SEC (kwasekondari), NITASOMA HIGH (kwa Alevel) na NITASOMA UNI (kwa elimu ya juu)kwenda 15767.
4Layers (T) Ltd.
P.O.Box 77901
Dar es salaam.
Masasani - Kimweri Rd.
Plot 696 Block "F"
0765 232383
http://www.nitasoma.com/
http://www.nitasoma.blogspot.com/
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 0
Tuesday, March 30, 2010
wajinyakulia lcd tv promosheni ya shangwe za tigo
Washindi wa promosheni ya Shangwe za Tigo Kombe la Dunia Mark Makundi (kushoto na Stuart Momani wakionyesha zwadi zao za LCD TV mara baada ya kukabidhiwa katika ofisi za Tigo, Dar es Salaam jana.
Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando akikabidhi zawadi ya LCD TV kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Shangwe za Tigo Kombe la Dunia, Stuart Momani jijini Dar
Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando akikabidhi zawadi ya LCD TV kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Shangwe za Tigo Kombe la Dunia, Mark Elias Makundi jijini Dar
Tuesday, March 30, 2010
~
Copyright: Michuzi Blog
~
Mtumie Rafiki Yako
,
Maoni: 1











































