





Archive for April 2010
Ngorongoro Heroes yaitungua Malawi 3-1 na kufuzu kucheza kombe la mataifa ya afrika kwa vijana
Intavyuu na Sporah
safari lager mdhamini mkuu mashindano ya pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu
Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) na ambayo ndio mdhamini mkuu wa mchezo wa pool hapa nchini imetangaza kuyadhamini mashindano ya kucheza poolkwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu yanayofahamika kwa jina la (Higher Learning Safari Lager pool Competition 2010).
Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha vyuo vikuu kumi na vyuo vya kati kumi na vinatarajiwa kutoana jasho kwenye mashindano hayo yatakayofanyika katika ufukwe wa coco Beach kuanzia may 14 hadi may 16,2010 jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naimu Waziri wa Utamaduni na Michezo Mh. Joel Nkaya Bendera.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema “Azma ya Safari Lager ni kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa pool hapa nchini, hivyo udhamini huu wa mashindano vyuo vikuu na vya kati ni moja kati ya malengo ya bia ya Safari kuhakikisha inatambua na kuthamini mchango wa wanataaluma katika nyanja ya michezo nchini Tanzania.”
Bwana Fimbo aliendelea aliendelea kusema “Washindi wa mashindano hayo watajipatia zawadi zenye thamani ya Tsh. 3,000,000/= za kitanzania –ambapo ni Chuo Bingwa 1,000,000/= mshindi wa pili 600,000/= na Chuo cha tatu 400,000/=. Kwenye mchezo mmoja mmoja mshindi atajipatia Tsh. 200,000/= wa pili Tsh. 150,000/= na wa tatu Tsh. 100,000/= yote ni kwa wanawake na wanaume na pia Mchezaji bora wa kike na wa kiume kila mmoja atapata 50,000/= huku Chuo bingwa kikijipatia Kombe kubwa la Safari Lager2010.”
Wakielezea juu ya uthamini huo wawakilishi wa vyuo hivyo wakiongozwa na Naibu Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana Kayumb Torokoko alisema “Udhamini huo umefika wakati muafaka kukokana na ukweli kwamba mchezo wa pool ni miongoni mwa michezo inayohitaji matumizi makubwa ya akili na kufikiri tofauti na michezo mingine ambayo hutumia nguvu zaidi.”
Aliendelea kusema “Ni nafasi nzuri kwa wanataaluma kote nchini kushiriki katika mashindano hayo ili kuweza kutoa nafasi kwa kila mmoja wetu kuonyesha uwezo wake kwenye kucheza pool.
Aidha waliipongeza TBL kwa mchango wake wa dhati kwa mchezo huu kwa kusema “Tungependa kutoa shukrani zetu kwa bia ya Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa mchango wao katika kuhakikisha mchezo huu wa Pool unakuwa na kuomba waweze kutoa nafasi ya kuukuza zaidi kwenye vyuo vilivyopo nje ya jiji na Dar es Salaam.
Wamekuwa ni mfano mzuri kwa kuweza kuutambua mchango wetu katika ngazi ya vyuo vya elimu ya juu nchini na pia kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa kwenye ngazi ya vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania.”
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia, vinywaji vya matunda vyenye asili ya kilevi (AFB’s) na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL inazo hisa pia katika Tanzania Distilleries Limited na kampuni shirika, Mountainside Farms Limited.
Bia maarufu za TBL ni pamoja na Safari, Kilimanjaro, Ndovu Special Malt na Castle.Vinywaji vingine vya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds Premium Cold.
TBL imo pia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na imeajiri watu kiasi cha 1,300 huku ikiwa na wawakilishi katika sehemu kubwa na Tanzania na viwanda vitatu vya bia na depot nane kwa ajili ya kusambazia bia na vinywaji vingine vya kampuni hiyo.
Kwa mawasiliano zaidi
Fimbo Butallah,
Safari Lager Brand Manager,
Fimbo.Buttallah@tz.sabmiller.com
Dorris Malulu,
Corporate Affairs Administrator,
Doris.malulu@tz.sabmiller.com
Innocent Melleck,
Integrated Communication Ltd,
Project Manager,
+255 786 110 150
innocent@integrated.co.tz
kanali ali mahfoudh
Mambo yote London Kesho!
TBL yaipiga jeki timu ya mkoa wa Kilimanjaro ya Taifa Cup
Fedha hizo zilikabidhiwa jana kwa katibu tawala msaidizi Huduma na miundombinu Hassani Bendeyeko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikabidhi fedha hizo kwa viongozi wa chama cha soka mkoa KRFA.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo kaimu meneja mauzo mikoa ya Kilimanjaro na Tanga Edmund Rutaraka alisema kampuni hiyo imetoa kiasi hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya udhamini pamoja na kuwapa motisha wachezaji.
Barclays Bank yazindua huduma ya Premier Life
The 3rd EAC Conference on Investment in Kampala
President Jakaya mrisho Kikwete delivers his speech during the closing session of the 3rd EAC Conference on Investment held in Kamapal
The Chairman of the East African Community Heads of State Summit President Jakaya Mrisho Kikwete, the host President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and Kenya's Prime Minister Raila Odinga hold an informal discussion shortly before the conclusion of the 3rd East African Conference on Investment held at Munyonyo Speke Resort in Kampala this afternoon.
The Secretary General for the East African Community ambassador Juma Mwapachu consults with the Chairman of the EAC Heads of State Summit President Jakaya Mrisho Kikwete during the closing sesssion for the 3rd EAC conference on investment held in Kampala this afternoon.Others from left President Museveni of Uganda,Kenya's Prime minister Raila Odinga and Rwanda's Prime Minister Bernard Makuza
a cross section some participants to the 3rd EAC Conference on investment held at the Munyonyo Resort in Kampala.
Some East African Heads of State and representatives of Heads of State who participated in the 3rd East African Community Conference on Investment held at Kampala Uganda pose for a group photograph with some members of their delegation.From left Rwanda's Prime Minister Bernard Makuza,Uganda's President Yoweri Kaguta Museveni,President Jakaya Mrisho Kikwete, Burundi's Vice President Dr.Yves Sahinguvu and Kenya's Prime Minister Raila Odinga.BREKING NYUUUUUZZZZZ: Kapuya atangaza kima cha chini cha mishahara sekta Binafsi.
katiba ya jamhuri ya muungano katika libeneke la wizara ya sheria
Katiba ya nchi tayari inapatikana katika
Ahsanteni kwa maoni,
haya tena nondozzzzzz ifakara!
DOCTORAL AND POST DOCTORAL STUDY OPPORTUNITIES AT IHI
Ifakara Health Institute (IHI) is a not-for profit research and training Institute whose mission is to develop and sustain a district-based health research and resource centre capable of generating new knowledge and relevant information for public health policy and actions. IHI is among the leading health research institutes in Africa and was awarded the prestigious 2008 Prince of Asturias Award for International Cooperation.
Due to expansion in its operations, IHI wishes to invite qualified young graduates from higher learning institutions in Tanzania or any other qualified Tanzanians working in foreign countries who intend to pursue their future career as Research Scientists. Candidates can be hired to work with IHI as part of post-doctorate or establish their own doctoral programme of studies within the institute. The Institute shall facilitate acquisition of funding for doctoral and post doctoral research studies in the following areas:-
1. Medical Statistics (1 post)
2. Clinical epidemiology and Public Health (1post)
3. Demography (1post)
4. Pediatrics (1post)
An attractive salary and other fringe benefits shall be offered based on right qualifications and experience
MODE OF APPLICATION
Interested candidates are invited to send their expression of interest attaching curriculum vitae (CVs) and photocopies of academic and professional certificates to the undersigned address. Potential and qualified candidates shall be invited for a first round of interviews in mid May, 2010 and the final round of interviews will be held in mid June, 2010. We will only communicate with successful candidates.
All expression of interest should be sent to:-
Human Resources Manager
Ifakara Research Institute
Kiko Street, Mikocheni
P.O.Box 78373
Dar es Salaam
Fax No. 022 2771714 or send your application through
The deadline for receiving expression of interests is 10th May 2010.
IHI is an equal opportunity Employer. Women are highly encouraged to apply.
msaada kwenye tuta
Final TV debate: Key moments in text and video
Skype Name: Kimbache1
dogo wa USWAZI leo
bongo tambarare, hasa wakati wa mvua...
ngoma imedata katikati ya barabara sehemu za mikocheni TMJ jijini dar
kila juhudi za kuiwasha inashindikanaglamourous event management contacts
For more info please visit:
Email: info@glamorous.co.tz
Tel: +255 22 2772230/0784 410254
msaada tutani
Namtafuta Bwana mmoja anaitwa kwa jina la Ukoo Mshauri. Huyu bwana alikuwa University of Dar es Salaam miaka ya 1999. Alikuwa anachukua BCom. Nadhani alikuwa anaishi Magomeni. Na kama sikosei aliacha chuo na kwenda USA, ama alienda USA baada ya kumaliza chuo.
Yeyote anayemjua naomba contacts zake kwa kupitia
Asanteni,
Mak.
stanbic introduces islamic banking
Stanbic Bank Managing Director Bashir Awale (C ) addressing a press conference about the launching of Stanbic Islamic Banking in Dar es Salaam yesterday. Looking on are banks Director Personal Business Banking, Douglas Kamwando (L ) and Stanbic Head of Marketing and Corporate Affairs, Abdallah Singano.
Stanbic Bank Managing Director Bashir Awale (C ) after addressing a press conference on the launch of Stanbic Islamic Banking. Left is the bank's Director Personal Business Banking, Douglas Kamwando and Stanbic Head of Marketing and Corporate Affairs, Abdallah Singano. Mfumo wa benki wa Shariah unaenda sambamba na kanuni za dini ya Kiislamu, ambao unakataza upokeaji na ulipaji wa riba. Pia uwekezaji wa fedha katika biashara ambazo huendana kinyume na maadili ya dini za Kiislamu hauruhusiwi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Stanbic, Bwana Bashir Awale alisisitiza umuhimu wa huduma hii katika nchi hii, hasa ukizingatia uwepo mkubwa wa waumini wa dini ya Kiislamu.
“Tukiwa kama benki inayoheshimu tamaduni na imani za wateja wetu, tumeona umuhimu mkubwa wa kuwa na huduma ya mfumo wa benki wa Shariah nchini. Zaidi ya asilimia hamsini ya watanzania ni waislamu, kwa hiyo ni muhimu kwa benki kuwapatia huduma zinazoendana na matakwa ya imani yao”.
Tanzania itakuwa ni nchi ya kwanza kati ya nchi 17 iliyomo benki ya Stanbic, inayojulikana pia kama Standard Bank, kuanzisha huduma hii.
Uzinduzi huu utashuhudiwa na viongozi na wakurugenzi kutoka makao makuu ya benki ya Standard pamoja na viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na viongozi wa dini ya Kiislamu.
“Tunaamini kuwa huduma hii itakuwa na mafanikio makubwa kwa watanzania na kuwa msaada kwa jumuiya ya waumini wa dini ya Kiislamu ambao hawaamini mfumo wa ulipaji na upokeaji wa riba”, alimalizia kusema Bwana Awale.
Kwa taarifa Zaidi:
kpindi cha power breakfast cha clouds FM kikirushwa sasa toka kempinski
Kutoka kulia ni Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Dr Kafumu,Muongozaji wa Kipindi Sebastian Maganga,Barbra Hassan,Paul James pamoja na Gerald Hando wakiwa Live asubuhi ndani ya hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk. Clouds Fm 88.4 kupitia kipindi chake cha Power Breakfast wakizungumza Live sasa hivi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk (Frame tree Lounge) na Kamishna wa madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Dr.D.P Kafumu ,kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya madini ikiwemo na sheria yetu mpya ya madini ambayo baadhi ya watu wamekuwa na walakini nayo. dogo wa USWAZI leo
The Next Level Season 6 Concert

The biggest gospel concert to hit Dar es Salaam is finally here!
Venue: City Christian Centre Auditorium (Opp Mzumbe University Dar Campus) http://www.ccc-upanga.org/
Guest Group : Krystaal from Canada
Time: 3pm
Entrance:
VIP: Tsh 10,000
Normal: Tsh 5,000
Children: Tsh 2,000
Get your tickets from the entrance gate
Or Email: thenextleveltz@gmail.com
Forward to all your address book
--
For
The Next Level Team
Email:thenextleveltz@gmail.com
Blog: http://thenextleveltz.blogspot.com/
Uwajibikaji, Umakini, Ukweli na Uwazi katika matumizi ya fedha ni nyenzo katika kuleta Maendeleo.
by Andrew M. Mwenda
In a discussion with President Paul Kagame, he told me that he had looked at some of the "poverty reduction" projects and they smelt bad. "There are projects here worth only $5m and when I looked at their expenses, I found that $1m was going into buying these cars, each one of them at $70,000.
Another $1m goes to buy office furniture, more $1m for meetings and entertainment, and yet another $1m as salaries for technical experts, leaving only $1m for the actual expenditure on a poverty reducing activity. Is this the way to fight poverty?" he asked as I shifted with glee in my chair.
Already, the government is auctioning these vehicles and so far has gotten over $3m from the sales. Mr Kagame has now issued a new directive, saying government should not purchase cars for its officials with more than 2,500 cc. But there is more: the government has placed a ceiling on mobile telephone expenses for all its ministers, military and security chiefs to 50,000 Rwanda Francs (Shs150, 000), and also ordered MTN Rwanda to cut off their international roaming access.
The directive also stops the holding of workshops, seminars and conferences on poverty reduction in posh hotels like the Intercontinental, Mille Collins etc, insisting they should be in government owned buildings at no cost. The order also requires all government ministries; departments and agencies to move from privately owned buildings where they pay high rents to government owned buildings.
I told Kagame that whereas some of the most highly skilled Africans are going to Europe and North=2 0America to clean streets and toilets, our development partners send us Å’technical experts on these projects at individual monthly salaries of between $10,000 and $20,000, a salary that could pay 12 Africans of better training and experience and save this continent from severe brain drain. In fact, most of these so-called experts are a miserable, career-stranded lot in their own countries, but are dumped in Africa and other poor countries through foreign aid protocols.
Donors never shy from lecturing our governments on fiscal frugality, yet their aid driven projects are the most profligate. Of total project aid to Uganda's ministry of Health, 93 percent of it goes into technical assistance (i.e. salaries and allowances for the experts) and overheads (i.e. four wheel drive vehicles, opulent office furniture, computers, stationary, tea and cakes).
Only a miserable 7 percent of this aid goes into purchase of drugs. Now you understand why, in spite of a huge health budget, our people cannot find drugs in hospitals. We in the media have been shouting ourselves hoarse against government corruption. It is time to expose the worse forms of profligacy, which forces our governments to pile up huge sums in debt.
A few weeks ago I presented the above facts to President Yoweri Museveni and asked him to act. My heart bleeds to say he is so deeply discredited by his inability to tackle corruption in his government, and his own profligate public administration expenditure that he lacks moral authority to take on donors.
The other reason is that his regime lives off this coalition of mutual deceit with donors that both are fighting to eradicate poverty in Uganda. Kagame, however, is able to act boldly because he occupies a moral high ground in fighting corruption, has ensured fiscal frugality and also because his government pursues strategies of survival - not necessarily dependant on donor approval.
In Rwanda, ministers and other high ranking public officials resign and or are fired by the week because of allegations of corruption. From the lowest clerk in a government office to the most powerful minister or military or security chief, no one is immune to jail when they steal; none close to the president, none distant from him. You steal, you get jailed.
If there is some prima facie case that you stole, but there isn't not enough evidence to convict you in a court of law, then you are asked to resign or get fired. What a tough guy this Kagame man is!!
Mdau Benedict Kimbache
skype Name: Kimbache1
FFU ughaibuni kupiga kwata Munich Mei 8, 2010
Wazee hawa wa kukaanga mbuyu wenye maskani yao huko Ujerumani wanatarajiwa kuwasili mjini Munich aka Muchen siku ya jumamosi ya 8 May 2010 kwa ajili ya kufanya onesho la shamra shamra ya Sherehe za kombe la kandanda la Dunia,ambalo kwa mara ya kwanza litafanyikia nchini Afrika Kusini aka Azania.
Wakazi na washabiki wa mji wa Munich,ambako ndipo makao makuu ya klabu ya mashuhuri ya kandanda "Bayern,Munich" ,watapata bahati ya kusakata mziki wa dansi kutoka kwa mzimu wa dansi "The Ngoma Africa Band".
Bendi ambayo inasifa za tabia ya kupelekana mchaka mchaka na washabiki wake kwa kutumia mdundo wake wa dansi. Hebu cheki mwenyewe:
Bendi hiyo ni juzi tu waliachia singo CD yao iliyobeba jina la "Jakaya Kikwete 2010" na kufanikiwa kuteka washabiki lukuki katika youtube!
Wadau wa Bayern kaeni tayari tayari kwa kusakata magoma mpaka asubuhi lakini hamna kukesha! Shotooooozzzzzzz GEUKA! Whaaaaam!
kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Temu
simu +49(0)179 6661748
good news from the american people
Chief Executive Officer of the U.S.-funded Millennium Challenge Account – Tanzania, Mr. Bernard Mchomvu, and representatives from Aarsleef/BAM signed a contract worth more than US $97.1 million for the upgrading of the km 96.5 Laela – Sumbawanga road on April 29, 2010 in Dar es Salaam.
wahenga wa kijitonyama wawalamba wa Afya 4-1
ajali ya basi tanga iliyoua 18 tanga kwa hisani ya ITV
Mara kadhaa watu wamekuwa wakitoa maoni kuhusiana na vyanzo vya ajali, ikiwemo vyombo vibovu vya usafiri, barabara mbaya, kukosa umakini kwa dereva na kauli chochezi za abiria.
Hili la baadhi ya abiria kuwa ni chanzo cha ajali za barabarani limedhihirika katika ajali iliyotokea mkoani Tanga ambapo wanafunzi wapatao kumi na wanane (18) walipoteza uhai na wengine mia moja, ishirini na watano (125) kujeruhiwa.
Wanafunzi wa chuo Cha Shamsil-Maarif, Dunga - Tanga walikuwa wamepakia lori aina ya Fuso wakitoka katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyokuwa katika kijiji cha Kibafuta.
Inasemekana abiria hao walikuwa wakimshawishi dereva kuongeza mwendo na walipofika sehemu ya kipita-shoto walimtaka dereva kurudia kuzunguka mzunguko huo na ndipo tairi ilipogonga katika kiambaza na kusababisha ajali katika eneo hilo.
Mtembelee SUBI kwa habari zaidi
AY na FA wanakuambia usije mjini...
Tungo zao mara nyingi zimekuwa na tabia ya kugeuka na kuwa misemo ya mjini,gumzo la mitaani na hata kutumiwa “kibiashara” na makampuni kadhaa ya biashara. Bila shaka unakumbuka chanzo cha misemo kama vile Habari Ndio Hiyo,Nangoja Ageuke, Unaoa lini:Bado nipo nipo,Bed and Breakfast nkNi vijana ambao mpaka hivi sasa wanaweza kusema ‘wana mafanikio” fulani kutokana na kazi zao za muziki.Walianzia East Coast na mara kundi hilo lililokuwa na makazi yake pale Upanga-Dar-es-salaam,liliposambaratika wao wameendelea kuwa pamoja kama marafiki na pia wasanii wanaoshirikiana.
Tunawaongelea Mwana FA na A.Y ambaye siku chache zilizopita alipata tuzo ya Teenz kutoka nchini Kenya kama Favourite Artist wa East Africa. Safari hii wimbo unaitwa Usije Mjini. Kwanini nisije mjini wakati mjini nasikia ndio mambo yote? Kila mtu anataka kuja mjini.Mjini hata kwa kuuza maji tu unaweza kujipatia kipato.Mjini kuna starehe zote…inaaminika. Sasa kwanini A.Y na Mwana FA wanasema Usije Mjini? Sikiliza kwa makini tungo hizi;
Sporah Show to be aired on Star TV!
sera ya TEKNOHAMA Tanzania
President Kikwete arrives in Kampala for The East Africa Investment Conference
Uganda's Vice President Prof.Gilbert Bukenya welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International airport for The 3rd East Africa Investment conference.
A young ugandan girl Clarissa Kanyenjeka presents a bouquet of flowers to president Jakaya Kikwete shortly after he arrived at Entebbe International Airport for the EAC investment conference to be held ta Munyonyo Speke Resort in Kampala.
Traditional dancers intertain President Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage shortly after he arrived at Entebbe airport for the crucial EAC conference on investment.
Uganda's Vice President Prof.Gilbert Bukenya escorts president Jakaya Kikwete through Entebbe airport shortly after he arrived for the 3rd East Africa Investment conference to be held at Munyonyo speke Resort in Kampala(photos by Freddy Maro)
SHEREHE YA JUMUIYA YA WATANZANIA READING
Jumuiya ya watanzania Reading inapenda kuwaalika watanzania wote waishio Uingereza kwenye sherehe ya kuwasimika viongozi wapya waliochaguliwa tarehe 24.04.2010.
Jumuiya imewaalika viongozi mbalimbali wa kitaifa na vyama visivyo vya kiserikali. Mgeni rasmi katika hafla hii atakuwa ni mh. Mama balozi Mwanaidi Maajar.
Jumuiya imeandaa shughuli mbali mbali siku hiyo ikiwemo nyimbo, mwakilishi wa reading post, wagombea ubunge kutoka vyama vya Labour, Conservative na Liberal Democratic pia wamealikwa kuwasimika viongozi.
Kingilio na vinywaji Bure
Ukumbi: The warehouse
1A Cumberland Road
Reading
RG1 3LB
Tarehe:03.05.2010
Muda: Kuanzia Saa 10 Jioni (4pm)
Mpaka Saa 5 Usiku (11pm)
Burundani: Italetwa na Dj Richie wa Bongo DEEJAYS
Kwa mawasiliano zaidi piga 07954563709, 07876126862, 07979428883
Nyote Mnakaribishwa
--
Jumuiya Ya Watanzania Reading-UK
http://www.tanzaniaassociation-reading.blogspot.com/
LIBENEKE LA LUGHA GONGANA....
YA UKRANE NUSURA YATOKEE KWENYE BARAZA LA MADIWANI WA MANISPAA YA MOSHI
Diwani wa kata ya Rau Christopher Limo akisoma taarifa iliyokuwa ikizungumzia mafaniko ya Halmashauri jambo lililopelekea kutokea varangati hilo
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Bernadete Kinabo akiomba mwongozo wa Meya Lameck Kaaya wa kumtaka kumtoa nje ya Kikao Diwani wa Pasua Japhary Michael Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilitoa hati ya eneo la Uhuru Park kwa kampuni hiyo ili iitumie hati hiyo, kukopa Shilingi Bilioni 1.5 benki kwa ajili ya kuendeleza eneo hilo.
Huku wakitoka nje ya kikao cha baraza hilo,Madiwani hao sita wakiongozwa na diwani wa kata ya Mji Mpya, Bw. Abuu Shayo alikuwa akirusha joho, kofia na koti lake la suti katika meza kuu ya viongozi huku wakisema wamechoshwa na vitendo vya kuburuzwa.
Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa kwa dharura ili kutengua uamuzi wa awali wa baraza hilo kumpa nusu hati mwekezaji kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam,kilitengua rasmi uamuzi wake wa awali wa Machi 31 mwaka huu.
Kauli hiyo iliunga mkono na madiwani wa Kiborloni Vicent Rimoy, viti maalum Hawa Mushi na mbunge wa viti maalum Lucy Owenya ambao walisema hawakubaliani na baraza hilo kuleta hoja juu ya hoja.
Kutokana na kitendo cha diwani Lyimo kuendelea kusoma taarifa hizo,madiwani Shayo na Michael walisimama na kutaka meya wa manispaa hiyo kuwapa nafasi ya kutoa taarifa lakini walipoona hawasikilizwi waliamua kutoka nje ya kikao.
“Mheshimiwa Meya nini mnatufanyia hapa……agenda ilikuwa ni moja ya Uhuru Park, hili suala la ujenzi wa madaraja na madarasa linatoka wapi,
Aliongeza”Umesikia yaliyotokea nchini Ukraine!! Acha kusoma hiyo taarifa yako nenda kaisomee katika vikao vya CCM, hamuwezi kutuchezea hapa, hii hoja si mliipitisha ninyi wenyewe, leo yamewafika mnataka kutunyima nafasi ya kuijadili”.
Kutokana na hali hiyo Meya Kaaya aliagiza madiwani Shayo na Michael kutolewa na askari nje ya ukumbi na askari wa manispaa,ambapo walikuja askari Dismas Raphael na Mwasiti Shabani ambao kwa maelekezo ya mwanasheria,Kisa Lyimo waliwatoa nje ya ukumbi madiwani hao huku wenzao wakiwafuata.
Wakati wakitoka nje ya ukumbi,diwani Shayo alivua joho lake na kumtupia meya Kaaya huku akivua kofia yake na kumtupia mkurugenzi Kinabo kwa madai kuwa wanayumbisha na madiwani wa CCM hivyo kushindwa kufuata kanuni na sheria zilizopo.
Kufuatia vitendo hivyo,Meya Kaaya alitangaza madiwani hao kufikishwa katika kamati za maadili huku diwani Shayo akisimamishwa kutohudhuria vikao vitatu vya baraza hilo.
Mapema mwezi Machi kampuni ya DTH iliyokuwa na mkataba wa mika 10 iliomba kupatiwa hati Usu ya kumiliki eneo hilo ili waweze kuomba mkopo huo wa Bilioni 1.5 ili kuendeleza bustani hiyo.
Baadaye wadau mbalimbali wakiwemo wananchi walipinga uamuzi wa madiwani hao huku wengine wakitishia kufanya maandamano ili kupinga hatua hiyo .
mwisho.








































