In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for May 2010

Ndovu Special Malt yapokea tuzo ya Grand Gold Ujerumani leo


Medali ya Grand Gold kwa Ndovu Special MartCheti cha ushindi wa Tuzo.
Meneja wa Ndovu Special Mart,Oscar Shelukindo na Mpishi Mkuu wa TBL, Mzee Gaudence Mkolwe wakiwa ni wenye furaha na fahari ya kupokea tuzo ya Grand Gold Quality 2010 waliyoipata usiku wa kuamkia leo jijini Wiesbaden,nchini Ujerumani.
Mmoja wa Watanzania waishio ujerumani akijiunga wadau wa Ndovu Special Mart kushangilia ushindi wa kilaji hicho.
Meneja wa Ndovu Special Mart,Oscar Shelukindo na Mpishi Mkuu wa TBL, Mzee Gaudence Mkolwe wakipokea tuzo ya Grand Gold Quality ya Ndovu Special Malt jijini Wiesbaden, Ujerumani, usiku kuamkia leo
Ndovu Special Malt ikitangazwa mshindi wa tuzo ya Grand Gold.


Vodacom yakabidhi madarasa mawili Kyela

Juu na chini wanaonekana Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kyela, Martha Mgeta, akitakata utepe wakati wa uzinduzi wa madarasa mawili ya shule ya Sekondari Ipinda iliyoko Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, aliyepembeni yake ni Mkurugenzi wa Vodacom, Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga na mwenye suti ya kijivu ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Agetile Mwakalinga, Mfuko wa Vodacom umejenga madarasa hayo kwa shilingi milioni 19.5


mchakato wa kumfanya mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu

Kiongozi wa Marian Healing Faith Centre cha River Side, Ubungo jijini Dar, Fr. Nkwera akisalimiana na viongozi wakati wa sherehe hizo mwezi juni mwaka jana
mama Maria Nyerere akimwagilia mti ambao ameupanda katika viwanja vya Kanisa la Namugonga nchini Uganda nje kidogo ya jiji la Kampala. hii ilikuwa Juni mwaka jana
Rais Museveni akimkaribisha Mama Maria Nyerere shereheni huko Namugogo. Chini akimwagilia mti alioupanda kama kumbukumbu ya siku hii

Na Paulo Malimbo wa
Globu ya Jamii, Namugogo,
Hizi ni baadhi ya picha za mchakato wa kumuombea baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na baadaye kuwa Mtakatifu. Kisheria na tofauti na ilivyoripotiwa awali, mtu hawezi kuwa mtakatifu kabla hujawa mwenyeheri.


Rais Yoweri Museven wa Uganda alisema kuanzia sasa (last year 2009) kila June mosi itakuwa siku ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ili aje kutangazwa kuwa Mwenyeheri na hatimaye kuwa mtakatifu.



Hivyo hajatangazwa kuwa mtakatifu na mtu yeyote hapa Duniani. Kilichopo hivi sasa na ambacho pia kitakuwepo Jumanne ambayo ni June mosi katika Kanisa la Namugongo nchini Uganda na ambapo marais mbalimbali wanatarajia kuhudhuria, kama siyo wawakilishi wao, Ibada hiyo ni kuomba mchakato wa kumfanya baba wa Taifa kuwa Mwenye heri na hatimaye Mtakatifu.


Familia ya Mwalimu Nyerere imeondoka Tarehe 28 kwenda kuhudhuria misa hiyo ambayo itafanyika June mosi na baadaye ibada kubwa ya hija ambayo itafanyika hapo hapo Namugongo. Namugongo ni eneo la hija ambalo lilitumika kuwatesa mashahidi wa Uganda 22 ambao waliuawa kwa kuchomwa moto na kukatwakatwa mapanga.


Kwa sasa maelfu kwa maelfu ya watu wamekuwa wakienda katika eneo hilo ili kuhiji wakitokea Ulaya, Kenya, Rome, Tanzania, Sudan, Rwanda, Burundi, Congo na kwingineko duniani. Wale walioko katika mikoa ya karibu nchini Uganda pamoja na nchi jirani za Rwanda na Kenya wamekuwa wakienda eneo kwa kutembea kwa miguu kutokea nchini mwao.


Mama Maria Nyerere yuko Namugongo akiwa ni sehemu ya wanahija ambaye ameongozana na wanamaombi wa kituo cha Marian Healing Faith Centre cha River. Aliyeanzisha mchakato wa kumuombea Baba wa Taifa kuwa Mwenye heri na hatimaye kuwa Mtakatifu ni askofu wa Jimbo Kuu la Musoma.




JK at the International Criminal Court Review Conference in Kampala

---President Jakaya mrisho Kikwete delivers his speech during the opening of the International Criminal Court Review conference in Kampala Uganda this morning.Seated second left is the UN Secretary General Ban-Ki-Moon
--President Jakaya Mrisho Kikwete, Uganda's President Yoweri Kaguta Museveni(centre) together with Former UN Secretary General Koffi Annan in conversation shorly after the opening of the International Criminal Court Review Conference in Kampala this morning.
Photos by Freddy Maro


WIZARA YA HABARI YAKUTANA NA WAHARIRI LEO

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Seith Kamuhanda akiongea na wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine ametoa changamoto kwa wahariri wawe chachu katika kuleta mabadiliko na kuhakikisha kuwa habari zinazotolewa zilenge katika kuchochea maendeleo nchini.
Juu na chini ni Wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda wakati alipokutana nao leo Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.





libeneke la ndovu ujerumani


viwanja vinauzwa Bunju

Naitwa ibra na naishi Dsm, ni Mfanyakazi katika shirika binafsi,ni mpenzi sana wa blog yako na kwakweli nimevutiwa nayo,Ombi langu kwako ni kwamba naomba unirushie hili tangazo langu kwan nimeona watu wengi wako interested na blog yako na wako siriaz na vitu uvitoavyo wewe.

Kwa mawasiliano apige No 0713 241030
Kuna shamba nauza liko Bunju "A"zaid ya Ekali 10 na tumekata na kupima vipande vipande so kwa mwenye kuhitaji viwanja vya kujenga ni sehemu tulivu na yenye mandhari mazuri.

aulize ndugu ibra ama 0712145237
Abdalla aka Kide

Bei Ya kila kipande chenye ukubwa hatua za miguu ishini upana na ishirini urefu ni 5 milion na itapungua kidogo

vipo viwanja 5,nitashukuru kwa msaada wako utakaonipa na pia tutasaidiana pindi mambo yatakapokuwa fresh!

Kazi njema
Mdau Ibra


MTARAJIWA MARIAM APENDEZA

BI HARUSI MTARAJIWA MARIAM AKIWA NA RAFIKI ZAKE KATIKA MNUSO WA SHEREHE YAKE YA HENNA PARTY


mamlaka ya elimu yafanya ziara mkoani mbeya

MWALIMU WA TAASISI YA TEKNOLOJIA NA SAYANSI MBEYA ,BW DANIEL SIKONDE (KUSHOTO) AKITOA MAELEKEZO KWA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) JUU YA MOJA YA VIFAA VYA KUFUNDISHIA VILIVYOTOLEWA NA MAMLAKA HIYO, KWA VIFAA VILIVYOTOLEWA NA TEA VINA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 436.
MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA BIBI. ROSEMARY LULABUKA (KUSHOTO) AKIANGALIA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI UYOLE ILIYOPO JIJINI MBEYA WAKITUMIA VIFAA VYA MAABARA VILIVYOTOLEWA NA MAMLAKA YA ELIMU KWA SHULE HIYO, PAMOJA NA VIFAA HIVYO PIA MAMLAKA YA ELIMU ILITOA VITABU, KWA PAMOJA MSAADA HUO UNA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 16.
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI UYOLE YA JIJINI MBEYA WAKIONESHA VITABU VITABU VILIVYOSAIDIWA NA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA), PAMOJA NA VITABU HIVYO TEA IMETOA VIFAA VYA MAABARA KWA SHULE HIYO, VIFAA VYOTE VINA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 16.


coconut fm zanzibar yatimiza miaka 5

Timu ya redio Coconut Fm 88.2 Fm ZanzibarMmoja wa watangazaji wa Coconut Fm 88.2 Zanzibar, akimlisha keki mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd, ambao ni wamiliki wa kituo hicho kwa niaba ya Uongozi wa Kampuni pamoja na Clouds Media Group.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions, ambao ndiyo wamiliki wa Redio Coconut Fm 88.2 Zanzibar Godfrey Kussaga akimlisha keki mmoja ya watangazaji nguli wa Redio Coconut Fm 88.2 Husna B.


Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI Lafanyika U/Taifa

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mariam Mwafisi akiongoza joging ya Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI yatakayofanyika mkoani Tanga Septemba 17-Octoba 2, 2010 mkoani Tanga
Wanamichezo Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika Joging TUMESHERIA Sports Club wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi akikabua timu ya Kilimo
Mgeni rasmi akikagua timu ya Uhamiaji.


Timu ya Ndovu yatua Ujerumani kupokea tuzo

Video ya mambo yalivyokuwa usiku wa kuamkia leo huko Wiesbaden, Ujerumani
Kushoto ni Bw. Edwin Gafa, kiongozi wa msafara wa Nile Breweries ya Uganda ambao wamepata tuzo ya kushiriki mara nyingi kwenye Monde Selection, Wawakilishi wa kampuni ya TBL ,Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo akiongozana na Mpishi mkuu wa kampuni hiyo (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe. Jioni ya leo Ndovu itanyakua tuzo yake ya Gold Grand Award kwa ubora
Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo (TBL) pamoja na Mpishi mkuu wa kampuni hiyo (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe wakiwa na bidhaa yao ya Ndovu ambayo leo jumatatu usiku itapokea tuzo ya Dhahabu kwenye sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yatazawadiwa.

Mpishi mkuu wa kampuni ya TBL (Chief Brewer) Gaudence Mkolwe akiangalia vinywaji mbalimbali vilivyopo kwenye sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yalizawadiwa.
Meneja wa Ndovu Lager Oscar Shelukindo (TBL) akiangalia moja ya kinywaji kilichoibuka kwenye ushiriki wa kunyakua tuzo usiku wa kuamkia leo,ambapo hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kurhaus mjini Wiesbaden,chini Ujerumani. Meneja wa kinywaji cha Ndovu Oscar Shelukindo na mpishi mkuu wa TBL Gaudence Joseph Mkolwe wakipeperusha bendera ya Tanzania katika sherehe za Monde Selection ndani ya ukumbi wa Kurhaus jijini Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo
Sherehe za ubora wa bidhaa za Monde Selection ambazo zimeanza rasmi katika ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo, ambapo makampuni kibao toka kile pembe ya Dunia ambayo bidhaa zake zimeibuka kuwa washindi wa ubora yatazawadiwa
Wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi wa Kurhaus jijini la Wiesbaden, Ujerumani usiku wa kuamkia leo.
Meneja wa kilaji cha Ndovu Oscar Shelukindo na mpishi mkuu wa TBL Gaudence Joseph Mkolwe wakijiandaa kuingia katika gari maalumu lililokuja kuwapokea katika uwanja wa kimataifa wa Frankfurt, Ujerumani, tayari kupokea tuzo ya dhahabu iliyopewa kilaji cha Ndovu
Oscar na Mzee Mkolwe wakiwa katika jumba la Kurhaus mjini Wiesbaden wikiendi hii ambako sherehe za Monde Selection za kutuza bidhaa bora duniani zinafanyika. Tuzo ya Dhahabu iliyopata kilaji cha Ndovu inatolewa jioni ya leo katika ukumbi huo.


JK arrives in Uganda for the International Criminal Court Review conference

A four years Ugandan pupil Christina Kwezi hands over a bouquet of flowers to President Jakaya Kikwete shortly after he arrived at Entebbe international airport this evening.President Kikwete is Uganda to attend the International Criminal Court(ICC) Review Conference.
President Jakaya Mrisho Kikwete inspects a guard of honour mounted by the Uganda's People Defence Force shortly after he arrived at Entebbe Airport in Uganda to attend the International Criminal Court Review conference.
Buganda Traditional royal Dancers entertains President Jakaya kikwete and his delegation shortly after he arrived at Entebbe airport this evening to attend the ICC Review Conference(photos by Freddy Maro)
---------------------------------------------------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya leo, Mei 30, 2010, kwenda Kampala, Uganda, kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Nchi Wanachama wa Mkataba Ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

Rais Kikwete anahudhuria Mkutano huo kwa mwaliko wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Mkutano huo unaoanza kesho, Jumatatu, Mei 31, 2010, miongoni mwa mambo mengine utapitia na kufanya marekebisho katika Mkataba ulioanzisha ICC.

Mkutano huo unatarajiwa kumalizika Juni 11, 2010, lakini Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani keshokutwa, Juni Mosi, 2010.

Aidha, mkutano huo unatarajiwa kupitia orodha ya makosa manne yanayoorodheshwa chini ya Mamlaka ya ICC kwa lengo la kuongeza ama kuyatolea ufafanuzi zaidi makosa hayo.

ICC ina Mamlaka ya kuhukumu makosa manne ambayo ni Mauaji ya Kimbari (Genocide), Makosa Yafanyikayo Wakati wa Vita (War Crimes), Makosa Dhidi ya Binadamu (Crimes Against Humanity) na Uchokozi ama Ushari (Aggression), kosa ambalo halijapata tafsiri inayokubalika kimataifa katika Mkataba huo wa Roma

Mkutano pia utafanya tathmini ya shughuli za Mahakama hiyo tangu ilipoanzishwa Agosti, 1998, mjini Roma, Italia na kupendekeza namna ya kuboresha shughuli hizo.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
Ikulu-Dar Es Salaam
Mei 30, 2010


Lovely Gamble Yazinduliwa rasmi nchini Uingereza

Washiriki wa Tamthilia ya Lovely gamble wakiwa na Viongozi wa TA pamoja na Afisa wa Ubalozi Amos Msanjila. Mwandishi wa TZ-ONE Ally Muhdin akiwa na mshiriki wa Tamthilia ya Lovely Gamble Ann Lynn Kapinga.


Urbun Purse wamezindua rasmi tamthilia ya "Lovely Gamble" katika mji wa Reading, nchini Uingereza.

Tamthilia hiyo inayohusu Mapenzi, Muziki, Usaliti na Uongo imetungwa na Frank Eyembe pamoja na Alan Kalinga.

Mhariri wa tamthilia ya "Lovely Gamble" Baraka Baraka amesema wamejaribu kutengeneza tamthilia hiyo katika kiwango cha kimataifa ili kuweza kulingana na tamthilia nyingine zinazoonyeshwa duniani.

Mtunzi wa tamthilia hiyo Frank Eyembe amesema jina la tamthilia limejieleza kwani kila kitu kinachohusiana ya tamthilia wamecheza pata potea kwani hawakujua jinsi gani wataweza kufikia hapo walipofikia.

Matukio na mambo yaliyofanyika katika tamthilia hiyo hayajalingana na tamthilia nyingine.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa tamthilia hiyo Mwenyekiti wa TA John Lusingu amesema amefurahishwa na kitendo cha Watanzania kujitokeza na kuonyesha kuwa na uwezo wa kufikia mbali katika utengenezaji Tamthilia.

Akiongea kwa niamba ya Balozi Maajar, mgeni rasmi Amos Msanjila alitoa shukrani kwa waandaaji na watayarishaji wa tamthilia hiyo kwa kukumbuka kama kuna ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kuweza kushikiana nao katika hafla mbalimbali.

Bw. Msanjila alifurahishwa sana na kazi waliyoifanya Watanzania walio nje ya nchi kwa kuweza kujitafutia ajira na kuitangaza nchi yao katika masuala ya tamthilia.

"Jamani tupende vyetu" miaka ya 90 hatukuwa na uwezo kama tuliofikia hivi sasa. Alisema Msanjila.

Amewashauri Watanzania wasiogope Uthubutu, wakubali kurekebishwa na tupeane moyo.
Akifunga hafla ya tamthilia hiyo, Bw. Eyembe alitoa shukrani za dhati kwa Watanzania wote waliojitokeza na kutoa michango katika kufanikisha kuitangaza tamthilia hiyo.

Pesa zitakazopatikana katika mauzo na maonyesho ya tamthilia ya "Lovely Gamble" zitachangia watoto yatima na jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Uingereza.
Ally Muhdin
wa


twiga stazz yakabidhiwa bendera tayari kwa kwenda kuwakabiri wa Eritrea.

Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi (shoto) akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya taifa ya Wanawake ‘Twga Stars’ Sofia Mwasikili wakati wa hafla ya kuagwa kwa timu hiyo iliyofanyika leo kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Eritrea kwa ajili ya mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Eritrea. wachezaji wa Twiga Stars wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ulinzi,Mh. Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati wakikabidhiwa Bendera ya Taifa kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye mechi ya marudiano na timu ya Erirtea.


singida mabingwa wapya kili taifa cup

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Mh. William Lukuvi akikabidhi kombe la ubingwa wa Kili Taifa Cup kwa Kapten wa timu ya Singida,Rajab Mohamed huku mfungaji wa magoli mawili kati ya matatu yaliyoizima timu ya Lindi katika mchezo wa leo,Kelvin Charles akishuhudia.wengine ni Rais wa TFF,Reodger Tenga (kulia) na Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. John Chiligati (kulia),Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mh. Parseko Kone (alieshika kombe) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya mkoa wa Singida mara baada ya kupata ubingwa wa Kili Taifa Cup katika mchezo uliomalizika jioni hii dhidi ya Lindi ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imenyakua ubingwa kwa kuichapa mabao 3 - 0 timu ya mkoa wa Lindi.
mshambuliaji wa timu ya Singida,Kelvin Charles akipachika bao la tatu katika mechi iliyochezwa jioni ya leo dhidi ya Lindi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imeshinda 3 - 0 na kuweza kunyakuwa ubingwa wa Kili Taifa Cup. mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Lindi,Omari Matwiko akijaribu kutaka kumtoka kiungo wa timu ya Singida,Rajab Mohamed.


Mkuruenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akibadirisha mawazo na wadau mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali baina ya Singida na Lindi uliochezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Singida imeshinda 3 - 0.


Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker