In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for June 2010

Miaka 50 ya taasisi ya dr. jane goodall

Naibu Balozi Uingereza Chabaka Kilumanga akiteta na Dr Jane Goodall kwenye tafrija ya miaka 50 ya Taasisi yake . Dr Goodall alikuja Tanzania kwanza 1960 alivyokuwa na miaka 23 . Utafiti wa Nyani ( Chimpanzee) Gombe ambayo imesaidia kukuza jina la Tanzania kwenye maswala ya hifadhi ya wanyama aina ya chimpanzee duniani.


uzee

Uzee kitu adhimu, huo ninauingia
Ujana sasa adimu, Shabani aliusia
Maungoni mwangu humu, uzee unanijia,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Mbali ninamuachia, rafiki yangu ujana,
Miaka inakimbia, ya leo siyo ya jana,
Nabaki nakumbukia, nilipokuwa kijana
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Shabani aliandika, kaulilia ujana,
Ni vipi unamtoka, kashindwa kuung’ang’ana,
Meno yalimdondoka, na nguvu tena hamna,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Taratibu waingia, uzee wabisha hodi,
Siwezi kuukimbia, hata niwe mkaidi
Hata nikitukania, ndivyo napigwa baridi,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee

Mvi sasa zanijia, nimejaribu kung’oa
Kidevu zasalimia, na miye nazichomoa,
Nikitoa zazidia, nami nazidi kutoa!
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Mapensi nayaachia, na macheni ya shingoni,
Hereni nilivalia, kwenye sikio jamani,
Mwendo nilibadilia, nilivyonesa njiani,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Niliwapata mademu, tena wengine kwa zamu,
Nikaitwa mtaalamu, wa mambo yale matamu
Sasa yanitoka hamu, nanyimwa hata salamu!
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Nilenda nilipotaka, wasiponitaka nilenda,
Sikuwa na hata shaka, ati mtu kunidunda,
Leo naogopa paka, ninavutwa kama punda,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Mwendo wa kudemadema, nikishika natetema,
Uso umenikunjama, natembea nikihema,
Magoti nayo yauma, uzee si lele mama!
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Kumbe maisha ni hivi, uzee haukwepeki,
Ninazikubali mvi, hata kama sizitaki,
Uzee siyo ugomvi, ujana haushikiki,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Kweli nilifurahia, enzi zile za ujana,
Kamwe sintoyarudia, yalopita naagana,
Uzee nakumbatia, kwani lingine hakuna,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Nasubiri wajukuu, nione na vitukuu,
Nakunja miguu juu, na mshukuru Mkuu
Kuona umri huu, enzi hizi ni nafuu,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Na. M. M. Mwanakijiji
(Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)


Balozi Juma mwapachu kufungua rasmi sabasaba 2010 kesho

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Baiashara ya Nje (TANTRADE), Bw. Ramadhan Khalfan akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar leo kuhusu maandalizi ya ufunguzi rasmi wa Maonesho hayo utakaofanywa kesho Alhamisi Julai 1, 2010 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu.


Banda la maonesho la JWTZ Sabasaba

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Banda lao katika Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa jijini Dar leo. Aliongelea pia juu ya ajali ya ndege yao iliyotokea jana, eneo la Kabuku, Kijiji cha Manga mpakani mwa mikoa ya Pwani na Tanga.Marubani waiwili wa ndege hiyo walifariki.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo akiangalia maonesho kwenye Banda la JWTZ katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Dar
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Andrew Nyumayo akipigiwa saluti na vijana wa
chipukizi alipokuwa akiingia kwenye banda la Jeshi la Wananchi Tanzania, kuangalia maonesho
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere leo.




kamanda wa FFU ughaibuni apigishwa kwata na dogo amsterdam

Kamanda wa FFU ughaibuni
Ras Makunja na dogo Prince Thabit


Dogo aliyejitambulisha kwa jina la Prince Thabit wa Amsterdam,akiwa na Kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Makunja wa Ngoma Africa band. Dogo alifanikiwa kumuweka chiini ya ulinzi kamanda huyo baada ya Ras Makunja kuvamia mitaa ya Amsterdam,Uholanzi bila ya taarifa!

Baada ya kufumwa na Dogo huyo, Ras Makunja alijitetea kuwa alikwenda mjini hapo kupangusa matongo tongo a.ka. mchanga wa uso. Baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na dogo huyo na kupigishwa kwata kwa masaa kadhaa Ras Makunja alijitetea kuwa kosa ni kurudia kosa hivyo baada ya kusamehewa aliasaidiwa lift kwa msaada wa Punda ulaya na kuambiwa arudi maskani kwake Ujeurimani huku akionywa kuwa siku ingine lazima aote taarifa iwapo ataingia katika jiji kubwa kama hilo. Kamanda alisalimu amri ya Dogo na kurudi mbio mbio katika kambi ya FFU wa ngoma Africa huko Ujerumani

Wakati huo huo habari zinasema FFU wa Ngoma Africa band watatumbuiza katika onyesho kubwa la World Music Festival,Loshausen,kando kidogo ya mji wa Kassel,Ujerumani,siku ya Ijumaa 23 Julai 2010,ambako washabiki wanasubiri kwa hamu kujimwaga uwanjani.
Taarifa hizo zimedatisha kwamba wazee hao wa kukaanga mbuyu mwaka huu hawataki mchezo. Wakiwa wameanza libeneke mwaka 1993 na kujizolea umaarufu kila kona duniani hivi sasa wanatamba na singo CD mpya iliyobeba jina "Jakaya Kikwete 2010".

jipendelee mwenye kwa kujipa raha at www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kujumika nao katika baraza la
www.facebook.com/ngomaafrica
pia usikose kubofya
www.world-music-festival.de


balozi mwapachu atangaza rasmi kuanza kwa soko la pamoja la afrika mashariki

Katibu mkuu wa jumuia ya Afrika ya mashariki, Balozi Juma Mwapachu, na naibu katibu mkuu wa jumuia hiyo, Alloysi Mutabingwa, wakitangaza kwa waandishi wa habari mjini Arusha leo kuanza rasmi kwa utekelezaji wa soko la pamoja la jumuia ya Afrika ya mashariki unaoanza rasmi kesho Julai 1, 2010 ambalo litalegeza masharti ya ajira,mitaji kuhamishwa kutoka nchi moja kwenda nyingine,huduma kuzunguka katika nchi zote pamoja na wananchi wa nchi hizo kuweka makazi. Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika ya mashariki, Balozi Juma Mwapachu, na Spika wa Bunge la Afrika ya mashariki Mh. Abdirahin Abdi, wakitangaza rasmi kuanza kwa utekelezaji kamili wa soko la pamoja la Afrika ya mashariki kuanzia kesho. Picha na habari na Novatus Makunga


mdau gladys kasesela awaombea mama na watoto msaada

Mama na watoto wake wanaoishi ufukweni
karibu na hospitali ya Ocean Road jijini Dar
Mdau Gladys Kasesela akipozi na mama na watoto
wake baada ya kuwapa zawadi ya miamvuli na nguo leo

Kwa wadau wa watoto wote
Kwa wale wanaopita barabara ya Ocean Rd karibu na Hospitali ya
Aghakhan utaomuona mama mmoja amekalia gogo akiwa na watoto wanne
wamemzunguka, mama huyu amekuwa anaishi eneo hili kwa muda mrefu.
Nasikitika kuwaeleza wapenzi wa watoto kuwa mama huyu amejifungua
mtoto wa 5, ukiangalia picha utaona kama amebeba katoto. Mama huyu na
watoto hawa wamekuwa wanaishi maisha ya hatari sana.

Mama huyu baada ya kuongea naye aliomba wasamaria wema wajitokeze kwa
ajili ya kulea watoto, wasi wasi wangu je sheria inasemaje, maana
sheria mpya watoto naamini ilipitishwa hivi karibuni, na pia juzi tu
tumetoka kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.
Kuna uwezekano kabisa mama huyu ana matatizo ya kiakili (mimi si mtaalamu kwa hiyo sina uhakika) lakini ana kumbukumbu kwamba baba ya watoto hawa, baba wa kwanza ni mchaga (mtoto anaitwa Haika), mtoto wa pili baba yake
Mkikuyu, mtoto wa tatu wa mgiriki , mtoto wa nne kazaa na Mkongo wa
nne anasema ni Mfaransa.

Leo hii nilipita ikabidi nimpe miamvuli na baadhi ya nguo, utaratibu
ambao nimekuwa nafanya mara kwa mara, pia ameniambia Mh Batilda Burian
amekuwa anamsaidia sana.

Nawaomba wadau mjitokeze kumsaidia mama huyu,
hasa watoto ambao wana kosa elimu na malezi bora.

Ahsante
Mdau Gladys Kasesela


shangingi lapiga mweleka maeneo ya manga mkoani tanga


Bro Mithupu,
"ndege" nyingine "ilianguka" sehemu hizo hizo za Manga Mkoani Tanga siku kadhaa zilizopita.Mwendo kasi sana wa shangingi-ndege ulisababisha gari kupaa na kugonga nguzo ya TANESCO iliyopo mlimani , na baadaye shangingi hilo kutua mtaroni.Abiria wote walipona.
Mshuhudiaji
Mdau Lawrence


utoaji tuzo kwa wanamuziki bora wa Zanzibar 2010

Mgeni rasmi Waziri wa kazi maendeleo ya vijana na watoto Mh Asha Abdalla Juma akimkabidhi tuzo ya Mh Mohammed Seif Khatib Meneja Masoko wa kampuni ya Zanzibar Media Corporation Ltd,Said Khamis akimkabidhi tuzo msanii Baby J
msanii Ali kiba akiwapa burdani walioshuhudia utoaji wa tuzo hizo
washindi wakipiga picha ya pamoja na mgeni rasmi


Mkutano wa Kuelimisha umma juu ya Mazingira na Umaskini wafanyika leo

Katibu Mkuu Ofis ya Makamu wa Rais Bi Ruth Mollel akifunguwa Mkutano wa wahariri wa Vyombo vya habari Magazeti,Redio,Televishen, Nchini Kuhusu Mazingira na Umasikini Ulioandaliwa na Kitengo cha habari Elimu na Mawasiliano Ofis ya Makamu wa rais
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Ruth Mollel (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa Vyombo vya habari nchini Mara baada ya Mkutano leo Mjini Dar es Salaam
Baadhi ya wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini Wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ruth Mollel [pichani hayupo} wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kuelimisha umma juu ya Mazingira na Umaskini uliofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam.{Picha na Ali Meja}


JK awasili Dodoma leo

wana CCM na wakazi wengine wa mjini Dodoma wakishuhudia ndege ya JK ikitua uwanja wa ndege wa mjini Dodoma. JK yuko mjini Dodoma tayari kwa kurudisha fomu za udhamini wa kugombea urais kupitia chama tawala cha CCM. Zoezi hili linategemewa kufanyika kesho tarehe 1 Julai 2010.


Tamko la BET la kupiga marufuku maonyesho ya Muziki na Ngoma za Utamaduni katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar

Habari wa ndugu wapendwa.

Chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJAtz) kimeshtushwa na kusikitishwa na uamuzi wa Bodi ya Biashara ya Nje (BET) wa kupiga marufuku maonyesho ya Muziki na Ngoma za Utamaduni katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kupitia waraka wake uliotolewa na UTAWALA, BET imepiga marufuku maonyesho yote ya sanaa za Kitanzania ikiwemo ngoma, muziki na maigizo eti kwa madai kwamba yanaleta kelele. wakati huohuo muziki unasikika ni ule wa wasanii kutoka nje ya nchi kwenye maspika makubwa. CAJAtz inatambua thamani ya sanaa na Utamaduni wa Taifa hili na inaamini kwamba sehemu kama hizo ndiyo muafaka hasa katika kutangaza shughuli za sanaa na Utamaduni wetu.

Tunaamini pia kwamba katika maonyesho hayo ya biashara makampuni na asasi mbalimbali huwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wao kwa watu mbalimbali hasa kwa kuamini katika nguvu ya sanaa. lakini tunashangaa leo hii kuona BET inawataza wasanii kutumia fani zao kutoa ujumbe kwa watu licha ya kuwa makampuni na asasi hizo zimetumia pesa kuwakodi wasanii hao. CAJAtz inaamini kwamba sanaa ni biashara hivyo kwanza ilipaswa kuachwa ili ijitangaze kupitia maonyesho hayo. Pia BET inapaswa kufahamu kwamba kwa miaka yote ambayo wameilezeza kuwa na Mafanikio makubwa katika maonyesho hayo, sanaa na hizo ngoma zilikuwa zinatumika sana katika kusherehesha, kutoa ujumbe na kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali ya washiriki. Kwa kitendo cha kupiga marufuku maonyesho ya sanaa BET imekosa UZALENDO na utamaduni wetu na pia imebana ajira ya wasanii wengi walikuwa wameajiriwa na makampuni kwa ajili ya kufanya shughuli za maonyesho kwenye mabanda yao.

Kwa Msingi huo kama wadau wa masuala ya sanaa na Utamaduni hapa nchini, CAJAtz tunalaani vikali zuio hilo ambalo halina tija na limeegemea zaidi ulimbukeni na Kasumba ya watu wa kuthamini sanaa za nje na kuwatukuza wageni wachache kwa visingizio visivyo na maana. Iweje sanaa za Kitanzania iwe kelele na hizo za magharibi iwe burudani? Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kulishughulikia suala hili haraka iwezekanavyo. Pia tunomba BET kutafakari upya zuio hilo.

Hassan Bumbuli
Katibu Mkuu CAJAtz


ankal danford mpumilwa atangaza nia ya uvuvuzela

Danford Mpumilwa

Dear Bro Michuzi
Nimefikishiwa maulizo mengi k
utoka kwa wadau na wapiganaji wengi wakisema
wamesikia kuwa nimetangaza nia ya kugombea ubunge mwaka huu kupitia CCM
kwenye jimbo la Njombe Magharibi. Napenda kuwajulisha kuwa ni kweli ingawa
ukiacha gazeti moja na habari chache tu ndio vilivyoandika habari hizo. Kwa
sababu mtandao wako unafuatiliwa na wapiganaji wengi ambao wameniulizia juu
ya habari hizo nimeona kuwa niwajulishe rasmi kuwa kweli nagombea kwenye
kinyang'anyiro hicho. Kwa wale ambao hawanijui kwa undani wanaweza kupata
maelezo yote kwenye libeneke langu:


vodacom foundation yamwaga vyandarua singida

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (wa pili kushoto)akifurahia jambo na wauguzi wa hospitali ya Wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi Mkoani singida baaada ya kukabidhi msaada wa Vyandarua 1,300 katika mkoa huo vyenye thamani ya shilingi Milion 10 katika hospitali hiyo.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akimkabidhi moja ya kati ya Vyandarua 1,300 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba iliyopo Kiomboi DK.Anthony Mburu (katikati)Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Peter Mwagiro akishuhudia upokeaji huo wa Msaada ambao watagawiwa wagonjwa wote waliopo eneo hilo. Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi moja kati ya 1,300 Esta Aron akiwa na mwanae mwenye umri wa miezi 6 Peter William ambaye ni mmoja wa Wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya akina mama katika hospitali ya Wilaya ya Iramba ilioko Kiomboi Singida mfuko huo ulitoa msaada wa jumla ya Vyandarua 1,300 katika mkoa huo.
Baadhi ya Wauguzi katika hospitali ya Wilaya ya Iramba wakibeba magunia yaliyosheheni Vyandarua 1,300 baada ya kukabidhiwa msaada huo na Vodacom Foundation kwa ajili ya kujikinga na malaria kwa wagonjwa wanaopata matibabu katika Hopitali hiyo iliyopo Kiomboi Mkoani Singida .





Mafia kunani tena???

Kisiwa cha Mafia

Sisi kama wenyeji wa kisiwa hichi na wenye nia uchungu na kisiwa hiki
tumesikitishwa na hatua ya baadhi ya wenye mahoteli ya kitalii kwenye
kisiwa hichi pamoja na uongozi mzima wa wilaya (DC) na halmashauri kutoa
kibali kwa kundi la burudani toka Ugiriki kuja kufanya vitendo vya ushoga
kwa kutumia mgongo wa Tamasha la muziki.

Pia tumesikitishwa uongozi hapa Mafia kukubali kutoa kibali kwa hawa vijana
3,000(revelers) bila kupata ridhaa ya wenyeji wa Kisiwa hichi (Public
consultation). Tungependa ifahamike kuwa sisi kama wenyeji wa Kisiwa hichi
tunakaribisha wageni lakini ni LAZIMA wazingatie na waheshimu mila na
taratibu zetu na moja kati ya hizo mila zetu USHOGA haumo!
Kitendo cha kutaka kuleta vijana hawa mashoga hapa kisiwani kufanya
vitendo vyao kwa siku 14 mfululizo hakikubaliki kimaadili na tunawaunga
mkono wana Mafia na hasa wazazi ambao hawako tayari kuona watoto wao
wakishuhudia vitendo vya kishoga, utumiaji wa madawa ya kulevya ambavyo
ni si mila na desturi yetu kama waTanzania.
Kama mjuavyo Mafia ni kisiwa cha amani na ndio maana kimekuwa kinaongoza kwa utalii wa scuba diving duniani na tunaendelea kuwakaribisha watalii ambao wanakuja na kutuheshimu na wanaoelewa umuhimu wa kutunza mazingira ya kisiwa hichi.
Kisiwa hichi hakina uwezo wala fedha za kuweza kutoa huduma za afya kwa
watu wake iweje leo tamasha hili la mashoga 3,000 ambao itabidi wajisaidie
kwenye mashamba ya watu kwani hakuna public toilets za kuweza kuhimili
kishindo hichi.
Hivi kwa mfano mazingira yashachafuliwa ni sisi watu wa Kisiwa hiki ndio
tutasafisha au halmashauri? je wanazo pesa za kusafisha na kuokota toilet
papers zitakazo achwa na hawa Mashoga kwenye mashamba yetu?
Hospitali zetu hapa zinatia aibu na mbaya zaidi huduma za afya kwa mama
zetu na dada zetu wanapojifungua zipo katika hali duni, hivi kweli
mheshimiwa DC na timu yake wameona kwa sasa tunachohitaji ni hili Tamasha?
Kwa kawaida ya Mashoga hawatokaa sehemu moja hapa kisiwani na watataka
kwenda kufanya uchafu wao kwenye fukwe zetu hapa kisiwani, hivi Uongozi wa
Kisiwa hichi utatoa polisi wangapi kwa kila kundi la hawa mashoga kufanya
mambo yao? kwani sidhani kama wananchi watakaa na kushangilia vitendo
hivi vikifanyika hadharani.
Tungependa kuufahamisha umma kuwa hawa waandaji tamasha hili lilipofanyika kwenye kisiwa cha Skyros, watu walililalamika sana pamoja na kuwa Wagiriki wana mitizamo ya ku liberali kwenye mambo haya lakini hali ilikuwa mbya kiasi cha Polisi kuvamia na kusitisha lile Tamasha kwani lilikuwa linaelekea kuvujinka kwa amani.
Katika kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi je ni kweli
Serikali inataka kuona uvunjikaji wa amani katika kipindi hichi
tunachoelekea kwenye Uchaguzi kwa kukubali hili tamasha la Mashoga?
Je jeshi la polisi linazo resources za kulinda mashoga 3,000 usiku na
mchana kwa siku saba mfulululizo?
Kwa nini mratibu wa hili Tamasha hili la Mashoga hataki kukutana na viongozi wa Kisiwa hichi na kuwaeleza kwa
kinagaubaga nia yake?
Maandaji wa Tamasha hili wamesema wamepata ushirikiano wa karibu na
kampuni ya uwindani na utalii inayojiita KARIBUSANA ambayo iko chini ya
Costa Coucoulis,Angela Damas,Chyrista Batou na Mark Evans ambao wanajiita
wahifadhi wa mazingira kwenye tovuti yao lakini wakati huo huo wako tayari
kuhakikisha kuwa mazingira ya kisiwa chetu yanachafuliwa na hawa wageni.
Je Mbunge na DC wa Kisiwa hichi watakuwa wanatekeleza ilani ya chama gani
kulikubali hili Tamasha la Mashoga?
Je wilaya iliyo masikini kuliko zote Tanzania inahitaji Tamasha la muziki
au tunahitaji miradi ya Maendeleo?
Je BASATA na Wizara ya Utalii wameamua


cheka unenepe: huduma ya kwanza

video


Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Rombo wazuru SUZA

Ujumbe wa Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ukiwa ziarani Zanzibar, hususan katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo wanaonekana katika mkutano wao na uongozi wa Chuo jana
Mkutano wa uongozi wa SUZA na waalimu wakuu wa sekondari za Rombo
mkutano ukiendelea
picha ya kumbukumbu baada ya mkutano. Picha na Hassan Hassan Simba wa SUZA





hongera TBC kwa kazi nzuri

Mtangazaji mahiri wa TBC Elisha Eliya
Ankal salamaleko,
Siku nyingi niko kimya, ila leo naingia tena hapa kutoa pongezi za dhati kwa TV yetu ya taifa ya TBC kwa kazi nzuri waifanyayo tokea kumekucha hadi kumekuchwa.
Hakika TBC imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwa njia ya TV, kiasi si ajabu kukuta ikiangaliwa kila kona hata kabla ya kombe la dunia. Pia nampenda sana kijana huyu Elisha Eliya anayejilawa kila asubuhi nakina Marin Hassan na wengine katika kipindi cha Jambo.
Ombi Elisha naomba abadilishiwe hiyo suti...
maana kila siku namwonaga nayo hiyo hiyo tu.
Kwani hana ingine ama ni jezi ya kazi?
Mdau wa Mafia


eneo la EPZ lavutia wengi

Mdau Constantine Thobias na mai waifu wake Nelly Sembuli wakipozi baada ya kumeremeta katika 'Mlima Kilimanjaro' uliopo katika eneo la Export Processing Zones (EPZ) lililopo Ubungo External jijini Dar wikiendi ilopita. Bw. Harusi anafanya kazi Parapanda na Bi. Harusi yuko katika kampuni ya Uzibora Maharusi wakipozi na familia
Maharusi wakiteremka wakati familia ikiwa kileleni 'Kibo'

Mandhari ya mfano wa mlima kilimanjaro uliojengwa ndani ya eneo la EPZ
Panapendeza
Bustani mwanana ya EPZ ambayo pamoja na mfano wa mlima kilimanjaro pamekuwa kivutio kikubwa kwa wadau ambao kwa sasa wanaruhusiwa kwenda kupiga picha za sherehe mbalimbali kwa mchango mdogo wa shilingi 10,000/- jambo ambalo limesifiwa na wengi kwani angalau kuna mbadala wa sehemu ya kupigia picha ukiondoa kwenye fukwe za bahari









libeneke la usajili wa namba za simu za mkononi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZA MKONONI
1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa namba
zote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1 2009 hadi
Desemba 31, 2009; na baadaye muda huo kuongezwa hadi tarehe
30 Juni 2010 ikitamkwa wazi kuwa muda huo wa ujasili
hautaongezwa tena. Sababu za kuanzisha utaratibu wa kusajili
namba za simu zimeelezwa mara kadhaa zikiwemo:
(i) Kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma za
mawasiliano
(ii) Kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiapo
huduma mbalimbali kama M – Pesa, Z-pesa, ZAP na huduma
nyingine za malipo ya Ankara kama za Umeme, Maji,
Televisheni n.k.
(iii) Kuimarisha usalama wa nchi.
(iv) Kuyawezesha makampuni ya simu kuwafahamu wateja wao
vizuri zaidi ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma
kwao.
2. Wakati tunakaribia tarehe 30 Juni 2010, utaratibu umepangwa
kupitia Makampuni ya simu kuwa kuanzia tarehe 1 Juni 2010
kuhakikisha laini yoyote itakayonunuliwa itatumika kwa kupiga au
kupokea simu na kutuma au kupokea ujumbe ikiwa imesajiliwa
tu na si vinginevyo.
2
3. Baada ya saa sita usiku tarehe 30 Juni yaani saa 00.00 kuanzia
tarehe 1 Julai, 2010 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa
itafungiwa kupiga ,kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi
(SMS) kwa siku 90 hadi tarehe 30 Septemba 2010. Katika kipindi
hiki cha siku 90 endapo mtumiaji ataisajili namba yake
itafunguliwa. Kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo
tarehe 30 Septemba zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandao
kabisa.
4. Mamlaka ya Mawasiliano imekubaliana na Makampuni ya simu
kufanya uhakiki wa usajili wa laini za simu za wateja kwa kutumia
namba 106 kupitia simu za mkononi. Kwa wateja wa mitandao
iliyoko katika mifumo ya GSM, kama Zain, Vodacom, MIC (Tigo) na
Zantel, wateja wanatakiwa kuingiza *106# na kwa wateja wa
mitandao inayotumia mfumo wa CDMA kama BOL, TTCL mobile na
SASATEL wateja watatakiwa kupiga namba 106 na watapokea
taarifa za usajili.
5. Hivi karibuni mswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na
posta ulipitishwa na Bunge kuwa sheria. Sheria hiyo inafanya usajili
wa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu wa
sheria hio kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai. Adhabu
ni pamoja na faini au kifungo au vyote pamoja.
6. Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuyashukuru makampuni ya simu
na watumiaji kwa ushirikiano ambao wameonesha mpaka sasa kwa
ajili ya kufanikisha zoezi hili.Tunawasihi wote waendelee kusajili
laini mpya kabla ya matumizi baada ya tarehe 30 juni 2010 na
kuendelea kuhakiki laini zote zilizosajiliwa ili kukamilisha usajili
kama ilivyokusudiwa.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)


Mkulo katika mkutano wa ECOSOC New york leo

WAZIRI WA FEDHA AKICHANGIA MJADALA KISERA KUHUSU WAJIBIKAJI NA UWAZI KATIKA USHIRIKIANO WA MAENDELEO; NAMNA YA KUJENGA USHIRIKIANO ULIO SAWA MIONGONI MWA WADAU MBALIMBALI. MJADALA HUO UMEFANYIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK.
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, DK. SERVACIUS LIKWELILE AKIFUATILIA MAJADILIANO
WAZIRI MKULO AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAJUMBE MBALIMBALI WA KIKAO CHA KILELE CHA KAMATI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII YA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA( ECOSOC

UWEZESHWAJI WA WABUNGE

NA MWANDISHI MAALUM
New York, 30/6/2010
Imeeleza kuwa, licha ya wabunge na taasisi za kijamii, kuwa na fursa na nafasi ya kushiriki katika ufuatilia wa upangaji na utekelezaji wa bajeti ya taifa, sera zinazohusiana na masuala ya fedha na misaada ya kimaendeleo kutoka kwa wahisani, imebainika uwezo wa vyombo hivyo kutimiza wajibu huo kikamilifu bado ni mdogo.

Waziri wa fedha na Uchumi, Mh. Mstafa Mkulo ameyasema hayo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York. Wakati wa majadiliano ya kisera kuhusu uwajibikaji na uwazi katika ushirikiano wa kimaendeleo; namna gani serikali zinaweza kujenga ushiriano ulio sawa kati yake na taasisi nyingine. Mjadala huo umefanyika ukiwa ni sehemu ya mkutano wa kilele wa Kamati ya Baraza Juu la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii. (ECOSOC).

Mh. Mkulo anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, anasema "Ushiriki wenye nguvu wa wabunge na taasisi za kijamii katika masuala yahusuyo fedha ni jambo la muhimu sana kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi, lakini ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uwajibikaji na uwazi. Lakini uzoefu unaonyesha kuna udhaifu kwa upande wa wabunge na taasisi za kijamii".

Akabainisha kuwa udhaifu huo ndio unaolazimisha kuwapo kwa hitajio la kuzijengea uwezo zaidi taasisi hizo ili kuhakikisha kwamba ushiriki wao katika mijadala ya kitaifa na kimataifa kuhusu ubora wa misaada ya maendeleo unakuwa na tija.

Akisisitiza haja hiyo ya taaisi hizo kujengewa uwezo zaidi, Mkulo anasema, sera zinazohusu fedha na hasa zile zinazohusu misaada ya wafadhili ni ngumu na zenye vipengere vingi, ambavyo anasema vinahitaji mshiriki awe uwezo na upeo wa kutosha wa siyo tu wa kuvijadili bali pia kivielewa na kuwa na mbinu za kufuatilia.

Wanajopo wengine katika majadiliano huo walikuwa ni Bi. Irene Freudenshuss-Reichal kutoka serikali ya Austria, Michael Anderson kutoka serikali ya Uingereza na Bi. Ingrid Srinath kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya CIVICUS.

Mh. Mkulo ambaye aliainisha hatua mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali lipokuja suala la uwazi na uwajibikaji, amewaeleza washiriki wa mjadala huo, kwamba kwa kiasi kikubwa Tanzania imefanikiwa kuwa na uhusiano endelevu na wenye kuridhisha kati yake na wadau wa maendeleo.

“ Kwa kujiwekea sera, mipango na mikakati mbalimbali ambayo tumeshirikiana na wadau wetu wa maendeleo, wabunge na taasisi za kijamii, Tanzania imeweza kuongeza kiwango cha umiliki wa ajenda zake za maendeleo, kupanua wigo wa majadiliano kati yake na wafadhili , na wadau wengine.
"Na kwamba kiwango cha uwazi na uwajibikiaji kimeongezea katika uandaaji na utekelezaji wa bajeti ya taifa na sera zinazohusiana na masuala ya fedha na misaada kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa” anasema Mh. Mkulo.
Hata hivyo anaeleza kuwa , dhana hiyo ya uwazi na wajibikaji bado inaelemea zaidi upande mmoja yaani upande ule unaopokea misaada ( serikali) kuliko upande wa pili yaani wafadhili.

“Suala hili la uwajibikaji kwa kweli kwa wafadhili bado halijawa na uzito wa kutosha. Mara kwa mara sisi nchi tunao pokea misaada ndio tunaolazimishwa kuwa wawazi na kuwajibika. Hii si haki kwa sababu inakwenda na kinyume na tamko la Paris la mwaka 2008 linalo sisitiza uwajibikaji wa pamoja”, ameongeza.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Uchumi anasema kuwa ujenzi wa ushirikiano endelevu na wenye tija kati ya serikali na wadau wengine, ni jambo linalohitaji kuaminiana, kujituma, uwazi katika majadiliano na kwamba litachukua muda mrefu.

Aidha anasema ili hilo liweze kutekelezeka, uwajibikaji wa kisiasa kati ya mfadhili na mfadhiliwa ni jambo la muhimu sana.Kwa sababu ndiko kutakako pelekea uwajibikaji wa pamoja kwa lengo la kuimarisha misingi ya uwajibikaji katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Wakati wa majadala huo, baadhi ya wazungumzaji pamoja na kukubaliana na hoja ya uwezeshwaji zaidi wa wabunge na taasisi za kijamii hasa katika mataifa yanayoendelea, walitaka pia uwezeshaji huo ushuke mpaka kwenye vyombo vya habari, kwa kile walichosema kwamba nao ni wadau muhimu katika kufuatilia utendaji wa serikali.

Wengine waliainisha kwamba, linapokuja suala ya uwazi na uwajibikaji, basi lisiishie kwa serikali na wadau wa maendeleo, bali uwazi na uwajibikiaji huo uwepo pia kwa taasisi nyingine zikiwamo Bunge na vyama visivyo vya kiserikali.


WANAMUZIKI WA CHUO CHA DCMA KUIWAKILISHA TANZANIA NCHINI CHINA

Wasanii wa DCMA Zanzibar wakikabidhiwa
bendera na Mh. Mahmoud Thabit Kombo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo (mwenye baraghashia) kabla ya kuanza safari ya China

Wasanii saba kutoka Chuo cha Muziki cha DCMA Zanzibar wanategemea kuondoka nchini wiki ijayo kwa ajili ta kuiwakilisha Tanzania nchini China ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya kimataifa ya World Expo. Kundi hilo ambalo lipo kambini katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) litashirikiana na wasanii wa taasisi hiyo kwa madhumuni ya kuunda onyesho la pamoja lenye vionjo vitakavyo wakilisha sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika sherehe za kuwaaga rasmi wasanii hao, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alilitakia kundi hilo mafanikio kundi katika kuiwakilisha Tanzania.

Maonyesho hayo ya kimataifa yanayofanyika nchini China kwa mara ya kwanza yamekuwa yakifanyika mjini Shanghai kunzia mwezi wa Machi na yataendelea hadi mwezi wa Septemba 2010. Taasisi za DCMA na TaSuBa wamepata fursa ya kushiriki katika maonyesho hayo kama sehemu ya uwakilishi wa kitamaduni wa nchi shiriki kupitia mwaliko wa Bodi ya Taifa ya Biashara za Nje.


Taasisi hizo mbili ni washika wa jadi katika miradi mbali mbali ya maendeleo ya mafunzo na miradi ya muziki hapa nchini. Wakiwa katika Maonyesho hayo, kundi hilo la pamoja linatazamiwa kufanya onyesho moja katika banda la maonyesho la pamoja la nchi za Afrika baina.

DCMA ni taasisi ya kimisaada na isiyo ya kiserikali (NGO) yenye kuendesha mradi mkubwa zaidi wa kusambaza elimu ya muziki nchini Tanzania kutoka makao makuu yake yalioyopo Mji Mkongwe, Zanzibar.

Kheri A. Yussuf
Development, Marketing & PR Manager
Dhow Countries Music Academy, Zanzibar
Mobile:077.362 0202

Email:press@zanzibarmusic.org


maandalizi ya mr & Miss East Afrika UK 2010

Utawala wa Urban Pulse unapenda kuwaletea exclussive behind the scenne kwa wadau wote wa libenekene kuhusu matayarisho na maandalizi ya Miss & Mr East Africa Uk 2010 yaliyofanyika katika kitongoji cha Edmonton, Ukerewe jumamosi 26.6.10

Fainali ya kuwania Taji la U Miss na U Mr East Africa UK litafanyika Jumamosi Julai 3, 2010 katika ukumbi wa Central Hall,Westminister, London


exclusive: wanajeshi wawili wapoteza maisha katika ajali ya ndege

sehemu ya ndege iliyopata ajali baada ya kutua barabarani kwa dharura na kugonga basi la watalii ambalo linaonekana juu kushoto likiwa limeanguka
askari wa jeshi la ulinzi na polisi wakiwa eneo la tukio

msururu wa magari yaliyokuwa barabarani

Askari wawili ambao ni marubani wa Jeshi la Wananchi Tanzania wa Kambi ya Ngerengere ya Morogoro, wamekufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kutua barabarani kwa dharura na kugonga gari la watalii na kupinduka jana katika eneo lijulikanalo kama Zimbabwe katika kijiji cha Manga wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.

Katika basi la watalii inasemekana kulikuwa na watu 24 ambao 19 kati yao ni raia kutoka Uholanzi, wanne kutoka Kenya na mmoja Mtanzania. Wote walinusurika kufa.

Inasemekana kuwa marubani hao walikuwa katika mazoezi ya kawaida katika anga ya eneo hilo, na kwamba wakati ikiwa angani ndege ilipata hitilafu ndipo rubani akaamua atue barabarani ili kuokoa maisha yao, kabla gari hiyo ikiwa kwenye mwendo mkali iliigonga.

Ndege hiyo ndogo ya JWTZ yenye namba F59119 ilikuwa inatumika katika mafunzo ya kijeshi. Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga, Afande Jafari Mohammedi, aliwataja waliokufa kuwa ni rubani wa ndege hiyo Meja Kathbet Leguna (41) na mwanafunzi wake Luteni Andrew Yohana Kijangwa (31).

Taarifa zinasema Meja Leguna alikuwa ni mwalimu wa mafunzo ya ndege za kivita katika kikosi hicho cha Ngerengere na alikuwa anamfundisha urubani Luteni Kijanga.



Africa evening


super nyamwela arejea kundini twanga pepeta


NIC ndani ya maonyesho ya saba saba

Meneja uhusiano na mawasiliano wa NIC,Mwanaid Shemweta (kulia) akijadiliana jambo na maafisa waandamizi wa bima ya maisha,Immaculate Maro (kati) na Ndina Nsaji (kushoto) katika banda lao la Bima lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere,kilwa road jijini Dar
Meneja wa NIC anaeshughulikia maswala yote ya Bima kasoro ya Magari,Ntimba Bunny akiwaeleza wateja waliofika katika banda lao la Bima lilipo ndani ya viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere,kilwa road jijini Dar

wadau wa NIC wakiwa katika picha ya pamoja, toka kushoto ni Henry Machoke (Meneja Masoko),Mwanaid Shemweta (Meneja Uhusiano na Mawasiliano),Adelaida Muganyizi (Afisa Masoko),Mary Kyomo (Meneja Mipango na Uwekezaji) na Meneja wa NIC anaeshughulikia maswala yote ya Bima kasoro ya Magari,Ntimba Bunny wakiwa ndani ya banda lao la Bima lilipo ndani ya viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere,kilwa road jijini Dar


MSIBA MZITO ROSE GARDEN

Marehemu Bernard Mbwambo (pili kulia) akiwa na viongozi wenzie wa chama cha mashabiki wa Manchester United nchini siku ya uzinduzi wake ambapo yeye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.BOFYA HAPA

WAPENZI NA WANACHAMA WA KLABU YA MICHEZO YA ROSE GARDEN YA JIJINI DAR, PAMOJA NA CHAMA CHA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED NCHINI, WAKO KATIKA SIMANZI KUBWA KWA KUONDOKEWA NA MWENYEKITI WAO, BERNARD MBWAMBO, ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA GARI MJINI TANGA BAADA YA GARI ALILOKUWA AMEPANDA KUGONGA KWA NYUMA GARI ILIYOKUWA IMESIMAMA.

MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU SEHEMU ZA KIJITONYAMA KWA ALI MAUA JIJINI DAR, NA KWA MUJIBU WA KAMATI YA MAZISHI MAREHEMU MBWAMBO ATAPUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE SAA KUMI JIONI KESHO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KUTOA MKONO WA POLE KWA WANACHAMA WA KLABU YA ROSE GARDEN NA WANA MANCHESTER UNITED POPOTE WALIPO. MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI - AMINA



Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker