In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for August 2010

watoto wawili wapoteza maisha katika ajali ya moto wilayani ulanga

Bi Sabina Nambalamoka (kulia) akimuuguma mama yake,Bi Kilala Magala alielazwa katika hospitali ya wilaya ya Ulanga baada ya kujeruhiwa kwenye ajari ya moto.


Na Sekela Mwasubila - Ulanga

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia na bibi yao kuungua vibaya kutokana na moto ulioteketeza nyumba yao majira ya saa nne usiku katika kijiji cha Isyaga wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Akiongea na mwandishi Bi Sabina Nambamoka (35) ambaye ni mtoto wa majeruhi amewataja waliofariki kuwa ni John Makamo (9) na Edwini Kologero (5) na Bi Kilala Mgala (60) ambaye ni mama yake mzazi.

Amesema yeye anaishi kijiji cha jirani na eneo la tukio hivyo alikuja kuitwa usiku kuwa na nyumba ya mama yake inateketea kwa moto na alifika eneo la tukio alikuta moto umetanda na juhudi za kumuokoa zikiendelea, baba yake alikuwa amekwisha okolewa na alijeruhiwa kichwani na mkononi.

Aliongeza kuwa baada ya mama yake kuokolewa moto ulizidi na kupelekea watoto kupoteza maisha yao kwa kuungua vibaya na kumfikisha mama yake hospitali ya Wilaya mnamo saa tisa za usiku.

Akiongea Dkt. Malekano toka hospitali ya Wilaya ambaye ndiye anayemhudumia mgonjwa aliyejuruhiwa kwa moto huo amesema kuwa baada ya kupata matibabu hali ya mgonjwa inaendelea vizuri japokuwa ameungua asilimia sabini na tano ya mwili wake.

Mkuu wa upelelezi wa Wilaya L.N Buya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha moto ni moto uliokuwa umeachwa nje kutokana na upepo ukashika nyasi zilizoezekewa nyumba na kupelekea kuungua kwa nyumba hiyo.


VODACOM MISS TANZANIA WAPEWA SOMO NA WADHAMINI WAO WAKUU

Afisa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania ,Elihuruma Ngowi akiwagawia Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 Line za simu, baada ya kumaliza kutoa semina kwa warembo hao iliyohusiana na huduma zinazotolewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania .iliyofanyika katika Hoteli ya Giraffe View .Meneja mauzo wa M Pesa wa Vodacom Tanzania ,Jerome Mnishi akifafanua jinsi huduma ya M Pesa inavyofanya kazi kwa Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010.iliyofanyika katika kambi yao iliyopo Giraffe Hotel.
Mmoja wa Warembo wanaowania Taji la Vodacom Miss Tanzania 2010, Irene Hezron (22) akiuliza swali kuhusiana na huduma ya M-PESA katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya Geraffe walikoweka kambi warembo hao.Jumla ya warembo 30 walipewa mafunzo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Vodacom Tanzania.


Rais Karume afungua mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume akifungua mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Augustino Ramadhani. Mkutano huo unaendelea katika Hotel ya Golden Tulip na unahudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Washiriki wa mkutano wa siku tatu wa Kikanda wa Kimataifa wa kukabiliana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa unaendelea nchini Tanzania wakimsililiza Rais Amani Abeid Karume wakati wa sherehe fupi za ufunguzi uliofanyika katika Hotel ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na Majaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.

(Picha na Tiganya Vincent-Globu ya Jamii)


hoja ya mdau kuhusu libeneke la globu ya jamii katika kipindi hiki cha kampeni

HOJA BINAFSI KUHUSU MALALAMIKO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA GLOBU YA JAMII KUA GLOBU YA JAMII INAPENDELEA ZAIDI CHAMA TAWALA. JE NI KWELI?

NANI KASEMA ANKALI ANAFAGILIA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI TUU ?NA NANI KASEMA ANKALI KANUNULIWA NA CHAMA HICHO?SASA MBONA ANATURUSHIA NA VYAMA VINGINE?

JAMANI TUSIMLAUMU SANA ANKALI MIMI KAMA MDAU MKUBWA SANA WA BLOG NIMESIKITISHWA SANA NA KAULI ZA WATU KUSEMA ANKALI HATENDEI HAKI VYAMA VINGINE SI KWELI NI KWAMBA HAO WENGINE HAWATUMI HABARI ZAO SASA ANKALI AOTEEE JAMANIIIII TUJIREKEBISHE MIMI NALETA HOJA APA KWENU........

MAANA INAKERA WEWE ANGALIA FACEBOOK NA MITANDAO MINGINE ATA APO KIJIWENI KWAKO MNASHADADIA TUU ANKALI KUA ANAPENDELEA CHAMA CHA MAPINDUZI. TUFIKE MAHALI TUBADILIKE WATANZANIA. NAOMBA KUTOA HOJA

MIMI MDAU WA GLOBU YA JAMII.


TEA yatoa msaada kwa wanafunzi wenye ulemavu UDSM.

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (TAALUMA) PROFESA MAKENYA MABOKO (KULIA) AKIMKABIIDHI MKUU WA SHULE KUU YA ELIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM PROFESA EUSTELLA BHARALUSESA MASHINE MAALUM YA KUANDIKIA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA KUONA, VIFAA HIVYO VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 153.2VILITOLEWA NA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA.
MKURUGEZI MKUU WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA BIBI ROSEMARY LULABUKA (KULIA) AKIMKABIDHI MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (TAALUMA) PROFESA MAKENYA MABOKO (KULIA) MASHINE MAALUM YA KUANDIKIA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA KUONA, TEA IMETOA VIFAA MBALIMBALI KWA SHULE KUU YA ELIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 153.2
MKURUGEZI MKUU WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA BIBI ROSEMARY LULABUKA (KULIA) AKIMKABIDHI MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (TAALUMA) PROFESA MAKENYA MABOKO (KULIA) BAISKELI MAALUM KWA AJILI YA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA VIUNGO. TEA IMETOA VIFAA MBALIMBALI KWA SHULE KUU YA ELIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 153.2


TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,John Tendwa.


Na Mary Kweka –Maelezo

Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM) baada ya siku tano.

Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.

‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya mlalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.

Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Msajili huyo wa Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya msajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi,Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.


yale yalee....

Ankal,

Pole kwa kazi.
Hivi karibuni nilisafiri kutoka Bukoba kuja Mwanza kwa MV Victoria. Kilichonishangaza ni wahusika melini kutozingatia umuhimu wa kuacha wazi eneo kunakohifadhiwa "life jackets" kama ilani inavyoelekeza. Ikitokea ajali (Mungu apishie mbali) mpaka mizigo ihamishwe ndo mlango wa life jackets ufunguliwe!
Nawasilisha.

Makame


uzinduzi wa kampeni za mnyika ubungo

Mgomea Urais kwa tiketi ya CHADEMA,Dr. Willblod Slaa akimpa baraka zote na kumnadi wanachama na wapenzi wa chama hicho Mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika katika kampeni zake za Jimbo la Ubungo na kumhakikishia kuwa naye bega kwa bega katika kuhakikisha wanashinda.
Mpendazoe naye alikuwawepo kumnadi Mnyika kwa wananchi wa Ubungo katika ufunguzi wa kampeni za chama hicho Kimara Suca.
Wasanii wa muziki wa Bongo Freva wakiongonzwa na mgombea Ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II (SUGU) wakilishambulia jukwaa la ufunguzi wa kampeni za Mnyika Kimara Suca


mgombea mwenza wa urais CUF,akiwa mkoani kagera

mgombea mweza wa Profesa Ibrahim Lipumba kupitia tiketi ya CUF, Haji Juma Duni (katikati) akiwa na baadhi ya vingozi wa chama hicho katika mkoa wa Kagera mara baada ya kuongea na waandidhi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho mkoani humo. Kushoto kabisa ni mgombea wa nafasi ya ubunge wa chama hicho wa jimbo la Bukoba Mjini, Christian Kasimbazi na wa mwisho kulia ni katibu wa chama hicho wa manispaa ya Bukoba Swahib Magayane.

BOFYA HAPA

upate habari kamili ya


ajali Junction ya Oysterbay karibu na ofisi za TTCL leo

askari wa usalama barabatani akiandika maelezo ya ajali iliyotokea hivi punde maeneo ya Oysterbay.
gari zilizopata ajali zikiwa bado zipo eneo la tukio huku zingine zikipita kwa shida kutokana na ajali hiyo.
sehemu ya vibao vinavyolalamikiwa kuwa ndivyo vinavyosababisha ajali kutokana na kuwekwa bila mpangilio.

Uncle Michuzi,

Hebu naomba uturushie hii kwa wadau wanaohusika hasa hasa watu manispaa hapa junction ya karibu na Oysterbay Primary school , hivi vibao vilivyowekwa hapa bila utaratibu mzuri vimekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara kwa kusababisha ajali mara kwa mara karibu kila wiki tunashuhudia ajali.

Hivi ninavyoandika hii email ni punde ajali imetokea kama inavyoonekana kwenye hizo picha hapo.

Mfano hiki kibao cha vodacom uwekaji wake si mbaya sana kwa kuwa kipo juu lakini hivi vingine huwezi kuona gari linalokuja mpaka uingie kidogo barabarani kitu ambacho ni hatari. Tunaomba mamlaka husika ishughulikie uwekaji wa hivi vibao au kuweka taa au matuta pande zote nne za barabara kuwezesha kupunguza ajali za mara kwa mara kama walivyofanya junction ya migombani karibu na nyumbani kwa mheshimiwa.

Tunaomba Uncle utusaidie kuturushia hii kwa wadau husika.

Angalia hivyo vibao vilivyojaa bila mpangilio

Ndimi mdau Oysterbay


number ten latinga mtaani kwa mara nyingine


SAFARI HII KUNA EXCLUSIVE INTERVIEWS TANO HAIJAWAHI TOKEA,HAYA NDO MAPINDUZI HALISI

NUMBER 10 USO KWA USO NA:

1. McDONALD MARIGA-KIUNGO WA INTER MILAN NA KENYA
2. PETR CECH- GOLIKIPA WA CHELSEA
3. RUUD GULLIT- NYOTA WA ZAMANI WA UHOLANZI
4. TONU PULIS-KOCHA WA STOKE CITY
5. JABIR AZIZI -KIUNGO MPYA WA AZAM FC


Ngeleja atembelea machimbo ya nyakagwe,geita

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akizungumza na Wachimbaji wadogo katika machimbo yasiyo rasmi ya Nyakagwe wilayani Geita muda mfupi kabla ya kutoa amri ya kufungwa kwa machimbo hayo baada ya kutokea uvumi wa kufukiwa kwa wachimbaji zaidi ya 70 wiki iliyopita.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akipata maelezo ya uvumi wa kufukiwa kwa wachimbaji wadogo zaidi ya 70 katika machimbo ya dhahabu ya Nyakagwe kutoka wa Ofisa madini mkazi wa wilaya ya Geira Donald Mremi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Nonosius Komba (Kulia) akiteta jambo
na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Geita SSP Kasabango.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa mwanza Nonosius Komba akizungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Nyakagwe muda mfupi kabla ya zoezi la ufukuaji wa wachimbaji wadogo 70 waliodaiwa kufukiwa katika machimbao hayo juzi
Greda la kampuni ya GGM ambao ni wamiliki wa mgodi wa Geita wakifanya zoezi la ufukuaji katika machimbo yasiyo rasmi ya Nyakagwe baada ya kusikika kwa madai ya kufukiwa kwa zaidi ya wachimbaji wadogo 70,hata hivyo hakuna mwili hata mmoja uliopatikana


Precision Air wazindua ndege yao mpya leo

Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh.Mohammed Babu akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa ndege mpya ya Precision Air aina ya ART 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 katika uwanja wa J.K. Nyerere International Air Port ambayo itafanya safari zake kati ya Dar - Bukoba - Dar, ndege hiyo ambayo iliruka leo kutoka Dar kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake hizo za Dar - Bukoba -Dar mapema mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CitiBank,Jamal Hussein , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji wa Precision Air,Allan Sharra na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk


Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo,Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu CitiBank na mwisho kushoto ni Lucy Malu Meneja Mkazi Kenya Airways.

ndege mpya ya Precision Air ATR 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abilia 48 itakayofanya safari zake kati ya Dar na Bukoba ikitua katika uwanja wa J.K.Nyerere.
baadhi wa Marubani wa Precisiano Air wakiwa katika uzinduzi huo leo.

(Picha na Full Shangwe Blog)


Urban Pulse waja na video nyingine



Salam Kaka

Mwezi Juni mwaka huu tuzo maarufu ya kimataifa iitwayo Ashden Awards iilitolewa kwa wahusika kadhaa duniani zikiwepo nchi za Afrika Mashariki.

Tuzo hiyo hutolewa na shirika maalum lililoundwa na duka maarufu la matajiri wa Uingereza yaani Sainsbury Kutoka katika Ashden Trust Charity ambapo mlezi wake akiwa ni Prince Charles. Lengo lake ni kusaidia kurekebisha na kuboresha mazingira duniani .

Tuzo ya mwaka huu ilitolewa kwa watafiti na wabunifu waliotengeneza zana za kutengeneza umeme kutokana na nguvu asilia za jua yaaani Solar Energy.

Ingawa wabunifu walitoka mataifa mbalimbali ya Marekani, Asia na Afrika washindi pia walihusisha Kenya, Uganda na Tanzania.

Umeme Jua, Bio gas( Gas Itokayo kwenye kinyesi cha ng'ombe) ni zana ambayo itawasaidia watu maskini hasa wanaotoka nchi kama yetu Bongo vijijini.

Baada Ya Mafanikio makubwa la movie ya £ovely Gamble Urban Pulse wakishirikiana na Msanii/ Mhariri Freddy Macha Wamepewa mzigo mwingine wa kutengeneza documentary ambayo itakuwa hewani tarehe 2 sept 2010 na kurushwa katika tv za hapa ukerewe na mabara mengine ya ulaya.

Hivyo basi utawala wa Urban Pulse Unawaletea trailer ya documentary hiyo na baada ya uzinduzi tutawapatia kipindi chote

Asanteni sana

Urban Pulse Creative


ONE LOVE LABOR DAY KICKOFF FRI SEPT 3


Designers visiting the Textile Sector Development Unit’s

Designers being shown the Modern industral Patern cutter BY PRODUCTION MANAGER PATRRICK LUMUMBA.
Designers Kemi Kalikawe , Manju Msitta and Ailinda Sawe seeing how a machine operates.
Designer listening to Patrick Lumumba of the Production Facility they Visited on 30 September 2010.
Designers attending to how the pattern drafting works


CRDB yachangia Shilingi Milioni 15 kwa shule ya Wasichana ya Visitation Bethel

Mgeni Rasmi,Mkurugenzi wa Benki ya CRDB,Dkt. Charles Kimei akihutubia katika sherehe za mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Visitation

Mgeni Rasmi, Mkugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei akizindua moja ya nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Visitation Bethel katika sherehe za mahafali ya kidato cha nne hivi karibuni.Dkt.Kimei akikata utepe kuzindua bweni la wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika sherehe hizo za mahafali .Baadhi wa wanafunzi wa shule hiyo wakiwa katika mahafali hayo.


Vodacom Foundation wafuturisha na kutoa msaada Pangani

Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa Maafisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon kulia na Mwamvua Mlangwa wa pili kutoka kulia huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili kushoto kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani wa pili kutoka kushoto, katika msaada huo pia Vodacom Foundation iligawa Mchele, Maharage, mafuta ya kula pamoja na vifaa vya shule.
Mwamvua Mlangwa Mratibu wa Uhusiano Vodacom Foundation akimkabidhi madaftari mtoto Mohamed Mtoo Ally wa Madrasat Tarba Mwera Pangani mara baada ya futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki mjini Pangani na kufuturisha wakazi wa mji huo na kugawa misaada ya vyakula na vifaa vya shule kwa watoto wa vituo vya watoto yatima na Madrasa, wanaoshuhudia tukio hilo ni Sheikh Mohamed Khalili Mwakilishi kutoka Tanga Mjini na kushoto na Sheikh Khamis Rashid mwakilishi wa Sheikh wa Pangani.
Wakazi wa mji wa Pangani wakipata futari mwishoni wa wiki ambapo Vodacom Foundation iliwafuturisha na kugawa vyakula na vifaa vya shuleni wa watoto yatima na madrasa mbalimbali mjini humo ambavyo ni Mchele, maharage, mafuta ya kula, sukari na vifaa vya shuleni kwa ajili ya wanafunzi.


msaada kwenye tuta

mkuu wa libeneke,ass.aleikum.naomba msaada,

mimi ni mkazi wa hapa dar,natafuta kausafiri ka bei nafuu kazuri na reasonable price.natafuta gari safi,nzuri ambayo haizidi 10 million cash.mwenye kuwa nayo anitumie picha na negotiable price kwa email
yahya.simon@gmail.com,tel .
0782 302164
workplace JMALL/Harbour View towers.
kama inawezekana ailete gari hapa JMALL anipigie au anibeep nitampigia tuonane tuongee tupatane na kumaliza biashara.Mkuu wa libeneke kutokana na umaarufu wako na kheri za mwezi huu utanisaidia na inshaallah sina cha kukulipa kikubwa ila mola atakulipa.Sifanyi mzaha kweli nahitaji usafiri soonest.

Sambamba na hilo pia mkuu nahitaji kununua plot/shamba hata nje kabisa ya mji-barabara ya morogoro-isizidi Kibamba,barabara ya bagamoyo-isizidi boko/bunju,barabara ya mbagala-isizidi mbagala,CAP price ni 10,000,000.ukubwa wa eneo walau eka moja(atleast one acre).

Nisaidie mkuu,

ndimi nduguyo Yahya.


Jeshi La Magereza Laonywa Kutoshabikia Vyama Vya Siasa Katika Kampeni

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Lawrence Masha akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam.
Kamishna Mkuu wa Magereza,Augustino Nanyaro akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Lawrence Masha leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara jana jijini Dar es salaam.



NA ZAHRA MAJID-MAELEZO
Serikali imelionya Jeshi la Magereza kutoegemea Chama chochote cha siasa wakati wa Kampeni za uchaguzi na kwenye zoezi zima la upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa kisiwa cha Amani na Utulivu.

BOFYA HAPA

kupata habari kamili.


Dr. Bilal akiwa masasi na nanyumbu leo

Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Bilal akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Masasi leo
Kamanda wa Chipukizi wa Wilaya ya Masasi, Fatuma Rajab akimvisha skafu Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiingia mpakani mwa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Newala leo mchana
Mgobea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Masasi, baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Newala, leo
Baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, wakiwa katika magari kwenye msafara wa kumsindikiza Mgombea Mwenza wa nafsi ya urais, Dk Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akitoka Wilaya hiyo kuelekea Wilaya ya Masasi leo asubuhi
wananchi wa Kijiji cha Lukuledi Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kumsikiliza mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia na kuwanadi wagombea Ubunge wa Jimbo la Lulindi,Bwanausi Dismas na Mariam Kasembe wa Jimbo la Masasi leo
Wananchi wa Kijiji cha Mangaka Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara Jimbo la Nanyumbu, wakimsikiliza mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji hicho leo mchana.
(Picha na Muhidin Sufiani)


Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker