In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for September 2010

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUFANYIKA OKTOBA MOSI, 2010 MKOANI MOROGORO

Baadhi ya wazee walioshinda michezo mbalimbali ikiwemo ya kuvuta kamba katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa ikiwani shamrashamra za siku ya wazee Duniani , Oktoba Mosi ya kila mwaka , wakizawadiwa zawadi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, ( wapili kutoka kulia) , leo baada ya kushinda kwao.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, Halima Dendego ( kulia) akitaniana bibi aliyeshinda mchezo wa kuvuta kamba kabla ya kupewa zawadi yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu) kutoka kulia, leo ikiwa ni maandalizi ya siku ya wazee Duniani Oktoba Mosi , mwaka huu , kitaifa inafanyika Mkoani hapa .
Bibi wa makamo akifanyiwa uchunguzi wa afya yake na Dk Baraka Nzobo kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ili kubaini kama anao ugonjwa wa kisukari ili awezekupewa ushauri na tiba katika Hospitali hiyo, upimaji huo ulianza kufanyika jana kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, ikiwa ni maandalizi ya siku ya Wazee Duniani ya kila mwaka, Oktoba Mosi, kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro
Baadhi ya wazee wakike na wakiume wakifanyiwa uchunguzi wa macho kwenye uwanja wa Jamhuri wa mjini Morogoro ili kubaini matatizo yao kabla ya kupewa ushauri na tiba kutoka kwa wataalamu wa macho, kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ,leo ikiwa ni maandalizi ya siku ya Wazee Duniani , Oktoba Mosi, mwaka huu , ambapo kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro.Picha na John Nditi.


CRDB yatwaa tuzo ya SUPERBRANDS

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,Dr. Charles Kimei akipokea tuzo ya 'Superbrands' kwa benki bora Tanzania, kutoka kwa Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw. Jawed Jaffer katika sherehe zilizofanyika katika hotel ya Holiday Inn Jijini
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei akipokea tuzo ya 'Superbrands' kwa benki bora Tanzania, kutoka kwa Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki Bw. Jawed Jaffer.katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo Bi.Tully Esther Mwambapa
Wafanyakazi wa Idara ya Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wao Bi.Tully Esther Mwambapa na Mkurugenzi wa SuperBrands Bw.Jawad Jaffer katika sherehe ya kupokea tuzo ya benki hiyo kuwa benki bora ya Superbrands kwa mwaka 2009-2010


WAZIRI MASHA AWATAKA POLISI WASIVUNJWE MOYO NA ONGEZEKO LA UHALIFU

Waziri wa Mambo ya Ndani,Lawrence Masha akimtunukia Cheo Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo uafisa wa Polisi. PC Happines Temu wakati wahitimu hao walipotunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo hayo kwenye Chuo cha maafisa wa polisi (Dar es salaam Police Academy) yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

NA MAGRETH KINABO NA MARY KWEKA- MAELEZO

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Lawrence Masha amelitaka jeshi la polisi lisivunje moyo kwa kuongezeka kwa taarifa za uhalifu katika vituo vya polisi bali wachukulie kama changamoto na kujidhatiti kukaimrisha mikakati ya kukabiliana na matukio hayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Masha wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo, iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Dar es Salaam.

“Mnao wajibu wa wa kuwa mstari wa mbele katika kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto hizi,” alisema Waziri Masha.

Alizitaja sababau za kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kuwa ni maendeleo ya Sayansi na teknolojia, ukosefu wa ajira, utandawazi, umasikini, ukuaji wa miji, ongezeko la makazi holela, kuzagaa kwa silaha, imani za kushirikiano,ongezeko la pengo baina ya matajiri na masikini pamoja na utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevyia.

Waziri Masha alisema kuongezeka kwa taarifa za uhalifu katika vituo vya polisi ni miongoni mwa mafanikio ya jitihada zinazofanywa na jeshi hilo, kuwahamasisha wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao.

Hata hivyo Waziri Masha aliongeza kuwa makosa yanayowakera wananchi kama unyanga’nyi na uvunjaji wa majumba na wizi yamepungua.

Alisema takwimu zinonyesha kuwa mwaka 2008 makosa uvunjaji yalikuwa 27,491 na mwaka 2009 yalipungua hadi 26,561 hivyo kupungua kwa asilimia 3.4, wakati makosa ya wizi mwaka 2008 yalikuwa 31,130 na mwaka 2009 yalipungua hadi kufikia 28,427, hivyo yamepungua kwa asilimia 8.7.

Waziri Masha alilipongeza jeshi hilo, kwa kuendelea na mpango wa kuratibu na kusimamia mafunzo ya walinzi wa amani kimataifa ikiwa ni pamoja na kushiriki kwa vitendo shughuli za kulinda amani sehemu mbalimbali duniani.

“Serikali inaendelea kuvijengea mazingira mazuri vyombo vya ulinzi na usalamana kutatua matatizo ya makazi na maslahi ya watumishi wake.

Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) katika mwaka huu wa fedha inaendelea na wamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za askari kwa kujenga maghorofa 30 kambi ya polisi barabara ya Kiliwa, sita kambi ya Mabatini Mwanza, sita Musoma , Mara, Tatu Byekera ,Bukoba, 12 Ludewa Iringa, nane Kiwanja cha ndege Arusha, mbili Unguja Kuu Unguja na mbili Finya Kaskazini, Pemba.

Naye Mkuu wa chuo hicho, Elice Mapunda alisema kitaanza kutoa diploma ya sayansi ya polisi kuanzia mwaka 2010/2011 ikiwa ni jitihada za kukipandisha hadhi.

Alisema jumla ya wanafuzi walioripoti katika mafunzo hayo walikuwa 356 na wote wamefaulu, lakini wawili kati yao walishindwa kushiriki kikamilifu baada ya kuumia wakati chuoni.


Mtangazaji mkongwe wa Idhaa ya Kiswahili sauti ya Ujerumani Ramadhani ali astaafu rasmi leo

Mkuu wa idara ya Afrika, Asia na Mashariki ya Kati wa Radio ya Ujerumani Dr Utter Schafer akipeana mkono na mtangazaji mkongwe wa Idhaa ya Kiswahili Bw.Ramadhani Ali huku mkuu wa idhaa ya kiswahili Andrea Schmidt akiangalia jioni hii katika ofisi za radio hiyo maarufu duniani mjini Bonn katika mnuso mdogo wa kumuaga rasmi mkongwe huyu baada ya kupiga mzigo hapo DW kwa miaka zaidi ya 40.
Mkuu wa Idhaa Andrea Schmidt akiwa na Ramadhani Ali akiwa kakumbatia rundo la zawadi alizopewa baada ya kuitumikia idhaa ya kiswahili kwa miaka zaidi ya 40 ambapo leo amestaafu na kuagwa rasmi
Watangazaji nguli toka shoto Sekione Kitojo 'Bundes', Ramadhani Ali,
Abdul Mtullya 'Konkoo' na Aboubakary Liongo ' Shekhe' Toka shoto ni watangazaji Bi. Halima Nyanza, Bw. Mohamed Abdul-rahman, Bw. Aliyu (wa Idhaa ya kihausa)na Aboubakary Liongo






JK aguruma uwoya, urambo leo

JK akihutubia mkutano wa kampeni Uyowa Wilayani Urambo leo
Wananchi wa Uyowa wakiwa na nyuso za furaha wakati wakifuatilia hotuba ya JK kwenye mkutano wa kampeni leo
Umati mkubwa wa watu wakimshangilia JK wakati akiingia Uyowa, Ulyankulu Wilayani Urambo leo.
umati mkubwa wa watu wa Uwoya,wilayani Urambo ukimsikiliza JK wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni leo.


hoja ya haja

Mkuu wa kaya pole na mihangaiko ya kampeni naona imepamba moto kweli kweli ! Uzuri ni kwamba libeneke bado linaendelea kama kawa hivyo lazima nikupongeze sana kwa hilo !

Sasa pamoja na kwamba nchi nzima iko kwenye harakati za uchaguzi ,mambo mengine lazima yaendelee kama kawa na hivyo nimeona ni vyema nikawajulisha watanzania wenzangu nini kinachoendelea kwenye soko letu la ajira tokea tufungue milango ya soko huru julai mosi mwaka huu.

Ikumbukwe kwamba lengo la soko huru lilikuwa ni kufungua milango ya uwekezaji na ufanyaji kazi kwenye eneo letu la Afrika Mashariki kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima na mpaka sasa makubaliano ni kwamba wananchama wa nchi 5 za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi kwenye nchi yoyote ila kwa hapa kwetu wageni lazima waombe vibali vya kufanyia kazi wanapopata kazi hapa kwa muda wa miaka 5 ijayo ambapo vitaondolewa kabisa.

Hivyo Mkenya, Mganda,Mrundi,au Mrwanda akija hapa akipata kazi kihalali ataomba kibali uhamiaji . Ikumbukwe kuwa wenzetu Wakenya walianza ubepari zamani hivyo si ajabu ni nchi ya 2 kufanya biashara kwa wingi na Tanzania baada ya Uingereza hivyo pia tunategemea wakenya wengi wawepo kufanya kazi Tanzania lakini kwa kushindanishwa na wazalendo .

Cha ajabu mzee ni kwamba hawa wenzetu badala ya kutumia ushindanishi unaotakiwa sokoni kwa kuangalia vigezo na uwezo wa mtu wao wameanza kutumia propaganda,mizengwe na mbinu nyingine chafu za kuwaondoa watanzania kwenye nafasi zao na kuwapa wakenya.

Utakuta mtu anapewa kazi kwenye kampuni ya kikenya then anapigwa zengwe kuwa utendaji wake ni mbovu na kesho yake analetwa mkenya hata kama mtanzania ni mzuri kwa vigezo vyote au pia kuna kazi zinahitaji training wao hawatakupa hiyo training kwa makusudi ili ionekane huwezi kazi wamlete mkenya!

Mbinu nyingine wanayotumia wanakupeleka training kwao Nairobi labda mwezi mzima na huku nyuma wanamleta mkenya anafanya kazi zako kisha wewe ukimaliza training unaambiwa hukufikia vigezo wanavyotaka hivyo ujiuzuru au wakufukuze kazi au watakutafutia kisa chochote tu hata cha maisha yako binafsi yasiyohusiana na kazi yako halafu unatishiwa kuwa watakufukuza au ujiuzuru nwenyewe! Kisha wanaenda uhamiaji kumwombea kibali mkenya wao wakitoa sababu kuwa mtanzania waliyemweka ameshindwa kufikia vigezo wananvyotaka!

Wadau hizi ni baadhi ya mbinu tu wanazotumia hawa wenzetu kunyakua kazi wa watanzania kwa nguvu ! Kuna mifano mingi na watu wengi wameathirika na hizi mbinu chafu za wakenya hivyo naona muda muafaka umefika wa mamlaka husika kufanyia kazi hili jambo!

Tunaelewa kuwa Kenya maisha ni magumu sana ndo maana wanakimbilia huku kutafuata kazi wakati hakuna watanzania waliofanikiwa kupata kazi Kenya kwa kuomba tu kwenye makampuni ya Kikenya ukiacha wanaopelekwa na makampuni nya kimataifa yaliyopo Tanzania . Hii ni kwasababu Wakenya wana dharau sana (Kenyans are very arrogant) kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki na wanajiona wao wanajua kila kitu. Hii imesababisha hata wao kwa wao wabaguane kimakabila hivyo kampuni ya Mkikuyu huwezi kumkuta Mjaluo au Mkamba ! hiki ndo chanzo cha wao kuuana mwaka juzi baada ya uchaguzi wao maake kule kwao wanaishi kwa mbinu za msituni (survival of the fittest) .



Hata hapa kwetu wafanyakazi wengi walio chini ya mabosi wakenya wanadharauliwa na kunyanyaswa kisa ni watanzania hata kama wana uwezo kuwazidi hao wakenya !

WATANZANIA TUFANYEJE

Ningependa kuwashauri wadau wanapokutana na hali hii wasikae kimya na kusubiri mungu awasaidie . wajue kwamba huu ni mpango maalum ambao wenzetu wamekuja hapa kupokonya ajira za watanzania hivyo tuchukue hatua madhubuti ambazo ni pamoja nazifuatazo:

-hakikisha kila unapofanya kitu kizuri ofisini kwako bosi wako anajua .Hii itakusaidia sana wakati wa kureview performance yako kazini . wenzetu wanaijua sana kuitumia mbinu hii inayoitwa corporate politics! Akifanya jambo dogo tu lazima amwambie bosi wake hivyo kujilinda pakitokea tatizo baadaye.

Watanzania tusikae kimya kusubiri bosi wako aone mwenyewe kuwa wewe unafanya kazi vizuri sana ! mfuate bosi mweleze mafanikio yako kazini na sio kujificha bosi akipita koridoni oooh utakula wa chuya !

Pili tuhakikishe tunazijua sheria za kazi vizuri na sio kutishiwa tishiwa tu na hawa wakenya wakati nchi ni yetu bwana ! tujenge utamaduni wa kusoma haki zenu ndani ya sheria ya kazi ili likitokea jambo tuweze kujitetea ipasavyo. Japokuwa sheria zenyewe zina mapungufu kwa mfano mwajiri anapewa uhuru wa kuchagua akurudishe kazini au akuachishe kazi na kukulipa mshahara wa miezi 12 tu ! sheria ibadilishwe hii !

Tatu tujifunze bargaining skills wakati wa kuomba kazi maake utakuta wengi wetu mishahara ni midogo sana kwani wakati wa kuomba kazi tunamwachia mwajiri ajipangie mshahara wa kukulipa matokeo yake hata ukimpeleka mahakamani atakulipa vijisenti vya miezi 12 na kukufukuza kazi huku nafasi yako akipewa Mkenya na kulipwa kama expatriate.

Nne tungependa vyombo vinavyohusika na kutoa vibali vya kazi kwa wageni (hasa wizara ya mambo ya ndani, wizara ya kazi na professional bodies ) vijiridhishe kweli hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi ambayo kibali kinaombwa. Hivi kweli jamani hatuna wahasibu wa kutosha mpaka Mkenya aje awe management account (mhasibu wa ndani) au financial controller (mhasibu mkuu ) hapa Tanzania wakati NBAA wanatoa CPA mara 2 kwa mwaka ! hawa vijana wanaomaliza hizi qualification watafanya kazi gani sasa ? Tuachane na njaa za muda na utamaduni wa kuabudu wageni ! Tuamini wazalendo na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi .



Tano watanzania tubadilike tujenge attitude ya kujituma kazini maake soko la kibepari ndo linavyotaka ! ukiwa mvivu kazini wakenya watazidi kuja na kuchukua nafasi zetu nasisi tutaishia kulalamika tu ! hivi sasa mabenki makubwa 3 madirector wao ni Wakenya ! mshahara wa director mmoja tu unatosha kuwalipa watanzania zaidi ya 20 wa ngazi za chini na hapo bado hujazungumzia wenzao waliowaleta toka Kenya na vitu wanavyonunua kwa makampuni yaliyo Nairobi hata kama kuna makampuni ya Tanzania yanazalisha kitu hicho hicho maake bosi ndo mwamuzi !

Naomba kuwakilisha

Mdau aliyetendwa na wakenya !!


KCB Tanzania yajitolea kulea watoto yatima

Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Center Margareth Mwegalawa akipokea msaada wa vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya milioni 2/- kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania ,Christina Manyenye wakati wa hafla iliyofanyika kwenye kituo hicho kinachohudumia watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dasr es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania, Christina Manyenye (kushoto) na Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Center , Margareth Mwegalawa wakiwasaidia kufungua maboksi yenye vitabu vilivyotolewa na benki hiyo wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni2/- jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wfanyakazi wa KCB Tanzania wakiwa wamewabeba watoto wa kituo cha yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Amani Orphanage Center cha Boko wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya milioni 2/-kwenyer hafla iliyofanyika shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya KCB Tanzania imeamua kubeba jukumu la kuwalea watoto 11 wa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kwa kukikisaidia na kukihudumia kwa mahitaji ya vifaa muhimu vya shule kwa watoto hao kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi milioni 2/- kwa ajili ya takribani watoto 45 wa shule hiyo,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Christina Manyenye alisema kwa kuanzia wametoa vifaa hivyo ili viwasaidie kwanza yatima.

Akifafanua alisema kutokana na kuguswa na watoto wa kituo hicho kilicho chini ya Shirika la Empowering Children and Community Organization kilichoanzishwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wameona wakisaidie kutokana na kuona kwamba ndoto za watoto hao ni sawa na za wanaotoka katika familia zinazojimudu kimaisha.

“Hivyo basi hatuna budi kuwasaidia watoto hawa na tunaahidi kuendelea kuwasaidia ili kukipunguzia mzigo kituo cha Amani jukumu la kuwalea watoto kituo hiki cha Amani ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kusoma. Ni wachache sana wanaoweza kufanya ubinadamu huu,” alisema Manyeye.

Hata hivyo aliongeza kwamba msaada huo umefuatia KCB Tanzania kutambua umuhimu wa jamii na kufahamu ukweli kuwa maendeleo ya jamii ni maendeleo ya taifa zima. Aidha alisema bila jamii yenye maendeleo uwepo wao kama benki utakuwa na mashaka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Margareth Mwegalawa alisema kuwa licha kuhudumia watoto yatima 11 wanaoishi bweni, pia wanahudumia watoto wengine wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya shule na mahitaji mengine.

Hata hivyo wanakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kulala watoto, vitanda, uchakavu milango na madirisha ya jengo la kituo hicho jambo linalochangia kituo kuchukua watoto wachache wanaoendelea kuishi kwenye mazingira magumu.

Kutokana na hilo waliiomba KCB Tanzania na taasisi zingine kujitokeza kukisaidia kituo hicho kwa kukipa misaada mingine ikiwemo magodoro, vitanda, vifaa vya kusomea watoto, vyakula, madawati ya kukalia na vifaa vya kufundishia.

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Bunju, Syzgo Alexander aliiopongeza benki hiyo kwa kuwa na moyo huo wa kujitolea na kusema kutokana na mahali kilipo kituo imeonesha imejitoa kuihudumia jamii kwa hali na mali jambo alilotaka liiungwe mkon o na Watanzania.

KCB Tanzania ni benki kubwa Afrika Mashariki ikiwa na rasilimali nyingi ikiwemo matawi zaidi ya 200 na mashine zaidi ya 400 za kutolea fedha (ATM) zilizotawanywa kote Afrika Mashariki na mtandao unaofikia nchi za Rwanda na Sudan Kusini.


UFUNGUZI WA SHINA LA CCM LUTON - LONDON UINGEREZA

TUNAPENDA KUWAATARIFU WATANZANIA WOTE NA WAKEREKETWA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KUWA KUTAKUWA NA UFUNGUZI WA SHINA LA CCM LUTON.

SHEREHE ZA UFUNGUZI ZITAFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 23.10.2010 KUANZIA SAA SABA MCHANA KATIKA ANUANI ILIYOTAJWA HAPA CHINI.

KADI ZA UANACHAMA ZITATOLEWA SIKU HIYO KWA PAUNDI TATU TU (£3ONLY)

ADA YA UANACHAMA KWA MWAKA NI PAUNDI KUMI NA MBILI TU (£12)

PIA KUTAKUWA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHINA SIKU YA UFUNGUZI.

NAFASI YA MWENYEKITI, MAKAMU MWENYEKITI, KATIBU, MWEKA HAZINA NA WAJUMBE.

TAFADHALI WAKILISHA JINA LAKO KWA AJILI YA NAFASI HIZI KWA KUWASILIANA NA UONGOZI WA MUDA KWA NAMBA TAJWA HAPA CHINI

PIA TAFADHALI WAKILISHA JINA LAKO KWA AJILI YA KUHUDHURIA SHUGHULI HII MAPEMA IWEZEKANAVYO.

WATU WA KUWASILIANA KWA AJILI YA KUFANIKISHA SHUGHULI HII NI;

1. ABRAHAM SANGIWA

2. ALBERT NTEMI

3. SAMSON MWAKALINDILE

Namba za simu: 07833571100, 07404863333,01582 481523.

ANUANI YA TUKIO: 557 DALLOW ROAD, LUTON LU1 1UW

IMETOLEWA NA UONGOZI WA CCM TAWI LA UINGEREZA


WATOTO MKOANI KIGOMA NA RUKWA KUPATIWA CHANJO YA POLIO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa kampeni ya utoaji wa Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Polio watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Rukwa na Kigoma litakalofanyika tarehe 4 hadi tarehe 7 mwezi Oktoba 2010. Kulia ni Mganga mkuu wa Serikali Dr. Deo Mutasiwa.

Na. Aron Msigwa - MAELEZO.

Serikali imewataka wananchi wa mikoa ya Kigoma na Rukwa kushiriki kikamilifu katika awamu ya pili ya zoezi la utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa kupooza (polio) kwa watoto walio chini ya miaka mitano litakolofanyika tarehe 4 hadi tarehe 7 mwezi Oktoba, 2010.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni amesema kuwa hatua ya kufanyika kwa zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto katika mikoa hiyo, inafuatia taarifa ya kutokea kwa mlipuko wa Ugonjwa huo katika wilaya ya Kalemie nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mwezi Agosti mwaka huu.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilichukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini kutokana na jiografia kati ya Tanzania na DRC ,pamoja na muingiliano wa watu katika maeneo hayo kwa kuihamasisha jamii na viongozi wa ngazi zote mkoani Kigoma na Rukwa na wadau wengine kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo .

Mbali na hatua hiyo amesema, serikali iliendesha zoezi la kutoa chanjo ya polio kwa watoto wote walio na umri chini ya mika mitano kwa njia ya Kampeni , Kuimarisha utoaji wa taarifa za wagonjwa waliopata ulemavu wa ghafla na uimarishaji wa utoaji wa chanjo za kawaida ambapo matokeo ya zoezi la awali yanaonyesha mafanikio kwa kufikia kiwango cha asilimia 90 ya chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.

Amesema mwongozo wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) unabainisha kuwa ili kudhibiti mzunguko wa virusi pori vya ugonjwa wa polio ni muhimu kutoa chanjo za ziada kwa njia ya kampeni kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka angalau kwa awamu mbili.

Hata hivyo amefafanua kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo watahakikisha kuwa vitendea kazi kwa ajili ya Kampeni hiyo zikiwemo chanjo na vifaa vingine vinaapatikana katika muda muafaka .

“Kampeni na zoezi la utoaji wa chanjo hii katika mikoa ya Rukwa na Kigoma litafanyika kwa mafanikio makubwa kutokana na kuwepo kwa vifaa muhimu kwa shughuli hiyo ambavyo tayari vimeanza kusambazwa” amefafanua Bi.Nyoni.

Amesitsitiza kuwa chanjo hii ya Polio itakayotolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wapatao 703,389 katika mikoa yote miwili ni salama na itatolewa na wataalam wa afya kwa njia ya matone kinywani kwa watoto wote bila kujali kama walipata chanjo hiyo hapo awali au hawakupata.

Ametoa wito kwa wazazi na wananchi wote kushiriki kikamilifu katika zoezi hili kwa kushirikiana na wataalam wa afya watakaopita nyumba hadi nyumba na kuongeza kuwa watoto wote watakaopata chanjo hiyo watawekewa alama maalum katika kidole kidogo cha mkono wa kushoto ili kusaidia ufuatiliaji na uhakiki pamoja na kuweka alama kwenye nyumba zitakazofikiwa kulingana na hali ya chanjo ya watoto waliopo katika nyumba hizo.


Balozi Peter kallaghe kuongea na Watanzania Birmingham


Habari Kaka Michuzi
Kaka naomba utuwekee hili tangangazo la Mh. Balozi kuzungumza na Watanzania wa Birmingham na vitongoji vya siku ya jumamosi 02/10/2010 kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11. address ipo kwenye hiyo flyer nimekutumia.
Naomba uwasisitize Wabongo watakuwa wanakuja kuzingatia sana muda.

Asante kwa kazi yako njema kaka.

Jackson M
Katibu TA-Birmingham / Mjumbe TA-Taifa


16 Semi Finalist Named for the emerging designers Competition

Judges sit ready for selecting 16 emaerging designers,from left to right is Mama Nshao Shalua,Mr. Charles Washoma and Mr. Manju Msita.Sketches from different emerging designers who compete for Ermerging Designers Competition.

==================

Three eminent Panelists Sit for Emerging Designer’s Competition Selection

16 Semi Finalist Named for the emerging designers Competition

“Contemporary Swahili" is the Theme of 2010 Competition

16 out of 31 neo talents have been selected as semi-finalist, for the Swahili Fashion Week 2010 Emerging Designer of the year Award.

The selection which was held on 29 September 2010 at the Southern Sun Hotel where 16 emerging designers were selected by a Panelist of Three Judges. The Judges were renowned designer Manju Msitta of Smart Afrika Design Label, Charles Washoma, CEO of African Life assurance and One of Dar es Salaams Fashionable man and Director of arts Nsao Shalua of Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council)

The selected 16 semi-finalist will once again yet undergo an Intensive Selection to select the 8 Finalist who shall compete for the prestigious title during the Swahili Fashion Week to be held in November this year.

Swahili Fashion week Fashion Coordinator Washington Benbella Commented “The response has been tremendous, and the Zeal and zest shown by the amazing talent we have in this country is phenomenal, but the journey of those who weren’t selected should not end here and not give up on their passion”

The semi-finals selections are Zarina Suleiman, Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urasa, ShaibMfaume, Annette Ngogi, Mwajabu Sadiki, Diana Malenge, Mgece Makory, Omary Bundalah, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Nadia. A. Ahmed, Angelina Muna, Jacqueline Chipeta, Bami Musese and Grace Kijo.

The judges were looking at various criteria to choose the candidates based upon the designers ability to sketch, sketch attractiveness, creativity, color and thematic relation.

Swahili Fashion Week is a platform for designers - both fashion and accessory - from Swahili speaking countries to showcase their creativity, market their art and network with their clientele. This is all aimed at promoting fashion as an income generating, job creating industry while emphasizing a “Made in East Africa “concept.

Initiating a dynamic and promising platform for the fashion industry in the region, Swahili Fashion Week is geared towards being the most sought out after fashion platform in Eastern Africa for the international market.

The third annual Swahili Fashion Week will take this November in Dar Es Salaam, Tanzania.

The competition, now in its third year has no age limit, and was open to anyone who believes he or she has the creative talent to be a fashion designer. “Swahili Fashion week is the perfect platform for a designer to showcases his creation, and the emerging designers competition, is a stage to jump start off ones career.” Added Mustafa Hassanali Swahili Fashion Week organizer


tangazo muhimu hili


klabu ya rotary ya Bukoba yaikabidhi manispaa ya Bukoba mabembea iliyoyajenga kwa ajili ya watoto

kaimu mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba Robert Kwela akipongezana na rais wa klabu ya rotary ya Bukoba mara baada ya kukabidhiwa mabembea yaliyojengwa na klabu hiyo kwenye ufukwe wa ziwa victoria yaliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 18.1.
Rais wa klabu ya rotary ya Bukoba,Elias Mashasi akisoma taarifa ya mradi wa mabembea kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Bukoba,Robert Kwela ambao ulitekelezwa na klabu hiyo kwa fedha za wahisani na baadae kukabidhi kwa manispaa hiyo kwa ajili ya kuuendesha.
baadhi ya wanachama wa klabu ya rotary ya Bukoba wakicheza kwenye mambembea waliyoyajenga baada ya kuyakabidhi kwa uongozi wa manispaa ya Bukoba, aliyesimama nyuma ya wanachama hao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Bukoba, Robert Kwela.Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba.


Msiba Columbus Ohio


Mr. Matthew Salukele (Marehemu)Date of Birth: 22/02/1941 - Died: 09/28/2010 @ 4:30 pm at St Ann’s Hospital Columbus Ohio.

Happyness na David Salukele wanasikitika kuwataarifu habari ya msiba wa mpendwa baba yao,Mzee Matthew Salukele uliotokea jumanne Sept 28,2010 saa 10 unusu(4:30pm),St Ann's Hospital,Columbus Ohio.

Tunaomba msaada wenu katika kukamilisha kusafirisha mwili wa marehemu Tanzania,Gharama za kuusafirisha mwili zinafikia $25,000.
Unaweza kusaidia kupitia Chase Bank Acc #917118267 Routing # 044000037.

Msiba upo Add:
1427 hideaway Woods Dr
Westerville OH 43081

Tunatanguliza Shukrani kwa msaada wako wa hali na mali utakaotoa hasa kwa kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa Baba yetu.

Baba Tulikupenda Sana lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,kimwili hatuko pamoja,kiroho tutakua nawe siku zote mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena,
Jina lake lihimidiwe.

For more information Please contact:
David Salukele cell# 614-859-9602
Walter kalosi cell#614-537-1448
Happiness Salukele cell#614-772-5126
Adella Njau cell#614-446-9710
Dorah Njau cell#614-589-5685
Jacqueline Mjengwa Cell# 614-804-5237


mzee khamsin awasili Dar tayari kwa usiku wa khanga za kale ijumaa hii

Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin ambaye ni gwiji wa ubunifu wa mitindo ya mavazi amenaswa usiku huu na Jiachie Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere alipokuwa akimpokea mumewe Mzee Khamsin kutoka huko Ughaibuni ambaye ametua rasmi kwa ajili ya onyesho la usiku wa Kanga za Kale litakalofanyika ijumaa usiku katika ukumbi wa Diamond VIP.


JK ahutubia bukene, nzega na tabora mjini

Umati ukimsikiliza JK mjini Bukene wakati wa
mwanzo wa ziara yake ya kampeni mkoani Tabora
Maelfu wakimsikiliza JK mjini Nzega

Umati mkubwa ulijitokeza uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kumsikiliza JK

JK akiingia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
JK akigonganisha tano na wakaazi wa Tabora
Sehemu ya umati wa mjini Tabora
JK akihutubia Tabora
JK akimnadi mgombea ubunge Tabora Mjini Alhaj Ismail Aden Rage
Mgombea ubunge Tabora Mjini Ismail Aden Rage akipiga soga na waandishi Ibrahim Bakari wa Mwananchi (shoto) na Halfan Saidi wa The Guardian uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora
JK akiongea na Bahati Iddi Nzimano, mwanadada mwenye ulemavu wa kutokuwa na mikono yote miwili ambaye mwaka juzi alimsaidia mtaji wa kufungua biashara na sasa Bahati maisha yake ni mswano kabisa licha ya ulemavu alionao. Bahati akiwa na ankal na mtaalamu wa kushuti video Adam Gire uwanjani hapo













CITY OF LONDON SCHOOL YASAIDIA ASASI YA MALAIKA KIDS YA MKURANGA

NAIBU BALOZI WA TANZANIA, BWANA CHABAKA KILUMANGA, AKIWA PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA ASASI YA MALAIKA KIDS NA WANAFUNZI WA CITY OF LONDON SCHOOL, BAADA YA KUKABIDHIWA HUNDI KWA NIABA YA ASASI HIYO YA MALAIKA KIDS YA KIJIJI CHA MKURANGA.
WANAFUNZI WA CITY OF LONDON SCHOOL, WAKISIKILIZA NA KUPOKEA SHUKRAN KUTOKA KWA NAIBU BALOZI NA VIONGOZI WA ASASI YA MALAIKA KIDS.


simba yaidungua mtibwa sugar 1-0 leo

mchezo kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliofanyika leo Septemba 29, mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro. Wekundu wa Msimbazi waliibuka kidedea kwa bao 1-0 lililopatikana kwa njia ya matuta, kupitia mchezaji Radhid Gumbo , baada ya kuangushwa katika eneo la hatari, Emmanuel Okwi na mchezaji wa Mtibwa Sugar, Salvatory Ntebe, penati hiyo ilitolewa na Mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii. Kikosi cha Simba
Kikosi cha Mtibwa Sugar
Benchi la Mtibwa Sugar
Benchi la Simba
Patashika langoni pa Mtibwa Sugar






msaada tutani

Hi Anko Michuzi,
Mimi ni mdau niliekua nakula nondo,Boxi na kuishi kwa miaka 15 Nchini USA, Baada ya kuchoka kubeba boxi nikaamua nirudishe timu home na mazaga zaga yangu hadi vijiko. Sasa basi baada ya Container langu kufika Bandarini pamoja na usumbufu wote siku naenda kulipia ushuru Tanzania Custums naambiwa pamoja na kwamba nilipata Tax exemption ya Gari langu na vitu vingine vya ndani maarufu kama Personal effects lakini kutokana na Gari langu kua na umri zaidi ya miaka kumi nikaambiwa siwezi kupata Tax Exemption ya hilo gari japo mimi nimelipakiza mwezi may 2010 na nimelitumia kwa miaka 11 nikijua kitakacho ni cost ni ushuru wa uchakavu tu.
Nilipoulizia nikaambiwa kuna sheria mpya imeanza kutumika majuzi ambayo imesainiwa na kamishina wa TRA bila kujari hiyo gari niipakiza lini hata kabla ya hiyo sheria haijaanza kutumika.
Naomba wadau mnisaidie kujibu maswali yafuatayo:-
1. Je sheria za nchi zinatungwa na kamishina ama Bunge?
2. Kama Kamishina anatunga sheria kwa nini asiangalie ni lini ulipakiza mzigo wako
3. Kwa nini kama sheria zina badilika tuzitangaziwe atleast miezi sita kabla sheria hiyo kuanza?
4. Je nifanye nini maana mpaka sasa hivi nimedata
Asanteni wadau
Mdau aliyechanganyikiwa


BIG BROTHER ALL STARS:AFRICA MUST VOTE THEIR FAVOURITE BARNMATE BACK INTO THE HOUSE

This week Africa has the power to send two Barnmates back into the House to play for the $200 000 prize money.

During last night’s (Monday September 27) live nomination show on DStv channel 198, Big Brother told Housemates that no one will be evicted.

Housemates cheered as Big Brother made the announcement, they kept saying, "Asante” as they embraced one another and headed straight to the Jacuzzi.

Meanwhile in the Barn Big Brother told the Barnmates that they were all up for eviction. Viewers now have the opportunity to vote two of their favourite Barnmates back into the House.

The names of the Barnmates that will make it back to the House will be announced during a two-hour special show on Sunday, October 3.

Big Brother All Stars is broadcast live 24/7 for the next 19 days on DStv Channel 198, with edited highlights shows every day of the week on M-Net and later on AfricaMagic. Big Brother All Stars is also available on DStv Mobile in Ghana, Kenya, Namibia and Nigeria.

Big Brother wants your vote - just remember, you are voting to send your favourite Barnmate back to the house!

Which means, the more you vote for your favourite barnmate, the better their chance of going back to the house.

The Barnmate who receives the least number of votes will be evicted.You can vote to send a nominated barnmate back to the house in three different ways:
1. Via the website, or the WAPsite on your mobile phone.
2. By sending an SMS
3. Using MXit


To vote on the website: Cast your vote by clicking on the barnmate who you want to send back to house.
(You can vote once per hour per registered email address.)

To vote via SMS: send the word VOTE followed by the barnmate’s name to the number for your country (displayed below). For example if you are voting from Botswana send Vote Thato to 15626. SMSes are charged per specified network tariffs in the various countries. VAS rates apply. Free minutes do not apply.
(You can vote 100 times by SMS per mobile number during each voting period.)

TanzaniaVodacom 15726 Tsh 600
Celtel 15726 Tsh 600
Tigo 15726 Tsh 600
Zantel 15726 Tsh 600
SASATEL 15726 Tsh 600

To vote using MXit: open the browser on your WAP-enabled mobile phone, and type in www.mxit.com/wap to download MXit for free. Then locate MXit on your phone in the applications or games section and register. Once in MXit, go to Tradepost -> Voting -> Big Brother Africa.
(Voting on MXit is free and you can vote up to 10 times on MXit per voting period.)

To vote using WAP [www.mnetafrica.co.za/bigbrother]: Register on the Big Brother network, or use your existing Vuzu or Oboma profile details to log in.
(Vote on the website or wapsite for free, once per hour during the voting period.)

Voting begins immediately after the Nomination show has been broadcast on M Net Africa at 21:30 EAT on Monday nights.

Voting closes at 07:00 EAT on the following Sunday morning. Find out who has received the least number of Votes and will be evicted by watching the Eviction Show on Sunday nights.


Mazingatio kwa mablogger juu ya libeneke


Siku za hivi karibuni tumeshuhudia kila mtu akija na blog yake,mlundikano wa blog umezagaa kila kona ya .com,kila mmoja ana malengo yake binafsi,wapo waliokuja na blog kama njia ya kujitangaza,kuna waliokuja kwa ajili ya kutafuta umaarufu,wengine kwa kuwa mtu fulani ana blog nami lazima niwe nayo,kuna waliokuja kwa ajili ya kusaidia jamii(kama AfroIT Blog) na kuna walioamua kuja na blog kwa ajili ya kutengeneza pesa. Hivyo madhumuni ya blog ni mengi ambapo hutegemeana na mwana bklog mwenyewe.


Hivyo basi ushindani unakuwa mkubwa mno,kumbuka mazingira ya ushindani siku hizi yanazidi kuwa magumu hivyo unahitajika kuumiza kichwa ili kuibuka kidedea kwenye uwanja wa wanablog.


Kuwa na blog bila ufahamu au maarifa yake kwa undani kuna uwezekano mkubwa sana usifikie lengo lako,ingawa niwengi wetu inatuwia ugumu kupima ufikiwaji wa malengo zaidi ya kuangalia figure ya takwimu za watembeleaji ambazo kwa upande mmoja au mwingine zinaweza kuwa na mapotezo makubwa.

Hapo zamani kuna watu walisema,ukitaka kumnyima kitu mwafrika basi kiweke kwenye maandishi(kitabu),ila kwa dunia ya leo hii,kila kitu kipo kwenye maandishi tena kwa urahisi zaidi vilevile hii imani imepotea kwakuwa tumekuwa na mapenzi makubwa na kusoma vitabu,hii ni kwakuwa kama unataka kufahamu mambo mengi ni lazima uwe msomaji mzuri ma wada na vitabu mbalimbali huku ukijumuika na wataalam ambao watakusaidia kuweza kufikia lengo.Sisi kama nchi tunazoendelea bado tunahitaji kujifunza na kujua mengi zaidi kila kukicha.

Hivyo basi nimeambatanisha kitabu ambacho naamini kitakuwa na msaada mkubwa kwa wanablog wa kitanzania ambapo utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza blog inayolipa na kufanikiwa. Yote haya na mengine meengi yanapatikanika bure ndani ya AfroIT Downloads.
Download kitabu hiki nenda AfroIT Downloads au link ya chini
http://download.afroit.com/?p=1166


uzinduzi wa ilani ya uchaguzi kwa wasioona

Katibu wa Taasisi ya Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA), Bi. Jairos (kulia) akisoma Ilani ya Uchaguzi ya wapiga kura ya mwaka 2010 iliyoandikwa kwa maandishi maalumu ‘Nukta Nundu’ kwa ajili ya kuwasaidia wasioona wakati wa uzinduzi wa ilani hiyo ambao umefanyika jijini Dar leo. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti SWAUTA, Bi. Cecilia Masika, Mkurugenzi wa TGNP, Bi. Usu Mallya na Mkurugenzi wa ADD, Sixbert Mbaya. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii
Sehemu ya waliohudhuria hafla hii
wahudhuriaji wakifuatilia hafla




Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker