In order to view this object you need Flash Player 9+ support!

Get Adobe Flash player
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT - BEYOND THE ORDINARY - NATURALLY' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.










  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com
  • P. O. Box 33909, Dar es Salaam, Tanzania.  Tel: +255 22 26647870/1/3  Fax: +255 22 2647872. www.giraffeoceanviewhotel.com












Archive for November 2010

kilimanjaro stazz yaitungua somalia bao 3-0 leo

Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya Kilimanjaro stars,Mrisho Ngassa akionyesha umahiri wake mbele ya beki wa timu ya taifa ya Somalia katika mchezo uliopigwa leo ndani ya uwanja wa Taifa jijini.Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kuichapa timu ya Somalia mabao 3-0. Leo uwanja umejaa kwani kulikuwa hakuna kiingilio
Kiungo wa kati wa Kilimanjaro Stars,Henry Joseph akipena misuli na mchezaji wa timu ya Somalia katika mechi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliani wa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars,Nurdin Bakari akipachika bao la tatu dhidi ya Somalia mara baada ya kupata krosi maridadi kabisa kutoka kwa Mrisho Ngasaa.hadi mwisho wa mchezo Kilimanjaro stars 3-0 dhidi ya Somalia.
Nyanda wa Somalia akifanyia msaada wa kuvishwa jezi mara baada ya kufanyiwa matibabu na mmoja wa matabibu waliokuwepo uwanjani hapo.
Kocha wa timu ya Kilimanjaro stars,Jan Paulsen akifatilia kwa makini mchezo huo.
Washabiki waliofurika katika uwanja wa Taifa leo wakishangilia mara baada ya kupatikana kwa bao la tatu la timu ya taifa ya Kilimanjaro stars.


JK azindua benki ya TIB leo

Kibao cha makao makuu mapya ya
benki ya TIB aliyozindua JK leo
JK akipeana mikono na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu wakati alipowasili kufungua makao makuu ya TIB pamoja na tawi la benki hiyo Mlimani City jijini Dar leo. Wengine toka shoto ni Mkurugenzi Mkuu Bw. Peter Noni na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Profesa William Lyakurwa.
JK akisalimiana na maofisa wa TIB
Maofisa waandamizi wa TIB wakimpokea JK
Mwenyekiti wa kwanza wa bodi ya wakurugenzi wa TIB,
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Cleopa Msuya akimlaki JK
JK na viongozi wa TIB wakitoka makao
makuu ya TIB baada ya kuyazindua
JK akitoka tawi la TIB la Mlimani City baada ya kulizindua
Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Bw. Peter Noni akisoma risala yake
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TIB Profesa
William Lyakurwa akisoma risala

JK akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TIB
JK akimpa zawadi Bw. Ibrahim Kaduma, mmoja wa wakurugenzi waanzilishi wa TIB. kulia ni Waziri Mkuu mstaafu Mh. Cleopa Msuya
JK katika picha ya pamoja na Bodi ya wakurugenzi wa TIB. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Fedha Mh
JK katika picha na Wakurugenzi na menejimenti ya TIB
JK akiwa na wakuu wa TIB pamoja na wafanyakazi
JK na viongozi wa TIB na wafanyakazi
Tovuti ya TIB


matukio mbalimbali morogoro leo

Mchezaji wa zamani wa Timu ya Yanga , Said Mrisho ‘ Zicco wa Kilosa’ aambaye kwa sasa ni mwalimu wa soka , akipata ushauri kutoka kwa Ofisa Lishe wa mpango wa huduma na tiba na Virusi vya ukimwi kwa lugha ya kingereza ‘ Management and Development for Health ( MDH) , aliyejitambulisha kwa jina moja la Charry , kwenye banda hilo na kumjulisha mchezaji huyo kuwa lishe yake ni nzuri licha ya kuwa hana maambukizi ya VVU. Lugha ya alama kwa walemavu wa kutosikia ‘ viziwi’ nayo ilitawala kwenye mabaanda ya maonesho ya wiki ya kilele cha siku ya Ukimwi Duniani , ambayo Kitaifa inafanyika Desemba Mosi, mwaka huu , Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Mipango wa Shirika la Maendeleo ya Watu nchini , ( HDT) ,Malanilo, Simon ( kushoto) akiwa pamoja na Mwandishi Mkongwe nchini na Mkufunzi mshauri , George Nyembela , wa AJAAT , wakitoa maelezo juu ya kampeni ya kupunguza maabukizi ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto walipokutana na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani ) Novemba 30, mwaka huu, ikiwa ni siku ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi, mwaka huu, kitaifa yanafanyika Mkoani Morogoro.
Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Morogoro , SUA, MZUMBE na Chuo Kikuu cha Waislamu wanaunda shirikisho la CCM la Vyuo Vikuu, wakisoma taarifa ya kumpongeza Rais Dk Jakaya Kikwete, kwa kuchanguliwa kuongoza nchi , pamoja na uteuzi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda sambamba na Mawaziri wachapakazi.
Picha zote na John Nditi wa
Globu ya Jamii Mji kasoro bahari






ushabiki wa ndani malinyi

Kama kuna utalii wa ndani, basi hata ushabiki wa ndani pia upo. Jina la Mchezaji wa Timu ya Taifa na Azam United, Mrisho Ngassa , ambaye pia aliwahi kuichezea timu ya Yanga , limekuwa gumzo hadi vijijini, ambapo Basi dogo la Abiria linalofanya shunghuli ya kusafirisha abiria kutoka Mjini Ifakara , Wilayani Kilombero kwenda Malinyi, Wilaya ya Ulanga likiwa limeandikwa jina la mshambuliaji huo mahiri. Picha na John Nditi.


Makamu wa Rais akutana na Mawaziri wa ofisi yake leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Ofisi yake wakati Mawaziri hao walipokwenda Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo, kwa ajali ya kujitambulisha rasmi. kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dk. Teresya Luoga Hovisa, katikati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mhe. Samia Hassan Suluhu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Mawaziri wa Ofisi yake wakati Mawaziri hao walipokwenda Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dk. Teresya Luoga Hovisa katikati Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais Muungano Mhe. Samia Hassan Suluhu.Amour Nassor VPO.


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akutana na wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Bw. Kim Jae-Shin Ofisini kwake Mjini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Bw. Kim Jae-Shin na Balozi wa Korea ya Kusini Nchini, Bw. Young Hoon Kim kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya mazungumzo yao jijini Dar es salaam leo.


MAWAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU WATETA NA WATENDAJI WAO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. William Lukuvi (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Bibi Fatma Mrisho wakati wa mapokezi ya Waziri huyo katika viwanja ya Ofisi ya Waziri Mkuu alipowasili kuanza kazi yake rasmi tarehe 29 Novemba 2010. Nyuma ya Waziri ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Mbonde.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Mbonde akiwatambulisha Mawaziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mary Nagu (Mb) anayeshughulikia (Uwekezaji na Uwezeshaji) na Mhe. William Lukuvi (Mb) anayeshughulikia (Sera Uratibu na Bunge) kwa Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizoko chini ya Ofisi hiyo (hawako pichani), tarehe 29 Novemba, 2010 wakati Mawaziri hao waliporipoti Ofisi ya Waziri Mkuu kuanza kazi rasmi baada ya kuapishwa.


Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mary Nagu (Mb) anayeshughulikia (Uwekezaji na Uwezeshaji) na Mhe. William Lukuvi (Mb) anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Bunge) baada ya kuapishwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 29 Novemba, 2010 waliripotii rasmi katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kuzungumza na Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakizungumza na Viongozi wa Idara, Vitengo na Taasisi zilizoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mawaziri hao waliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa ubunifu, ushirikiano, upendo, uwazi na bidii zaidi ili kukidhi matarajio ya wananchi.

“Kinachotakiwa ni ushirikiano, upendo na uwazi baina ya watendaji na wafanyakazi wote ili kufikia malengo ya Ofisi” alisisitiza Mhe. Mary Nagu.

Mhe. Nagu alisisitiza umuhimu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pasipokuwa na ngoja ngoja ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wawekezaji. Alisema hakuna uchumi wowote duniani uliofanya vizuri bila uwekezaji, iwe wa kutoka nje ya nchi hiyo au ndani ya nchi husika. Alibainisha kuwa Watanzania ndiyo wanaotakiwa kushika hatamu ya uchumi wao.

Kwa upande wake, Mhe. Lukuvi alisisitiza watendaji kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuongeza ufanisi na hatimaye kufikia malengo ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taifa kwa ujumla.

“Tujipange vizuri kufanya kazi kwa ubunifu na kasi zaidi ili kumsaidia Waziri Mkuu kutekeleza majukumu yake na hatimaye Serikali nzima ifanye vizuri kama inavyotarajiwa na wananchi,” alisisitiza Mhe. Lukuvi.

Mapema akiwakaribisha Mawaziri hao, Kaimu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Mbonde aliwapongeza kwa uteuzi wao na kuwaahidi ushirikiano mkubwa. “Tuna imani kubwa nanyi na tunawaahidi ushirikiano na hatutawaangusha,” alibainisha Bw. Mbonde.

Aidha, Bw. Mbonde aliwaeleza Mawaziri hao majukumu makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa ni pamoja na uratibu wa shughuli za Serikali katika Sekta zote na ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, uratibu wa maafa, uwekezaji na uwezeshaji na masuala ya UKIMWI. Masuala mengine aliyataja kuwa ni ya uchaguzi na ya vyama vya siasa.

Ofisi ya Waziri Mkuu hivi sasa inaundwa na Idara saba (7), Vitengo saba (7) na Taasisi nane (8).


Peacock Hotel yaja na usiku wa mtanzania

Mwenyekiti wa Peacock Hotel,Joseph Mfugale (kulia) akizungumza leo katika uzinduzi wa usiku Mtanzania uliofanyika katika hotel ya Peacock,jijini Dar asubuhi hii.kushoto ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Hotel hiyo,Damas Mfugale.
Meneja Masoko wa Precision Air,Emillian Rwejuna akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Peacock,jijini Dar.
Baadhi ya wawakilishi wa makampuni yaliyojitokeza kufanikisha usiku huo wa Mtanzania,toka kulia ni Meneja Masoko wa Tanzania Distilleries Ltd,Martha Bangu,Meneja wa Benki ya Posta,Noves Mosses,Meneja Masoko wa Precision Air,Emillian Rwejuna pamoja na Mwenyekiti wa Peacock Hotel,Joseph Mfugale.Shoo hii inaratibiwa na kampuni ya 1Plus Communications Ltd.
Baadhi ya wanahabari waliohudhuria katika mkutano huo wa uzinduzi wa Usiku wa Mtanzania.

======= ======= =======

Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.

Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.

Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.

Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.

Washiriki wenzetu katika kuunga mkono Usiku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.


ankal ahamasisha wasanii waendeleze libeneke

Ankal akionesha wasanii namna Youtube inavyofanya kazi wakati wa mkutano wa kila Jumatatu wa Jukwaa la Sanaa katika ukumbi wa BASATA Ilala Shariff Shamba jijini Dar. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti, Habari na Mafunzo wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza Lebejo
Kiongozi wa Kilimanjaro Band 'Wana Njenje'
Waziri Ally akichangia mada ya libeneke

Mmoja wa wasanii akitoa yake ya moyoni
Wasanii wengi wanahudhuria Jukwaa
la Sanaa kila Jumatatu ukumbi wa BASATA

Na Aristides Kwizera wa BASATA
Ankal amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani. Mwenyewe anaita kuendeleza Libeneke.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa jana katika ukumbi wa BASATA huku Ilala Shariff Shamba jijini Dar, Ankal aliweka wazi kwamba blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.

Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.

Katika kuonesha kwamba teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.
Pitia intavyuu ya Ankal katika BabKubwa


KUMBUKUMBU

Marehemu Col.Godfrey Kajana Makaya
Leo tarehe 30 November umetimiza miaka mitatu toka ututoke baba mpendwa. Tunakukumbuka sana kanali.
Tunakupenda sana na tunajua upo nasi kiroho mpaka mwisho.
Unakumbukwa na watoto wako, wake zako, na ndugu, jamaa, na marafiki.
Upumzike kwa amani, GK


kajinondozzzzz....

Mtoto EVE DANIEL CHEGERE akiwa amepozi baada ya kula Kajinondozzzz
kidogo cha kumaliza Nursery pale St. Mary's International School- Mwanza Campus tarehe 20/11/2010. Mwakani anaingia Grade 1 hapohapo St. Mary's


african night in michigan saturday december 11, 2010


Come and enjoy the Night with Full of Flavors.
Old School, New Joint, Bongo Flavor, Rumba and other African Hits.
DJ. MENDRAD and other Michiana DJs will drop the hits, come and have funny.
Venue: Honeys Night Club/Cowboy Saloon
405 N. 2nd St
Niles, MI 49120
Date: December 11, 2010(Sat)
Cover Charge: $ 5:00
Time: 10:00 till LATE
NB: Age, must be over 21 to enter.


haja ya hoja

POLISI NA MAGARI MABOVU
YA KUBEBA SARUJI-WAZO

WADAU,
NIMELAZIMIKA KUANDIKA HAYA KUTOKANA NA AJALI ZA MARA KWA MARA ZA MALORI HAYO TOKA KIWANDA CHA SARUJI WAZO NA MACHIMBO YA MCHANGA BOKO NA BUNJU. JUZI ALFAJIRI LORI MOJA LILIACHA NJIA NA KUTUA KWENYE DUKA MOJA PALE TEGETA KIBAONI, HII NI MARA YA PILI NDANI YA WIKI TAKRIBAN MBILI BAADA YA AJALI KAMA HIYO KUTOKEA HAPOHAPO! WAKAZI WA TEGETA NA PAMOAJA NA WATUMIAJI WA BARABARA YA BAGAMOYO TUMEKUWA KATIKA HALI YA WASIWASI KUTOKANA NA AJALI HIZI AMBAZO CHANZO CHAKE NI UBOVU WA MALORI YANAYOBEBA SARUJI NA MCHANGA.

HALI YA KUSHANGAZA;
· KUNA KITUO CHA POLISI NDANI YA ENEO LA WAZO; KWA NINI MAGARI MABOVU HAYAKAMATWI ? JIBU NI RAHISI RUSHWA!
· KWA NINI UONGOZI WA KIWANDA UNARUHUSU MAGARI MABOVU KUINGIA KIWANDANI NA KUPAKIWA SARUJI? KUNA RUSHWA? MFANO; KUNA MAGARI MENGI KWA JINA ' KOMBE' MENGI NE HAYANA HATA BIMA WALA LESENI ZA BARABARANI LAKINI YANATEMBEA KARIBU BARABARA ZOTE ZA DAR KUSAMBAZA SARUJI.
· KIWANDA CHA SARUJI MBEYA( TEMBO CEMENT) HAKIRUHUSU MAGARI MABOVU KUINGIA ENEO LA KIWANDA; KWA NINI WAZO (TWIGA)WASIIGE MFANO HUO?
· KUNA KITUO CHA POLISI ENEO LA TEGETA; KWA NINI MAGARI MABOVU HAYAKAMATWI NA KILA MARA POLISI WAPO BARABARANI? JIBU NI RAHISI RUSHWA!

TAHADHARI KWA KAMANDA WA POLISI DSM NA IGP MWEMA;· MHE. RAIS HUTUMIA NJIA HII KWENDA NA KURUDI KWAO BAGAMOYO HALI ISIPODHIBITIWA TUTASHUHUDIA MAAFA MAKUBWA YA AJALI KATIKA MISAFARA HASA PALE TEGETA KIBAONI NA KWINGINEKO BARABARA YA BAGAMOYO

· POLISI WA WAZO NA TEGETA WAHAMISHWE KWA SABABU WAMEKUWA WAZEMBE KUDHIBITI AJALI ZINAZOHUSISHWA NA UBOVU WA MAGARI YA SARUJI NA MCHANGA YANAYOTUMIA BARABARA YA BAGAMOYO.
Wadau naomba kutoa hoja.
Mdau


Real madrid yapigwa 5 mtungi na barca usiku huu

kocha wa Real Madrid Jose Mourinho hana hamu baada ya kupigwa 5-0 na Barcelona na kuchezewa kama waoto wadogo daika zote za mchezo uwanja wa Camp Nou huko Barcelona usiku huu. 'The special one' leo kawa mdebwedo...
Yaani aibu.... hadi wanarusha hadi ngumi....kadi kibao...kama Yanga vile
Habari kamili nenda BBC SPORT


Wadau wa Arusha wala Nondozz

Mdau Frank Kileo ambaye ni mfanyakazi wa Vodacom kanda ya kaskazini kama MPESA Manager akiwa na Mke wake baada ya kutunikiwa nondozzz ya MBA katika Chuo Kikuu cha ESAMI mjini Arusha.
Mmoja ya Wahitimu wa chuo kikuu cha ESAMI Aika James akiwa kwenye tafrija baada ya kutunukiwa nondozzz ya MBA.
Mdau Riziki Mwalupindi akifungua Champaigne kama ishara ya ufunguzi wa hafla fupi ya kumpongeza Frank Kileo baada ya kutunukiwa nondozzz za MBA katika chuo cha ESAMI tarehe 27/11/2010 katika hotel ya OlDIVAI GAUGE Arusha.


NEWS ALERT: MUHIDIN MAALIM GURUMO ATOKA ICU

Mwanamuziki wa siku nyingi Mzee Makasy akimjulia hali mwanamuziki mwenzie Muhidin Maalim Gurumo (KAMANDA) aliyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili. Uncle Gurumo yupo wodi ya Mwaisela namba 1 kwa sasa baada ya kutoka katika chumba cha wagojwa wenye uangalizi maalumu (ICU). Kunradhi kwa picha haionekani vizuri.Picha na mdau Rajab Mhamila.

Globu ya Jamii inamtakia Kamanda Gurumo nafuu ya haraka na inatoa wito kwa wapenzi wa muziki kujitokeza kumsaidia mzee wetu huyu ambaye ni mmoja wa wanamuziki wachache waliosalia wakiendeleza fani kwa weledi wa hali ya juu huku ukikuza vipaji vipya kwa wakati huo huo.

Wakati huo huo, Rais

Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu, Novemba 29, 2010, amemtembelea hospitali na kumjulia hali mwanamuziki mkongwe wa Tanzania, Bwana Muhidin Gurumo, ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Bw. Gurumo ambaye amelazwa Wodi Mosi, Mwaisela, amekuwa hospitalini hapo tokea Alhamisi iliyopita, Novemba 25, 2010, akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Rais Kikwete amekaa na mwanamuziki huyo kwa kiasi cha dakika 15 na baadaye madaktari bingwa wa moyo wa MNH wamethibitisha kuwa hali ya Bw. Gurumo imetulia na kuwa akiendelea na hali ya sasa anaweza kutolewa hospitali wiki ijayo.

Rais Kikwete ambaye baada ya kumjulia hali Bw. Gurumo alitaka kumtembelea na kumjulia hali mwanamuziki mwingine, Bw. Remmy Ongala, ambaye naye amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matatizo ya figo.

Hata hivyo, Rais Kikwete amejulishwa kuwa Bw. Ongala wakati huo alikuwa nje ya wodi yake kwa ajili ya kufanyiwa vipimo katika sehemu nyingine ya hospitali hiyo. Bw. Ongala naye amelazwa Wodi ya Sita, Mwaisela hiyo hiyo.

Kwa miaka mingi, wanamuziki hao wawili wenye vipaji vikubwa vya muziki wametamba katika muziki wa Tanzania. Bw. Gurumo amekuwa nyota wa muziki katika Tanzania tokea miaka ya 1960 na amepigia ama kuongoza baadhi ya bendi maarufu za muziki katika Tanzania zikiwamo za NUTA (baadaye JUWATA na OTTU) ambayo sasa inaitwa Msondo Ngoma Music Band, Orchestra Safari Sound (OSS) na DDC Mlimani Park (Sikinde).

Naye Ongala kwa miaka mingi aliongoza bendi ya Super Matimila, kabla ya kuingia katika muziki wa Gospel.




Idadi ya watu
Idadi ya watu
eXTReMe Tracker