Mnadhimu Mkuu (Chief of Staff) wa JWTZ
Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo akiongea leo

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Jeshi la Wananchi wa Tanzania litafungua Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa kitakachotoa Mafunzo ya Udhamili wa Stratejia ya Ulinzi na Usalama kwa muda wa mwaka mmoja ifikapo tarehe 10 Januari, mwaka huu katika maeneo ya kunduchi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Abdulrahman Shimbo amesema elimu hii haikuwahi kutolewa hapa nchini na waliohitaji elimu hiyo waliipata nje ya nchi.

“Elimu hii ilikuwa haipatikani hapa nchini na wote waliobahatika kuipata iliwaladhimu kwenda katika nchi za nje ambapo gharama ni kubwa sana kwa mfano mimi nimesoma elimu hii kwa fedha za kitanzania milioni 80.’’ Amesema Shimbo.

Mnadhimu Mkuu Shimbo amefafanua kuwa chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 60 kwa mwaka lakini kwa kuanzia chuo hiki kitachukua wanafunzi 20 tu.

Chuo hicho kilichoanza kujengwa Machi mwaka jana na kumalizika Desemba mwaka huo huo ni mahsusi kwa maofisa wa ngazi za juu za polisi, uhamiaji na jeshi.

Kufanikishwa kwa ujenzi huo kumetokana na ufadhili wa Serikali ya Tanzania na china ambapo mpaka sasa Tanzania imetumia kiasi cha fedha za kitanzania bilioni mbili na china imetoa takribani dola za kimarekani bilioni tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Dola za kimarekani bilioni tatu au ni milioni tatu? Bilioni tatu dola sio mchezo matatizo ya nchi mbona yanaweza kuisha!! Bush alitupatia milioni mia saba tu, lakini ni nyingi sana kwa msaada.

    ReplyDelete
  2. Chereko chereko Serikali, hiki chuo ni kizuri kama lilivyokua wazo la kukianzisha.

    Kimsingi inasaidia sana kuokoa fedha za walipakodi mambo haya tukifanyia hapa hapa nchini.

    Hata hivyo nadhani hata kikiwa kinaoperate katika maximum capacity mbona watu sitini ni kidogo sana.

    Majengo kule kunduchi ni kuvutia sana na imesaidia kupandisha hadhi eneo la Kunduchi Bahari Beach.

    Serikali imejitahidi sana twatarajia kuviona vyuo na initiatives za namna hii nyingi tu.

    Mdau
    Kwa Kondo
    Kunduchi.

    ReplyDelete
  3. Tanzania imetoa Tshs Billioni 3 na China imetoa Tshs Trillioni 3.6 ndiyo Tshs Trillioni 3.6(Dola Billioni 3), nadhani mtoa habari amezidisha maji ktk unga.

    Hata hivyo ujenzi wa Chuo hiki ni hatua nzuri, maana mambo nyeti ya kiusalama lazima yatolewe humu humu nchini Tanzania kwa sababu za kiusalama.

    ReplyDelete
  4. mi nadhani tuna-complicate mambo..hakina faida yoyote kwa sasa..matatizo ya usalama wa watanzania mengi yapo kwenye huduma muhimu kama hakuna maji salama wala watoto wetu hawapati chakula bora..hayo ndo mambo hizo hela zingefanyia kazi,Dar es salaam maji hakuna,umeme wa shida nyie mnaomba msaada wa chuo cha kijeshi!!!!!!!!!!!!!kuna kitu kwa kingereza kinaitwa Priotization hapo naona hakuna..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...