Kaka Ankal na Wadau
Hebu angalieni hii aibu ya Kigoma Airport
na hicho kiingereza hapo mlango mkuu wa kuingia uwanjani.
Mdau David Mziray

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. Haha hahah this is so funny....Ndio maana ajira hamna bongo...Wasomi wako kibao lakini kazi wanagawiana wao kwa wao.. matokeo yake ndio haya...Tenda ya kuandika hayo matangazo alipewa mtoto wa mjomba.... ?????

    ReplyDelete
  2. Hahahaaaaaaaaa ankal na wadau wako wanaokutumia haya mavituzzzz noma!
    Unajua nimeshapita sana hapo uwanjani lakini wala sijawahi kuangalia juu. Hii kweli noma. Nadhani Mkuu wa wilaya Mh. Mongella atarekebisha aibu hii kwa taifa. Ankal hii ndio inayokuweka juu ya mabloga wengine. kukaribisha mambo toka kila pembe ya nchi na dunia kwa jumla. Hahaaaaaaaaaa nimecheka hadi nimepaliwa. JAMANI!

    Auntie Sheba
    Frankfurt

    ReplyDelete
  3. Halafu usikute watu walioandika hapo wanamcheka Kanumba wa watu masikini...

    ReplyDelete
  4. Holly cow, thats what im talking about, welcome to the club,ina nikumbusha enzi zile za ZEE KUKU ZE BATA, iko siku pale mwana nyamala mzungu aliuliza i need rice and meat, Mmatumbi akajibu samahani mzungu raisi yuko ikulu kulee na ana ulinzi mkali kweli kweli lakini miti hipi hapo uani karibu na jalala la Ustadhi Hemed!!! Bongo bwana tambarare kweli kweli... huku tuapoelekea watu wanakuwa mabingwa wa riverse walakhi tena... Kwee kwee kwee!!!! Home sweet Home

    Mdau

    Toronto

    Canada

    ReplyDelete
  5. Hahahaha!!!!!mimi Maimunaa,nimesema maimunaa....hahaha!!mama mbavu zanguuu!!!kwi!kwi!kwi!

    ReplyDelete
  6. Si ndio hapa ambapo Mhe. Dr Zitto Kabwe anapita kila siku?!! Au ninakosea.

    ReplyDelete
  7. Jamani!kweli tuna safari ndefu kufika kule wenzetu walipo, ningependa kujua kiwango cha elimu ya Meneja wa uwanja...

    ReplyDelete
  8. Wadau mbona mmenoti kingereza tu kilivyokosewa lakini hamna anaecomment kuhusu kiswahili pia kukosewa

    ReplyDelete
  9. TANZANIA AIRPORT AUTHORITY MPOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! WAPI AFISA UTAWALA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! SHAME ON YOU.

    ReplyDelete
  10. Hii Kali.... lakini hata huyu aliyepost hii msg naye amenichekesha sana kwa kusema "UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA INTERNATIONAL AIRpot..." makosa kibao.

    ReplyDelete
  11. This is too much

    ReplyDelete
  12. yaan nimecheeeeeeeka mpaka basi,mdau big up

    ReplyDelete
  13. wala sishangai,ndo ulimbukeni wa watu tuliowachagua na waliopo maofisini

    ReplyDelete
  14. HII NDIYO TANZANIA, MA PROFESA KIBAO WAMEJA JAZA MATUMBO TU, WANAONA LAKINI HAKUNA ANAYECHUKUA HATUA HATA YA KUSHAURI....

    ReplyDelete
  15. Jamani hii ni kweli au mwenzetu kaamua kutengeneza kitu chake? tuulize mwingine aliyeshuhudia? isije ikawa hadithi za mtu kuota manyoya.Please let us be serious and inform the authority. Siyo aibu ya aliendika bango peke yake ni sisi WATANZANIA wote whether upo TORONTO, FRANKFURT, ARUSHA, AU HAPO KIGOMA KWENYEWE TUCHUKUWE HATUA KUJIREKEBISHA WENYEWE. TUSIISHIE KWIKWIKWI TU!!!!!!

    MWNAKIGOMA

    ReplyDelete
  16. Inachekesha na kukosea lugha katika hali ya kawaida siyo tatizo. Ila katika sehemu kama hiyo kupatikana kwa udhaifu huo kunamaanisha yafuatayo.

    1. Huduma zinazopatikana hapo hazina ni mbovu na hakuna anayejali
    2. Upatikanaji wa kazi/Tenda hapo hautegemei uwezo wa mtu kumudu kazi hiyo, bali kujuana, rushwa nk.

    List inaendelea!

    ReplyDelete
  17. hahahahahah! Jamani...mimi hata siamini kama ni kweli! Hee hivi inawezekana kabisa kuwa na tangazo kama hilo! Basi iko kazi!

    ReplyDelete
  18. WAHESHIMIWA WABUNGE NA VIONGOZI WENGINE WA SERIKALI IKIWA NA WANAUSALAMA RAISI ANAPOTUMIA UWANJA HUO INAMANA HAWAJA NOTISI MIAKA TOTE HIYO,KISWAHILI PIA KIBOVU KIMETUMIKA HAPO.

    ReplyDelete
  19. PASSANGARS ONLY damn english

    ReplyDelete
  20. Makubwa haya, sasa hata kama akina brother Kalumanzira mnajiita brother K hapa mmezidi jamani. Watendaji wote katika uwanja huu mjisikie vibaya, hii ni aibu. Tujifunze kupenda kazi zetu. Meneja wa uwanja kwa kweli upo kama vile haupo. Tubu na anza kupenda na kuheshimu kazi yako

    ReplyDelete
  21. Aisee meku eeh..hii kwakweli sasa imesi...imesidi kweli!.maana hapa ni fichekesho fitu;;..fitupu kweli!.Unajua meku..hapo tatiso ni wa tu wengi sana..yaani tatiso linaanzia kulee darisalama kwa huyo mkuu wa fiwanja fya ndeke,kule kigoma pia,wale wote waliowahi kutumia uwanja huo kwa safari sao mbalimbali,na Watansania wote kwa ujumla..yaani wote kabisa ni mambumbu..!mambumbumbu kweli..!!.Pole yetu sote meku,yaani ni aibu tupu msee wangu!

    ReplyDelete
  22. Jamani mimi kwetu Kigoma Ujiji. Naskia kichefu chefu kwa hilo tangazo. Hata sielewi imekuwaje, utadhani airport ya mshihiri mmoja na siyo ya wizara husika

    ReplyDelete
  23. Mi sioni tatizo la mwandishi- ninachoona ni upepo unavyovuma katika siasa za tanzania. unasikia ziiiii kila upande wa sikio lakini ukigeuka huoni kitu. Wanasiasa haijalishi huyu ni kiongozi mdogo, kiongozi wa watu, kiongozi wa tumbo ama kiongozi fisadi. wote wanatazama kwa mbali ni jinsi gani watastaafu, halafu watoto wao watawaongelea vipi watakapokuwa wanakula pensheni zao na kujinadi kuwa wao walikuwa wa kwanza kipindi wanasoma huku wanakunywa glasi za bia kama si mvinyo. kutokana na hilo basi, miaka mitano ya Mheshimiwa Zitto kabwe na wengine wote ni utundu uliovuka mipaka kama hawakuona boriti hili kabla ya kuinadi Kigoma kuwa ni sehemu nyeti katika uchumi wa Tanzania. na msishangae hili, kwani hili ni la musa, la firauni ni hasira za maprofesa baada ya kuona wenzao waliokimbia taaluma na kuingia kwenye siasa watastaafu salama na vibindo vya fedha ndogondogo(mpya)wakati wao wanaendelea kuwa ngazi na madaraja ya watoto wa wanasiasa waliokuwa wafanyakazi wenzao.
    Tanzania, tanzania, nakupenda kwa moyo wote.....

    ReplyDelete
  24. Kawaida lazima uanze na kichwa cha habari(Title) na unapotumia lugha mbili basi uanze na lugha inayotumiwa zaidi na wenyeji a.k.a lugha mama(kiswahili);

    ILANI/NOTICE:
    Abiria tu ndio wanaoruhusiwa kuingia.
    Entrance is to passengers only.
    Adhabu ni dola 100 endapo amri itakiukwa.
    The fine for violation is 100USD.

    David,Kimara DSM,Tanzania

    ReplyDelete
  25. hahahaha Jamani eeeh, na sisi Tanzania tunaanzisha Dialect yetu ya English taratibu taratibu kama Nigeria,Jamaica n.k
    Tujitahidi kwakweli hahaha Khaaaa, Yaani Watalii hao watakuwa na mengi sana ya kusimulia wakirejea kwao hahaha

    ReplyDelete
  26. FAIN tehteh hata wewe umekosea kichwa cha habari AIRPOT umeandika

    ReplyDelete
  27. Je, kama aliyepewa tenda ni mtoto wa mjomba, akichemsha basi imetoka? Waheshimiwa wanaopita hapo kila siku si lazima wasome tangazo hilo. Lakini wana-usalama wanakagua kila sehemu ya jengo hilo mara kwa mara. Je, wamesharidhika na kilichoandikwa hapo? Au labda nao ni watoto wa mjomba! Ungependa kujua kiwango cha elimu ya Meneja wa uwanja! Kama naye ni mtoto wa shangazi je, itakuwaje, utazimia?

    ReplyDelete
  28. Hicho ni Ki-Faransa, Ki-Belgiji au Kingwana ?

    ReplyDelete
  29. namuomba mdau aliyetuletea hii habari arudi tena atuletee walivyobadilisha,
    naungana na aliyesema kazi za kupeana ki ndugu,ina wezekana kabisa watu walishakosoa lakini aliye mleta mwandika bango akawa kichwa ngumu,HATAKI KUKOSOLEWA
    patrick Mwamlima
    Moshi

    ReplyDelete
  30. HUYO JAMAA HATA KISWAHILI KIMEMPIGA CHENGA ABIRIA TO HAJAANDIKA TU.

    ReplyDelete
  31. Hili ni jambo la aibu na kusikitisha sana,Inadhihirisha jinsi watanzania tusivyojali kazi zetu na kutokutilia maanani mambo yoyote ya maana au ya maendeleo,Kazi yetu hasa ni starehe,ruswha,ngono nk.Inaonekena kuwa tangazo hilo limekuwa hapo kwa siku nyingi na watu wengi wakiwemo viongozi wa serikali,wasomi nk.wamepita na kuliona tangazo hilo,lakini kutokana na tabia zetu watanzania za kutojali kila jambo matokeo yake ndiyo haya,na hili silo kosa la kwanza na siyo Kigoma peke yake,ukifuatilia sehemu nyingi utakuta upuuzi huo huo,tofauti na nchi za wenzetu kama Kenya,Uganda,Zambia,Zimbabwe nk.huwezi kukuta makosa kama haya.Watanzania tujitahidi kujikomboa kotoka katika ujinga huu kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
    mdau Marekani.

    ReplyDelete
  32. alieandika hilo bango alikuwa amelewa

    ReplyDelete
  33. Bongo tumeiua elimu, matokeo yake ndio haya. Kichekesho kama hiki kinasameheka kama mtu atakiona kwenye biashara zetu uswahilini, lakini sio uwanja wa ndege ambapo kila aina ya wageni wanapita.

    ReplyDelete
  34. Ha ha ha ha ha haaa!!!!! Kwiii kwi kwi kwi kwi!!! Tehe tehe tehe tehe!!! Jamani mbavu zangu mie! Halafu tukiambiwa Watanzania wajinga tunataka kuzichapa.

    ReplyDelete
  35. Hivi...kwanini Watanzania tunapenda kucharge kila kitu kwa Dollar (USD). Au hatuthamini Shillingi yetu.....hata kama mtu ana Dollar yake, mfanye aibadilishe ili alipe hiyo faini kwa pesa ya madafu....mwishowe tutaanza kuuza kila kitu kwa Dollar sasa (kama bado!!!).

    ReplyDelete
  36. Ha ha haaa you will eat until you say, brother hasheem dont kill me with food!!

    ReplyDelete
  37. nani kawaambia hicho ni kiingereza na kiswahili? hamjui kuwa kigoma kuna lugha mchanganyiko za kigeni kiasi kuna lugha mpya ya "taifa" huku? nani kawaambia kigoma wanatumia english na swahili? hebu njoni muone wenyewe! kuna mji ambao kuna shule ktk tanzania hii ambao una shule (primary to high school) ambayo ni French Medium? basi kigoma ipo, mkitaka kujua huku sio "Tz". Kaeni na linchi lenu na mtuachie kwetu!

    From Kasulu!

    ReplyDelete
  38. he he he he he kazi kwei kwei wabongo kingeleza kinawapiga chenjii.

    zee besdei faza mazaaa kazui kawei kwei

    ReplyDelete
  39. mmh hapo airport kama kulivyo kama gheto la msela fulani hatari,kwa muonekano wake hiyo lugha iliyotumika inastahili.

    kigoma usikute alipewa tenda mkimbizi kutoka burundi,bora angeandika kifaransa tu.

    **abiria TO wanaruhusiwa kuingia** my favourite line

    ReplyDelete
  40. Mbona kila mtu anasema Watanzania kiingereza kina wapiga chenga! Lakini kwa mtazamo wangu hata kiswahili kilichoandikwa siya sahihi lakini Watu wameona Kiingereza tu.Cha kustaajabisha Mzungu (Mu- ingereza) akikosea hatii aibu wakati ni lugha yake amezaliwa nayo na hajui lugha nyingine yoyote.Wao wanakosea sana kupita hata sisi kwa mfano neno beutiful linatumika kwa mwanaume,myama hata kikombe!Tofauti na sisi ambao tunaouwezo wa kuongea lugha zaidi ya mbili naamini kila Mtanzania anaongea lugha angalau mbili kiswahili na Traditional language.

    ReplyDelete
  41. Welawelawelaaaaaaaaa!.....Kwa taarifa tu aliyeandika hapo ni POLISI kutoka DODOMA ambaye alimgonga kwa makusudi na gari yao mwanachuo anayesomea ualimu chuo KIKUU {UDOM} siku ya maandamano wk iliyopita.NIMTAJE WADAU?????...Poa lkn hayo ndo madhara yanayokuja taratibu km mbuyu unvyoanza.Tupige magoti tusali.......Jamani namaliza kuandika msg hii kisha nazimia ili nitende haki ya MSHTUKO HUU WA FUNGUA MWAKA.

    ReplyDelete
  42. Hii inabidi tuipeleke kwenye mtandao wa www.engrish.com

    ReplyDelete
  43. MWANDISHI WA BANGO LILE ALIAGIZWA TOKA NG'AMBO YA ZIWA LUGHA ANAYOFAHAMU NI LINGALA NA KIFARANSA CHA MTAANI!!!

    ReplyDelete
  44. Kukosea kupo lakini maandishi haya yana muda mrefu sana, naomba uongozi wa uwanja kufanya mabadilko haraka na ikiwezekana ifanyike ukaravati mkubwa kwa kuwa hata hali ya uwanja hairidhishi kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...