Hili ni gari pekee linalotumika na kikosi cha zimamoto katika uwanja wa ndege wa Nduli,Mkoani Iringa.Wadau mnaliongeleaje hili?? (Picha na Mdau Francis Godwin)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. wao!gari la fire?du!

    ReplyDelete
  2. haki ya nani..naomba nisiseme

    ReplyDelete
  3. gari chokesti mbaya linatia aibuuuuuuu yani hii nchi puuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  4. Tehe teh tee te!

    Huu si utani huu jamani? Hilo gari la Fafa hata lita 10 za maji hazifiki sasa mdude kama huo ukilipuka ndo utaweza kuzimwa na hizo lita 30 zilizobebwa humo kwenye hiyo PIKAP?

    Khaah!

    ReplyDelete
  5. Bongo tambarare !!!!

    ReplyDelete
  6. Hilo gari lenyewe linatakiwa litupwe tena ni aibu kwakweli na haliwezi kuzima moto kama umetokea kweli moto!Hilo gari lingekuwa ichi za wenzetu lisingepewa kibali tena cha kutembea!

    ReplyDelete
  7. Tuache utani na mambo ya msingi.

    ReplyDelete
  8. This is a real plain joke. In an incident of fire will this 1986 Datsun so called fire tank manage to battle with a blaze from the plane on the ground? Please it is time for related ministry to be serious and provide fire equipments which can save people lives.

    ReplyDelete
  9. Hii kwa kweli ni aibu kwa taifa, Je ni sawa kwa mkuu wa mkoa huo kutembelea V8 huku uwanja wake wa ndege hauna gari la zima moto? Wadau hebu wenye data, gari la zima moto ni shilingi ngapi? Je mkoa na wilaya zake una magari ya zima moto au ndio tunategemea kudura za mwenyezi mungu.
    Viongozi inabidi kuamka.

    ReplyDelete
  10. mbona poa sana...,uwanja wa ndege huku kwetu Mbambabay na Liuli tunazima kwa maji ya kwenye madumu!

    ReplyDelete
  11. HIKI NI KICHEKESHO!!!!!

    ReplyDelete
  12. Acheni ku complain...... Kitu new model hiki

    ReplyDelete
  13. Uwanja wenyewe mbovu, ndege zinazotua na kuondoka hazipo, wasafiri wa ndege wa msimu, sasa gari kuuuuuuuubwa na la kisasa la fire la kazi gani???????????????????
    Ndege ndogo moja ya abiria 10 inatua uwanjani hapo mara moja baada ya miezi miwili au mitatu. Hilo gari la fire la kazi gani?

    ReplyDelete
  14. Bongo kila kitu ni kuomba mungu. Alafu kuna mkurugenzi wa viwanja vya ndege. Kwa wao maadamu Dar es Salaam kila kitu kiko shwari basi huko kwingine ni "non of their business". Hapa najua lawama zitakwenda CCM lakini ukweli mkurugenzi wa viwanja vya ndege ndiye mhusika mkuu. Hawa viongozi wawe na aibu jamani lol!!!

    ReplyDelete
  15. WANASUBIRI CHAKUTOKEA KITOKEE THEN WAUNDE KAMATI YA UCHUNGUZI YA WATU 50. ULAJIIIIII HUOO

    ReplyDelete
  16. pick-up WALIUZIWA NA MJESHI MSTAAFU JINA KAPUNI ILA TULO WAHI ISHI IRINGA MTAKUMBUKA TZJ 1445....

    ReplyDelete
  17. lazima hizi...habari hii ni yakusikitisha sana...je rais anajua habari hizi au anasoma hii blog yako kaka michuzi anaona hii aibu?je watu wakiandamana kudai haki zao ni makosa?lazima wawajibike suala kama hili la hatari kuweka fire ya mapipa ndani ya pick up..anyway mungu ibariki tanzania na watu pia..ameen

    ReplyDelete
  18. Haya ndugu watanzania hii ni haki? Angalieni matumizi ya ikulu kwa siku muheshimiwa katika misafara yake ndani jiji la dar es salaam magari 15 ni kiasi gani cha mafuta anatumia, Leo hii mbunge anapewa million 90 kwa ajili ya usafiri bado marupurupu mengine lakini wanaridhika na wala hawajali wanapoona gari kama hilo kwenye uwanja wa ndege mimi nasema hii iwe mifano hai ya serikali yetu iliyo madarakani na mkubali kuwa kuna makataba Mdau hapo juu haoni thamani ya gari la fire hapo kiwanjani ki taaluma kila mkoa inabidi kuwe na uwanja lakini utaona kama rais ataelekea huko kwa ndege hata hayo mashimo hutayaona watu wanao thaminiwa nchini kwetu ni viongozi tu na familia zao wengine hatuna mpango si ndiyo kama ndege itawaka moto au iingie kwenye mishimo hiyo hakuna noma, UJUMBE MSIWAPE TENA KURA ZENU AMKENI NYIE WATU kama kuiba imetosha maana hapa ni ufisadi hakuna lingine, mdau

    ReplyDelete
  19. KITENDA WILI

    Wasemaje umuonapo mtoto awinda tembo na manati?

    This is a joke until some catastrophic event, then its blame game time
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  20. hilo gari la fire kituko kiukweli nchi hii bado hatuko serious

    ReplyDelete
  21. Jamaa amekosea, hiyo pickup ilipeleka ulanzi kwa ajili ya kuuagiza Dar kwa Wanyalu wa huko na hasa mbunge wa Idodi

    ReplyDelete
  22. Tunacheza na maisha ya watu hata kama kiwanja kinapokea watu wawili maisha yanabaki kuwa palepale na thamani yake. hivi ndege ikiungua tume itakula bei gani kuchunguza chanzo ambacho police pekee wanaweza kuchunguza kwa gharana ya mshahara wao tu. Tanzania zaidi ya uijuavyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  23. kama uwanja hauna gari la faya sababu hakuna ndege zinazotua mara kwa mara, si dhani kama kuna haja ya kuwa na gari la gharama kuwa hapo muda wote, ila hata hivyo nimeshaona gari la faya (landrover) used hata kwenye show room za magari bongo, yaani ndio mkoa unashindwa kununua?mamlaka ya viwanja vya ndege je?wizara husika ya ujenzi je?ina magari mangapi?haiwezi kununua gari la zima moto hata kuukuu?

    Na huyo aliyetoa agizo la hilo pik up la madumu kubeba maji ya kuzimia ndege?its a joke! hilo gari halifai hata kubeba mbege toka machame kwenda moshi mjini! isingekua busara kuhakikisha gari la fire la mkoa kuwa hapo airport muda wa hio ndege kutua na kupaa tu?nafikiri hio ingekua akili zaidi!au hata mkoa hauna gari la fire?

    mi nimechoka, ila YANAMWISHO!

    ReplyDelete
  24. JAMANI JAMANI JAMANI,HIVI WANAOHUSIKA SI WASOMI NAWAMETEMBELEA VIWANJA VIKUBWA NA WANAJUA SHERIA ZA VIWANJA VYA NDEGE?

    LINI TANZANIA TUTAAMKA? UONGOZI JAMANI SIO KUVAA SUTI NA KUENDESHWA KWENYE SHANGINGI,

    HAYA BWANA, IMEANZA TUNISIA, MISRI, LIBYA LETS SEE WHAT NEXT.

    ReplyDelete
  25. Good lord no! This is a huge joke...jamani jamani hii nchi...hivi lini wahusika watakuwa serious? Tanzania hoo hata pale International Airport ikitokea issue ambayo emergency respond inahitajika quickly just to save lives, maisha ya watu yatapotea kwa sababu ya mzaha!

    ReplyDelete
  26. Serikali inazo fedha za kukopesha mashangigi lakini kwenye mambo ya usalama wa raia na mali zao,Serikali hiyo hiyo haina hela!! Ngoja nikae kimya nisije ambiwa navuruga amani.

    Mdau ( USA)

    ReplyDelete
  27. hayo mandege natumaini yanalipa ushuru wa kutumia huo uwanja..Wanaochukua hiyo hela wawajibishwe. Na mimi ningekua insurance agent ningehakikisha ndege yenye safari za huko insurance yake ni kubwa sana.

    ReplyDelete
  28. mi nafikiri hata hawa polisi wangejiuzulu au waache kazi maana kama ndege ikiwaka wataambiwa waandike maelezo sasa kama hali ndo hiyo maelezo ya nini pili naomba kuuliza hivi iringa kuna safari za ndege kama kuna mdau anajua anijuze

    ReplyDelete
  29. Bongo tambalaleeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  30. Mi napinga vikali wanaposema akili ya mtu mweusi haina maarifa,lakini kwa mtaji huu nashindwa kutetea point yangu ukizingatia serikali imenunua private jet kwa bei si ya kitoto.Haya private jet imeland nduli airport alafu ikaanza kuwaka itakuwaje hapo??

    ReplyDelete
  31. Yaani bongo kila kitu ni mazingaombe,reality hai exist

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...