JK akiifariji familia ya Marehemu Shekhe Kassim Mtopea aliyefariki jana nyumbani kwake Temeke, jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Rais Kikwete alifuatana na mkewe Mama Salma Kikwete. Marehemu Shekhe Mtopea alikuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM na tangu mwaka 2002 hadi 2007 alichaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo,Mjumbe wa Kamati ya Siasa kata ya Azimio,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.Marehemu ameacha mjane mmoja watoto kumi na mbili na wajukuu ishirini na moja.
JK akizungumza na kuwafariji waombolezaji na ndugu wa Marehemu Shekhe Kassim Mtopea wakati a lipokwenda nyumbani kwa Marehemu Temeke jijini Dar es Salaam kutoa pole kwa familia na ndugu leo mchana.
JK akisalimiana na baadhi ya watoto baada ya kuifariji familia ya marehemu Shekhe Kassim Mtopea nyumbani kwake Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. muheshimiwa si umeona michoro ya tanroad kwenye ukuta haya basi linda familia ya marehemu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...