Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai Mh. Freeman Mbowe leo wakati wa sherehe za Siku ya Sheria nchini katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. This is one good photo. I was dying to see some unity between these two parties especially after the elections. Big up Mr. Mbowe you made my day.

    ReplyDelete
  2. Duh! hii kali ya mwaka kaka mithupu. Big up.

    ReplyDelete
  3. Nyinyi msiojua siasa basi ndio hii..... mtaumia bure!!!

    ReplyDelete
  4. Ndio demokrasia hiyo ikumbukwe upinzani sio uadui na hata chadema walipo hojiwa walisema hawana chuki na Rais na wanapingana na mfumo that is why walitoka bungeni. Hivi huyu jamaa hana pamba nyingine maana kila time magwanda.

    ReplyDelete
  5. Oh my god! baada ya kunji lote la kutoka nje ya bunge leo tumefika hapa? Chadema kweli wamekomaa sasa. safi sana mbowe. you the hero.

    ReplyDelete
  6. Mbowe bado yupo kwenye Kampeni? Haya, 2015 siyo mbali, goodluck!

    ReplyDelete
  7. Hicho kicheko cha kweli au cha kupigia picha tuuuuu

    ReplyDelete
  8. wasiojua siasa hii ndio siasa mnachonga sana watu msiojua makoo yatawauma sanaaaaaaaaaaaa shaurizenu hakuna uadua hapo maneno kibao mmeona sasa?mtajaza na chuki zenu

    ReplyDelete
  9. Don't be fooled by smiles read the BODY LANGUAGE!!! angalia mkono wa Kikwetwe na position ya mwili wake unasema 'let my hand go, pls don't touch me' very uncomfortable; normally mkono shoto wa Kikwete ungekuwa umeshika bega la Mbowe. On the other hand, Mbowe is 100% committed to that greeting.

    ReplyDelete
  10. yan kwa moyo mweupee Mh.Mbowe anampa heshma yake mkuu. viongozi wa chadema ni werevu sana. mnastahili kuongoza TZ.

    ReplyDelete
  11. Nakubaliana na Anoy,Wed Feb 02, 08:53:00 PM 2011

    ReplyDelete
  12. Tatizo la sisi Wabongo (sijui kama ni rika zote - wazee na vijana)hatupendi kusoma habari au kusikiliza habari za matukio kwa makini: tokea awali CHADEMA walishaeleza vizuri sana kuwa HAWANA CHUKI na JK kama JK, bali wana usongo na mfumo wa uchaguzi usiotenda haki na katiba. Waliposusia hotuba ya JK ilikuwa ni njia muafaka ya kufikisha huo ujumbe, ambao (kama mnafuatilia masuala ya siasa kwa makini) ndio umefungua mjadala wa kitaifa kuhusu MABADILIKO YA KATIBA (ambayo hata JK mwenyewe ameridhia hoja). Jamani fuatilieni siasa kwa makini!! Picha hii inaonesha aina fulani ya muafaka: Mbowe alisusia hotuba, ujumbe ukafika, JK akaridhia hoja (ambayo inaendelea kujadiliwa hadi vijijini). That's the beauty of politics.

    Mdau unayezungumzia pamba: kila vazi ni pamba - JK amevaa sare ya global capitalism na Mbowe amevalia sare ya chama chake. Zote ni sare na zote ni pamba!!!

    ReplyDelete
  13. Mh, waTZ Bwana, kweli mna chuki na JK wetu za bureee nimegundua! sasa hapo hizo big up saana kwa Mbowe ni zipi hasa? It takes two to tango! Kelele zoote za Chadema bado wanapata mwaliko kwenye shughuli za kiserikali. Mpaka Mbowe kuwepo hapo ina maana kaalikwa, sasa hapo mkomavu kisiasa nani? Acheni hizo mnatuchosha sasa

    ReplyDelete
  14. Ukisitajabu ya musa utayaona ya filauni, Kele kele za mlango hazimzui mwenye nyumba kulala, Jana ulisema JK sio Rais leo unasema nini? Kazi kwenu,ila angalie msichafue hali ya hewa wala usijeruhi mtu.

    ReplyDelete
  15. Lazima JK aogope maana maneno ya chuki ni mengi mno, ila hata hivyo kumbukeni, mafahari wawili wapiganapo ziumiazo nyasi, sasa hawa wanacheka lakini ukienda kwenye vijiwe vya walala hoi, CCM na chadema hakuna kusemeshana! Tujifunze kuheshimu Amani Mungu aliyotupatia, hasa sisi watu watu wa chini, maana chokochoko zinaanzia kwetu, hao huko juu hawana neno, wanapingana bila kupigana, lakini huku chini tunauana wengine hata Kikwete hatujawahi kumwona kwa macho lakini du, iko kazi

    ReplyDelete
  16. Inasemekana huyo kaka mvaa magwanda analazimisha hiyo salamu,watu wamemshitukia anabembeleza ili mzee amkingie kifua kwenye kesi yake na nssf.Hapo hakuna ukomavu wa siasa bali ni janja yake tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...