Waziri i wa Maji Prof.Mark Mwandosya akiwa na furaha baada ya kada wa C.C.M Mustfa Sabodo kumhakikishia kuwa ametenga takriban Sh 1.8 kugharamia uchimbaji wa visima. Mh.Waziri alimtembelea Mzee Sabodo nyumbani kwake Upanga jijini Dar leo.

Waziri wa Maji Mh.Mark Mwandosya amemtembelea nyumbani kwake kada wa C.CM Mustafa Sabodo na kumshukuru kwa msaada wake wa kusaidia uchimbaji wa visima vya maji 600 nchi mzima.Akimshukuru kwa niaba ya Serikali Waziri Mwandosya alisema kuwa, yeye binafsi anashukuru kwa mchango mkubwa ambao bwana Sabodo anasaidia Serikali katika kutatua matatizo ya maji. ‘’Kimsingi msaada wako unaendeleza tuu sera ya kuwapatia wananchi maji safi na salama kwa hilo mzee Sabodo tunakushukuru’’ alsema Mh. Waziri.

Kwa upande wake Mustafa Sabodo alimueleza Mh.Waziri kuwa ,ili kukamilisha azma hiyo ametenga bajeti ya Sh 1.8 bilioni kugharamia uchimbaji wa visima hivyo. ’’kawa sababu umekuja kunishukuru basi nasema nakupa visima 100 kwa Mbeya pekee hivyo kufanya idadi ya visima vitavyochimmbwa kuwa 700 nchi mzima’’ alisema mzee Sabodo.Baada ya mazungumzo mafupi Mh Wazri alimkabdhi Mzee Sabodo nakala ya Sera ya maji na pamoja na makakati wa maendeleo ya sekta ya maji.Hata hivyo, Mh Waziri alimhakikishia mzee Sabodo kuwa Wizara ya Maji itashirikiana kwa na kamati aliyoounda kwa kutoa ushauri na watalaama pale watakapo hitajika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Huyu Mzee mimi namfagilia sana. Mafisadi jifunzeni kuhudumia wananchi kama SABODO!

    ReplyDelete
  2. "Kwa sababu umekuja kunishukuru nasema nakupa visima 100 kwa Mbeya pekee hivyo kufanya visima vitavyochimbwa kuwa 700 nchi nzima" alisema mzee Sabodo.

    Pengine angempigia simu angepewa visima 50 kwa Mbeya pekee na hivyo kufanya visima vitakavyochimbwa kuwa 650 nchi nzima.

    ReplyDelete
  3. Bila kujali Mzee Sabodo anatoa misaada hiyo kwa profits zipi kwake, kuna kila sababu ya watanzania kumshukuru na hata wale wenye uwezo kama wa kwake ama zaidi kuona umuhimu wa kujifunza toka kwake kwa kusaidia Tanzania. Na naamini kwa kufanya hivyo watakumbukwa kwa uwepo wao na utajiri ama chochote kile Mungu alicho wajalia! Mungu bariki mioyo ya watu kama Sabodo!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana SABODO, wewe mtu kati ya watu. wenye uwezo kama wewe wapo wengi lakini hawatoi wala hawazungumzii shida za watanzania. Jitahidi pia usaidie wazee wenzako wa nchi hii wanapata shida sana, wangetamani kutoa misaada kwa wajukuu wako kama wewe lakini ndio hivyo hata chakula tu wanaungaunga.

    Kama unaridhia wazo hili, wasiliana na NGO moja ya Ruvuma inaitwa PADI ama Help age Tanzania ili uone ni jinsi gani ya kuwasaidia wazee wenzako, usije ukapitisha msaada kwa wajanja wakala kabla ya wazee kupata kitu.

    ReplyDelete
  5. huyu mzee sabodo kiboko. na inaonyesha biashara zake ni za halali ndio maana haogopi kutoa misaada. nakupa big up sana

    ReplyDelete
  6. An act to follow.. Kweli mafisadi wajifunze

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...