Pichani kulia ni Meneja Mauzo na Usambazaji Bwa.Reginald Mosha pamoja na Mkurugenzi Mauzo na Usambazaji Bwa.Bwa.Nicholas Brooks wakiwa katika picha ya pamoja na Mawakala wanne bora waliojishindia zawadi mbalimbali,baada ya kufanya mchakato wa kuwatafuta mawakala bora waliofanya vyema kwa mwaka 2010.Toka kushoto ni Bwana & na Bibi Mkandama wa Mkandama Store,Valence Msoki (Wazo Road Haulage Co.Ltd),Andrew Sindabaha pamoja na Fidelis Bashasha (Bashasha Merchandile).
Mkurugenzi Mauzo na Usambazaji Bwa.Bwa.Nicholas Brooks akimkabidhi zawadi mmoja wa mawakala,Bwa. Andrew Sindabaha aliyeibuka mshindi kati ya washindi wanne bora waliochaguliwa na kampuni ya TBL.
Pichani kusho ni Mkurugenzi Mauzo na Usambazaji Bwa.Bwa.Nicholas Brooks,Meneja Mauzo na usambazaji Bwa.Reginald Mosha pamoja na Meneja Usambazaji Bwa.Albert Mallya wakiwasikiliza baadhi ya mawakala waliokuwa wakiuliza maswali ya hapa na pale kwa ufahamisho na ufafanuzi zaidi.
Baadhi ya Mawakala hao wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa na Mkurugenzi Mauzo na Usambazaji Bwa.Bwa.Nicholas Brooks usiku wa kuamkia leo,hafla hiyo imefanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Double Tree,Masaki jijini Dar.
Pichani watatu kulia ni Mkurugenzi Mauzo na Usambazaji Bwa.Bwa.Nicholas Brooks akimpongeza mshindi mmojawapo wa wakala hao aliyejishindia TV flat screen (plasma) kutoka Bashasha Mercandile,Bwa. Fidelis Bashasha wakiwa katika picha pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TBL,hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya hoteli ya Double Tree,Masaki jijini Dar.

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji Bwa.Nicholas Brooks akizungumza na mawakala wa TBL kutoka kanda ya kusini usiku wa kuamkia leo kwenye hafla yao fupi iliofanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Double Tree,Masaki jijini Dar.lengo kubwa ikiwa ni kutoa zawadi kwa washindi wanne waliofanya vyema kwa mwaka 2010,na pia kufahamiana na kujadili mikakati mbalimbali ya kibiashara.
Kampuni ya bia ya TBL,usiku wa kuamkia leo imewazawadia zawadi mawakala wake wanne bora waliofanya vyema katika mwaka wa 2010,zawadi hizo zimetolewa mbele ya mawakala mbalimbali kutoka kanda ya kusini iliyojumuisha mikoa ya Lindi,Morogoro,Dodoma,Pwani pamoja na Zanzibar,zawadi hizo zilitolewa mbele ya mawakala hao (kama wanavyoonekana pichani) waliojumuika kwenye hafla fupi iliofanyika kwenye hoteli ya Double Tree.,Masaki jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera TBL .... Kwa kuona jitihada kati ya wadau na kuchukua hatua ya kuwapongeza.... Niwashauri muwaone na wadogo wanaojitahidi kukua....Wasaidiwe kuinuka. Hongereni wadau, Hongera sana TBL.... Mpango uwe endelevu.
    Mdau Moshi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...