Na Elvin Stambuli
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Askari wa kutuliza ghasia (FFU) jana badala ya kutuliza walikuwa chanzo cha fujo pale walipoingia kama wendawazimu katika ofisi za Kampuni ya Global Publishers na kuanza kupiga makofi na mabomu wafanyakazi.

Polisi hao walifika katika ofisi hizo ghafla huku wakiwa na bunduki na kuanza kufyatua mabomu ya machozi na baadaye polisi kadhaa waliingia ndani huku wakiwa wameshikilia bastola maalum ambapo kulikuwa na kikao cha kupitia magazeti kikiendelea, polisi mmoja alitoka nje na mtumishi mmoja. Kifupi hali ilikuwa mbaya kutokana na kipigo cha polisi hao kwa wafanyakazi wasiokuwa na hatia.

Kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mhariri Mtendaji Manyota aliwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, (IGP) Saidi Mwema na kumueleza kila kitu kuhusiana na fujo za kikosi cha kutuliza ghasia ambapo kiongozi huyo alishtuka na kutoa pole huku akiahidi kushughulikia suala hilo.

Wapiganaji na wadau wa habari wamelaani kitendo hicho cha askari kuvamia chombo cha habari na kupiga wafanyakazi wake bila sababu. Wamemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Said Mwema awachukulie hatua za kinidhamu wote waliohusika.

Wamewashangaa askari hao kushindwa kumuiga bosi wao Saidi Mwema ambaye hutumia zaidi akili badala ya maguvu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Polisi wa Tanzania hawana tofauti na armed robbers, hawajui maadili ya kazi yao. Ndiyo maana kila kukicha kazi yao ni kuwavamia watu wanaofanya peaceful demonstrations.

    ReplyDelete
  2. hawa pilisi ni wendawazimu kabisa...ndio tatizo la kuwachukua darasa la saba bila ya kuwafundisha nidhamu na haki za binadamu..

    ReplyDelete
  3. Ni wakati muafaka wa wanahabari kususia kuandika habari yoyote inayolihusu jeshi la polisi maana bila hivyo kutakuwa hakuna mabadiliko. Kwani mbona habari ni nyingi? Na pia tupewe up date ya muendelezo wa suala hili. Poleni wana habari wa Global publishers.

    ReplyDelete
  4. Global Publishers, wamefanya makosa ya kumpigia simu IGP na kupewa pole! Wanachotakiwa kufanya ni kuandaa timu ya wanasheria na kulishtaki jeshi la POlisi, Mwanasheria Mkuu n.k kwa hilo. Swali la kwanza ambalo watatakiwa kulijibu ni je polisi waliingia wakiwa na search warrant ambayo ilikuwa halali?

    Wakikaa na kuombea kuwa IGP atawachukulia "hatua" watu waliofanya hivyo ni sawasawa na kuombea nyani achukue hatua kali dhidi ya ngedere waliokula mahindi!

    Wake Up GP - tatizo mlijifunika nao kitanda kimoja mkidhani kuna mapenzi!

    ReplyDelete
  5. good job polisi narudia tena kazi nzuri

    ReplyDelete
  6. Ujinga mtupu, yaani huu upuuzi utaisha lini.
    Saidi Mwema naye ni kichwa cha mwendawazimu tu.
    FFU wametumwa na serikali ya Kikwete.
    Saidi Mwema hawezi kufanya kitu hapo.

    Ni mtazamo tuu.

    ReplyDelete
  7. jamani inaudhi sanaaaa,haiwekazi polisi waingie katika office na kuanza kupiga wafanyakazi na kurusha mabomu,hivi wamesoma kweli hawa?pole itasaidia nn,wachukuliwe hatua hao polisi..ankal uendelee kutuulisha kinachoendelea tafadhal.

    ReplyDelete
  8. mm naona waajiriwe polisi wasomi na sio mijitu iliyofeli form four na darasa la saba kujiunga na jeshi la polisi. polisi wanatakiwa kuwa ni watu wasomi ili wafanye kazi kwa akili sio kujua kurusha bomu na kufyatua risasi tu ndo unasifa ya kuwa askari.

    ReplyDelete
  9. Kwangu mimi ninashindwa kuelewa ni jinsi gani polisi, hata kama hajaenda shule na siyo mmoja kundi wanainuka kuvamia ofisi, naomba maelezo zaidi, kulikuwa na nini hasa, maana hiyo ofisi haikuanza kazi leo? ni nini hasa kilifuatwa hapo leo? Kama hakukuwa na issue basi nafikiri hao polisi ni vichaa au walivuta bangi. Tunaomba maelezo zaidi kuhusu chanzo cha polisi kwenda hapo. Na kwa kweli hawa kama walikurupuka au hata kama walikuwa na sababu sasa kwa nini wasiwakamate wahusika na kuwapeleka mbele ya sheria|? Jamani mambo Tanzania yanakwendaje, je mmechoka amani zawadi ya thamani Mungu aliyotupatia? Hawa polisi wachukuliwe hatua mara moja, sijui ni nani amewaruhusu polisi kuchua sheria mkononi siku hizi? Kiboko yao ni kuwaweka ndani wajue kuwa hii nchi ina wenyewe na wenyewe ndio wanaowapa polisi kula ili wawatumikie na siyo kuleta upuuzi. Hii habari iandikwe kwa kirefu zaidi ili ieleweke tujue kulikoni Tanzania. Kama vile polisi wamerogwa jamani

    ReplyDelete
  10. Yani kweli polisi wetu ni mafisadi. Kama hao jamaa hilo gazeti siyo la fisadi basi mjui matakiona cha moto. Mafisadi watawaandama mpaka mjui mwisho wenu. Hopo polisi wametumwa na mafisadi.

    ReplyDelete
  11. Wananchi wenye hasira waanze kuwapa kipondo cha paka mwizi hao polisi ili wapate adabu.

    ReplyDelete
  12. Tanzania ingekuwa na sheria kama nchi nyingine Duniani kama mtu akidhalilishwa na polisi ana lipwa fidia na aliomdhalilisha ana chukuliwa hatua, nadhani hata hao polisi wangekuwa waanglifu kabla ya kufanya upuuzi wowote. Tatizo hii sheria ipo kwa matajiri na watu Wakubwa tu.Raia wa kawaida akionewa hana sauti na akiwa na bahati atapewa pole.Hata kama atakuwa amepewa kilema Masikini Tanzania hana thamani yoyote hata kuku ana thamani kuliko Mtanzania wa hali ya chini.Kama mnabisha tuone kama hao Polisi watafanywa kitu chochote na huya dereva aliye umizwa atalipwa fidia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...