Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakifyatua mabomu ili kuwatawanya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliokuwa wakiandamana leo asubuhi kuelekea Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kufikisha malalamiko yao ya posho ya Sh 5,000/ ambayo wanadai ni ndogo haitoshi kwa matumizi na badala yake wanaishinikiza Serikali kuwapa Sh. 10,000/=. Hata hivyo maandamano hayo yaliishia maeneo ya Savei baada ya kukuta ukuta wa polisi hao umetanda Barabarani huku wakitoa matangazo ya kusitisha maandamano hayo na kutawanyika, baada ya kutoa matangazo hayo na wanafunzi hao waliendelea kuwa maeneo hayo huku wakiimba ndipo askari hao waliamuliwa kuanza kufyatua mabomu ili kuwatawanya. Katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa ila ni wanafunzi wachache tu waliokamatwa.Bomu la machozi limeshaachiwa hapa likianza kufyatuka...Wanafunzi hao wakitawanyika kwa kukimbia kila mtu na njia yake baada ya mabomu kuanza kufyatuliwa.Wanafunzi hao wakiandamana, kutoka chuoni...Wakiwa na mabango yao yenye ujumbe kuhusu kile wanachodai na wasichohitaji.Safari ilikuwa ni ndefu huku wakitembe, kukimbia na kuimba ili kuifanya safari hiyo kuwa fupi zaid lakini waaapi, iliishia karibu zaidi.Maandamano bado yalikuwa yakiendelea kutokea chuoni hapo.Mkusanyiko ulianza kama hivi...

Picha zote na Sufiani Mafoto Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Maisha ss hv ni magumu jamani kila kukicha vitu vimepanda bei si sokoni si madukani, nawasapoti 5,000 ni hamna kitu.

    ReplyDelete
  2. Mie kwa maoni yangu ni kuwa, hawa wanavyuoni wanachodai ni kweli kwa maisha ya sasa hiyo Shs.5,000/= haitoshi. Lakini naomba tujiulize hiyo hela wanayotaka waongezewe, Serikali haina majukumu mengine kama vile afya, maji (visima) n.k. ila ni wao tu wanavyuo? Naomba kujua hawa wanvyuo wamefanya jitihada gani ya kuona wenzao waliotangulia ambao walichukua mikopo, wamerejesha mikopo yao ili Serikali iweze kupata fedha za kufanya mzunguuko kwa kila mwanachuo? Au wanafikiri mkopo kwao ni kwamba wamepewa na hawahitajiki kuzijeresha???? Naomba kuwafahamisha kuwa mie mtumishi wa Serikali mshahara wangu wa kima cha chini haufikii Shs.10,000/= kwa siku. Licha ya hiyo, naomba waelewe walipa kodi wakubwa ambao hawawezi kukwepa kulipa kodi ili hao wanavyuo wapata hizo hela ni Watumishi wa Umma peke yao. Naomba watuoneee huruma nasi wafanyakazi wa Serikali kwani kodi yetu wanataka kuitumia vibaya!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. hakuna kitu kama kusema serikali haina hela, ina hela, kama haina hela hizo za kuilipa dowans zinatoka wapi? yote haya serikali ndo imesababisha, ikisema haina hela tutakuwa tunaona kama changa la macho..

    ReplyDelete
  4. Hiki kizazi kikizoea mabomu haya je hatima yake nini.Mnyonge mnyongeni haki yake mpe.

    ReplyDelete
  5. KInachonishangaza tu ni kuwa wanafunzi wanaitumia vibaya hii njia ya kuandamana. Yaani kila kitu maandamano, mwishowe tutawaona kama mtoto aliyelia Mwa mwitu kwa dhihaka, ikija jkutokea kitu cha maana zaidi watakuwa hawana njia nyingine ya kulalamika. Kuna vijana waliandamana sana wiki chache zilizopita, tukawaonea huruma tukaanza kuilani bodi ya mikopo, kuja kujua ( Baada ya bodi ya mikopo kujieleza kilichojili) kuwa hawakujua tu pa kupeleka malalamika yao.
    Kwa nini hawa vijana wasitumie serikali za vijana kupeleka maombi yao serikalini? Kuna njia nyingi ambazo wangeweza kufanya, kama kuandika malalamiko yao kwenye vyombo vya habari , kupeleka mwakilishi wao serikalinietc. Haya maandamano yanaanza kuwa kama ya Nairobi University miaka ya 70 na 80. Vijana walikuwa hawasomi ni kuandamana na chuo kufungwa na mzunguko huo kujirudia.

    ReplyDelete
  6. Wanachodai wanachuo ni haki yao kabisa na wanastahili kupewa pesa inayoendana na hali halisi ya maisha ya sasa ili waweze kusoma bila wasiwasi.lakini kwa nini kila mgomo na maandamano viwe vya kuongezewa pesa tu? Hawaoni matatizo mengine yanayoikumba Tanzania wanayoweza kuandamania? Kwa nini wasiandamane kushinikiza serikali isiilipe Dowans?

    ReplyDelete
  7. ndugu mtoamaada siokila hela ya serikali ni ya kulipa wanafunzi wanachotaka utakua wendawazimu unafikiri serikali inamuangalia mwanafunzi tu pekee yake ukizingatia watu wenyewe ni wakudai haki kila siku?wanafikiri wakimaliza chuo hela hiyo wataipata kirahisi?mbona wazazi wao hawawapi hiyo hela kama nindogo?tuoneeni huruma sisi wazazi hata sisi tumepita hukohuko tena wakati huo chuo hicho kilikuwa na jina sio sasa hata kwenye vyo bora 1000 duniani hakimo

    ReplyDelete
  8. Yale yale ya Mubarak!!! Hawa vijana wanafanya maandamano ya amani (hawana hata jiwe mkononi)ili kufikisha malalamiko yao kunakohusika. Kwa nini uwaletee FFU? Watawala wa Bongo wanahitaji kupatiwa kozi ya PSYCHOLOGY 101. Ukiwaacha wakaandamana hadi walikotaka alimradi hawavunji amani, watapungunza munkali wao na wanaweza kukaa meza moja na huyo wanayemlalamikia na kuyamaliza kwa amani!!! FFU ifanye kazi ya kuwakamata majambazi na mafisadi, na sio kukimbizana na wanafunzi.

    ReplyDelete
  9. Serikali ina hela ile mbayaaaa! We mfanyakazi wa serikali endelea kulia lia ...

    Kwanza wafanyakazi wa serikali mnafanyakazi gani? Kwenye Afya - uozo, rushwa; Nishati - vishoka, ukiritimba, rushwa; Fedha - rushwa, ukiritimba, kujuana; Habari - mnachojua ni kutetea serikali na kuchakachua habari zenyewe; Elimu - ... halali yenu kulipwa 1,000 kwa siku!!!!

    ReplyDelete
  10. NINA MATATU KUCHANGIA:
    1.Kwanza huu mtizamo wa kusema pesa za serikali ni makosa, hizi ni pesa za Watanzania/Walipa kodi, si za serikali, serikali imewekwa tu kusimamia, ndio maana nchi za wenzetu wananchi ni wakali sana iwapo serikali itatumia vibaya pesa zao/walipa kodi.

    2.Ni kweli 5000 ndogo kulingana na kupanda gharama za maisha, lazima serikali itumie pesa za walipa kodi ku-invest katika elimu ya juu kwa maendeleo ya Taifa.

    3.Ubinafsi- Licha ya yote hayo, tungetegemea pia kuaona hawa wanaoitwa wasomi wawe changu ya kuikosoa serikali kutokana na hali mbaya ya uchumi, ufisadi, umasikini unaosababisha na uongozi legezi, au mbaya nk.
    Lakni cha ajabu hawa jamaa wao kila mara tunaona wanaandamana kudai maslahi yao binafsi tu, hata siku moja hatujaona wakiandamana kupinga ufisadi, hali mbaya ya uchumi, nk. Wananchi wengi mijini na vijijini ni masikini sana, kwanini? Na kwanini tunaridhika na hali hii?
    Waone mifano ya wasomi na vijana wenzao Misri, Tunisia, nk. Tuangalie utaifa zaidi na kushikamana na sio ubinafsi kila siku kudai posho, naona hao wasomi ni kama fake na hasara tupu!

    Pia hii tabia ya serikali kuzuia maandamano kila siku, imepitwa na wakati, waache watu waandamane kwa amani usikilize hoja zao, ili ujue nini ni ni hasa kinawakera , kama serikali muweze kutafuta ufumbuzi haraka, kabla nyumba haijaungua moto.
    Haiingii akilini, kuzuia watu kuandamana kwa amani, hii inaashiria ukandamizaji nk, na ndio mambo tulivyoyaona kama Misri, watu walikuwa wakifanyiwa hivihivi miaka mingi tu , na sasa wamechoka. Kama serikali ina busara ingekuwa inawaachia watu waaandamane pasipo vikwazo, hakuna haja ya kutumia ffu kila mara kuleta vurugu mitaani, kupiga watu,nk. Hali kadhalika ni kupoteza pesa za wananchi pasipo sababu kuleta FFU nk kila mara. Wahenga walisema, asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    Lazima tukubali kuwa ulimwengu umebadilika sana hivi sasa, tukubali enzi za ubabe zimepitwa na wakati.

    ReplyDelete
  11. Wewe mtumishi wa ummma kama unavyosema hivi unataka kama wewe una shida na ukaridhika na shida zako unataka na wengine wakubaliane na hali waliyonayo.

    Unaserma kuhusu kurejesha hiyo unayoiita bodi ya mikopo imefanya jitihada gani ili waliokopa warejeshe mikopo yao?

    Unaweza kukubaliana na mimi kuwa ni serikali iliyokurupuka kuanziasha hiyo bodi bila kuwa na mipango thabiti ya kuhakikisha watu wanarejesha mikopo?

    Serikali imefanya juhudi gani ya kuhakikisha wanaomaliza vyuo wanapata ajirazinazoweza kuwawezesha kulipa madeni hayo?

    Ni ngumu sana kwa serikali kujinasibu na kujisifu kuanzisha bodi, ni wakati sasa wa kuanza mchakato wa kupata vitambulisho vya uraia ili kuweza kupata uhakika wa marejesho hayo.

    Nawaunga mkono hawa vijana kudai haki yao maana wanadai nyongeza ya dola mbili na nusu tu ya kimarekani ili kuweza kujikimu.

    ReplyDelete
  12. elfu 5 cyo kitu mdau yaan noma sana kwan cyo maisha hata kidogo,kwan kama vip wape bajeti ya siku basi kama wewe unadahi inatosha hyo sh 5000 kwa siku acha wivu kwan watu wanasaidiwa na wazaz wao ili waweze kuishi na cyo hyo tu elfu5 ndo inatosha kwa maisha haya

    ReplyDelete
  13. kwa mara nyingine serikali inatumia police kuzuia maandamano!

    Hivi demokrasia itapatikana vipi TZ? hao police wameambiwa kwamba wanafunzi hao wangefanya fujo ama uaribifu wa mali ya umma? hata kama wangepania kufanya uaribifu, wahusika wangefikishwa kwenye vyombo husika kujibi mashitaka na kuwajibishwa.

    Jeshi la police na serikali kwa ujumla awajifunzi kutokana na matukio yaliyopita? Inabidi Jeshi hili lipatiwe mafunzo na kukumbushwa kazi, ikiwepo kulinda amani , hivo hata maandamano hayo yalibidi kulindwa yawe ya amani.

    Serikali iache ubabe usio na sbb, ambao unakwamisha demokrasia nchini, Freedom of expression ni haki ya raia wote

    Tujifunze ya Egpyt, Tunisia etc.

    ReplyDelete
  14. Serikali ina pesa,tatizo ni kipaumbele. Ubinafsi tu umewajaa viongozi. Na isitoshe haya maandamano ni ya amani,kwa nini polisi wanayazuia? Nakubali siijui vizuri katiba kama wengine wengi, lakini hata hayo machache ninayojajua yanahitaji marekebisho mengi tu.
    Kwa mtoa maoni wa pili,naelewa hoja yako lakini sidhani kama ina nguvu,sijui hata nianzie wapi! Tembelea muhimbili uone wagonjwa wanavyotaabika kwa huduma mbovu;hakuna vitanda,magodoro wala vyandarua vya kutosha.Unalazwa hospitali kwa pneumonia ukitoka una malaria. Wodi ya wazazi,akina mama wanalala chini na vichanga vyao. Hayo maji yako wapi zaidi ya mikocheni,masaki na upanga? Wenye vijiuwezo wanchimba visima vyao kuondokana na karaha ya serikali
    Suala la kuhakikisha mikopo inarudishwa ni la serikali hivyo sidhani kuwa ni haki wanafunzi walioko chuoni waadhibiwe kwa kosa lisilo la kwao.
    Nchi yetu inakatisha tamaa sana.Hebu fikiria ni viongozi wangapi wanapokea mamilioni? Wabunge wanalipwa pesa lukuki,kwa kipi hasa wanachokifanya huko bungeni? UONEVU MTUPU!

    ReplyDelete
  15. KWAKWELI MATUMIMZ YA FEDHA NI MUHIMU SANA TENA ULICHANGIA KUWA DUNIA IMEKUWA NA MATUMIZI MENGI YA FEDHA NA YENEYNYE MSINGI, POINTI YANGU NI KWAMBA WANAFUNZI HAO WA UDSM WANAHAKI YA KUDAI ONGEZEKO HILO LA FEDHA ..NA KUJIBU POINTI YA HUYO MFANYAKZI WA SERIKALI AMBAE ANADAI KUWA HAWALIPWI 10000 KWA SIKU INAWEZEKANI NI KWELI ILA WAO WANA MARUPU RUPU.NA WANAFUNZI WENGINE WANATEGEME HIZO HELA KWASABABU FAMILIA ZAO HAZINA UWEZO WA KUWALIPIA KARO NA HELA ZA KUJIKIMU ,NI BORA SERIKALI ILI FIKIRIE WAZO HILO LA WANAFUNZI KWAKUA MADAI YAO NI YA MSINGI UKITAZAMA KUWA BADO KILA M2 ANAITAJI MAHALI BORA NA MAISHA BORA KAMA ILIVO SERA YA SERIKALI HII, TUKUMBUKE KUWA UKIMUELIMISHA MTOTO WA MASKINI UMELIMISHA TAIFA ZIMA.
    MIMI KWA UPANDE WANGU NASA SUPORT HYO MGOMO.

    ReplyDelete
  16. Nitaendelea kulaani vitendo vya askari police kuendelea kutumia mabavu kudhibiti maandamano ya amani.

    ReplyDelete
  17. Pangeni na mkutane huko huko kama wenzenu tulivyokuwa tukifanya zamani, tena bila polisi kujua. Kuandamana toka Mlimani mpaka ferry mtavunja haki za wengine wengi ambao hawana hatia yeyote.

    ReplyDelete
  18. Kama ni mkopo na wanafunzi watairejesha hapo mbeleni then sioni tatizo kwanini wasipewe iyo 10,000/= kwa sababu maisha gharama sana now esp bongo dar es salaam. Na hamna kitu kama serikali haina pesa.

    ReplyDelete
  19. hongereni polisi safari hii hamjaua mtu... bravoooooooooo! oh nimesahau, mngeua mngesingizia ni viongozi wa maandamano ndo waliosababisha?

    ReplyDelete
  20. kwanini TZ hawaruhusu maandamano ya wanavyuo? kila wakati wanatumia nguvu za jeshi kuwatawanya? haki ya mwanafunzi iko wapi? mbona nchi za ulaya mfano Uingereza wanafunzi waliandamana tena sio mara moja na hawakupigwa mabomu ya machozi bali walikua guarded ili wasilete uharibifu. japo wengine walifanya uharibifu, hakukua na mabomu ya machozi?? Huu ubabe iko siku utaleta yanayotokea Egypt manake wananchi watasema enough is enough!

    ReplyDelete
  21. Bora nikae kimya tuu. Shule yenyewe wanasoma bure halafu wanaleta upumbavu huu. "Haitoshi, haitoshi..." pesa mnayopewa ni ya kujikimu nyie watoto siyo ya kulewa, kungonoana na kununua blackberry.

    ReplyDelete
  22. Ngoja waingie mitaani huku wakiwa na familia halafu tuone kama wataacha matumizi ya byumbani ya shs 10,000 kwa siku kwa familia nzima, ilhali hiyo 5000 kwa siku kwa mtu mmoja wanaiona haitoshi! Halafu sasa waziri mkuu ndiye anayewakopesha? Mbona nchi nyingine mikopo wanafunzi wanakopa taasisi za fedha kwanini wao wanadai mikopo serikalini?

    Hayo mambo ya mikopo ya wanafunzi serikali ijitoe ila iweke scholarships kwa vigezo maalum mwenye kutaka kukopa akakope benki watajuana huko huyo mkopaji na mkopwaji kiasi gani wanakopeshana na kiasi gani watalipana na hiyo ndio dawa!

    ReplyDelete
  23. Tanzania inagueka kuwa Misri!

    ReplyDelete
  24. Hivi hiki chuo hakina mademu siku hizi mbona siwaoni kwenye hizi picha kasoro mmoja tu!

    ReplyDelete
  25. we anon 03:55:00 mavi yako..eti serikali haina hela wewe mtoto wa fisadi nini?watu wana hasira kama mbogo sasa..hela haitoshi wakati baba zenu wanaifilisi serikali shenzi kabisa..tena usirudie kusema tena...angekuwa kaka/dada yako au mtoto wako ungeona chungu yake...muulize uncle michuzi ana ndugu yake ud pale kila siku anapigwa mizinga,hali mbaya jamani kuna vitu vya kutetea vingine sio vya kupuuzia.

    ReplyDelete
  26. hawa jamaa ndio majiniasi wa nchi, wanafaa wapewe posho kubwa kuliko vyuo vingine vyoote (ukiacha SUA).

    hiyo itafanya ubongo uchemke zaidi na wasiwaze chakula dasarani. pia itakuwa changamoto kwa majiniasi wadogo kujiandaaa na kujiunga na chuo hiki bora tz.

    ud alumni

    ReplyDelete
  27. hivi mnajua hiyo hela mnayogombania ni kodi yetu sisi tunaoungua na jua mtaani? lakini mkitoka huko na kutukuta mtaani mnatudharau na kutuona hatufai... kama haitoshi nendeni kwa baba zenu wawaongezee, watanzania mmezidi kujidekeza... mbona nchi zingine hamna kusomeshwa na serikali...wajinga nyie

    ReplyDelete
  28. one hizo zinateswa na mafisadi.

    ReplyDelete
  29. mmmh kweli kuna wenye shida nayo ila wengine hapo wanatafuta za kuhonga na kulewea..tumeona mengi sana huku vyuoni...kuna familia zinaishi kwa 2000 kwa siku ...hawa wanajifanya kushindana na wenye nazo..utavikuta vimekaa samaki samaki mlimani city navyo vinazungusha round....acheni hizo..

    ReplyDelete
  30. Big up sana UDSM! Mlichokifanya ni chamaana sana.

    Wafanyakazi wa serikali mnaopondea hili inatakiwa mpewe somo, kwani karne mlizosomea si za sasa. Mlizoea kula chakula cha 500, kutoa copy sh 10, accomodation bure, medical fee sawa na bure, library fee bure, hamkutafuta materials kwenye internet, mawasiliano ya CM hamkufanya, . Ndio maana mnaona hiyo elfu 5000 ni kubwa kwenu. Siku hizi mambo yamebadilika. Acheni kuwavunja moyo, kama mlisoma kwa shida ilikuwa halali yenu kwasababu pesa mlizopewa mlikuwa hamzirudishi. Sisi tunakopeshwa na tutalipa, kwa hiyo lazima kukopeshwa kiasi chochote tunachohitaji. Hebu sikilizeni, mimi pia ni mwanafunzi wa chuo flani cha uma, ambapo napewa hiyo elfu 5 kwasiku na matumizi yake yako hivi:
    1 Medical fee nalipa sh laki moja kwa mwaka kutoka kwenye hiyo elfu 5 ya kila siku.
    2. Seheme ya kulala kwa siku nalipa 500.
    3. Chakula milo miwili + chai+ maji ya kunywa sh 3000 kwa siku.
    4. Kutoa copy kwasiku naweza kutumia sh 2500.
    Bajeti hii sijaongele habari za kununua vifaa vya masomo, vifaa vya usafi binafsi, mawasiliano. Je ukipiga mahesabu kuna kiasi kitabaki??? Au itatosha???

    Achene unafiki wa kutusema vibaya sisi wanenu, huku mkiifisadi nchi kimya kimya.
    Madai ya wanafunzi wa UDSM nayaunga mkono asilimia 100+

    ReplyDelete
  31. KUNA WATU WAPUMBAVU HUMU CJAPATA KUONA,yaan wewe unadiriki kumponda mtoto wa udsm anayedai haki yake?????hawa walifeli nin then wakaungaunga kifisadi mpaka sasa ndo mnaishi kitapeli then unajifanya mjanja.wapewe haki yao mbona dowans wanalipwa kwa nin hawa wasilipwe kwa vile elfu5 jaman haitoshi,nchi zote zinasomesha wanafunz wake chuo kikuu tena wanakopeshwa kama kawaida sasa mtu hunadai wakakope bank???achen roho mbya.serikali wasikilizen vijana kwan maisha yamepanda jaman,hiv watoto wenu wanasoma wap nyiny????au ndo ulaya

    ReplyDelete
  32. Perhaps the best way to deal with government loans is to let private banks provide loans to students according to individual's request and keep these students accountable for their loans. The government of Tanzania should not involve itself on such issues. Granted that the loans have to be paid, the bank can deal with each student individually.

    Furthermore, there should be an organization (a neutral entity) at the institution to oversee such transaction. This arrangement will allow students to concentrate with education and free the headaches of the politician dealing with student loans. Imagine the cost the government is undergoing placing the military and the use of tear gas unnecessarily. Oh goodness, we need help in our beloved Tanzania.

    ReplyDelete
  33. Ni nchi za Scandnavia na Uholanzi pengine peke yake ambako elimu ya chuo kikuu kwa wazawa tuition fees hakuna, ila pesa za kujikimu ni jukumu la mwanafunzi na mzazi wake na si serikali. Nchi nyingine kama UK na US tuition fees na pesa za kujikimu mwanafunzi na familia yake watajua watakaozitoa. Na vyuoni ni wakali kweli kudai pesa yao na wala hawajali utaitoa wapi, mkopo au scholarships.

    Suala la mikopo serikali iachane nayo kabisa maana ni kuendekeza rushwa na malumbano na wanafunzi yasiyokwisha. Ikiwa mikopo itatolewa na taasisi za fedha na serikali ikaweka sheria kwa kuweka kipindi maalum cha kulipwa tofauti na mikopo mingine mfano ilipwe ndani ya miaka kumi au ishirini, basi itakuwa ni jukumu la mkopaji kuamua kiasi gani anataka kukopa kwa ajili ya shule yake na atakopa kiasi ambacho anaona ataweza kumudu kulipa. Tena hakuna mtu atakayekopa kwa minajili ya starehe maana tunaona huku Ulaya vijana wanakopa pesa kwa ajili ya shule na wanajibana kweli kweli wengine mpaka wanakwenda kuchukua vyakula vilivyotuwa vinavyokaribia kuexpire wenyewe wanaita "food diving" ili kubana matumizi, wengine wamejiunga na food recycling na mbinu kibao wanatumia kusurvive. Nimeona wasichana kutoka Amerika shuleni wanaoshindia crakers na cornflakes na maziwa na soda, maisha yanaenda hakuna kupika chakula wala nini. £6 wengine ni matumizi yao ya wiki nzima hapo yaani siku 7 ukibadili kwa shilingi ya kitanzania ni kama 12,000 hivyo hata huko wako watu wanaoishi under £1 kwa siku. Na ikiwa unajijua wewe masikini ni ya nini kutaka kuishi maisha ya juu?

    Ushauri wangu kwa serikali yenyewe iachane na hiyo mikopo ya pesa za kujikimu, haiwahusu, serikali iamue kuwa vyuo vyote vinavyomilikiwa na serikali kusiwe na tuition fees, au serikali iwalipie wanafunzi tuition fees basi. Sasa sijui nauli, posho na mengineyo iwe ni jukumu la mwanafunzi mwenyewe kukopa benki ila mazingira yawe tofauti ya mikopo ya kawaida na mikopo ya elimu. Hapo hata huyo mwanafunzi atakwenda chuoni kusoma na pesa anayokopa ataionea uchungu. Vile vile timetable za shule nazo ziache kuwa za kishamba na za kizamani ziendane na wakati ili hata kama mwanafunzi akitaka kufanya kibarua cha kufagia au kuosha vyombo hotelini aweze kufanya na hata akitaka kufanya kibarua cha kusafisha hapo hapo chuoni aweze kufanya ili aongeze kipato chake.

    ReplyDelete
  34. hey mimi kama mimi naona elimu ya juu siku hizi serikali inaipeleka ndivyo sivyo maana haiwezekani kufuatilia masuala ya DOWANS baada ya kufanya mambo ya msingi kama haya sasa ona wana vyuo ndipo wameona kuwa maandamano ndio soln kwa kuwa tz bila kugoma haiendiiiiii.CONGULADULATION UDSM

    ReplyDelete
  35. kwakweli sh 5,000 haitoshi.Nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza mwaka 2004 hapo UDSM tulikuwa tukipewa pesa hiyo.Inashangaza sana kuona tangia kipindi hicho licha ya kupanda kwa maisha siku hadi siku bado tu wanawapa wanafunzi kiasi hicho.Sisi wenyewe ilikuwa haitutoshi,sembuse wao.Haki ni yenu kuandamana kwani naona serikari inafanya watu km watoto kila siku.Serikari kuweni na aibu,miaka zaidi ya 6 iweje msiwaongeza pesa hao wanafunzi au mbaka waandamane muwapige mabamu ya machozi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...