KWA KWELI HUDUMA KWA WATEJA (CUSTOMER CARE ) HAPA KWETU TANZANIA NI TATIZO KUBWA SANA AMBALO HALIPASWI KUFUMBIWA MACHO AU KUMEZEA KWANI LITATUPELEKA PABAYA SANA .

Mnamo tarehe 19/2/2011 saa nane na nusu 14.30 mchana Bint yangu alizidiwa ghafla wakati anaelekea Airport, ikabidi tumpeleke Aga Khan Hospital aweze kupata huduma za matibabu ya haraka.

Tulipofika Hospitalini hapo tulipokelewa kitengo cha dharura (Emergency) tukalipia malipo yote waliyotaka tulipe na wakaanza kuchukua maelezo ya mgonjwa na vipimo.Mnamo saa moja na dakika arobaini usiku (19.40) wakatuambia kwamba wanataka kumpima kipimo cha Utla sound tukalipia na kwenda kungoja kuchukua kipimo.

Tulisubiri hadi saa nne na dakika arobaini usiku (22.40) kipindi chote hicho tumekaa tunasubiri kipimo bila mafanikio wala taarifa ya kinachoendelea , tulipowauliza wanadai kwamba Daktari amefuatwa na dereva aliyemfuata hapatikani katika simu.

Kinachosikitisha ni kwamba unalipia Huduma mbovu.Pia watumishi wao hawana lugha ya kumtia moyo mteja wabishi , jeuri wao wanachojali ni pesa tu hakuna kingine zaidi ya pesa.Cha kuwauliza hawa Ndugu zetu wanadhani tunakwenda pale kununua huduma mbovu au matibabu mazuri?

Tunapenda wafahamu tunakwenda pale kutafuta huduma nzuri si vinginevyo ,tusilalamikie Hospital zetu za Mwananyamala tu hata Aga Khan ni madudu tu. Katika Taaluma za utabibu cha kitu cha kwanza kinachompa unafuu mgonjwa ni huduma nzuri ,upendo na huruma toka kwa wahudumu wa afya .

Wakumbuke tunalipia hizo huduma tuna haki ya kupata huduma nzuri na za kuridhisha. wajitahidi kurekebisha mapungufu yao.

Ni mimi muathirika wa huduma za Aga Khan
S.Kessi Mtambo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Umeongea kweli kabisa hospital za Tanzania zina kasoro nyingi sana kuanzia customer care hadi hap madaktari wenyewe , mimi huwa nashangaa sana hawa watu wana ubinadamu wa aina gani?? mtu anaumwa cha muhimu ni kumpokea mgonjwa kwanza na kumpa first aid hao cha kwanza ni kuchukua pesa huku mgonjwa yuko taabani . hawa madakatari wote wa hospital kuanzia hapo customer care hadi vyumbani sijui ofisini kwenyewe kumeoza kabisa. na kikubwa nashangaa usomi wao + utu mgonjwa anahitaji upendo kama alivyosema huyu muathiriwa hapo juu na si lugha ya matusi ama vipi.
    Hivi nyie madaktari,manesi na viongozi wengine mna utu kweli?? mmezaliwa na wanyama ??? unaishi na wanyama??? na je kikubwa zaidi elimu na taaluma zenu zinasaidia nini hili taifa> mimi naona ni wapumbavu kabisa hamna akili mna mtindio wa ubungo maana mtu ambae yuko radhi amuue mgonjwa kwa kutompa matibabu ni mwehu ndiyo nyie.


    hata aibu hamna.Ny******ko


    Mdau: muumiaji wa nchi hii.

    ReplyDelete
  2. si hospitali tuu hata maeneo mengi mengine hata hoteli tu, unayokwenda kula kwa kulipa!!! Sijui tutafika???!!

    ReplyDelete
  3. kaka pole. ulienda wrong hospital.ungeenda Amana, mwananyamala au sinza ziko huduma fresh tu we ndo hujui. pamoja na matatizo kibao wako fresh sana na wana wataalamu. hapo Agha Khani ni HOLIDAY PLACE/RESORT ya wagonjwa.zero experts....

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu jaribu ukiwa unatoa comment zako unaexclude na wengine,kifupi haitakuumiza kwamba ukisema neno baadhi ya madaktari,kwanza ungekaa ukafikiria baadhi ya watu waliojitoa kufanya kazi hiyo ya udaktari wamejitoa kiasi gani kwa hilo,hii ni kazi km ilivyo ualimu ni kujitolea tu maslahi hakuna mpk ujulikane,kuna watu wanaharibu taaluma hiyo kwa kuweka maslahi mbele na ndio sababu wamesababisha waue baadhi ya watu ila si wote coz kuna watu wanajituma na wanasaidia jamii na sidhani km ww mara zote hujatibiwa ukaridhika na huduma,kila kitu hakikosi kasoro ila jaribu kutoa sifa zake,mishahara midogo plus conditions za kazi nazo,wafikiri angekuwapo huyo mtaalamu wa ultra sound ungewekwa?madaktari wangekuwa wameshakuhudumia muda wote,usilaumu madaktari plz inauma coz wengine ukiwaona wanavyojituma haifananishwi kabisa na hao wanaoiba mamilioni ya walipa kodi huko bungeni,nadhani niishie hapa maana nahisi niliyonayo ni mengi hakuna space ya kuyaandika na kuyamaliza......

    ReplyDelete
  5. CUSTOMER SERVICE NI KITU MUHIMU SANA KWA MAENDELEO YA BIASHARA; WAHUSIKA HAPA KAMA MNA MASIKIO NA MSIKIE HII NI KARNE MPYA; MAMBO YA KULINDANA YAISHE, VIONGOZI MUACHE KUTAFUTA MCHAWI WENU...HII NI TABIA CHAFU SANA - KAMA MUHIMBILI NDO USISEME!! WATU WAKO WENGI SANA WANAHITAJI KAZI - KWANINI HAKUNA DESTURI YA KUIPENDA KAZI YAKO, KAMA UNAONA HAIFAI ACHA! TAFADHARI AGA KHANI JISAFISHENI KABLA HATUJAWAUMBUA!!

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo juu nakuunga mkono kabisa, mimi nimetibiwa TMJ hospital siku mbili zilizopita lakini customer care ni mbovu hamna mfano, unapanga foleni zaidi ya masaa wahudumu wanaongea na simu tu muda mrefu hawajali hata kama kuna mgonjwa mbele yao. Ukienda upande wa chumba cha sindano manesi niliokutana nao hata kusoma maelekezo ya daktari ili waweze kujua dawa kiasi gani kinahitajika kumchoma mgonjwa ni taabu wanaulizana kama hawajasoma vile! watatuua na ni aibu wanaonekana ni matokeo ya CHEAP LABOUR! Sidhani wanyama wamefikia hatua hii ya kutojaliana kama sisi binadamu sijawahi sikia mbuzi kamuua mbuzi mwenzake ila sisi ni zaidi ya wanyama. Muathirika mama Kelvin

    ReplyDelete
  7. Kwa Agakhan tatizo ni kwakuwa wewe sio mhindi, ungekuwa mhindi ungepata huduma kwa kiwango cha kimataifa,pale kunaubaguzi wa rangi na sijui hii hali itaendelea hadi lini.

    ReplyDelete
  8. Ndugu nyumbani ni aibu,kichefuchefu mpaka hasira.Si hospital tu kila mahali Dar Express basi ndo usiseme yaani wote from dukani to daladala hawajali mteja.Its sad ila ndo hali halisi something must be done

    ReplyDelete
  9. Yani mimi nawashangaa sana mnaolalamikia matibabu, kwani ktk nchi yetu ni eneo gani lililotengemaa ambalo unaweza kutatua tatizo lako kwa haraka? Si hospitali, si polisi, si elimu, si idara zote,zooote kabisa hakuna,labda mniambie leo ndo mabadiliko yameanza nitaamini, msisumbue vichwa vyenu bure,kila kona ktk nchi yetu ni matatizo.

    ReplyDelete
  10. Pole sana ndugu yangu.

    Ila napenda muathirika wa hili na watu wengine wafahamu kuwa Aga khan sio hospitali bali ni HOTELI ndio maana hata wakaguzi waliokuja kukagua viwango (levels/grades) walishindwa kuipitisha kwakuwa hawana hata Dakitari ambae wamemuajiri wao ila wote wanafanya part time kwani ni waajiriwa wa hospitali nyingine sasa wanapomfata akiwa yuko na kazi za muajiri wake ndio wagonjwa wanapozeekea kwenye mabenchi kusubiri huduma

    ReplyDelete
  11. Haya mbona ni ya miaka nenda rudi kamwe hayataisha. Wauguzi wa nyumbani hudumia wateja kwa matusi. Nenda nchi zilizoendelea uenda mteja alivyokuwa mali kuliko hata kitu anachonunua. Customer Care ni First and Highest Priority. Mazungu wanaita PIKO.

    ReplyDelete
  12. Ndo maana wamegoma hata kusaidia waathirika wa mabomu Gongo la Mboto, wao pesa kwanza, nafuu ya mgonjwa sio kipaumbele. Utafikiri hawakula kiapo cha kuokoa maisha. Wafahamu kwamba maadam wameingia kwenye huduma ya afya, nafuu na kupona kwa mgonjwa ndio inapewa kipaumbele.

    ReplyDelete
  13. Msilalamike tu jamani you should have health insurance. Ukifika unaflash tu card yako unapewa huduma.

    Hospitali kama hiyo ya binafsi ni biashara na mmiliki anatumia pesa nyingi kutoa hizo huduma kwa hiyo ni haki yake kabisa kudai pesa kwanza.

    Bongo utamaduni wetu ni malipo kwanza, mambo ya kuanza kufuatiliana madeni baadae ni kero sana hakuna mfanyabiashara anayependa.

    ReplyDelete
  14. AGA KHAN NI HOSPITALI AMBAYO IMEPOTEZA MUELEKEO KABISA. TATIZO KUBWA LA AGA KHAN HOSPITAL NI KUWA HUDUMA HAZITOLEWI KI-HOSPITAL, ZINATOLEWA KIOFISI ZAIDI. KAZI ZA KIKARANI NI NYINGI NA ZINACHUKUA MUDA MREFU KWELIKWELI. NIMESHUHUDIA SIKU MOJA MZEE MMOJA WA KIGENI, NADHANI ALIKUWA MTALIANO AU MGIRIKI, AMEKAA ANANGOJA HUDUMA KARIBU MASAA MAWILI, HUKU AKITETEMEKA KWA MALARIA, MPAKA KIJANA MMOJA AMBAE NADHANI ALIKUWA MWANAWE ALIPOKASIRIKA NA KUMCHUKUA KUMPELEKA KWINGINE, NADHANI HATA PESA HAKUDAI, KWANI ALIISHALIPIA. MIMI NILIKUWA NIMEMPELEKA WIFE KUTAKA KUPATA HUDUMA ZA CLINIC YA WAJAWAZITO, PAMOJA NA KULIPA, SIKUENDELEA KUMPELEKA PALE, NI KERO! NA KINACHOUDHI ZAIDI, ULE MUDA MREFU UNAOKAA KUSUBIRI PALE, KUNA HARUFU MBAYA YA BAHARINI INACHEFUA KWELI. MIMI NADHANI ILE KAMATI INAYOSHUGHULIKIA KUCHUNGUZA MAHOSPITALI NA ZAHANATI WASIISHIE KUCHUNGUZA TU LESENI, WAANGALIE HATA UTOAJI WA HUDUMA, WASINGOJE MPAKA HESABU YA VIFO ITOLEWE NDIO WASEME KITU. AGA KHAN HUDUMA NI MBOVU NA ZISIZOMJALI MGONJWA, LAZIMA WAAMBIWE!

    ReplyDelete
  15. Kiukweli nampongeza mdau aliyepewa nafasi ya kutoa maoni yake ktk hili! sio aga khan pekee pia hata Regency hospital na Burhan Hospital. yaani imekua wao wanataka hela tu bila kuangalia hali ya mgonjwa! huduma kwa wateja ni mbovu kabisaaa! hawana lugha nzuri kwa wagonjwa kabisa! niliwahi kwenda Regency kumpeleka mwanangu akiwa anatapika sana lkn pale mapokezi niliishia kuwatukana tu, wanakwambnia usubiri mtu analeta faili lako wkt hakuna aliyetumwa kulifuata na ukiwa mkali wanakwambia "eeh wewe kaka ni msumbufu" bila kujali kuwa mwanangu anatapika sana nilikaa mapokezi kwa dk 30 bila kupata au kuona dalili zozote za huduma,nikaamua kuondoka na kumpeleka mtoto ktk kituo cha afya cha serikali cha mnazi mmoja ambako huwezi kuamini nilipata huduma ya haraka na nzuri ambayo sasa kila mtoto wangu akiumwa lzm nianzie mnazi mmoja kwanza kabla ya kwenda kwingine.
    kwa upande wa Burhan Hospital hata kama una kipele kidogo tu utafungiwa dawa kibaooooo!!! sijui hawana pa kiziweka au ndo kumaliza stock yooote ya dawa ambazo zina muda kdg pale pharmacy na kingine ktk hospital hii nikwamba wana mtaalamu mmoja tu wa magonjwa ya kinamama(GYNOCOLOGIST) na anaingia saa 8 mchana kila siku na yuko bize ile mbaya maana huwa anatokea Amana hospital kija pale, huwa hana muda kabisa wa kumchunguza vzr mgonjwa yaani yeye ukumwambia tu unaumwa nini hata kusema akukague ajiridhishe na unachosema wala hana muda, anakuandikia dawa tu! na wkt mwingine badala ya kukuhudumia anaongea na simu na watu wa wizara ya afya kuhusu ishu za Amana Hospital "duh naomba niangalizie ktk riport kuna maternal death ngapi kwa mwaka huu,maana nanihii.......amebanwa kwenye kikao"hebu fikiria hapo umekwenda ni mjamzito na una matatizo ktk ujauzito wako halafu mtu unayemtegemea akuhudumie vzr unamsikia akiulizia MATERNAL DEATH unapata wazo gani!!!???? Ikitokea unahudumiwa na na Dr flani na hayupo basi hakuna Dr ambaye atakuwa tayari kukuhudumia hata kama una hali mbaya kiasi gani! TAFADHALI WAJIREKEBISHE NA KUTAMBUA KUWA MGONJWA NI MTEJA NA ANAPASWA KUPEWA HUDUMA NZURI!!!!

    CHARLES.

    ReplyDelete
  16. pole sana!
    ila wewe ni complicator tu. masaa matatu kwa jumamosi usiku kufanyiwa ultrasound ni kawaida - na ukiona hivyo ujue daktari anahitaji ku-confirm tatizo ambalo sio urgent. Tatizo nyie mnaojitia mnaojitia mna pesa hamna subira, ungeenda hospitali nyingine hasa ya serikali (labda) ungelia!
    punguza complains, ulaya na marekani kusubiri kwa masaa kumuona daktari au kufanyiwa kipimo ni hivi hivi ukiwa huna appointment unless ni urgent situation.
    tupe hali ya mgonjwa.

    ReplyDelete
  17. pole sana mdau. mi mwenyewe yashanikuta, nilienda pale hoi usiku nikapokelewa emergency room, natibiwa kwa kadi ya bima basi ikawa issue kwamba haitoki dawa yoyote wala faili haliendi kokote hadi nikaweke fingerprint kwenye mashine zao, nikabebwa hadi hapo dirishani kuweka hiyo fingerprint. nikajiuliza sasa akija mtu ambaye amezimia anawekaje hiyo fingerprint, maana mtu akija na emergency case ni kwamba mtu amezidiwa sio anatembea kama kawaida! he

    ReplyDelete
  18. Nakubaliana na hayo yaliompata Ndg yetu pale Aga Khan kwani kuna mchezo mwingine wameanzisha kama ifuatavyo:
    1. Aga Khan wakiona bili inalipwa na Shirika au kampuni wanahakikisha unapata vipimo tele bila sababu ili waweze kukulipisha gharama nyingi tu. Waache mara moja jambo hili

    2. Lingine ni kuwa watu wengi tukienda pale kupima malaria parasites hazionekani ila ukienda sehemu nyingine unakuta malaria unayo. Ukiwauliza wanadai eti mashine zao ni sophiscated. Waache hizo.

    ReplyDelete
  19. Nenda AE za UK ndio ujue kuwa bora hata Bongo utapata huduma haraka ukiwa na pesa. Tena Weekend hata GP wako hafungui hospitali kabisa utaenda kutibiwa kwa walk in centres au community hospital tena huko baada ya kupiga simu ermegency na kukwambia muda gani uende yaani kukupa appointment. Na tena weekenda utaenda kukutana na madaktari wa kutoka eastern europe wanaokuja kufanya part time. Na kama ni siku za kawaida umeumwa ghafla na unataka kumuona duty doctor basi utakaa wee mpaka umuone huyo dr kisha akucheki afanye reference kwenye internet na kufungua vitabu! Na hata hiyo ultra sound ungesubiri weekdays usingefanyiwa weekend!

    Muwashukuru madaktari wa nyumbani wanafanya kazi katika mazingira magumu hawana kupumzika wala nini, wanajitoa kwa moyo wao wote.

    ReplyDelete
  20. mdau hapo juu anaedai kusubiri ni kawaida naona hajaelewa kitu, mimi yalinikuta hapo aga khan nilikwenda saa 1 usiku nikaandikiwa hiyo ultrasound nilisubiri kwa masaa 4naomba uelewe kinachosubiriwa hapo sio majibu ila ni huyo anayepiga hiyo picha anakua hakai hapo hospitali anaondoka saa kumi hivyo akitokea mgonjwa ndio atumwe dereva amfuate, mimi ilinibidi nisubiri tuwe wawili ndio afuatwe jamaa mwenyewe ni mkenya akija ana hasira huyo. hiyo nido aga khan hospitali paka unamaliza huduma una lundo la makaratasi.

    ReplyDelete
  21. Hospitali za private zina penda wagonjwa wa insurance.watu wa kawaida hawatakivi.Private hospitali wana tegemia madaktari wa kutoka hospitali za serekali.

    Waziri wa Afya alitukumbusha sheria inasema kwamba madaktari wanao ajiriwa na serekali hawarusivi kufanya kazi private.Sijui imefikia wapi.

    ReplyDelete
  22. Na mimi nina complain zangu , mimi shida yangu ilikua kwenye wauguzi , nilikua mjamzito wa miezi 5 , nilipata shida nikiwa kazini kwavile ilikua ni mimba yagu ya kwanza sikuweza kujua ni nini kinaendelea nilimpigia Dr wangu kumueleza ile shida niliyopata alinitaka nifike hospitali haraka sana , nilipofika aliniangalia then akanitaka nikapige ultrasound lakini kabla sijaenda kule aliniambia kabisa kua nahisi mimba yako imetoka lakini wacha tusibitishe kwanza , nilipotoka kwa Dr nilienda moja kwa moja chumba cha ultrasound bila ya kufanya malipo si kama sijui kama natakiwa nilipe ila nilichanganyikiwa kwa kile nilichoaambiwa kufika kule mume wangu akaambiwa aende akafanye malipo kwanza sasa alipokua anafahamishwa alikua hajakufahamu nikawa namfahamisha akaruka yuke nesi kwa ujeuri mkubwa kama ulikua unafahamu kila kitu kilikuleta nini huku? bila ya kujali nina shida gani wala nini yule dada alikunya mbovu zake akishaakaondoka , kwa kweli nilijisikia mnyonge sana kwa yale maneno na kubwa zaid kilichonihidhunisha ni mwanamke mwenzangu ambae anatakiwa awe na huruma ndio wa mwanzo kunisemea ovyo wakati nae huenda akapata shida kama ile , kweli mahospitalini kuna watu wanaharibu sifa za wengine kwa uwajibikaji wao mbovu nimemchukia sana sana yule dada na yy Mungu atampa shida kama ile aone vipi inakua unastahili kusemewa ovyo au kufarijiwa , lakini alienifanyia kipimo alikua ni dada mstaarabu sana Mungu ambarik na atamlipa kwa ilo.

    Kazi nyengine ni ngumu sana kama hatuziwezi tusitake , tunabeba majukumu ya bure huo ni wito jamani imani kubwa inahitajika.

    ReplyDelete
  23. Niliweka maoni yangu ankal asubuhi but sijui umeyapotezea? au ? maana wala sikuchafua hewa.
    narudia!

    Poleni ambao bado mnaendaga Aga Khan huku mkijijua kuwa sio wahindi.
    kwanza zile kilomita za from one huduma to the other?
    pili, clerical work supersedes kazi za kitabibu.

    tatu, hujafanyiwa kedi na wahudumu

    nne, mifoleni kwenye mabenchi/viti vya kusubiria

    tano, usalama wa gari ( kama umeenda nalo) kule nje!

    Uliye comment kuhusu Burhani, nakuunga mkono kiasi maana mie mtibiwaji mashuhuri pale.
    Pale pana nafuu ila mmh wataalamu wa kuwasubiria balaa.
    Huyo Gyno akija, foleni nakwambia basi ni kurashia tu.. akikucheki anakwambia, i quote ' umri wa mimba unaendana na ukubwa wa mimba'

    ha ha ha ha . nacheka kama mazuri vile!
    kupima malaria nini , hadi ujiombee. na fikiria malaria ilivyo simu kwa mjamwepesi.
    sasa kliniki yaani consultation ni dakika mbili na robo! khaaa!

    namba zenyewe zinachukuliwa mapema, unajikuta wewe umewahi umefika saa nane unapata namba 10 na kuendelea!

    sijui tutatibiwagwa wapi walahi!

    ila walau penyewe unapona kwa tabasamu na bado wahudumu hawajaambukizwa tabia mbaya kiviiile ( nasikia kuna kamera, so may be wana pretend)

    Msukuma mwenye swaga

    ReplyDelete
  24. Kwanza kabisa hii inasikitisha lakini pia kuna uzuri wa ubovu huu wa hospitali za wenye pesa. Uzuri wa ubovu huu ni kwamba sisi wa-uswazi tunaotibiwa amana na mwananyamala, na nyie mafisadi mnaotuibia pesa, wote tunatoka ngoma droo katika swala zima la huduma za afya.

    ReplyDelete
  25. Of all hospitals Regency ni afadhali. Nadhani ni kwa kuwa ni medical center (ndogo) na owners wana supervise closely. Nimeshashuhudia mara kadhaa mwenyekiti wa hiyo hospitali ambaye nae ni dactari anawafokea manesi kwa ku mistreat customers. Regency wako juu. That is why ni kahospitali kadogo lakini watu kibao, wagonjwa wengi wanahama toka aghakan

    ReplyDelete
  26. MICHUZI, TAFADHALI FANYA MUHTASARI WA ISSUES KAMA HIZI NA RESPONSE ZA WADAU UWE UNACHAPISHA KWENYE MAGAZETI HASA YA JUMAPILI WATU WASOME. CHAPISHA KWENYE GUARDIAN, MWANANCHI, NIPASHE ETC. KWA NJIA HII, UTASAIDIA WENGI KWANI KELELE IKIZIDI WATAJIREKEBISHA. ASANTE.

    ReplyDelete
  27. Kwanza natanguliza pole kwa hii service mbovu uliyoikuta hapo, lakini "Wait a second people!!!".
    Hizi complaints mpaka lini? Wote nnajua tatizo liko wapi. Insurance hamtaki, watu wakiwapa suggestions kuwa hizi investments nyinyi wenyewe mnaweza kufanya na sio kusubiri wahindi, wagiriki, wazungu wawafanyie mnabaki kimya. Mkipata mgonjwa hapo ndio mnakumbuka kusema uozo huu. Jiulize, miaka mitano iliyopita, wewe, familia yako mmetumia kiasi gani cha pesa katika matibabu? Ni watu wangapi unaosema wapo kwenye foleni za mapokezi wakati wewe unaenda pale. Sasa jiulize, je, suggestions za kuwa na community hospital ambazo zitahakikisha kuwa ina madaktari wake, shift zinapangwa kuhakikisha kuwa muda wote, specialists wote wanapatikana na sio hizi safari za kumtafuta Mkenya kwenye mabaa hapo ndio solution itapatikana. Mjue kuwa hii yote inahitaji pesa. Hizi ultrasounds sio pesa nyingi kununua na kuwa nazo za kutosha, kuwa na specialists wa kuwa ofisini 24/7, lakini tukiambiwa kuwa, hata kama ni preventative costs kwa familia ni TSH 250,000 ni shida, Hospitali kama hii kuwa na wadau wa kutosha basi inaweza kutoa huduma zinazofaa, kuwa na madaktari na wauguzi wa kutosha na wanalipwa inavyostahili.

    Customer care kamwe haitaboreshwa kama hamna example au reference site watu wanaweza kutoa kama mfano.

    ReplyDelete
  28. Naona watu wameguswa sana na hili jambo hasa ukizingatia ni huduma muhimu kwa kila mwananchi. Mimi naungana na aliyesema Burhani hata kama unaumwa kichwa utapewa dawa mfuko tele (za aina tofauti) na huyo dada Gyna mh.. ndo usiseme! Anakuhudumia huku anapiga dili zake hapohapo na washkaji kwenye simu na kiswahili chake cha mjini!! Namuombea Mungu na yeye apate ujauzito ili a-experience hiyo hali labda atajifunza.

    ReplyDelete
  29. HI MICHUZI NA WADAU,
    KWAKWELI NAMI NAOMBA NICHANGIE KUHUSU AGA KHAN, KWANI NIMESHAMPOTEZA MMOJA WA WAZAZI WANGU PALE, KWAKWELI AGA KHAN NI KIBOKO, YAANI FULL USUMBUFU, JAMANI MALIPO YA PALE NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NITOFAUTI. HAUWEZI AMINI MZAZI WANGU ALILAZWA PALE SIKU 6 NILILIPA ZAIDI YA MILIONI TANO (5,000,000) NA MWISHO WA SIKU HAWAKUWA WANAJUA HASA NI NINI KINACHOMSUMBUA, BAADA YA KUPIMA VIPIMO VINGI MNO LKN WALICHEMSHA, WAHUDUMU WALIKUWA NI WAJEURI KUPITA KIASI MPAKA NIKAWA NAWAHONGA, KWANI ILINIBIDI NIKAE NAO KUULIZA KWANINI WAO HAWANA HURUMA KWA WAGONJWA NIKAPATA JIBU KUWA WANALIPWA MSHAHARA MDOGO SANA, HIVYO WANAIFANYA ILE KAZI KWAKUWA HAWANA CHA KUFANYA, NIKAGUNDUA NINI TATIZO NA KUANZIA HAPO NIKAANZA KUWALIPA RUSHWA ILI ANGALAU WANISAIDIE KWA MZEE WANGU MPENDWA YULE, NDIO KIDOGO HALI YA HUDUMA IKAKAA SAWA, LKN HAUWEZI KUAMINI HATA BAADA YA KUONA MAMBO YA MGONJWA WANGU HAYAENDI SAWA NI WAO HAO HAO WALINISHAURI NIACHANE NA AGA KHAN NIENDE MUHIMBILI NA WAKANAMBIA KAMA NITAHONGA PALE MUHIMBILI BASI MGONJWA WANGU ATAKUWA KAMA MALAIKA KWA JINSI ATAKAVYOHUDUMIWA. HAUWEZI AMINI NILIKWENDA MUHIMBILI NA MGONJWA WANGU NA KUHONGA PESA CHINI YA LAKI 2 TU BASI ALIHUDUMIWA MGONJWA WANGU ANA AKAGUNDULIKA ANAUGONJWA WA UTI WA MGONGO LKN NDIO IKAWA TUMECHELEWA MATIBABU AKAFARIKI DUINIA.
    YAANI TATIZO ILI HATA SIJUI MTU UNALITATUA VIPI, YAANI HAKUNA PAKUKIMBILIA KTK HIZI HOSPITALI ZETU. JAMANI KWA WENZETU WENYE MITAJI MIKUBWA HOSPITALI NI SEHEMU MUHIMU YA KUWEKEZA, TENA KAMA UTAJITAHIDI UKAWALIPA WATU VIZURI NA UNKAWA NA WAHUDUMU WENYE KAULI NZURI KAMA HOSPITALI ZA MASISTA NAKWAMBIA UTAFANYA BIASHARA MNO NA WATU WATALIPA PESA YOYETE UTAKAYOTAKA.

    NAWAKIRISHA.

    MUDDY NICE

    ReplyDelete
  30. MICHUZI,
    Nakubaliana na Anony 03:09, imefika wakati blog yako ikaacha kutumika kama mahali pa ku "dump" complains tu pasipo kuleta mchango wa kuleta mabadiliko yanayokusudiwa kwenye jamii, wewe uko kwenye position ya kuleta mabadiliko kupitia blog yako,
    so take a further step kwa kushirikiana na magazeti au TV unaweza ukawa unafanya summary ya surveys na maoni ya wana blog, uwe makini hata hivyo, kwani ni eneo linaloweza kukuletea matatizo ya kisheria,
    lakini kwa wanataaluma wa habari kama wewe, utajua namna ya ku handle

    ReplyDelete
  31. kwa kweli umenigusa sana na hii issue ya aga khan, yaani pale wanaangalia kwanza rangi baada ya hapo unatumia kadi gani na kama ni wewe ndio umeajiriwa au ndio umepewa hali ni mbaya sana kuna mambo mengine unabidi uvumilie lakini SOMETHING MUST BE DONE ABOUT AGA KHAN

    ReplyDelete
  32. OT---Hivi Tanzania hamna Universal heath insurance? Inaelekea una hela sana lakini inashangaza unakwenda hospital na kulipa cash cash. Hivi hatuna hizi services au hatuna knowledge ya hivi vitu..Aliyesema ngoma droo kwa mafisadi na maskini katika health care hakukosea...

    aliyesema heri kuwa mbwa ughaibuni kuliko tajiri bongo...Dog dentist ushasikia hiyo? Niambie bongo millionaires lakini lini alikwenda just for dental check up? Mpaka jino limuume mtu ndio anakwenda kwa doctor au mpaka mtu aumwee ndio hiyo mnapokwenda mnapigwa mirays isiyona sababu..Utra sound zingine ni unnecessary na madhara yake ndo hayo...Tunatakiwa tuwe smart na siye kidogo sio kuwa na hela tu bila kuwa na knowledge... ndio maana hao sijui wahindi wanatudharau na kula hela yetu tu na kututreat as if we are nothing....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...