Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa bunge ), William Lukuvi ( wa pili kulia) akipata kikombe cha babu kutoka kwa mchungaji mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwasapila (kushoto) alipokwenda huko Loliondo.kulia ni Rosemary Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Sasa JK nayeye akipata kikombe mambo yatakuwa super hakuna tena ruswa…te te te….te. hata nusu…. kweli babu ni babukwubwa, na yeye nimkombozi jamani kwa jelo tuu… Angekua enzi za Mwalimu tunge natinalize faster faster

    ReplyDelete
  2. Duh Hii ya leo kali, Waziri mzima unakwenda kwa babu kupata kikombe wakati serikali haijatoa maelezo kuhusu uhakika wa tiba atoayo babu, hatujaelezwa jinsi inavyotibu na kama kuna madhara ya baadae (side effects). Nimechanganyikiwa kabisa kuona UOZO unaendesha nchi. Hii ni aibu wa wote tunaosoma Sayansi. Au kwasababu stori ya babu inafanana na ya YESU, maana anasema alikuwa fundi seremala halafu akaoteshwa, ina maana Mungu anapendelea mafundi seremala tu. JE HII INAMAANA HOSPITALI ZISITISHE MATIBABU NA WAGONJWA WAPELEKWE LOLIONDO? nataka majibu

    ReplyDelete
  3. hapo ndo uamini kuwa kwa mungu wote tuko sawa na wagonjwa ni wengi babu angeweka laki moja kunyuwa dawa wangekunyuwa wao tu viongozi na wenye uwezo jero halichagui masikini wala mwenye nacho yaani hapo ni sawa na kwenda kanisani na msikitini si kwa masikin wala tajiri ndaga ambalikile mwasapile we si unaona mwenyewe lakini kwa kikombe hicho cha dawa kama yangekuwa maji umemtembelea rafiki yako wa zamani kijijini wengi tusinge kunyuwa tungekataa dawa oyeeeeeen

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuzi hii ilikuwa ni Ijumaa au Jumamosi week iliyopita! huo ndiyo ukweli kabisa kibanda unachokiona hapo kando ndiyo mizizi inacharangwa kuwa vipande vidogo vidogo tayari pamoja na kuhifadhia dawa ambayo ni tayari, ikichanganywa na maji baridi ili isiwe moto sana kwa mnywaji...!Ukweli ni kwamba watu ni wengi sana na wa kila rika na aina mbali mbali katika maisha(Different life styles). It doesnot matter who you are!Na Imani ni kubwa sana kwa watu wote utakaokutana nao kwa Mchungaji. Watu wa huko (Sonjo)wanakuambia ukikutana na Mchungaji akisalimiana na wewe akikupa mkono ni baraka tele....

    ReplyDelete
  5. kunywa baba itakutibu kila kitu, wanaodharau watajibeba kwa babu tutaenda tuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  6. Naanza kuiona nguvu ya Lowasa ktk nchi hii, maana baada ya yeye kwenda na kutangazwa kwenye vyombo vya habari ndipo tunaanza kusikia vigogo wengine nao wanakwenda!!!

    ReplyDelete
  7. kudadeki!hakuna wale majumbani kwao wanajidai oooh!y? ujaleta kikombe cha moto or uvugu vugu....WOTE KWA BABU SAWA TUMESHARE KIKOMBE KIMOJA ZAIDI YA WATU LAKI MOJA.........................

    ReplyDelete
  8. KWELI babu Mungu akupe maisha marefu.kwani inaonyesha wagonjwa ni wengi sana na wote wanaamini kwa Mungu kila Goti litapigwa

    ReplyDelete
  9. kaka michuzi naomba sana ujitahidi kama ingewezekana, badala ya kuandika na kutoa picha nyiiiingi na melezo meeeeeeeengikuhusu babu wa loliondo, nigependelea na hata watu wengine wangine nadhani wangependelea kupata habari sasa za ushuhuda kwa wale waliopata kikombe na kufanikiwa ili hili la babu wa loliondo lituto mashaka, manake kwa maeezo ya babu dawa hii inafanya kazi na kuonekana matunda yake baada ya wiki tatu. sasa n muda mrefu wa kutosha japo kupata 10% ya watu waliopata mafanikio.

    ReplyDelete
  10. Waziri umefika Loliondo na wewe tayari umepiga kikombe cha babu...sasa jiandae na upange watendaji wanaohusika waweke miundo mbinu ya afya kama vyoo na kadhalika ili watu wasishambuliwe na magonjwa mlipuko. 'Imani yako itakuponya'

    ReplyDelete
  11. Suala lipo pale pale, je hiyo dawa inatibu? Mbona hamtuonyeshi hao wagonjwa waliopona kwa hiyo dawa?

    ReplyDelete
  12. Michuzi ee sikiliza mkubwa, achana na anayedharau kwani hata kipindi cha Yesu pia kulikuwako wenye maneno machafu kama hao wanaoponda, nachowashauri wapondaji wajongee kwa wanazuoni au washauri wa mambo ya kimani ili wapate kujua hatma ya roho zao. Hata kwenye simu unaulizwa "Kama umependa wimbo huu bonyeza nyota na utakuwa wa kwako, gharama zitatozwa" thats means kama hupenzi usibonyeze. Kama hawataki wasiende na sio kuponda!!!!!!!! Regards.

    ReplyDelete
  13. Hata mkuu alishaenda, wewe unashangaa nini? Yeye ni miongoni mwa walioenda mwanzoni kabisa kabla jina la babu halijavuma sana.

    lakini michuzi mimi naomba usipige watu picha ukatoa hadharani havi. Haya sio maadili kabisa

    Halafu kwa nini serikali haifanyii utafiti dawa hiyo ili itoe tamko? Pamoja na kwamba ni mambo ya kiimani lakini mitishamba hiyo ilikuwepo hata enzi na enzi pengine ni ugunduzi tu wa babu.

    Pia hairuhusiwi kwenda na kikombe chako? Manake naona vikombe ni vilevile siku zote. Kiafya mnaionaje hiyo?

    ReplyDelete
  14. Ina maana kumbe Lukuvi naye kashauvaa? ama kweli ngoma kiboko, haiangalii wewe waziri wala mbunge.

    ReplyDelete
  15. JK anende mara ngapi wewe ? Babu alisema ukishakunywa tu hutakiwi kurudia. JK alienda mwanzo mwanzo kabla hata magaezit hayajaanza kutangaza hii ishu. Alienda kucheck masalia ya wtu wa kale akaunganisha huko huko kwa Babu.

    ReplyDelete
  16. Prezidaa mwenyewe alipotoka Oldoinyolengai kuangalia nyayo za watu wa kale alipitia kwa babu ndio akarudi

    ReplyDelete
  17. Kwa taarifa yenu yule 'tajiri' aliyekuja kwa helikopta akitokea South Africa (kama ilivyoripotiwa na media) alikuwa mzee Mandela! Inawezekanaje vyombo vya habari vya South na hata hapa havikunasa taswira hiyo! Hizi ni habari za ki-intelijensia kutoka kwa mwana intelijensia...

    ReplyDelete
  18. Unayesema watu watoe ushuhuda waliopona, ungejua maandiko ungekuwa umejua wale wenye ukoma kumi walioponywa na Yesu ni mmoja tu aliyerudi na kushuhudia na kushukuru.

    Pia inaelekea siyo msomaji sana wa makala nyingi maana watu wengi wameshuhudia kuponywa kisukari na hata Daktari mmoja huko Moshi ameshuhudia mgonjwa wake mmoja kuwa hana kisukari baada ya kunywa kikombe cha Babu.Kama watu wasijua kuna kupona wasingeendelea kusongamana kwa Babu.

    Kama mna wasiwasi na tiba ya Babu, mbona watu wanaenda mahospitalini siku zote hata kukimbilia huku Ulaya lakini bado wanakufa na magonjwa yao.Iweje Babu ndiye umshupalie kihivyo?

    Ann wa kwanza umesema hata waziri anaenda, jamani kuwa waziri kuna maana gani hasa?Unadhani ana tofauti na wewe?Kwa nini asiende na Babu anatibu?Kama kisukari kimeshindikana kupona mahospitalini waende wapi sasa?Asiyejua kufa aangalie kaburi.Wengi hamjapatwa na magonjwa sugu ndiyo maana mnaropoka tu mpendavyo subirini mtayaona wenyewe yakijiri maishani mwenu.Mnadharau tiba ya babu aliyooteshwa na Mungu!!

    ReplyDelete
  19. Jina la Yesu Lihimidiwe. Kaka Michuzi mimi ningeomba huyu Babu apewe kiti ili aweze kukaa chini na kupumzika. Ijapokuwa sijui ni masaa mangapi kwa siku huyu Babu hufanya kazi, ila kwa umri wake, kama mtu aliyestaafu, sijui kama ana uwezo wa kusimama siku nzima na kuhudumia watu bila kuchoka sana. Kama haiadhiri utoaji wa huduma yake, nadhani ingekuwa vyema Babu akapewa kiti (comfortable)akae chini huku akitoa huduma. Mungu akubariki na kukulinda Babu. Mungu akupe amani na maisha marefu. Mungu akubariki zaidi na zaidi katika yote uyafanyayo katika Jina Lake. Jina la Yesu Laponya kwa wote waaminio, Amen.

    ReplyDelete
  20. Science goes far then comes GOD!That's what 'tis.

    ReplyDelete
  21. hahaha, mnadanganywa na nyingi mnakubali! Tunataka scientific proof. Watu 100 kisukari, 100 pressure wapime kabla na baada ya kunywa hiyo dawa. Tupewe report ya majibu yao. Tunadanganywa hapa kisa alikuwa askofu. Mnatangaza dini tu hapa ambayo hakuna proof zaidi ya huwo mstari. Wasipopona watasema hawakuamini ndio maana hahaha!! Vert smart! Na hiko kikombe kimoja cha kuchangia kifua kikuu kitaongezeka tutaanza kuulizana kumbe babu....

    ReplyDelete
  22. huo waziri itakuwa kasukumwa kwenda na familia yake , huoni yuko nao benneti hapo kwenye bench na makombe yao ??

    ReplyDelete
  23. Haina haja ya kupiga kelele. Kama wapo wagonjwa wamepona kisukari na b.p na ukimwi kwa kutumia dawa hiyo ya padre mstaafu basi si kungetengenezwa kiwanda cha kuiweka hiyo dawa kwenye chumba na kusambazwa nchi nzima? Au huyu babu ni mchawi? Nakumbuka kuna watu walikuja na dawa ya meno ya dental power formula ambayo ukitumia meno hayaozi, na wao waliweka kwenye chupa, japokuwa dawa ilikuwa haitibu meno. Walijaribu kufungua maduka nchi nzima kusambaza baada ya watu kuistukia kuwa ni kamba wauzaji waliingia mitini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...